mkurugenzi mkuu wa zain tanzania khaled muhtadi na bosi mwenzie wakionesha modem na simu zinazoweza kutumika kwa huduma mpya ya 3.5G iliyozinduliwa leo na kampuni hiyo
paparazi wakimpiga mande mkurugenzi mkuu wa zain tanzania khaled muhtadi alipokuwa akizindua huduma ya intanet ya kasi ya teknolojia ya 3.5G yenye spidi ya mebiti 7 katika hoteli ya kempinski, dar. tanzania na ghana pekee ndizo nchi zenye huduma ya 3.5G katika nchi 16 ambazo zain imesambaa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Mh! Yaani wote hao wanampiga mande? 'Watamuua' kwa mionzi na miali ya kamera zao. Toba Kiswahili

    ReplyDelete
  2. Balozi,
    Hizi lugha unazotumia si mchezo!!

    ReplyDelete
  3. Hawo paparazi wana zoom lens ktk camera zao mbona wanamsogelea jamaa hivyo. Michuzi wapeleke kwenye blog ya taswiraz wajifunze.

    ReplyDelete
  4. Michuzi itabidi umtake radhi haraka sana Mkurugenzi mkuu wetu wa zain. Paparazi wakimpiga mande? eh!

    ReplyDelete
  5. hivi kwa nini mapaparazi huku huvamia msemaji kiasi hiki? sasa hao wengine waliohudhuria huo mkutano hata hawapati nafasi ya kumuona msemaji!

    ReplyDelete
  6. Sasa wewe balozi , nilidhani unalipwa n Zein kuwatangaza,
    Maana hapa nilikuwa nataka info kuhusu hiyo service yao inapatikana kwa kiasi gani , nilidhani hapa ni sehemu muafaka wakutupa habari zaidi ,ila umekalia tuu kuandika wanampiga mande.

    ReplyDelete
  7. Naam...hayo ndio maendeleo,simu kama hizo nasikia kule kwa mabeba maboksi bado hayajafika!!!yaani zile zile kama kunguru atupatie habari!!!

    ReplyDelete
  8. Brother Michuzi, pole sana kwa kutumia neno zito "kumpiga mande". Hiyo ni kali. Sasa kama wote hao wakimshambulia mande basi huyo mkurugenzi nadhani leo hatanyanyuka hata hapo kwenye kiti alichokalia.
    Pia hawa paparazi wakitoka kwenye mande wakaamua kumrushia viatu walivyomsogelea hivyo si hatari. Ataweza kweli hata kukwepa kama alivyofanya Bush? Michuzi nadhani anzisha shule ya paparazi wafundishwe mambo ya Taswirazzzzzzzz hata kwa mbali. Si vema kumzonga hivyo msemaji anapoongea na wandishi wa habari.
    Mdau

    ReplyDelete
  9. Vipi sisi wenye Laptop ambao tungependa kutumia huduma hii tunaweza kupata huduma hii??
    Michuzi umeelezwa hapo juu,wewe kama Balozi wa Zain ulitakiwa kutoa maelezo ya kutosha hapa na siyo kutumia utani!Nitumiwe maelezo zaidi na Zain kwenye fridokazadi@gmail.com tafadhali.

    ReplyDelete
  10. mtowa maoni wa December 22, 2008 10:09 PM pole sana. wewe baki tu na kuamini kila unachosikia.

    ReplyDelete
  11. michuzi "kumpiga mande" sio neno sahihi, sote tanzania tunajuwa nini mande bwana wacha vituko vyako bro

    ReplyDelete
  12. David Villa

    Nadhani tatizo ni kupeana kazi na pesa kwa kujuana, ukiangalai Kevin kafanya ndio kazi , lakini bado pale pale hayuko makini a ufanisi wa kazi anazo zitoa ku sponsa hizi blog, na dhani Michuzi kapewa kwa kujuana tuu, maana anashindwa hata kutoa info zaidi , hapo hela ya Zain inakwenda bure tuu wakisha katiana Michuzi na Kevin , mambo ya 30$ hapo. hakuna kujali habari ina fika vizuri au ni ujinga ujinga tuu.

    ReplyDelete
  13. Hii huduma inabidi utumie hiyo HSDPA modem (3.5G USB modem) kutoka kwao Zain au kokote kule. Lakini kwa kutumia simu za mkononi hasa hiyo Nokia 95 8GB waliyoonyesha katika picha hauwezi kupata 7Mbps wanayotangaza. Simu nyingi zilizopo sasa haziwezi ku downlink zaidi ya 3Mbps.

    ReplyDelete
  14. Na wewe uliwafanzaje, mbona uliwapiga picha wote wakiwa wanampiga mande huyo mzee?

    Wadau, ingekuwa ni uwezo na maamuzi yangu mwenyewe ningependekeza Kiingereza kiwe lugha ya kufundishia kuanzia vidudu hadi elimu ya juu. Kiswahili kingekuwa kama somo tu, kama kilivyo kiingereza shule za msingi. Sioni faida, naapa, SIONI FAIDA YA KUFUNDISHWA KWA KISWAHILI shule ya msingi halafu turudie na kuendelea kwa kiingereza shule za upili.

    Kuna faida? Kwa nini tusifundishe kwa kiingereza?

    Papa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...