.JPG)
mpigania haki za wanyonge mashuhuri angela davis alitembelea bongo miaka ya 1980 na kuzuru sehemu kadhaa ikiwa ni pamoja na chuo kikuu cha dar ambako umoja wa vijana uliandaa ziara hiyo. pichani akikaribishwa ukumbi wa nkrumah kuhutubia. shoto ni JK alipokuwa denti hapo udsm na mmoja wa wanakamati walioandaa ziara hiyo. cheche a angela davis unaweza kuziona hapa:
http://www.marxists.org/subject/women/authors/davis-angela/housework.htm
ama hata hapa:
/article/0,9171,903405,00.html.JPG)
angela davis alipendwa sio tu kwa msimamo wake kwa kutetea wanyonge bali pia afro na mabuga ambapo inasemekana aliyachochea mno kiasi hata alipoondoka kila kona utakutana nayo
.JPG)
angela davis akiongea
.JPG)
angela davis alipotembelea makao makuu ya umoja wa wanawake. shoto ni mwenyekiti wa wakati huo mama sophia kawawa
sorry just a question, during the 80's ladies were strutting it in short minis and fine dresses,
ReplyDeletenow they are today's woman who condem others on the same ?? i have noticed numerous good old days pictures with micro minis and where are all those wazee wa busara...then??, or those kariakoo chingas who will follow you around and rip you off your mini if you dare flaunter in one in their neighbourhood ?? mmomonyoko wa maadili then and now, then they were nice ladies just doing fashion wht about now ?
am in crossroads
Nafikiri miaka hiyo ni ya 1970s na JK alikuwa kiongozi wa wanafunzi hapo UDSM. Ilikuwa kawaida viongozi wa serikali ya wanafunzi kukutana na Julius Kambarage Nyerere kwa mazungumzo ikulu kujua vijana wana mawazo gani kuhusu mustakabali wa nchi yao,dunia na pia ma-denti.
ReplyDeleteNdio maana migomo ilikuwa nadra maana viongozi wa wanafunzi UDSM wanajua ipo siku wataalikwa Ikulu kwa chai na Mwl.Nyerere atakuwa msikilizaji wa wanayoongea na yeye kuhitimisha chai hiyo kwa 'comments' ambazo zitawabainisha kama kweli ni viongozi wa wanafuzi au la.
Nafikiri utamaduni wa kuwakutanisha viongozi wa wanafunzi na watu mbalimbali ungeanzishwa ili kuweza kupata viongozi wa kweli wa wanafunzi ambao baadae wanaweza kupata nyadhifa nzito ktk maisha yao ya uraiani.
angela davis that afro is whoa whoa whoa
ReplyDeleteBibi Umeme, waswahili husema, wakati ukuta ukishindana nao utaumia.
ReplyDeleteMiaka hiyo unayoitamani kulikuwa na uhamaji mdogo wa watu toka vijijini kuja mjini kutafuta maisha au toka mji mmoja kwenda mwingine.
Hivyo Darisalama, Arusha, Mwanza haziwezi kubakia vilevile, Ila Pemba,Lindi,Moshi,Sumbawanga zimeweza kubakia vilevile ilivyokuwa miaka ya 1970/80 kwa vile miji hiyo haina wahamiaji toka pande zingine za Tz.
NAHISI KAMA KUNA KITU KIZURI UMEANDIKA HAPA ANONY WA KWANZA ILA TATIZO UMECHANGANYA SANA LUGHA SISI WENGINE HUJATUPA FURSA YA KUELEWA. NAOMBA UFAFANUZI
ReplyDeleteNadhani alitembelea miaka ya 1970's. Miaka ya 1980's Bi Angela Davis, alipunguza hiyo 'trademark afro'.
ReplyDeleteenzi hizi wanaake ilikuwa fasheni kuvaa vilemba si waislam au wakristo
ReplyDeleteSI KWELI ENZI ZA NYERERE KWAMBA HAKUKUWA NA MIGOMO ILIKUPO PIA, NAKUMBUKA MMOJA WA 1967 LILIPOANZISHWA JKT WALIGOMA MLIMANI KUHUSU KWENDA JKT COMPULSORY BAADA YA AMA KUMALIZA KOZI AU FORM SIX, WALIANDAMANA KUELEKEA IKULU NA NYERERE MWENYEWE ALIENDA UNIVERSITY NA KUCHARAZA BAKORA KAMA NJUGU HIVI MMOJA WAPO ALIYEMCHAPA VIBOKO ALIKUWA MAREHEMU MWABULAMBO AMBAYE ALITOKEA KUMPENDA BAADAYE BAADA YA KUMALIZA DEGREE YAKE NA ALIBAHATIKA KUULA VYEO, ALIWAHI KUA RDD RUVUMA, MAKAMU WA MKUU WA CHUO CHA IDM MZUMBE, KATIBU MKUU WIZARA YA UTUMISHI, HIVI VYEO VYOTE HUTOLEWA NA RAIS, HUU MGOMO NAKUMBUKA NILIKUWA NA MIAKA SABA HIVI, PIA KUNA MINGINE MINGI TU ILIKUWEPO, SIKU HIZI NI MINGI KWA VILE HALI IMEBADILIKA WANAFUNZI WANACHANGIA ELIMU KWA KUPEWA MIKOPO AMBAYO KUPATA NI SHIDA NA RATE ZAKE HAZIENDANI SAMBAMBA NA HALI HALISI YA UCHUMI, ENZI ZILE WANAFUNZI WALIKUWA WANAKULA NA KULALA BURE, WANAENDA LIKIZO MAKWAO KWA PESA YA SERIKALI,ON TOP OF THAT WALIKUWA WANALIPWA KITU KAMA MISHARA HIVI, NA UKIMALIZA ULIKUWA UNAPEWA GARI JIPYA, TUNAWEZA KUSEMA WALIKUWA WACHACHE NA MISAADA YA DONORS ILIKUWA MINGI NA ILIKUWA HAIIBWI NA WAJANJA KAMA SASA, KULIKUWA NA MISAADA KIBAO TOKA KWA OUR FORMER COLONIAL MASTERS BAADAYEC WALIIKATA BAADA YA SISI KWENDA KWA SIASA YA UJAMAA NA KUFUKUZA WAZUNGU NA KUWANYANG'YA ARDHI WALIOKUWA AMA WAMEPEWA BURE NA WAINGEREZA AU KUNUNUA PAMOJA NA KUTAIFISHA MALI KADHAA IKIWEMO NA MAJUMBA, BIASHARA NA MASHULE. KWA UJUMLA HALI SASA NI MBAYA NDO MAANA KUNA MIGOMO GUNIA.
ReplyDeletekumbe mr. michuzi una picha nzuri za zamani. tafadhali jaribu kutafuta kwenye archives za magazeti uangalie zile picha za miaka ya early sixties za akina nyerere, kawawa, kambona, kahama n.k. na wake zao. that will be a very nice collection.
ReplyDelete