
Majuzi Avant alitembelea VOA na hivi sasa yupo kwenye tour ambayo alianzia huko Iraq na Kuwait maalum kwa wanajeshi wa Marekani walioko huko na sasa anaendelea Marekani.Maelezo zaidi tega sikio kwenye kipindi cha Burudani cha sauti ya Amerika kila Jumamosi ambapo Sunday anadodosa mambo yote ya wizara ya Burudani na starehe hapo Washington DC ama kwenye tovuti
au kwenye face book ambapo mambo yose utayajua mapema!
JAMANI HAWA WATU MBONA KAMA NDUGU WANAFANANA SASA HASA MACHO
ReplyDeleteHUU NI UPUUZI MKUBWA:
ReplyDeleteWALIMU WANACHAPWA VIBOKO!
Mkuu wa wilaya aamuru polisi kucharaza bakora walimu 32
* Ni kutokana na matokeo mabaya ya mtihani darasa la saba
Lilian Lugakingira, Bukoba na Saa Mohammed, Tanga
MKUU wa Wilaya ya Bukoba, Albert Mnali aliamuru polisi mmoja kuwachapa viboko walimu katika shule tatu za msingi zilizo Bukoba, kutokana na wilaya hiyo kuwa ya mwisho katika matokeo ya darasa la saba.
Tukio hilo la aina yake lilitokea juzi wakati mkuu huyo wa wilaya akiwa ameambatana na koplo huyo wa polisi alipowalaza chini walimu hao na kumuamuru askari huyo wa usalama, kuwachapa walimu hao viboko viwili kila mmoja makalioni na mikononi.
Walimu waliocharazwa viboko, tisa wanatoka Shule ya Msingi Katerero, 11 wa Shule ya Msingi Kanazi ambao walichapwa viboko viwiwili kila mmoja na walimu 12 kutoka Shule ya Msingi Kansenene walichapwa viboko vinne vinne kila mmoja.
Akizungumza jana na waandishi wa habari juu ya tukio hilo, mkuu huyo wa wilaya alisema alilazimika kuwatandika viboko walimu hao baada ya kugundua kuwepo uzembe kazini, ikiwemo kuchelewa kufika kazini na kutofundisha kama mikataba yao ya ajira inavyoeleza.
Alisema uzembe huo umesababisha wilaya ya Bukoba kuwa ya mwisho kimkoa katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka jana na kuwa uamuzi huo utasaidia kuwakumbusha walimu wajibu wao.
“Nikweli nimewachapa, mara hii nimewachapwa wakiwa wamefungiwa, wakati mwingine watachapwa hadharani,” alisema mkuu.
Kitendo hicho cha ubabe kimevuta hisia za wadau wa elimu, kikiwemo Chama cha Walimu Tanzania (CWT), ambacho kimeitaka serikali kumchukulia hatua kali za kisheria mkuu huyo wa wilaya kwa kosa la kuvunja sheria na kuwadhalilisha walimu 32 wa shule mbalimbali za wilaya ya Bukoba Vijijini kwa kuwachapa viboko.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa Rais wa CWT, Gratian Mukoba alisema suala hilo si jepesi na kwamba mkuu huyo wa wilaya ametonesa kidonda kibichi kwa kukitia chumvi hivyo aliyemweka serikalini mkuu huyo ndio atakayemtoa na kumchukulia hatua.
“Hivyo akaona ni bora kuwaadhibu kwani walimu hao wanadai fidia zao serikalini na yeye akaona hakuna wanachokifanya... kwamba hawafanyi kitu ndio maana kiwango cha elimu kimeshuka,’’ alisema Mukoba
Alisema kitendo hicho ni cha kibabe ambacho kinatumiwa na watu wanaofuja madaraka yao.
Aliongeza kuwa CWT itatoa tamko rasmi kwa ajili ya kumpeleka mahakamani mkuu wa wilaya huyo wa Bukoba, kutokana na kukiuka haki za binaadamu.
Alisema taarifa hiyo waliipata saa 5:00 asubuhi juzi ofisi yake walipokea barua pepe kutoka katika chama cha walimu, tawi la Kagera iliyoeleza kuwa mkuu wa wilaya anatembelea shule za msingi wilayani kwake na kutoa adhabu ya viboko kwa walimu.
Alisema kuwa baada ya taarifa hiyo uongozi wake ulitembelea shule ambazo mkuu huyo alipita na kukuta walimu hao kwenye vituo vyao vya kazi na walimu hao walithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Alisema kitendo hicho kimewafanya walimu hao kutokuwa na amani darasani na kufanya hata wanafunzi kuwadharau walimu hao na hata kuwacheka wanapoingia madarasani kwa ajili ya kufundisha.
“Kutokana na hatua hii walimu wanaona kuwa hatua iliyochukuliwa ya kuchapwa viboko ni kitendo cha udhalilishaji na uvunjaji wa heshima ya mwalimu mbele ya mwanafunzi na jamii anayoishi ambayo haijapata kuona tangu waanze kazi,’’ alisema Mukoba.
Alisema kuwa baadhi ya walimu walioadhibiwa wanafanya kazi bila ya kulipwa kwa zaidi ya miezi sita, lakini madai hayo yanaonekana ni usumbufu na wanalipwa viboko, badala ya kupewa haki zao.
Mwenyekiti wa CWT mkoa, Dauda Bilikesi alisema wanachama wake wanaitaka serikali kuchukua hatua ili kurudisha heshima zao. Alizitaja hatua hizo kuwa ni kulipwa fidia ya kudhalilishwa na kuvunjiwa heshima kwa kuwa walimu wa kike walipigwa makalioni huku nguo zao zikibaki wazi wakati wamelaala wakiadhibiwa, tena na mwanaume mbele ya kadamnasi.
Pia serikali iwaombe masamaha walimu hadharani na kumtaka mkuu wa wilaya hiyo awajibishwe kwa kutumia madaraka yake vibaya, kutenda kosa la jinai kwa kuwachapa walimu kwa kutumia nguvu kubwa ya dola wakiwa kwenye vituo vyao kazi na kwenye majengo ya serikali na pia kuwakashifu walimu kuwa ni mafisadi kinyume na sheria kwa kuwa wanaidai serikali haki zao.
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Magembe alikiri kuwa na taarifa hyo na kusema kwamba kamwe hawawezi kulivumilia.
"Ni kweli kuna tukio la aina hiyo na nimeshamwagiza mkuu wa mkoa kufanya uchunguzi na endapo ukweli utapatikana, serikali itachukuwa hatua kali dhidi ya wahusika," alisema Profesa Magembe na kuongeza:
"Nchi yetu haiwezi kuongozwa na watu wa aina hiyo na kamwe serikali haiwezi kukaa kimya... mara tu baada ya mkuu wa mkoa kumaliza kazi yake, atatuletea taarifa na sisi tutalifikisha kwa waziri mkuu kwa hatua zaidi kwani hao wote wako chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu".
"Hilo ni tukio la aina yake na lakusikitisha sana kwa sababu binadamu hawezi kuongozwa njia kwa kuswagwa kama ng'ombe... ni lazima serikali ichukue hatua kali dhidi ya wahusika".
Gazeti la Mwananchi
doh, i wanted to comment on how good tht brother is looking ( sunday shomari) but hii issue ya kuchapwa walimu viboko imenithrow out of my chair,
ReplyDeletenikiamka nitaendeleza libeneke; wakatabahu.
heeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeh,,jamani?hii kali ya mwaka mpya siamini kabisa,,,annon wa 3 ni kweli acha uanguke tu,me ndo akili imegoma apa yan naona km miujiza ivi uwa sisomi taarifa ndefu ivi ila imebidi nisome yan walimu wamechapwa????
ReplyDeleteduh!
aisee sunday shomari kaoa?
Sunday long time kamanda...Duh hii ya viboko kweli kiboko aisee I cant believe this 2009.
ReplyDeleteMIMI KAMA MKEREKETWA NA MPINGA USENENE NAMBA WANI ORGINO NA MPENDA MAENDELEOO
ReplyDeleteKUMPONGEZA BRAZA SUNDAY SHUMARI KWA KUTOKA MCHICHA UTAZANI MONICA LEWINSKY YUKO NYUMA YAKE. SASA BRAZA SUMARI, NAOMBA SIKU WANENE WAPYA WANAHAPISHWA. WEWE PAMOJA NA WADAU WENGINE KAMA VILE
CHARLES HILLARY
SUNDAY SUMARI
UNCLE J NYAISANGA
FULORA NDUCHA NDIO WASHIKE USUKANI WA KUTANGAZA SIKU HIYO ILI DUNIA YOTE ISIKIE. KWA MAANA HIZO SAUTI MWANANGU, SIYO MUCHEZO
MH. MASHAKA, JANUARY, DR.SHAYO NA RIZWANI HATA WAO WATAZIPENDA. KWA HIYO ENDLEENI KUTAYARISHA HIZO SAUTI WANANGU 2015 SIYO MBALI
MSISAHAU HATA MIMI NA WILAYA MPYA YA YOMBO VITUKA SIKU HIYO NITAHAPISHWA NA NITATAKA ITANGAZWE MOJA KWA MOJA TOKA V.O.A NA BBC, REDIONI WANI, TBS-TAIFA ETC....
SIKU HIYO ITAKUWA HARI MPYA, NGUVU MPYA NA KASI MPYA !!!!!
WOTE PIA MUTAPEWA NAFASI NYETI KULE TBC, HABARI MAELEZO, NA WIZARA NYETI ZA JUU, JUU KABISA KWA KUWA WANANCHI WEMA, ILA UFISADI NDO MWIKO KWENYE SIRIKALI YETU YA 2015
HAU VIPI WADAU???
WANAOPENDA MAENDELEO TUPO PAMOJA, LAKINI YALE MASENENE YANAYOPENDA KUCHAFUA HALI YA HELA MKOME. TENA NARUDI MASENENE TOKA NJE YA NCHI NDIYO YALE YENYE ROHO ZA KOROSHO BAADA YA MAISHA KUWASHINDA HUKO ULAYA WALIKO.
SASA WANATAKA KUTUCHAFULIA HALI YA HEWA SISI TULIO HAPA TANZANIA KWENYE JUA
HEBU MASENENE INABIDI MTULIE KABISA KWA MAANA HATUTAWARUHUSU KUTUPELEKESHA.
ZIDUMU FIKRA ZA MZEE WA PAMBA JK
ZIDUMU
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
KIDUMU
KIDUMU FIRKA ZA LAIS MTARAJIWA 2015
ZIDUMU
ZIDUMU FIKRA ZA MAKAMU 2015
ZIDUMU
ZIDUMU FIKRA ZA WATANGAZAJI WETU 2015
ZIDUMU
MASENENE WOTE WAKAFIE HUKO U.S.A NA U.K. WABEBE BOXI HADI WAFE KWENYE SHIFTI NA UROHO MBAYA
MKEREKETWA, YOMBO VITUKA !!!!_____________________________
Dakika 30 Za Internet Cafe Zimekwisa
michuzi naomba hii habari ya mkuu wa wilaya uiweke kwenye link yake yenyewe ili watu wapate kuisoma vizuri ni muhimu.
ReplyDeletemkuu wa wilaya atamchapaje mwalimu?
nakusihi mkuu wa wilaya ya nanihii naomba na wewe usiwachape walimu. tunakujua wewe mstaarabu uta weza kufanya hivyo
Sunday u're so damn cute man!!! the problem u're so damn player man.But guess what umri unayoyomaaaaaa think about settling down and focus about the future.
ReplyDeleteJumaPili, huyo Nephew nini. Mna fanafana kiushkaji... lol
ReplyDeleteSunday,
ReplyDeleteStill qute!
Radio one, salamu za j'mosi asubuhi
kweli sisi wabongo ni malimbukeni yani nikiona kitu watu wanadiscuss huku ndani ni upuuzi tu wajinga ndo waliwao naona aibu kuwa mbongo sababu ya wapuuzi wachache! mungu ibariki tanzania
ReplyDeleteSunday!you are still cute,are you single? mn,usa
ReplyDeleteSunday aka Jumapili kama alivyokuita annony hapo juu. Kweli sura yako ina mvuto sana..... duh! haya kama bado unatafuta jiko muombe sana Mungu akuchagulie jiko linalofaa sio linalofuka moshi likakuletea mafua. Kama umeoa basi bibie anabahati na kazi kubwa ya kukulea ili isikasirike ukachoropoka.
ReplyDeleteDu Duniani wanne wanne!! hahahah
ReplyDeleteSunday kafanana na OJ Simpson, ila kakosa "physique" ya OJ Simpson.
Ndimi mchora katuni ya maneno hapa
London