Home
Unlabelled
JK akutana na kiongozi wa mabohora duniani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
MBONA ANAINAMA CHINI!!! SURA IYO VIPI AU NDO "UTAKATIFU WENYEWE IMAN YA KIBOHORA"??
ReplyDeleteivi awa wanaamini katika nini??
Samahani kuuliza c ujinga.Mabohora(neno siyo geni) ndiyo watu au dini gani?,wanaabudu vipi? na historia yao kwa ufupi.Anayewaelewa naomba anisaidie kunielimisha.
ReplyDeleteKiongozi huyo wa Mabohora amekula chumvi nyingi, yaani ana umri zaidi ya miaka 90, ndo maana kusimama wima amenyooka inamwia tabu.
ReplyDeletemuulize polisi wa kibongo watu wasioa angalia watu machoni ni nani? utapata jibu zuri sana
ReplyDeletejamani mimi najua mabohora kwa kimombo ni passion (yaani matunda. sasa hii bohora ni imani gani tena?
ReplyDeleteMabohora wanafuata dini ya kiisalamu (Madhehebu ya SHIA), wanaabudu kama waislamu wengine.
ReplyDeleteWengi wa mabohora wanatoka jimbo la Gujarat huko India, na wameenea kote ulimwenguni. Wengine wanatoka sehemu ya Yemen. Hapa Tanzania wako karibu 7,000. Wengi wao wamezaliwa hapahapa Tanzania, mababu zao walitoka India na wameishi Tanzania karibu ya miaka 150. Wengi wamezaliwa Dar es Salaam, Zanzibar au Tanga, Lakini hivi sasa wengi wao wako bongo.
Mabohora wengi ni wafanya biashara wa vifaa vya ujenzi na vitambaa.
Kiongozi wa Mabohora Dr. Syedna Burhanuddin ana umri wa miaka 98, na anatembelea wafuasi wake kila nchi waishio.
Katika historia yao, waislamu wa Mabohora wamekuwa wakiheshimiwa kwa tabia yao ya amani na kujitegemea. Hii imewezekana kwa kiasi kikubwa kwa sababu ya mifumo ya jumuiya ya kijamii, kiutamaduni, uchumi na elimu ambayo inawahimiza Mobohora kusaidiana hususan kusaidia maskini.
Si tu kwamba wanafanya shughuli hizi kuwanufaisha wanajumuiya pekee, bali pia wanahakikisha kuwa wanakuwa wachangiaji muhimu katika maendeleo na mafanikio ya taifa.
Njia mbalimbali zimekuwa zikitumika ili kufikia lengo hili.
Kupanga familia: Familia zinazoweza kufanya hivyo zinaweza
Kuchukua zile familia ambazo ni maskini kuzileta na kutoa misaada muhimu.
Kufundisha biashara:- Wanachama wanahimizwa kutoa mafunzo ya kitaalamu na Kiweledi pamoja muda wa kujifunza kwa wote unaowakukua ili baadae waje waweze kujitegemea kiuchumi.
Misaada ya Kifedha:- Mikopo isiyo na riba na namna nyingine za misaada ya Kifedha imekuwa ikitolewa kwa wale wanaohitaji.
Nafikiri nimeelimisha ya kutosha... kujua mengi zaidi uliza maswali kwenye blog hii ili nijaribu kuzijibu kinaganaga.
- Bohora...
Bohora hao ni dini ya kihindi haswa gujerat na huyo kiongozi wao anaishi kule mumbai,tena wamegawanyika katika vikundi viwili yaani wale wanaomuabudu huyo mzee pichani na wanajulikana kwa jina la wenye vyeti na wale wanaompinga huyo mzee yaani wasio na vyeti (hivyo vyeti ni vitambulisho vitakavyowachukua hao mabohora eidha peponi au jahanamu...ni kundi lenye wafuasi takriban 20,000 kote duniani!
ReplyDeleteYakhe JK,huyo mzee mchawi kweli kweli...kaja kukuibia bila wewe kujua...na wewe kuchekacheka tu!!!
ReplyDeletehii dini ya bohara naona ni kiboko. Yaani Raisi ndio amemfata huyu imamu kwenye msikiti badala ya imamu kumtembelea Raisi?
ReplyDeleteNdugu Michuzi,
ReplyDeleteNafahamu kuwa una haki ya kuchapisha maoni unayotaka. Sijatukana na nilieleza kwa nini kuna mabohora wa aina mbili Kenya na kuna wale wanaolalamika kuwa hawana uhuru na kulazimishwa kulipa ada kila mwaka mwa kiongozi wao na kulazimishwa kuenda misikitini kila siku. Pia wanalazimishwa kuacha ndevu wanaume an kuvaa baibui za rangi rangi kwa wanawake wao.
Kama unapinga maoni kama haya, pasi utuambie kabisa ili tusipoteze muda wetu kuandika maoni pengine wewe binafsi huyapendi kwa sababu zako mwenyewe. Muulize bohora yoyote atakuambia kuwa nayosema ni kweli. Tunachoka na tabia hii ya censorship bila ya mtu kutukana.