
Asalaam Aleikum.
Hiki ni kitabu kipya kinachoelezea mchango wa wazalendo waliopigania uhuru.
Kitabu kinaeleza yale yaliyotendeka mwaka 1958 wakati TANU ilipoingia katika uchaguzi wake wa kwanza uliojulikana kama Uchaguzi wa Kura Tatu.
Waingereza waliweka masharti ya kibaguzi yaliyopelekea TANU itishie kususa kuingia katika uchaguzi.
Matokeo yake TANU ilikuwa karibu ijigawe katika mapande mawili hasimu - ya wale wanaounga mkono kushiriki uchaguzi wakiongozwa na Mwalimu Julius Nyerere Rais wa TANU na wale wanaopinga wakiongozwa na Sheikh Suleiman Takadir, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU.
Kitabu kimewafufua wazalendo wengi ambao leo wamesahaulika.
Waingereza waliweka masharti ya kibaguzi yaliyopelekea TANU itishie kususa kuingia katika uchaguzi.
Matokeo yake TANU ilikuwa karibu ijigawe katika mapande mawili hasimu - ya wale wanaounga mkono kushiriki uchaguzi wakiongozwa na Mwalimu Julius Nyerere Rais wa TANU na wale wanaopinga wakiongozwa na Sheikh Suleiman Takadir, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU.
Kitabu kimewafufua wazalendo wengi ambao leo wamesahaulika.
KITABU KINAPATIKANA IBN HAZIM BOOKSHOP MKABALA NA MSIKITI WA MANYEMALUMUMBA NA MAFIA STREET, KARIAKOO, DAR ES SALAAM
AMA WASILIANA NA:
Mohamed Said
Kinauzwa kiasi gani?
ReplyDeleteNikisoma historia ya vitabu vyetu Tz, ina onyesha kama kuwa Mwl. Nyerere alikuwa msomi wa kwanza kupata degree, hivi kuna kuna wadau wanao jua wasomi wa Tanganyika na Zanzibar waliopata elimu ya juu miaka ya 1890, 1900, 1910, 1920, 1930, 1940, 1950 atufahamishe.
ReplyDeleteMdau
Handeni
ni habari nzur sana kwa kutoa kitabu hicho. lakini mie nasikiti kuwa watunzi wengi wanatwambia historia ambazo sio kweli, mfano inapoongelewa mapinduzi zanzibar haongelewi JOHN OKELO wala huta mskia akitajwa pamoja na wahanga kibao wanaoishi uhamishoni, okelo alikuwa raisi wa zanziba kwa miezi miwili baada ya mapinduzi.
ReplyDeletehatusikii historia za afrikanization zilizoleta mapinduzi tanzani, wala hutawasikia kina ALY SYKES NA WENGINE KIBAO.
MNATULETEA HISTORIA ZA WAZUNGU KUUONA MLIMA K,NJARO KABLA YA WACHAGA, AU ZIWA MAGHARIBI[VICTORIA]KABLA YA WASUKUMA.
tunahitaji vitabu zaidi kama hivi. Historia ya nchi muhimu. People need to know more about their country...........
ReplyDeleteBalozi michuzi.Hivi vitabu ni vizuri.Ila naomba uweke topic ya kitoto tujikumbushe nyimbo za zamani zilizokuwa zinatufanya haswaa tujione watanzania kweli kweli.
ReplyDeleteMfano:
"Tazama Ramani utaona nchi nzuri....Majira yetu haya(sikumbuki vizuri kama unaweza kuuandika vizuri tafadhali)..Utumwa wa nchi Nyerere ameukomesha.Au "Twaiona/Mwaiona TANU HIYO..Mwaionaje TANU hiyooooo mwingereza kafunga virago!!Enzi hizo kulikuwa hakuna mambo ya viongozi kuwaza ufisadi walikuwa na uzalendo na nchi.
wewe unataka nyimbo za zamani? mimi nataka wazanzibari wenzangu tukumbushane maneno ya hekima ya maraisi wetu tuliyokuwa tukilazimisha kuyasema kila siku asubuhi assembly. mimi hadi leo nakumbuka hili moja kwa sababu hadi hii leo nimeshindwa kufahamu maudhui yake "afadhali kuwa na chakula kidogo na tukagawana kidogo kidogo kuliko kuwa na chakula kingi na tukaanza kukigombea" marehemu karume.
ReplyDeleteTunampa hongera mwandishi na mchapishaji. Tunakumbuka 'mkiki mkiki wa siasa - ch kada M B Barongo. Hivi historia lazima iandikwe na John Illife au A Coulson? nawakumbuka kina Isaria Kimambo na A Temu walichechemea kwa kukosa uhuru wa kuandika. Hata Ebarahim Hussein alileta historia ya maji maji kwa tamthlia badala ya maandishi rahisi.
ReplyDeleteBaadhi ya wadau tuko nje ya nchi. Wakati tunasubiri kukipata, tunaomba tuonjeshwe'mapitio'. Fanyeni msaaaadas kwenye tutazzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz