Marehemu Laura Dausen Munis-Mesaque

Familia ya Dausen Munis tunapenda kutoa shukurani kwa wote walioshirikiana nasi katika kufanikisha kusafirisha mwili wa marehemu dada yetu mpendwa Laura Dausen Munis-Mesaque kutoka Uingereza kuelekea Tanzania kwa mazishi.

Tunapenda kutoa shukurani za zati kwa watanzania, ndugu, jamaa na marafiki waliojitolea kwa hali na mali. Simu kutoka pande zote za dunia kwa ajili ya kutufariji, harambee za Wichita (KS) na Houston (TX), michango ya Dallas- Fort Worth na Uingereza, na wengine walio tumia akaunti tunashukuru sana.

Kutokana na Taarifa za madaktari, kifo cha dada yetu kilisababishwa na mgando wa damu kwenye mapafu. Mgando huo wa damu ulianzia kwenye mguu (deep venous thrombosis) na ikatembea na mishipa ya damu mpaka kwenye mapafu (Pulmonary embolism) na kusababisha mapafu kukosa oxygen. Marehemu amefariki akiwa na umri wa miaka 38.

Mwili wa marehemu dada yetu umeshawasili Tanzania kwa mazishi. Heshima za mwisho zitatolewa ijumaa ya tarehe 13 februari saa 4 asubuhi hapo kunduchi nyumbani kwa wazazi na baadae dada yetu atapelekwa kwenye makaburi ya kinondoni kwa mazishi saa 10 jioni.

MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA PEPONI.

AMEN.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Poleni sana ndugu wa marehemu Laura. Naelewa mko kwenye kipindi kigumu sana cha kumpoteza ndugu yenu ghafla lakini kwa mapenzi ya mwenyezi mungu awajalie moyo wa subira. Raha ya Milele Umpe Ee Bwana na Mwanga wa Milele Umwangazie, Apumzike kwa Amani, Amina.

    Joyce.

    ReplyDelete
  2. poleni wafiwa ni siku nyingi sasa tangu muanze utaratibu wa kumrudisha ndugu yetu nyumbani hatimaye kumlaza katika makazi ya milele.
    Nauliza kwa ndugu zangu waislamu, inakuwaje mwislamu akifia mbali na nyumbani na shughuli za mazishi zikachukua siku nyingi, kwani kwa sheria zetu inatakiwa mtu kuzikwa siku hiyo ili kuwahi adhabu ya kabri. maoni.

    ReplyDelete
  3. anon 12:23 sidhani kama kuzika mapema ni kuwai adhabu ya kaburi vinginevyo familia zote zisingependa kumzika ndugu yao ilikwenda kuadhibiwa..pili syo lazima kil hoja i inajadiliwa kidini kwani wakristo wana maadili yao na waislamu vilevile.
    KICHU

    ReplyDelete
  4. Tafuta wakati mwingine wa kujadili hoja zako za kidini, mazishi nk. watu wana machungu, ya mwanafamilia kUWATOKA DUNIANI, ndugu ,jamaa na marafiki Wanataka kusoma maoni ya Faraja na yanayotia matumaini katika kipindi hiki, SIO HABARI ZAKO HIZO.GROW UP.
    POLENI WAFIWA.

    ReplyDelete
  5. KUWAHI ADHABU YA KABURI ILI IWEJE? ADHABU NI ADHABU TU UWAHI AU UCHELEWE ADHABU IKO PALEPALE HATA KAMA ITAONGEZWA HAINA TOFAUTI. STOP THAT NONSENSE.

    ReplyDelete
  6. tunakuombea mungu akupokee roho yako dada yetu mpendwa! roho ya marehemu ikapumzike kwa amani! amen

    ReplyDelete
  7. Poleni sana wafiwa. Mungu amlaze mahali pema peponi.

    Nadhani aspect ya waislamu kuzika hapo hapo ilikua relevant zamani kwenye jangwa. mwili ulikua unaharibika haraka na kulikua na hatari ya magonjwa hivyo ikabadilishwa badilishwa kutisha watu kuwa kwa dini lazima kuzika hapo hapo. lakini kama mwili unaweza kuwekwa mda mrefu hamna tatizo na siku hizi waislamu wengi husubiri ndugu zao wafike ndo wanazik ingawa wote wakristo na waislamu tanzania hawaweki sana mwili kwasababu ya facilities kukosekana siku tatu utakuta watu wanazika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...