baadhi ya wadau wakiwa uwanja wa felix houphet boigny muda mfupi kabla ya mechi ya stars na senegal kuanza dakika kama tano toka sasa. timu zinakaguliwa sasa baada ya nyimbo za taifa
mashabiki wa stars wakiwa na bonge la bendela la taifa. wadau wako 30 tu lakini kashikashi zao utadhani wako milioni 4





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. watch live online www.tv.abidjan.net

    ReplyDelete
  2. Mpira unaendelea Senegal 1 Tz 0
    http://tv.abidjan.net/

    ReplyDelete
  3. Kipindi cha kwanza kimeisha Senegal 1 Tanzania 0.

    Kipa wa Senegal yuko likizo maana Taifa stars hawaingii ndani ya 18 ya Senegal wala Taifa stars hakuna krosi, au watu kupanda kwa kutumia wingers au walinzi wa pembeni kina Shadrack.

    Kwa kifupi Senegal wana hamisha mpira toka upande mmoja wa uwanja kwenda upande mwingine wanavyotaka. Ila Taifa stars imewaonjesha wachezaji wa Senegal machela za huduma ya kwanza mara kibao na kupelekea wapate huduma nje ya pitch.

    ReplyDelete
  4. Mbona bendera ya Tanganyika, msitutenge jamani sisi wazanzibar !!

    ReplyDelete
  5. ZAMBIA WAMEIPIGA IVORY COAST 3-0. HAWA SI TUNAWAWEZA? SI WALISHINDWA KWENYE CHALLENGE KAMA SIYE? HAYA KAZI KWETU.

    ReplyDelete
  6. ama kweli kaka michuzi quality is better than quantity.

    ReplyDelete
  7. Senegal wanatufunga. Hii aibu kubwa.

    ReplyDelete
  8. Mzee mbona hubandiki update? au ndo jamaa wametuua nini?

    ReplyDelete
  9. fuatilieni live mechi kwenye TV hii.....


    http://wwitv.com/portal.htm?http://wwitv.com/television/index.html?http://wwitv.com/tv_channels/b5059.htm


    toka kwa Madiba!
    Cape Town.."the Cape of Good Hope"

    ReplyDelete
  10. Shukrani kwa Mr. Supu na wote waliotupatia links za mpira huu. Ingawa tumefungwa, mpira umenifurahisha. Ila tunakosa football agressiveness (sio hooliganism)na ndio maana tunafungwa. Angalia jamaa wanavyoanguka na kudai fouls against etc

    ReplyDelete
  11. Bao pekee la Traore Mamadou wa Senegal ktk kipindi cha kwanza kwa kichwa limeizamisha Tanzania.

    Mpaka mwisho wa mchezo matokeo ni Senegal 1 Tanzania 0.

    Kipindi cha kwanza wachezaji wa Taifa hawa kujituma sana. Ila Kuanzia dakika ya 78 ya mchezo Taifa Stars walionyesha kujituma, labda baada ya kutambua ukweli kufika Abidjan Ivory Coast haina maana wamejipatia usajili wa kuonekana na timu za ulaya kama hawataonyesha vitu vya ziada ndani ya dakika 90.

    ReplyDelete
  12. daaah hii noma tumelambwa bao aibu lakini ndo mchezo wasoccer ukubali kushinda na kushindwa japo inauma
    toka kwa mdau wa stellenbosch wine land capestad

    ReplyDelete
  13. Wabongo bwana. Kuna wadau wanadai kwamba eti timu imeathirika na ganja kuwekewa vikwazo.

    ReplyDelete
  14. Tanzania tunaongoza kwa ubwege duniani.

    ReplyDelete
  15. Eti jamaa wengine wanadai "ooh..Usiku jamaa walitutembelea vitandani..".Hahahaha.Msijali sana bado tuna mechi za kurekebisha makosa. Kazeni buti vijana wa JK mechi zijazo tushinde zote. Zambia na Ivory cost tunawamudu

    ReplyDelete
  16. Sasa Bro Michuzi naomba nisaidie kitu kimoja. Kama nakumbuka vizuri Kuna jamaa mmoja anaitwa Mtikila, enzi hizo alipokuwa "hai kisiasa" wanasiasa wengine na viongozi wetu walikuwa wakimpinga sana kutumia hii bendera ya Tanganyika. Hivi sasa hili suala limekaaje? Maana naiona inapepea pale kwenye jukwaa la Watanzania.Sasa hii sio kwamba hizi ni dalili za kuanzisha Utanganyika na kuanza kukubaliana na Mtikila na wenzake akina Njelu Kasaka? au ni alama tu ya kuonesha kuwa hii timu inayocheza hai include Zanzibar? Je huku sio kuwachanganya watu wengine duniani ambao wamezoea kuona bendera yenye rangi nne?.....mimi sio mwana siasa, but I'm just thinking aloud. Jameni Mi nimiulizi tuooo...Ten penyewi hapa mkianzi kunishambulii wala mi siwajiboni...mi nitabanish kimya mbaka wenyewi mtachoki!!!
    Hahahaha

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  17. Hao washabiki wanatakiwa kushtakiwa kabisa waliopeleka hiyo bendera mie ni mtanzania bara hakuna kitu kama bendera ya tanzania Bara kaeni ukijuwa hiyo ni bendera ya tanganyika na tanganyika haipo tena.

    ReplyDelete
  18. Kaka Nashukuru nimepata jibu. ile haikuwa bendera ya Tanganinyika wala bara, ni bendera ya TZ kamili.Kumbe ni mpiga picha ndiye aliyechemsha, kamera yake ilikuwa na makengeza. Mwambie asirudie tena kosa kama hilo siku nyingine ebo!

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  19. sio bendera ya taifa hiyo ni rangi tu

    ReplyDelete
  20. uwiiiiiiiiiii sina mbavu

    bendera ya tanganyika hahahaa zanzibar sii mnayo yenu tena na timu yenu ya soccer?
    so msijali iyo ni tanganyika,na nyie mkienda soccer peperusheni yenu ya zenji

    BENDERA YA TANGANYIKA OYEEEEEE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...