Orodha ya makabila ya Tanzania
Kuna matatizo kwenye majina kadhaa katika orodha hii, kwa sababumbalimbali. Orodha hii inatokana na orodha ya Ethnologue ya lugha zaTanzania, pamoja na tovuti nyingine. Inawezekana kwamba baadhi ya majina ya makabila ni majina ya lugha au lahaja badala ya makabila, na labda majina mengine yaliandikwa vibaya.
Juu ya hivyo, hakunaufafanuzi wa wazi kusema kwamba kikundi fulani ni kabila au siyo.Vikundi kadhaa katika orodha hii vina wenyeji mamia tu, lakini vikundivingine vinavyo mamilioni ya watu; labda kila kikundi kinaitwa"kabila," lakini ni jamii za aina tofauti kabisa. Vikundi katikaukurasa huu vimeorodheshwa kuwa vikundi tofauti kutokana na ushahidikutoka Ethnologue kutofautisha lugha zao.
Hii ni orodha ya makabila ya watu ambao wamekuwa wanaishi tangu zamanikatika eneo ambalo sasa linaitwa Tanzania, pamoja na makabilayaliyogawiwa na mipaka baina ya Tanzania na nchi za jirani. Orodha hiihaizingatii makabila yanayoishi katika Tanzania kama wakimbizi kutokavita katika nchi za jirani. Ukurasa huu hauorodheshi vikundi vyawahamiaji kutoka nchi za kigeni, kama wahamiaji au wazao wao kutoka Arabia au Uhindi.
* Waalagwa (pia wanaitwa Wasi) * Waakiek * Waarusha * Waassa * Wabarabaig * Wabembe * Wabena * Wabende * Wabondei * Wabungu (au Wawungu) * Waburunge * Wachagga * Wadatoga * Wadhaiso * Wadigo * Wadoe * Wafipa * Wagogo * Wagorowa (pia wanaitwa Wafiome) * Wagweno * Waha * Wahadzabe (pia wanaitwa Watindiga) * Wahangaza * Wahaya * Wahehe * Waikizu * Waikoma * na Wairaqw (pia wanaitwa Wambulu).
Wengine ni * Waisanzu * Wajiji * Wajita * Wakabwa * Wakaguru * Wakahe * Wakami * Wakara (pia wanaitwa Waregi) * Wakerewe * Wakimbu * Wakinga * Wakisankasa * Wakisi * Wakonongo * Wakuria * Wakutu * Wakw'adza * Wakwavi * Wakwaya * Wakwere (pia wanaitwa Wanghwele) * Wakwifa * Walambya * Waluguru * Waluo * Wamaasai * Wamachinga * Wamagoma * Wamakonde * Wamakua (au Wamakhuwa) * Wamakwe (pia wanaitwa Wamaraba) * Wamalila * Wamambwe * Wamanda *
Wengine ni Wamatengo * Wamatumbi * Wamaviha * Wambugwe * Wambunga * Wamosiro * Wampoto * Wamwanga * Wamwera * Wandali * Wandamba * Wandendeule * Wandengereko * Wandonde * Wangasa * Wangindo * Wangoni * Wangulu * Wangurimi (au Wangoreme) * Wanilamba (au Wanyiramba) * Wanindi * Wanyakyusa * Wanyambo * Wanyamwanga * Wanyamwezi * Wanyanyembe * Wanyaturu (pia wanaitwa Warimi) * Wanyiha * Wapangwa * Wapare (pia wanaitwa Wasu) * Wapimbwe * Wapogolo * Warangi (au Walangi) *
Wengine ni Warufiji * Warungi * Warungu (au Walungu) * Warungwa * Warwa * Wasafwa * Wasagara * Wasandawe * Wasangu * Wasegeju * Washambaa * Washubi * Wasizaki * Wasuba * Wasukuma * Wasumbwa * Waswahili * Watemi (pia wanaitwa Wasonjo) * Watongwe * Watumbuka * Wavidunda * Wavinza * Wawanda * Wawanji * Waware (inaaminika lugha yao imekufa) * Wayao * Wazanaki * Wazaramo * Wazigula * Wazinza * Wazyoba
Mdau
Peter C. Shirima
-------------------------------
Mtani wangu mbona umesahau makabila muhimu sana hapa Tanzania?
Kama vile
Warombo,
Wamarangu,
Wamachame,
Wasanya juu,
Wauru
Mdau Mbwambo j.
Hamna wapare, wabungu, wasunva, etc, mmh!
ReplyDeleteMi Mndamba Bwana
ReplyDeleteKwanza nashangaa sana kuwa umeorodhesha Waha, Wahangaza na Wahaya wakati kutokana na utafiti wa athropolojia ya jamii inafamika kuwa Mha akiendelea anakuwa Mhangaza na kisha Mhangaza akiendelea anakuwa Mhaya. Sasa watakuwaje makabila tofauti?
ReplyDeleteWapanga Ludewa Line
ReplyDelete..duh, hapa ndo tutarudi tena kwenye zama za 'kabila ni nini'?, na 'taifa ni nini' na kadhalika.. Hao ma-ethnolojisti/ethnolojia (hiyohiyo!) pia 'wamepiga chanjo/mkasi' kaumu kubwa sana tena muhimu hapa nchini...inaitwa wamanyema. Japo najua ni 'kabila tata' - kwani huku nchini mwetu ni mkusanyiko wa makabila tofauti meengi..
ReplyDeletebado wanyagatwa
ReplyDeletepumbaf, hapo kabila moja tuu, waswahili.
ReplyDeletePia kabila ya wanyantuzu na wataturu sijaona kwenye hii orodha.
ReplyDeletehamna wanyasa?????
ReplyDeleteAsante sana, umenisaidia kweli, maana nilikua naulizwa idadi ya lugha tulizonazo tz nikawa nakisia tu
ReplyDeletesijakupata kabisaaaaa,,,
ReplyDeletelugha ulotumia siielewi kiswahili cha wapi icho??
wapare (wasu) wapo wee annon juu huoni??
ReplyDeleteKuna kabila linaitwa Wanyisanzu wapo wilaya ya Ibaga mkoa wa Singida
ReplyDeleteHii orodha yake katoa kwenye ndoto zake au vipi maana hakuna kabila linaloitwa wamachinga,na sijui kwa maana hiyo anasema wako mkoa gani na wilaya gani kama lindi kuna makabila mengi machache nayo jua ni wamwera,wayao,wamakonde na ukienda mtwara kuna makabila mengi pia na kubwa sana wamakonde,wamakuwa.mengine nimesahau kwa kifupi machinga ni jina la utani kwa watu wa kusini lakini hakuna kabila rasmi linaloitwa wamachinga.Mdau kajifunze tena kamabila yetu>Na warufiji ndio wakina nani pia hakuna kabila kama ilo pia kama sikosei kuna makabila mengi pale rufiji wakiwepo wandengereko wakina mbonde kwa kupiga vishoka kwenye basi na mikono kutolewa na matawi watani zangu hao maana ni shemeji zangu,na wana usemi wao maarufu ambao ni miprwera katili minyahi..maana yake ana pesa kama majani hapo anamsifia mtu mwenye pesa.
ReplyDeletewakimbu,wataturu,wangindo na mengi tu ina maana sisi wakimbizi?
ReplyDeleteMr. Peter Shirima, I hope your aim is not to find who is pure Tanzanian and who is not!!! I frankly believe your aim is not separate, but educate.
ReplyDeleteThank you
Wapare ni kabila la wenyeji wa Milima ya Upare. Kilugha kabila hilo lina Wagweno na Wathu/Wasu. Hivyo hakuna kabila la Wagweno tofauti la lile la Wapare. Hakuna lugha ya Kipare.
ReplyDeleteHivi wabulushi (waburushi) ni kabila la tanzania au ndo hao hao wasangu?
ReplyDeletekuna pia makabila haya: mwafrika, mtanzania, mbara, mzanzibari, mmunguja, mpemba, mtanganyika.
ReplyDeleteah by the way marehemu nyerere mekataza ukabila tanzania
aaalllaaa hivi kumbe wamachinga,waswahili,warufiji ni makabila!!!!??
ReplyDeletemimi nikikuwaga sina habari siku zote hizoo,ahsente mdau kwa kutufumbua masikio kuona makabila mengi namna hii.
sasa haya ni makabila ya Tanzania au Tanzania bara? hatujaona hata moja la visiwani.
ReplyDeleteWewe AL MUSOMA ni kichwa maji wa mwisho Tangu lini ulisikia sisi WAHANGAZA tunajiita WAHAYA. kwa taarifa yako WAHANGAZA hatuchanganyi Damu na Wahaya hata siku moja. WAHANGAZA tupo POSH kuliko WAHAYA. Write it Down,Take a picture.Punk.
ReplyDeleteWarombo,
ReplyDeleteWamarangu,
Wamachame,
Wasanya juu,
Wauru
HAWA WOTE NI WACHAGGA JAMANI hio ni miji wanayotoka lakini wote ni WACHAGGA
Wanyantunzu mbona hawapo!!!!
ReplyDeleteWahangaza kutoka Ngara...mwiriwe!mbona umawasahau
ReplyDeleteMi nafikiri kuna kitu wanachanganya hawa kuhusu kabila linaloitwa WACHAGGA na kila siku nagombana nao. Hakuna kabila duniani linaitwa WACHAGGA hata siku moja. Ila kuna Wamarangu,Wamachame, Warombo, Wauru, Waold Moshi,Wakibosho,Wakirua vunjo, e.t.c.
ReplyDeleteNa hii inathibitishwa na utofauti wa mila na desturi na hata lugha. Inawezakaje Mchaga wa Marangu asisikilizane lugha na Mchaga wa Machame???!!!
Wakati Msukuma wa Shinyanga anasikilizana lugha na Msukuma wa Mwanza??
Hakuna watu wanaoitwa WACHAGGA duniani.
Ukabila, Ukabila wa nini? Kuwa Watanzania haitoshi tu tena wanozungumza lugha ya Taifa Kiswahili? kuendeleza ukabila yataja kutupata yalotokea Rwanda, Kenya na kwingineko endeleeni tu!
ReplyDeleteMr. shirima hiyo unayomaanisha ni orosha ya makabila ya Tanganyika au Tanzania? kwani Tanzania haiwajumuishi na wapemba na waunguja? mbona makabila yao hayako? sioni wangazija mie na wengineo?? huku si ndo kushajiisha ukabila,huku? ugomvi na vita??
Haya, nasema tu mie!
Na Waungurimi wa Musoma,Wayao huko kusini, Wanyantuzu huko Maswa na Bariadi vile vile Wakurya wanajulikana kama Washashi mbona sijawaona
ReplyDeleteNaomba niongelee kuhusu kabila ambalo nimetoka la WAIRAQW. Sikubaliani kabisa kuwa Wairaqw pia wanaitwa WAMBULU. Hilo Neno mbulu asili yake ni Wakoloni ambao walishindwa pronounciation ya neno IMBORU, ambalo ndilo eneo wanaloishi sasa WAIRAQW. Kwasababu ya kushindwa kwao kulitaja IMBORU badala yake wakafanikiwa kutaja Mbulu. Mimi ukiniuliza kabila lako linaitwajwe nitakujibu Mwiraqw kwa Kiswahili lakini nikiulizwa na babu yangu kabila lako nilinaitwajwe nitamjibu IRQWATU. Hilo neno MBULU halipo kwenye misamiati ya lugha ya kiiraqw. Nikiwa JKT nilishakutana na wadau ambao waliniuliza ni kwa nini tunakasirika tukiitwa WAMBULU. Ukweli ni kwamba hatukasiriki ila ni kwamba hatuelewi ni kwa nini tuitwe WAMBULU wakati sisi tunalo jina la kibila letu tulilorithi toka kwa mababu zetu.
ReplyDeleteHayo yaliotajwa hapo ni makabila ya Tanzania au makabila ya Tanganyika?, manake sioni hata kabila moja kutoka visiwani Unguja na pemba.
ReplyDeleteEeh mbona hajaweka kabila la Wanguu?
ReplyDeleteMheshimiwa Michuzi, naona huyo amesahau vilevile kabira la WASUBI wa Biharamulo, kwani kuna washubi na wasubi!
ReplyDeletesijaona kabila ya Waluli
ReplyDeleteWe AL MUSOMA acha dharau kabisa! Sisi WAHA hatuna haja ya kuwa WAHAYA hata siku moja. Atleast hata ungesema kwamba tuko karibu na WAHANGAZA. MAANA TUNAONGEA LUGHA ALMOST SIMILAR Ila dharau zako hazifai....Eti tukiendelea tunakuwa WAHAYA? Get life!!
ReplyDeleteN mimi proud Muha wa Kazuramimba
kuhusu makabila mfano mkoa wa kagera ni wahaya lugha nikhaya lakini tuna mila na utamaduni unao tutenganisha na kuwa namajina lakini lugha yetu ina bakia palepale mfano mziba ,myaiangilo and so on bado hao watu wanaongea kihaya ila tofauti ni mila zao ndio zinaleta jina kutofautiana kwaiyo makablila mengi ulio yataja hapo yanaongea lugha moja ila mila zao ndio tofauti tunacho taka kujua mzee tuna lugha ngapi tanzania kama vile kiswahili tofauti na kihaya na wewe mjinga unaye sema muhagaza ni bora kuliko muhaya koma tume kukalibisha wewe tuko burundi na rwanda ili usife sasa unajiona bora zaidi yangu kwanza ata possport ya tanzania upaswi kuitumia ka sababu lugha yako niya nchi ya bundi na rwanda kiswahili chenyewe kina kushinda .
ReplyDeletenamuunga mkono aliyetaja makabila yaliyosahaulika. Kaka na wauru tupo bwana.
ReplyDeletemdau kutoka netherlands
Mdau wa 2:27PM ni kweli kuna kabila la Wamachinga liko Mkoa wa Lindi na wanatokea Mchinga kama unatokea Dar unafika Mchinga kabla ya kuingia Lindi mjini na kuna kabila lingine limesahaulika hapa Watumbatu....
ReplyDeleteSijaridhika na hayo makabila kwani mengine sijawahi kuyasikia sasa ninakupa kazi itabidi uandike kabila na mkoa au wilaya husika ili tupate picha kamili. Umefanya kazi nzuri anyway.
ReplyDeleteMimi Mkaguru wa Kilosa Morogoro.
mbona mmesahau WAMAWIA ambao ula watu na wanatoka uko kusini. nafikiri ni watu wa kilwa, mtwara, songea nk. hawa watu pia hutoboa seheme kati ya lips na pua zao na kuweka kopo kama la soda kwenye hilo tundu. hivi ndio kujirembesha kwao.
ReplyDeleteYote kwa yote watu tumejifunza.
ReplyDeleteTanzania kutowa na ukabila haina maana makabila hayapo.
Wachaga wapo ingawa tofauti za lugha zipo lakini mila na desturi zao zinafanana kuanzia Siha hadi Rombo.
Yesu wangu iki nini sasa??
ReplyDeletemdau wa feb 03,3:21 AM unasema kuna kabila linaitwa wamachinga ilo kabila hakuna na kama utanaka kujua muulize mbunge wa mchinga,akujulishe kama kuna hilo kabila na huo mji wa mchinga ni sehemu ya lindi vijijini na huko kuna makabila ya wayaho na wamwera sasa unataka kutaja miji yote ilioko kwenye barabara ya dar lindi ndio useme makabila yao hakuna hicho kitu,ndio unasema kuna warufiji ndio wakina nani??basi kutakuwa na wakibiti,wamnazimmoja,wautete,wandundu,wanangurukuru bado upo?maana yote hiyo ni miji ya njia ya dar lindi,acha ukosefu wa kufikiri kijana.Mchinga ni mji ulioko lindi vijijini na kabila kubwa huko ni wamwera.
ReplyDeleteIt's really interesting...despite all these tribes in Tanzania hatuna upuuzi wa ukabila...we rolling as one.... I dnt mind my tribe, Iam proudly Tanzanian...
ReplyDeleteMdau
New England,US
Sorry mbona mkoa wa Iringa sijaona kabila la wabena, wakinga, wamahanji,wahehe?
ReplyDeleteMbona sioni wamasai koko a.k.a Wataturu, na majirani zao Wanyiramba, wanyaturu
ReplyDeleteMdau Kiwoso, UK
ndugu yangu wahehe wapo apo ktk list,ila hao wabena,wakinga nk walitoka ndani ya wahehe na kujitenga full stop,,angalia historia toka Mkwawa
ReplyDeletedah washashi?hahahahhaaaa
God bless Tanzania we r so lucky
HAKUNA KABILA LA WAMACHINGA HUKO MCHINGA, MCHINGA NI KIJIJI KARIBU NA LINDI, NA KINAKALIWA NA MABALABA, PIA WENGI WAO HAPO NI MACHOTARA WA KIARABU, WAARABU WALISHUKIA HAPO KUFANYA BIASHARA ENZI ZA UKOLONI, PIA WAMAWIYA NI KABILA LA MSUMBIJI WALIKUJA MIKOA YA KUSINI KUKIMBIA VITA NA MRENO WALIKUJA KAM WAKIMBIZI LAKINI ENZI ZA MWALIMU MWAFRIKA HAKUWA ANAMWIITA MKIMBIZI WENGI WAO WALIJICHANGANYA TU NA WENYEWE NA KUISHI MOJA KWA MOJA KAMA WATANZANIA, KUNA WENGINE WALIKUJA KABLA YA HAPO AMBAO WALIKUJA KAMA MANAMBA/MA-NUMBER KUJA KUFANYA KAZI KATIKA MASHAMBA YA MKONGE LINDI, MTWARA, MOROGORO, DAR NA TANGA. NA SI KWELI KUWA WANAKULA WATU HUO NI UZUSHI TU. MIMI NIMEISHI NAO SANA HUKOKUSINI TUKIENDA SHULE PAMOJA NA WENGINE KUOLEANA NA WAPO HADI LEO NA WALA SIJAONA WAKILA WATU ACHA KUPOTOSHA WATU HASA WATOTO HUO NI UZISHI TENA MBAYA SANA. STOP IT PLEASE, THAT IS OFFENSIVE
ReplyDeletekuna mtu kauliza wanyantuzu mbona hawapo,jibu ni kwamba wanyantuzu na wenyewe ni wasukuma sema jamaa kidogo wako faster kama wachaga kwenye hela.wanatoka Shinyanga aili yao ila wote ni wasukuma.
ReplyDeletemakabila yooote yakiendelea ndo wanakuwa WAJITA,
ReplyDeletekutiki masika?
wasengejuu wa Tanga tuko wapi apo?
ReplyDeletewaswahili wapo
anony wa 11:52 pm nimekusoma mugabo!pia tabia ya kuita sisis waha eti warundi inanikera sana,hasa makazini!
ReplyDeleteni mimi muha wa Buha,proudly Kigomanian!
WADAU KUNA KABILA LINAITWA WABARABEIGHI WAPO ARUSHA MNALIJUA HAO NI TOFAUTI NA WAIRAQW AU A.K.A WAMBULU???????????? WAMASAI NISAIDIENI.
ReplyDeleteWADAU KUNA KABILA LINAITWA WABARABEIGHI WAPO ARUSHA MNALIJUA HAO NI TOFAUTI NA WAIRAQW AU A.K.A WAMBULU???????????? WAMASAI NISAIDIENI.
ReplyDelete