katika kuitikia wito wa kuomba wadau walete taswira za mikoani, mdau blandy alitembelea bukoba, mkoani kagera na kutuletea hizi. juu ni sehemu ya ufukweni inavyoonekana kwa juu
nje kidogo ya bukoba kuko hivi...
bukoba ni kijani kila mahali
uwanja wa ndege
city centre





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Hivi ndivyo vitu majirani wetu wanavitolea mate ya uchu. Utawasikia wanasema there is a lot of opportunities. Federation ni kwa ajili ya biashara tu baada ya hapo kila mtu kwake. Nchi pekee inayoqualify kufanya nao federation ni USA, kwani na wao wana ardhi ya kutosha na pia wanaweza toa ajira, uongo watu tuishie zetu holywood.

    ReplyDelete
  2. Wale wa umri kama wangu na zaidi wanaweza kukumbuka "...gari ya mjomba Rweyemamu, ya baba Rweikiza, ya mzee Rugemalila..." zilivyochukuliwa na askari wa Idi Amini "...zikapakiwa ndani ya motokari...". Kuepeka hilo unaweza tafadhali kutufafanulia huu uwanja wa ndege ni wa ndege ya namna gani?

    ReplyDelete
  3. "Aise".Mdau Blandy hapo umecheza,umenikumbusha mbali sana,nimesoma shule ya sekondari maarufu sana ya serikali hapo mjini karibu na posta 1986-1989.Hicho kisiwa kinachoenekana uwanja wa ndege kwenye 'Background'kinaitwa MUSIRA/MUSILA?teeeh teeh WAKOLA MUNO(Asante sana).

    ReplyDelete
  4. Bomba!

    Kwa kweli Bukoba ni kuzuri, nilikuwa huko likizo December 2008 panavutia sana, pametulia, hakuna joto, uoto wa asili, miti mizuri, mabonde, miinuko, kila sehemu ni kijani. Natamani nipate kazi huko nisirudi tena Dar maishani.

    ReplyDelete
  5. hapo njiapanda ya muleba na kyaka umenikumbusha mbali sanaaaaaa

    ReplyDelete
  6. DUh Mie nilijuwa Ukerewe nilitaka kubishana kumezidi zaidi ya ukerewe wamenirudisha sasa hivi niko kijiweni kuna viwanda jamani Bukoba mie nije kupiga mzigo? Town yao wakiiendeleza itazidi kupendeza.

    ReplyDelete
  7. Bro Misupu naomba uweke picha za Arusha enzi za Mwalimu..........
    Chukua japo picha mbili tatu za kuvutia...kwenye website yangu
    http://www.ntz.info/gen/b00988.html

    Ndimi
    Mzungu!

    ReplyDelete
  8. Iwe Michuzi, In fwakt mazima kwa kweli umenikumbusha nyumbani. Next holiday itabidi nikae zaidi mwezi. Maana hapa LA hakupendezi kama BK. Wakora muno Michuzi.

    ReplyDelete
  9. Bro Michuzi, pamoja na huo ukijani kibichi wa mji wa Bukoba, mimi umenikumbusha mbali sana na hilo jina la "mkoa kwa mkoa". Nimekumbuka enzi za redio moja ya Taifa nchini, Radio Tanzania Dar Es Salaam. Enzi hizo niko kijijini babu yangu akiwa na ile radio yake ya 277, alikuwa akiifungulia kuanzia saa moja usiku (kusevu betri). Maana betri alikuwa analetewa na Mama kwa mwezi mara moja toka Dar Es Salaam(wenyewe tulikuwa tunaita mtoni). Katika vipindi ambavyo mimi na babu tulikuwa tukipenda sana kuvisikiliza kimojawapo kilikuwa mkoa kwa mkoa. Kipindi hicho kilikuwa kinatusafirisha toka Mtwara mpaka Mara, kigoma hadi Unguja bila hata kulipa nauli. Nilikuwa najifunza vitu vingi sana kwenye kipindi hicho. Sijui kama mpaka sasa bado kipo au la. Nashauri mleta picha awe walau anatoa dondoo chache za mkoa huo ili kukoleza utamu kwenye hizo picha, zilete maana zaidi.

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  10. Wewe mzungu those are very interesting pictures and good memories too. I would love to see current photos of those kids if they are still living and may be what they know or think of Arusha today.

    ReplyDelete
  11. Jamani, BK ndo hiyo!!! I miss my mother land, last time nilikua hapa 2006.
    Thanks for the memory, waitu bakasinge(asante)

    ReplyDelete
  12. Tukiwa tunamaliza JKT (Ruvu 1972) tulipelekwa Kaboya JKT na baadaye kupelekwa kusaidia kulinda mahali nyeti hapo mjini...oh, Hamgembe na Coffee Tree!

    ReplyDelete
  13. Sehemu za ndanindani zaidi kuna majumba mazuri ya kifahari katikati ya mashamba ya migomba yenye rutuba.
    Ah!! wenyewe walitutangulia kwenda mbele ya mola wetu mtukufu baada ya ugonjwa wa "JULIANA" kutushambulia kwa nguvu sana maeneo hayo. Baadae ugonjwa huo ulikuja kupewa jina la "UKIMWI".
    Sasa majumba hayo yanakaliwa na wajukuu na bibi zao na babu zao.
    I LOVE BUKOBA ESPECIALLY "KATERERO STYLE.

    ReplyDelete
  14. ndogra waitu! mh mpunga kitenesi tonge kama rimau...

    ReplyDelete
  15. Nyie watu wa Bukoba nina swali. Huo uwanja wa ndege ni wa ndege njiwa au...

    ReplyDelete
  16. Ahsante saan kaka michuzi kutukumbusha kwetu mambo yote KAMACHUMU bwana pale IROGERO dah nakumbuka mbali sana.NYEGERA WAİTUUUU

    ReplyDelete
  17. watanzania tujivunie nchi yetu. ninashukuru sana bro michuzi kwa kutuonyesha sehemu kama hizi. wengi wetu hatujaweza kutembelea sehemu nyingi za nchi yetu lakini kwa picha kama hizi inatufanya tukija nyumbani tutake kutembelea sehemu nyingi. jamani sisi watanzania tujue hata sisi tutalii nchi yetu na sio wazungu na watu wengine peke yao. nchi yetu ni nzuri sana.

    ReplyDelete
  18. YAANI MICHU UMENIBANIA COMMENT YANGU JAMANI. ENEWEI MIE NILIKUWA NATOA DUKUDUKU LANGU KWA HAWA WACHAPA VIBOKO. SAWA MICHU HAMNA NOMA WALA NINI

    ReplyDelete
  19. Yaani enzi hizooooooooooooooo nasoma Rumuli miaka ya 1983-1985 na akina..... shule ikahamishiwa Zamzam duh! Kweli Bukoba pazuri pamoja na kwamba enzi hizo kulikuwa na vuguvugu la kukamatwa "walanguzi" magari ya KUGIS.

    kucheza halaiki ya kuzima mwenge wa uhuru viwanja vya Kaitaba hahahahha, mkuu wa chipukizi kijana shupavu alikuwa anasoma Rumuhi na yeyey du! kweli BK bomba. Wanafunzi wa Belele wapi???

    ReplyDelete
  20. HEEEEEEEEEEEEEEEE!
    NINASIKIA HARUFU YA MAGOVI NA K**A CHAFU PUH! WALALANA NDUGU KWA NDUGU HAOOOOOOOOOOOO!

    ReplyDelete
  21. Duuuh,
    Nimefurahi saana to see the pictures. Had been there in september for the first time.I lyk flight, so landing there it was a great expirience.One of those smoooth landing on such a runway.
    I had been there for few days, but i loved the weather.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...