huu ni ukurasa mpya ambapo wadau mnakaribishwa kutuma picha za mandhari ya mikoa mbalimbali mnayoishi ama mnayotembeleaga. mdau rita alikuwa tanga karibu na ndiye anayetufungulia pazia
tawi la exim tanga
kitega uchumi ambalo ndio jumba refu kuliko yote tanga

uhindini




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. kama wataka ona majumba yaliyopambwa na rangi za kuvutia tofauti tofauti, karibu tanga.

    ReplyDelete
  2. Tanga inazidi kupendeza siku hadi siku. Hata hivyo vijumba vya makuti na mabati yaliyochakaa yanaharibu mandhari ya jiji letu.
    Tuendelee kulikuza jiji letu.

    ReplyDelete
  3. kusema ukweli mikoa mingi ni misafi ukilinganisha na jiji la darisalama

    ReplyDelete
  4. amejaribu lkn hajavuka hata hatua kumi hizi picha zimepigwa mtaa mmoja tu.
    ¨
    BY MDANZI

    ReplyDelete
  5. Alaaah umenikumbusha home sana i miss de place manake ukikunja kona nyuma kidogo upo lakassa mambo ya totoz plae utasahau kwenu

    ReplyDelete
  6. PICHA TU, ZINANITIA MIHAMU. NINASIKIA HARUFU YA MAHABA TOKEA KWENYE PICHA MICHUZI!

    ReplyDelete
  7. TANGA TUNA KILA KITU, MUNGU KATUPENDELEA.ASANTE.KARIBUNI JAMANI.

    ReplyDelete
  8. Tanga tanga ..waja leo waondoka leo..

    Bado naikumbuka vema sana..Nakumbuka Majani mapana(FFU) nakumbuka makorora..Nakumbuka ze mfugos maeneo ya kwa michi sababa au Nguvumali kwa mzee Mguto..

    Nakumbuka sana..mambo ya La casa chika...pembeni Meridian..

    Naikumbuka TA ambayo baiskeli kukodi kwa saa ilikuwa shilingi 50..

    Nakumbuka wazee wa kusaga yale majani yanayopitia Horohoro au wazee wa pariki..

    Nakumbuka meeting point..TEXAS kwa Eddy ..wapi prof Jay,Wagosi Mr Ebbo ..Parklane.

    Nakumbuka Raskazone kuvuta upepo wa baharii

    Barabara ya kwanza hadi 21...

    Nakumbuka mambo ya ubani,asumini,udi...lol..

    One day..nitarudi kunywa ANJALI na chpis kwa kaka Yohane kona ya uwanja wa mkwakwani...

    salamu zao Chumbageni bila kuwasahu watoto wa TARIMO mjengoni..Eckernforde

    ReplyDelete
  9. Bro Michuzi,

    Thank you sana kuanzisha ukurasa hiyo ya mkoa mbali mbali. Good Job

    ReplyDelete
  10. NAKUMBUKA WAKATI NIKISHIRIKI MICHEZO YA SHIMIWI NILIPATA HUDUMA NZURI SANA PALE TANGA MABINTI WA TANGA NI WAKARIMU SANA. MBARIKIWE SANA

    ReplyDelete
  11. BAB KUBWA wadau naikumbuka sana tanga MKOA WA WASTAARABU hapo kwenye iyo picha ya kwanza kama unatokea POSTA ukikata mkono wako wa kuume kama unaelekea BANDARINi kuna AMII anauza KAHAWA PALE chini zamani ikijulikana kama PAMCORT jamani WADAU naoma sana kama kuna mtu anaweza nichukulia ile namba ya yule AMII muuza kahawa nimemis sana zile KASHATA zake , pale tulikuwa tunakaa na watu tunapiga story sana namkumbuka sana mwalimu wangu KASSIM EL SIAGI.

    Sasa hapo jamaa kapiga picha kwa juu akiwa ghorofa la BANDARi naona nyumba ya mdosi SAMEER BANDAAL kwa mbaali, nawakumbuka sana watu wangu wa tanga wapiii WALTER FARE mkuu FREDY TAYASAR ebwana eheeee ....

    Mambo ya tanag raha jamani naikumbuka sana R/zone watu wangu woite wa R/zone na Bombo area mkuu RAMA,THOMAS,elias,SEFU TOTO KANKO,BUJI NA EDI MIKE,ISSA WENDO,OMARY MUSSA,KESSY Duh nickson tenga,God Boimanda hahaha dah ebwana imetulia wapi FRANK TEMU wazee masakani ilikuwa kona ya HARBOURS CLUB pale tulikuwa tunapiga sana story tukitoka makazini ebwana nawakumbuka sana popote mlipo mazeeeeee TANGA NI YENYEWE.wapo wengi siwezi kuwataja wote hapa nitamaliza kurasa kuna BOB,BEDO,STANFORD, RIP JAMES MWKIZU kama kawaida BIA tulikuwa tunakunywa HARBOURS wapi pref JAy,Maiko MHINA,omaru mobitel haha wapi RAHIM CELTEL ,KITOJo,NIKO tanga raha asikwambia mtu

    Nakumbuka sana sahare,makorora,chuda mambo ya gesti kule huulizi kwa mzee RAHA LEO,kwaminchi,bara ya kwanza mpaka 21 haha wazee wa ECKNFORDE, wazee wa BROKYLIN wapi papaa FREDY weee chumbageni noma,

    tanga hotel,jet club,Nyinda,panory,mkonge,yatch club,in by the sea,kwa mzee macha raskazone hotel ivi wale watoto wa mzee macha wapo wapi eward na alex macha, bandari chafu kwa sepocho,usagara kwa sisi tuliosoma usagara mazeee noma,mambo ya spendid hotel, duh najuwa nimesahau vijiwe vingi sana mnikumbushe wadau mambo ya silvarado, mambo ya FOOD PALACE duka la magazeti MAZAO hahaha ebwana eheeee,

    tanga kwa baiskeli usipime namkumbuka sana fundi wa baiskeli mmoja yupo mkwakwani aliweka stearing ya gari bike yake jina lake silikumbuyki ila ni mmakonde yule,
    muuza chips enzi hizo julius posta pale hawa kina yohana walikuwa vijana wake wa kazi enzi izo kabla jully hajalewa sifa na kufilisika mazima, mambo ya supu ya pweza kwa wapembda scandnavia, mihogo mkwakwani na juice ya miwa weeeeeee

    majestick duh ebwana natamani kurudi tanga

    Ivi lacasa chika ipo namkumbuka meneja jamaa alikuwa menen ivi alafu kulikuwa na DJ mmoja wa kila siku anapiga nyimbo zile zile DJ RAPH sijui kama bado yupo, mpiga picha maarufu ABASI na yule MAKAME aiseee

    watu wa majani mapana nguvumali kisosora ukanda wa galanosi ebwana eehee wapi IVAN MINJA na mkuu SEBA

    eazee nitaongea sana ila TANGA NAIPENDA sana nitarudi tanga nasikia kuna club mpya kibao kibao. waliokuwa tanga tupasheni jamani tunamis mengi sana salamu sana kwa watoto wa mzeee TARIMO wa ecknforde tanga na wale mafundi mabiti matapeli
    salamu pia kwa kenedy,mkonge na sele mafundi pikipiki maarufu sana tanga salamu pia kwa fundi suphiani wa baiskeli tanga nawasalimu mafundi wote wa magari pale lary auto garage nawakumbuka sana.

    NAIPENDA TANGA

    ReplyDelete
  12. Kwa kuangalia picha kweli kunavutia sana. Ila napenda kufahamu mambo machache kama yamefanyika.

    1. umeme, maji, usafiri, Shule,
    Hospitali na usafiri
    vimeboreshwa vile vile.
    2. Mifereji ya maji machafu
    imerekebishwa? Maana itakuwa
    kila mara maradhi kwa mituamo
    ya maji.
    3. Idadi ya watu itakapoongezeka
    baadae tuna uhakika barabara,
    mifereji ya maji itatosha kutoa
    huduma kwa wananchi?

    Majengo pekee si kama yanaleta maendeleo, tunachotaka ni maendeleo. Ingewezekana ni vema kuwa na huduma muhimu kwa mwanadamu kuliko kuwepo majengo mazuri lakini huduma muhimu hakuna.
    Haya ni maoni yangu tuu wadau, Michuzi usinibanie.

    Mchangiaji.

    ReplyDelete
  13. Ooh hata mimi nimekumbuka sana Tanga. Jamani enzi zetu tunasoma pale Popatlal yaani shule ilikuwa nzuri, watu hata wakipasi kwenda Usagara Secondari School, walikuwa hawaendi wanakuja Popatlal. Enzi hizo Mr Chaudry ndo alikuwa Head Master. Tulikuwa tunamuogopa. Tukiona kigari chake kwa mbali, sio mbio hizo yaani alikuwa kama baba yetu. Nakumbuka mitaa ya Tasma Road, karibu na ofisi za mamlaka ya Mkonge, pembeni shule ya Mkwakwani ooh, yaani hadi machozi yanitoka. Outing zetu enzi hizo ni sinema. Nakumbuka lile jengo la sinema pale karibu na uwanja wa Mkwawani, jina limetoka kidogo. Halafu si mapicnic hayo. Ooh it was wonderful. Kuna mchangiaji mmoja amemtaja Mwalimu Mr. El Siagi. Jamani mwalimu alikuwa bomba sana akiingia darasani, hata ukibanwa na mkojo hutoki maana unaona kama utakosa material zake. Thx mdau kwa kutuletea picha nzuri za Tanga, we real appreciate

    ReplyDelete
  14. kwangu nikozaliwa,,,
    mtoto wa pwani sii mchezo tanga
    siku ntarudi apo japo!

    ReplyDelete
  15. Jamani Tanga! Tanga Tanga hiyo! aah Tanga.

    ReplyDelete
  16. mnakumbuka mnakumbuka1!! what kind of nostaligia!!! rudini basi kama mnakumbuka. Tuliokumbuka kweli we are now here. karibuni. msione soo rudini tu

    ReplyDelete
  17. TANGA NIMEFURAHI SANA, KWANI WADAU WAMENIKUMBUSHA SIKU NYINGI SANA WAKATI NASOMA USAGARA, VIJIWE VYOTE HIVYO NAVIKUMBUKA KUANZIA MIHOGO KWA YOHANA, JUICE YA MIWA, TEXAS ETC. MWAKA JANA NILIKWENDA TANGA, VIJIWE VYOTE VIPO ILA WATU WA KIPINDI KILE WENGI WAO HAWAPO. NIMEFIKA NAONEKANA KAMA MGENI KWANI NI WACHACHE SANA WANAONIFAHAMU. MI NILIKUWA NAISHI KIJIJI CHA MIAKA 21 YA TANU (NYUMBA ZA MBAO), NIMEPITA PALE MACHOZI YAMENITOKA NYUMBA ZIMEKWISHA MATUNZO HAKUNA TENA, ILA NIMEAMBIWA WANATAKA KUBOMOA KUJENGA BUSINESS CENTRE. OK ALL THE BEST, LAKINI TANGA NI NYUMBANI NA KUTABAKI NYUMBANI MILELE, MUNGU AKINIPA MAISHA NITARUDI KUSTAAFU NA KULA PENSHENI PALE.

    ReplyDelete
  18. ndaki umenifurahisha sana eti unakumbuka udi, asumini lazima ulikamatwa na li mama pale tanga. maana hayo mambo uwezi pata kwa wanafunzi wengio wa kwa TARIMO. ila huyo mshikaji ambae hajajitaja jina ila amewataja washikaji wake wa BOMBO jamaa nomaa yaani karibia washikaji wote mimi nawajua ila unaonekana wewe maskani yako ilikua ya BOMBO na ikiwa kama maskani yako ilikua ya bombo mbona hujaitaja maskani el maarufu ya WATOTO WA CENTRAL PIRATES??? watoto wa town texas??? el siagi hivi bado anafundisha au aliisha aacha anafanya movie tuuu. yohana alianza pale majesti alikua anauza mihogo ya kukaanga mambo yakawa safi akaanza kuuza chips pale mkwakwani ndio ilikua sehemu ya watoto wa kwa TARIMO, mliosoma popatlal mnamkumbuka bibi mmoja alikua anauza mihogo ya kuchemsha na kachumbari na chapati na chai? na yule SAID aliokua anauza chips? je MGOGO mnamkumbuka? musa je yule mfanyakazi pale popatlal? sio wote hao bado wapo au ila HELTHO AKA ANJARI sijaona bongo nzima zile soda. TANGA RAHA

    ReplyDelete
  19. Nimetembea sehemu nyingi, lakini Tanga ni mahali special kwangu. Ninakumbuka ukarimu wa watu wa Tanga.

    Mungu akipenda nitaiona Tanga na watu wa Tanga tena.

    Former Usagara Student

    ReplyDelete
  20. Ebwana eheee wewe mdau umesema sikusema maskani yangu nimeelza maskani yangu ilikuwa HARBOURS CORNER pale kama unaelekea harbours club na pia maskani ya CENTRAL naijuwa sana kwa fundi AYOUB MZAIRE fundi wa baasikeli sema watoto wa pale walikuwa mabitozi sana wakina SALUM POJO na mwenzake SHARIFU BOHERO mbona nawakumbuka wengi watoto wa mzee ZAKWANI wapo wengi pale kina bakari mchezaji yule na braza wake ni trafic nasikia siku hizi

    ebwana dahhh

    ReplyDelete
  21. sijawahi kufika tanga lakini nilipokua tanzania nilikua nafahamu watu wengi kutoka tanga. wengi niliokutana nao had nothing bad to say about tanga. wengi niliowafahamu kutoka tanga walikua watu wazuri kwa sura na tabia. hizi picha zimenifanya nipende kutembelea huko.

    ReplyDelete
  22. Tanga raha jamani ukifika huko lazima unasikia harufu ya amani kila kona yaani unajisikia upo home kabisa sio ugenini

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...