Magazeti ya Taifa Tanzania, Taifa Letu na Sema Usikike yamepewa siku saba yajieleze kwa nini yasichukuliwe hatua za kisheria kwa kuandika habari za kukashifiana, uzushi, uchochezi na uongo. Na yametakiwa kuwa yamefanya hivyo ifikapo Februari 19 mwaka huu saa 10 jioni.

Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika, amesema hayo leo alipokuwa akitoa tamko la Serikali kuhusu mwenendo wa vyombo vya habari nchini.
Amesema Serikali imesikitishwa na mwenendo wa magazeti hayo na hairidhiki na mwenendo huo, kwani yanakiuka Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, ambayo alisistiza kuwa itaendelea kutumika hadi itungwe nyingine.
Akifafanua, Mkuchika alitolea mfano wa Taifa Tanzania toleo la Februari 6-12 mwaka huu, lililomshambulia Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi kwa kuandika kuwa harusi yake imezua utata na la Taifa Letu la Februari 9 mwaka huu, lililoandika kuwa Karamagi (Nazir) anadaiwa kudandia wake za vigogo wenzake.

Pia Waziri alizungumzia Sema Usikike toleo la Februari 10 mwaka huu lililoandika kuwa Waziri "Mkuu wa zamani amweka kimada shoga...".

Kutokana na hali hiyo, Waziri aliwataka wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuacha mara moja kutumia vyombo vyao kwa maslahi binafsi yanayoweza kuhatarisha amani na utulivu.

Pia aliwataka wahariri wa habari kuacha kuandika na kushabikia habari za watu binafsi ambazo hazina maslahi kwa Taifa.

Waziri aliwataka wamiliki na wahariri hao kuzingatia kifungu cha 30(1)(2) cha Katiba ya nchi kisemacho: "...kwamba haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma, haviathiriwi na matumizi mabaya ya Uhuru na Haki za Watu Binafsi."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. Mimi ni raia wa kawaida, ila ninavyojua ni kuwa mahakama ndio yenye wadhifa na wajibu wa kutafsiri sheria za nchi yetu. Viongozi wa serikali hawana wadhifa huo wa kutuambia nani kakiuka sheria ipi. Masuala hayo yapelekwe mahakamani. Serikali inapaswa kuonyesha mfano wa kuheshimu sheria za nchi na haki za raia wote.

    ReplyDelete
  2. wakati walipokuwa wanazushiwa wananchi kwenye magazeti mlikuwa mnakaa kimya sasa yamewafikia viongozi mnachukuwa hatuwa .mlikuwa wapi siku zote wakati macelebrity walipokuwa wanazushiwa na kuvunjiwa hadhi zao??????????????????

    wakati alipokuwa anazushiwa BB na family yake,Hoyce,Miriam,Nargiss,Fide,Kusaga na wengine wengi hamkujari sasa ,mnaona wananchi wenu walivokosa raha?kama mnavokosa nyinyi viongozi?

    huo ni mfano mzuri sana.
    tunawashukuru wenye magazeti kuvuka mipaka mpaka kutukana viongozi,mana wasingevuka mipaka wananchi tungekosa uhuru mpaka leo.

    ok viongozi rumba liko kwenu.tuone sasa hizo hatuwa mtakazochukuwa,mana hawa wenye magazeti wananjaaaaaaa,ya haibu hawapati ridhiki midomoni mwao mpaka wakoseshe watu heshima na raha ndo watauza magazeti ili wapeleke vitoweo makwao kwa wake na watoto zao
    cha muhimu apigwe mwandishi wa habari mpaka auwawe ndo itakuwa fundisho kwa wengine wote

    itabidi njemba zenye misuri zipewe pesa kwenda kufuwa wandishi walala hoi wote mpaka washindwe kuweka tonge la ugari midomoni mwao kwa kipigo.
    piga paparazi zoteeee,isipokuwa zile zenye kuandika mambo ya kweli na busara.

    MISS TZ.200?

    ReplyDelete
  3. duh bongo kweli tambararee,lakiini always lisemwalo lipo,sasa kama kweli waziri mkuu ana kimada shoga na ikathibitishwa,mkuchika atafanyaje?tatizo waziri ana vitisho mno,acha magazeti yaandike tupate stori sie....aaghhhhh

    ReplyDelete
  4. Funikeni kombe mwanaharamu apite. Huyo Karamagi si wa kumtetea kuhusu uasherati.

    ReplyDelete
  5. kwani uongo????????
    vitu viko wazi kweupe,watu tunajua mwazo mpaka mwisho..wasitake kutufanya wajinga

    ReplyDelete
  6. Serikali isiingilie habari zinazoandikwa kwa ajili ya burudani zisizo na maana yeyote hata watoto wadogo wanajua hivyo. Mimi ninavyoona hao vigogo au watu wengine wa kawaida wanaoandikwa na kuchafuliwa majina yao wana uwezo wa kuyapeleka mahamakani hayo magazeti na kuomba fidia. Kama mahakama itaona magazeti yamesababisha maovu kwa hao jamaa, mahakama itaamua ni fidia gani walipwe. Kama fidia hizo zitazidi uwezo wa magazeti hayo kuendeleza biashara zao wamiliki watayafunga magazeti yao wenyewe.

    ReplyDelete
  7. Mkapa tells leaders to respect oaths
    By Reporter, Daily News
    Mon, Apr 18, 2005



    PRESIDENT Benjamin Mkapa yesterday urged religious and public leaders to stand by their oaths of allegiance by affirmative action.

    Mr Mkapa said this in Dar es Salaam yesterday when addressing the congregation of the Eastern and Coast Diocese of the Evangelical Lutheran Church of Tanzania (ELCT) at a special service to consecrate the new diocesan bishop, Bishop Alex Gehaz Malasusa, held at the Azania Front Cathedral grounds.

    Bishop Malasusa (50) was elected in December last by the executive committee of the diocese at a special meeting held in Bagamoyo.

    His election follows the removal from office of the former bishop, Jerry Mngwamba, in 2002, on allegation of misconduct. The diocese has since then been under the transition leadership of Bishop Dr Hans Mwakabana, who held the office for two years and nine months.

    President Mkapa expressed concern over some individuals entrusted with the responsibility of running various government and political offices who act contrary to their oaths of allegiance, pointing out that some of them have been undermining both public and national interests.

    “As president, I swear-in many top government leaders, who take oaths using their respective holy books whose objectives are of profound significance. But I sometimes tend to question myself how many of those who take oaths stand by them,” the president said.

    Mr Mkapa told the congregation that the problem of unfaithful and uncommitted leaders was not in the government alone, but also at many levels of leadership in society, including religious institutions, NGOs, political parties and even at family level.

    He also implored religious institutions to speak for the poor and voiceless by defending their rights from family, national and international levels.

    “We as the government, you as religious leaders and human rights activists… we should stand firm and collaborate in defending justice for the poor, who are the majority, as we execute our daily leadership roles,” said the president, adding:

    “We must not forget that corruption is the root cause of all injustice in our society. Christians also constitute part of the community, if mobilised against the evil and say that no Christian would solicit, give or receive bribe, we will achieve success in the war against corruption,” said the president amid cheers from the congregation.

    Mr Mkapa appealed for unity, solidarity, peace, love and harmony among Tanzanians during the countdown to the general elections slated for October this year.

    Earlier, in his special message, Bishop Malasusa said he was taking the leadership of the church at a time when the community was facing serious challenges that needed both spiritual and moral guidance.

    He promised the church’s continued cooperation with the government in the war against HIV/AIDS, poverty and ignorance.

    Bishop Malasusa has also urged for solidarity among Christians as well as people from other faiths in order to enhance peace in the country.

    “There is need for Christians to pray for peace as the country prepares itself for the general elections on October, this year. The special consecration service was also attended by all the 20 Bishops of ELCT in Tanzania, partner Lutheran churches from Canada, Finland, Sweden, Germany and the Geneva-based World Lutheran Federation.

    Services were conducted by the vice-president of the United Evangelical Mission (UEM) responsible for Africa region and the Bishop of the Evangelical Lutheran church of Namibia, Bishop Dr Zefania Kameeta. UEM joins the Lutherans from Africa, Europe and Asia.

    ReplyDelete
  8. Mapaparazzi wa bongo nawasifu ila kitu kimoja ni kwamba wanatoa kashfa kama hiyo bila picha.

    Huwa tunasikia kuwa Waheshimiwa wanapoanza bunge Dodoma makahaba wote wa Dar huhamia huko.

    Sasa cha kushangaza mbona picha za hao wabunge wakitanua na makahaba hatuzioni???!!

    ReplyDelete
  9. kama kuna mtu ambayae alichafuliw avibaya,na alipaswa kulalamika basi ni sinta,

    maana alianikwa akaniiikika,lakini wapi!!! hakuna hata siku 1 waziri alisimama na kukemea.

    leo hii kwkuwa akaramagia ameandikwa basi mnaongeaaaaaaa,
    baraza la habari liko wapi?
    maana mengi baada ya kuchafuliw alipekeleka malalamiko barza la habari wakaa kimya.

    megi amejibu mashambulizi,karamagi amekimbilia kwa waziri a habari.karamagi huwezi mziki wa engi,we ni bwanamdogo sana.

    kutoa makontena pale bandarini usijifanya una hela,mengi kila sekunde inayopita duniani anaingiza hela.
    usipokunyw amaji ya kilimanjaro ya mengi basi utaangalia tv,usipoangalia tv utasiliza redio one,kama si redio one utasikiliza ea radio,utangaalia itv,ama capital tv,utakunywa soda za mengi(bonite)utanunua madini ya mengi(maana ana migodi mereeani)utanunua magaeti zaidi ya 5 yatokayokial siku ya mengi.
    huyu mzee humuwezi karamagi,we hadi wale wazunguw wa tics wakulipe mwenzako anaingiza hela kial sekunde

    anawafanyakazi wa makampuni yake zaidi ya 1000 wanaishi wantanua mjini,wanajenga,wanasomesha kw asababu ya mengi.

    mengi wakati hyo bilionea,we karamagi unasoma.
    sara50@yahoo.com

    ReplyDelete
  10. MTAJIJUA WENYEWE NA MISKENDO YENU YA KILA SIKU .MNAFANYA WATANZANIA MAHANITHI KWA KUENDESHA NCHI KAMA BIASHARA ZA NYUMBA YENU.MTAJIJUA WENYEWE NA MABALAA YENU.
    na michuzi na wewe utajijua pia kama unataka kupost hii au hutaki endelea kutetea maovu.

    ReplyDelete
  11. Dalili za kutaka kuzuia magazeti kutochapisha habari za serikali na za wakuu. Mbona Mkuchika hakuja juu wakati Mengi alipozushiwa na magazeti ikiwa ni pamoja na Daily News? Haya madaraka ya waziri kuchukulia hatua magazeti tunaomba yaondolewe, maana mara zote alipokuja juu ni pale serikali yake ilipoguswa. Huwezi kuwa mtuhumu na jaji kwa pamoja. Mtuhumiwa lazima atashindwa.

    ReplyDelete
  12. karamagi mwambie mkuchika akae chini, anapata aibu sababu yako.

    ReplyDelete
  13. huyo mengi labda ana pesa kwa kiwango cha tanzania;

    kama anazo basi tungemuona kwenye list za kimataifa za wenye pesa;

    kampuni hizo zaweza kuwa makaratasi matupu;

    hawa matajiri wa tanzania huwa haijulikani kiasi gani wanaco;
    kuwa na pesa siyo crime ; na kukitangaza ni vizuri kwa taifa

    ReplyDelete
  14. mkuchika baada ya kulifungia mwanahalisi anataka kusawazisha mambo kuyafungia magazeti mengine ili isionekane kama ilikua ni mwanahalisi tu.

    ao viongozi lazima waandikwe wakiwa wanazini hata hapa uk viongozi wanaandikwa sana. nilikua nasoma gazeti la bongo online nikaona eti takuru wamemkamata mtu kwa rushwa ya ngono, hawa viongozi wa juu ndio wanaongoza kwa rushwa ya ngono. wanapenda mademu/watoto wa wenzao bali wewe ukiingia kwenye anga zao wanakumaliza.

    mimi simpendi mkuchika, anaiendesha wizara kwa kutumia nguvu za kijeshi na sio elimu, hajafanya mabadiliko yoyote.

    wewe mkuu wa wilaya naomba umpe ushauri kidogo mkuchika afanye mabadiliko labda atakusikiliza.

    pia na wewe uwache mambo yako ya u-mkuchika(namaanisha kubana comment zetu, samani sana kwa kukuita mkuchika nimeshindwa kujizuia).
    naomba usibane habari hii

    endeleza libeneke
    mdau uk

    ReplyDelete
  15. wewe karamagi umemuandika mimi(mengi) kwa ajili nanaandika habari zako za ticts, sasa hivi nimejibu mapigo unamwambia rafiki yako mkuchika afungie magazeti haya bwana

    ReplyDelete
  16. mbona mengi alipeleka malalamiko yake baraza la habari wala hakumpelekea mkuchika?

    mbona mkuchika ulikaa kimya, inamaanisha ulikua unafuraia mengi anavyoaziriwa sasa yamekuta karamagi unaanza zako.

    mkuki mtamu kwa nguruwe kwa binadamu mchungu

    ReplyDelete
  17. Date::2/12/2009
    Spika Sitta akiri kupitiwa kuruhusu magazeti machafu bungeni
    Na Habel Chidawali, Dodoma

    SPIKA wa Bunge Samuel Sitta jana aliomba radhi kwa kuachia nakala za magazeti yanayoonekana kuwa ya habari za udaku kusambazwa ndani ya kikao cha Bunge la Jamhuri, akisema kuwa "alipitiwa".


    Juzi, kabla ya kufungwa kwa Mkutano wa 14 wa Bunge, waziri mmoja 'kijana' anasemekana kununua nakala zote za gazeti hilo linaloandikwa kwa lugha ya Kiswahili na ambalo linatoka kwa wikina kuwapa wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge kugawa kwa kila mbunge.


    Habari zilizoandikwa kwenye gazeti hilo zinaonekana kuwa ni za kushabikia tuhuma kuwa mfanyabiashara mmoja amefunga ndoa na uandishi wa habari hizo hauonekani kuheshimu maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.


    "Nilipitiwa na kushtukia magazeti yamegawiwa kwa wabunge ndani ya ukumbi," alisema Spika Sitta akizungumza kitendo cha magazeti hayo kusambazwa na wafanyakazi wa Bunge wakati kikao kikiendelea.


    Gazeti hilo jipya linaitwa "Sauti ya Umma" na tarehe zilizochapishwa juu ya kurasa zake zinaonyesha kuwa lilitakiwa kuwa sokoni kuanzia Februari 12, lakini lilitua Dodoma juzi jioni. Kuna habari zinasema kuwa nakala za gazeti hilo zilisafirishwa kwa ndege kuwahi Bunge.


    "Baada ya kusoma habari hizo, niligundua kuwa habari zilizoandikwa zilikuwa ni mbaya," alisema Sitta. "Nilichukia sana baada ya kuyasoma na kugundua kuwa yalikuwa na habari hizo. Ni kitu kibaya sana.


    "Nilipitiwa... hiyo ni hali ya kawaida ya kibinadamu. Mambo kama hayo hutokea... naomba hilo liishie hapo."


    Katika siku za karibuni kumezuka magazeti mpya na mengine yakiwa yamefufuliwa ambayo yamekuwa yakiandikwa habari za mwandani wa watu maarufu, hasa wafanyabiashara na wanasiasa.


    Habari nyingi kati ya hizo zimekuwa ni kuhusu maisha yao ya ndoa, ufuska na uchafu wa shughuli zao za kisiasa na kibiashara.


    Sitta pia alisema kuwa kumekuwa na baadhi ya wabunge wanaolalamika kuwa analipeleka puta bunge na kusema kuwa maneno yao yanatokana kutojua anachotaka kifanyike na kwamba yeye ni mtu wa kanuni na anaamini kuwa ataendelea kuwa hivyo siku zote.


    Spika huyo, ambaye aliwahi kusema kuwa ataongoza kwa kasi na viwango, bado alikuwa anazungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Bunge, siku moja baada ya chombo hicho cha kutunga sheria kuahirisha mkutano wake 14 juzi.


    Alitolea mfano kuwa nyumba za serikali zilizouzwa kwa bei ya kutupwa ambazo ziliwekea azimio na bunge ili zirejeshwe mara moja na kwamba nyumba hizo zimeanza kurejeshwa na serikali ilitoa ufafanuzi wa kina bungeni tofauti na siku za nyuma.


    Kurejeshwa kwa nyumba hizo kulitokana na hoja binafsi iliyowasilishwa bungeni na mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro alisema kuwa nyumba za serikali ziliuzwa bila ya kufuata utaratibu maalumu huku maeneo mengine yakiwa ni nyeti kabisa ambayo hayakufaa kupewa watu wengine zaidi ya serikali.


    "Zamani ilikuwa ni vigumu kwa serikali kujieleza mbele ya bunge kama ilivyo sasa... sehemu kubwa ilikuwa ni ubabaishaji, lakini kwa sasa ni kujieleza kwa upana na ikitokea hakuna uhakika katika jambo fulani ni lazima tuseme kuwa bunge halijaridhika," alisema Sitta.


    Alisema kuwa majibu ya serikali yanahitaji urasimu kidogo tofauti na ilivyo kwa bunge kwani serikali ikitaka kwenda kwa spidi sana inakutana na vikwazo vya kisheria.


    Kuhusu yeye kuonekana kuwabana wabunge katika ukumbi wa bunge, Sitta alisema kuwa yeye hambani mtu yeyote kutokana na kufuata kanuni.

    je huyo waziri kijana ni nani
    na mfanyabiashara ni nani

    ReplyDelete
  18. Mambo ya kijinga haya. Kama mtu ameandikwa na ameonewa aende mahakamani. Huu ni ujinga tu.

    ReplyDelete
  19. Karamagi wala simtetei dhamira yake ndio inamsuta ndio maana anahangaika mshahara wa dhambi ni mauti ndio maana kila kitu chake kinmtelezea sasa kumpora mtu mke na kuvunja familia ni dhambi kubwa kwa Mungu waliokosewa wasimame tuone kama watafunga magazeti waacheni waandike uozo ili tuwe na viongozi bora, sijui kwanini hawaoni mtu asiye anayeshindwa kujitawala ataongozaje wananchi?

    ReplyDelete
  20. HIZO HABARI ZOTE ZINAZOANDIKWA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE ZINA UKWELI.ILA HUYO WAZIRI NA SERIKALI WANATAKA TUWAONE VIONGOZI KAMA MALAIKA AU MIUNGU HIVYO HAWANA TATIZO LOLOTE WAKATI WAO NI BINADAMU NA WENGI WANA VIMADA TUNAWAJUA ILA KWA SABABU WANATAKA WAONE KUWA WAO NI WASAFI NDIO MAANA WANAJARIBU KUZUIA HABARI ILI WANANCHI WASIZIPATE...AIBU.JE NI NANI ASIYEJUA KUWA WAZIRI MKUU ALIYEPITA ALIKUWA NA VIMADA TENA SI MMOJA? JE NI NANI ASIYEJUA KUWA MAHITA ALIZAA NA HOUSEGIRL WAKE.OFFCOURSE WANANCHI WASINGEJUA BILA YA MAGAZETI...HIVYO KUTISHIA KUFUNGIA MAGAZETI NI KUUA UHURU WA WANANCHI KUPOKEA NA KUTOA HABARI NA NI SAWA NA KURUDISHWA KWENYE UDIKTETA WA KUNYIMWA DEMOKRASIA.NIMESHANGAA KUMUONA WAZIRI ANAUMA MENO YAKE BILA SABABU....AIBU!!!!

    ReplyDelete
  21. Richmond: Msabaha, Karamagi in danger

    2009-02-12 10:23:52
    By Lusekelo Philemon, Dodoma


    Two former senior cabinet ministers who resigned after being implicated in the controversial Richmond Development LLC power generation deal are among high-profile figures likely to be dragged to court over the scandal, Prime Minister Mizengo Pinda said here yesterday.

    He made the revelation in the National Assembly when presenting a report on the implementation of various recommendations contained in the final report of a parliamentary probe committee into the Richmond saga.

    ``The government, through its organs, is in the final stages of investigating the matter,`` he said, naming the ex-ministers as Nazir Karamagi and Dr Ibrahim Msabaha.

    The PM explained that, although both Karamagi and Msabaha had long resigned in connection with the scam, national security organs were putting final touches to investigations into the saga.

    He said the government deemed it necessary for its relevant agencies to investigate the matter thoroughly in order to establish whether the two ex-ministers had engaged in any corrupt practices.

    If elements of corruption are discovered in the course of the investigations, the two former ministers would face legal charges, Pinda stated.

    At the time of their resignations, Karamagi was Energy and Minerals minister while Dr Msabaha held the East African Cooperation portfolio.

    The power generation contract between the US-registered Richmond Development Company LLC and the state-owned Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) was signed in June 2006 when Dr Msabaha was Energy and Minerals minister.

    He was later replaced by Karamagi in a mini-cabinet reshuffle made by President Jakaya Kikwete.

    It was the former who then oversaw the controversial transition that saw Dowans Holdings S.A take over from Richmond Development LLC in December 2006.

    The PM said the relevant disciplinary organs within the government had already worked on the explanation given by the public officials concerned.

    Among these were nine officials from the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB), who were part of the government team that negotiated the Richmond contract.

    PCCB Director General Edward Hosea was one of the officials taken to task, according to recommendations by the parliamentary select committee endorsed by the House in February last year.

    Others included Attorney General Johnson Mwanyika, former Finance and Economic Affairs ministry permanent secretary Gray Mgonja, now facing charges of abuse of office, and Energy and Minerals ministry PS Arthur Mwakapugi.

    However, Pinda noted that all the officials were given the opportunity to present their defence before any further action was taken against them ``in accordance with the principles of natural justice``.

    ``All of them have already tendered their defence and we are waiting for the relevant organs to advise us (the government) on the proper disciplinary measures to take against them,`` he said.

    On the committee`s other recommendations, the PM said a special reference library had been set up in the National Assembly Hall where copies of all important contracts which the government was party to would henceforth be kept for the benefit of legislators.

    Turning to the recommendation of involving parliamentary committees in the preliminary stages of preparing such contracts, he said: ``The government is studying the experience of parliaments in other Commonwealth countries to see if that`s practical.``

    Pinda further told the House that the government had terminated its contract with Dowans Holdings effective from August 1 last year, as recommended by the House team.

    ``The government has also terminated its contract with IPTL and is currently reviewing the deal between Tanesco and Songas,`` he added.

    He also explained that the government was planning to table a bill in the next parliamentary session to amend the law on public procurement, with a view to giving the Public Procurement Regulatory Authority more autonomy.

    Presenting the position of parliamentary energy and minerals Committee, legislator Abdul Jabir Marombwa, called on the government to swiftly but exhaustively work on the remaining recommendations.

    He cited a recommendation that the government probe into the extra payment of USD4.865 million made to Dowans Holdings A.S.

    ``The committee is not satisfied with the response given by the government on the matter,`` said the MP, who is a member of the committee.

    He wondered why the government was reluctant to involve parliamentary committees in the early stages of contract preparation.

    SOURCE: Guardian

    ReplyDelete
  22. Jamani,
    Huenda mimi niko tofauti kidogo. Lakini haya magazeti yaliyotajwa yalikuwa yamezidi. Kwa sababu kila kukicha yalikuwa yanaandika watu na wala sio sissues za maana. Lakini bongo mahakama hazifanyi kazi ya vizuri na pia hakuna mtu wa kuyashitaki haya magazeti. Mimi nadhani haya magazeti yalizidi. Usilinganishe lessen ya taifa letu na Kiu. Majarida kama Kiu, Ijumaa, Sani na mengineyo ni haki yao kuandika udaku, sio kama Taifa letu. Kwa hiyo ninachoona hapa ni kuwa haya magazeti yalikuwa yanaandika udaku badala ya kazi ya kuandika issues katika jamii

    ReplyDelete
  23. KAWANI KABAKA? HUU NI UZUSHI, HATA KAMA INGEKUWA KWELI, KAPEWA NAYE KALA, MBONA MSITUHUMU HAO WANAWAKE?

    ReplyDelete
  24. NA WEWE MKUCHIKA SUBIRI YAKO YANAKUJA MAANA NI MENGI PIA,NIMEFURAHI SANA KUSOMA HAPO JUU ANONY ALIYESEMA WAKATI WANANCHI WAKAWAIDA WANAANDIKWA MBONA HUWA HAMSEMI WANAANGILIA MAISHA YA WATU? ILIANZWA KUANDIKWA HIVI HIVI KUHUSU MAFISADI NA NDO MAANA LEO HIII WOTE WANAVUMBULIWA OFCOURSE WEWE UKIWA KIONGOZI WA NCHI SIDHANI KAMA UNA MAISHA PRIVATE ANYMORE MAANA UNASHIKA UCHUMI WA NCHI YETU UKIWA NA VIMADA MARA MKE WA MKUU WA WILAYA TUNAJUA UNATUMIA PESA ZET KUNYANYASA WASIOKUWA NAYO SASA TUKIKUHOJI AU TUKIKUWEKA WAZI TUMEINGILIA MAMBO YAKO YA NDANI KIVIPI?VIONGOZI WA NCHI YETU MMEZIDI BWANA LAZIMA MTINGISHWE KIZAZI KILE KILIPITA LAZIMA MKUBALI TUMECHOKA KUNYANYASWA TUNAWASHUKURU WATOTO WETU KWA KUWEZA KUYAJUA HAYA NA KUYAVALIA NJUGA WAKATI BADO TU HAI.......HAPO NDIPO NAPOIPENDA MAREKANI UJINGA UJINGA HUU WA VIMADA SIJUI KUBAKA UNADHALILISHWA WAZI WAZI NA MPAKA UTUBU MBELE YA VYOMBO VYA HABARI NA WANANCHI WARIDHIKE ACHILIA MBALI KAZI HAPO USHAFUKUZWA AU UMEJIONDOA MWENYEWE.

    ReplyDelete
  25. We anony wa 5:35 kwa taarifa yako hakuna hata mtu mmoja anayeandikwa katika gazeti anaweza kwenda mahakamani kwakuwa anajua kabisa kilichoandikwa ni sahihi, mi nafikiri huyu mkuchika hakupaswa kuviwekea mkwara vyombo vya habari bali KAMA KUNA ANAYEANDIKWA AKADHANI AMEKASHIFIWA AENDE MAHAKAMANI TUONE TAKAVYOUMBUKA, MAANA WAANDISHI HUWA HAWAANDIKI BILA USHAHIDI NA SOMETIMES HUTOA HABARI BILA PICHA ILI KUMSTIRI MHUSIKA NA SI KWAMBA HAWANA HIZO PICHA. Viongozi wa Tanzania wanatumia madaraka yao kuishi watakavyo si wanavyostahili. HATA UK KUNA The Sun, hili ni gazeti la udaku na linaandika habari za wakubwa daily, sembuse Karamagi!

    ReplyDelete
  26. MIMI MWENYEWE NIMEZUSHIWA MAMBO MENGI HUMU LAKINI MICHUZI HAJAWAHI KUWACHUKULIA HATUA YOYOTE. WENGINE WAMESEMA ETI MIMI SINA AKILI NYINGI DARASANI, SIKUMALIZA MUZUMBE UNIVERSITY YA MUROGORO, WENGINE WAMESEMA MIMI SIYO MTOTO WA NALITOLELA WENGINE WAMEDILIKI KUNIITA MBUMBUMBU. HAYA SASA MBONA MICHUZI AMEONA NI HAKI YAO KUNIKASHIFU NA NI HAKI YANGU KUENDELEA KUELIMISHA JAMII HUMU HUMU BULOGUNI! BASI MHESHIMIWA WAZIRI AWAACHIE KINA SUMAYE KARAMAGI NA MENGI WAJITETEE HUMO HUMO MAGAZETINI KWANI MENGI NA YEYE SIANA GAZETI BASI AWATUKANE KWENYE GAZETI LAKE. LAZIMA KUWEPO NA FREEDOM OF SPEECH KAMA HUKO MAREKANI NA ULAYA. NI MIMI BRIGHT MAN NIMEHAMIA UPANGA SIKU HIZI SIKO TENA TANDIKA.

    ReplyDelete
  27. HABARI KAMA HIZI NA ZA CCM-ZIARANI HUWA MICHUZI HUNA AIBU,NI KINARA WA KUZIWAISHA.lAKINI ZA MAFISADI MPAKA TWENDE BLOGS ZINAZOMILIKIWA NA WATU AMBAO SIO WANAFIKI!!hata usipo post== message delivered.

    ReplyDelete
  28. Nafikiri viongozi wasiingilie kabisa vyombo vya habari, wakisikia wameanikwa huko, mbona watu wengine wameandikwa na magazeti, serikali haikuchukua hatua yoyote imefurahia tu, sasa inakuja kwao wanaanza kuleta ugumu wa kufungia gazeti. Gazeti halifungwi na inatakiwa kama ametenda maovu yake bora anyamaze maana sasa siri ndio zitatoka nyingi tu.
    Wananchi tunatakiwa kujua viongozi wetu na tabia zao,sisi sote ni binadamu, uwe kiongozi uwe raia wa kawaida wote ni sawa.

    ReplyDelete
  29. wewe jamaa wa 5:35
    mambo kama hayo ya ngono mara nyingi yanaambatana na utumiaji mbaya wa madaraka hapa UK na nchi za ulaya ni issue kubwa sana, kama unahari ya kiongozi na ushahidi wa picha na kiongozi wa ngazi ya juu unatengeneza £200,000 - £500,000 bila matatizo yoyote yale na hamna mtu atakayekufanya chochote. "ili nchi iendelee lazima vyombo vya habari viweze kuandika habari zozote zile na kama muhusika anasema za uongo aende mahakamani kudai fidia".
    rais wa benki ya dunia alijiuzulu kwa kashfa ya ngono, maziri wa mambo ya ndani uk (david blanket nae wanawake walimponza). hayo mambo ya wanawake yana athiri sana utendaji wa kazi wa viongozi

    ReplyDelete
  30. Hii Ndio issue ya kwanza ambayo nimeona waziri amekemea bila ya kusubiri JK aseme. Mawaziri wa JK issue nyeti kama za ATCL, TRL, Mafuta,TRA, THA, Uchumi nk hawachukui hatua mpaka JK atembelee wizara. Hizi issue zisizo na kichwa wala miguu ndio wanazishikia bango??! Kweli tuna Kazi. Kama wanasema habari ni za uongo na uzushi si waache tu.. magazeti yatabwata yatachoka. Lakini nadhani wanajihami zaidi ili wasizi kuumbuliwa !!

    ReplyDelete
  31. Hata mimi nimewahi kuandikwa vibaya na gazeti la UHURU na Alasiri. Waandishi hawakupoteza hata muda kupata upande wangu wa habari unasemaje. Waliokoteza vineno vya mitaani wakaongezea na vya kutunga wakaweka gazetini. Wangekuwa makini wakaniuliza ningewaonyesha vielelezo kuonyesha ukweli uko wapi. Serikali ilikuwa wapi kuingilia kati?
    Wamelipika sasa walinywe kudadadeki.

    ReplyDelete
  32. Uhuru wa vyombo vya habari sio kusema eti Mkuu wa wilaya ya Tegeta ameoa mke wa pili je kama kabila au dini yake inaruhusu wewe kinakuwasha nini mwandishi usie na hila weye wacha mfunguiwe kabisa

    halafu waandishi njaa jamani waliweka kalamu mdomoni na plasta wakasema eti hawaandika habari za mkuchika sasa hpo wamefanya nini?

    ReplyDelete
  33. I worry about any government minister having to shut down any newspaper for any reason... kama huyu waziri ana hiyo power, inabidi anyang'anywe.
    Kidumu!

    Mdau, Boston, US

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...