huyu ndiye shabani dihile, kipa nambari moja wa taifa stars, ambaye ameweza kuchukua nafasi kutokana na ustadi wake langoni, pamoja na kuwa na umri wa miaka 23 tu, akiwa anachezea timu ya JKT Ruvu inayoshiriki ligi kuu. leo maximo anatarajiwa kumtaja katika kikosi cha taifa stars anachokitangaza tayari kwa safari ya ivory coast kwenye michuano ya wachezaji wa afrika wanaochezea nyumbani ama CHAN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Tatizo la wachezaji wetu washirikina mno, si ajabu makipa wenzake sasa hivi wanamuwangia. il tumshukuru pinda kuwapiga stop waganga wa jadi

    ReplyDelete
  2. Tanzania One aliyepo ni Juma Kaseja Juma tu wengine ni photocopy. Maximo anambania tu. Tutafungwa Ivory Coast we acha tu.

    ReplyDelete
  3. washirikina utawajuwa tu na mawazo yao. Huyu Shaban udogoni mwetu nilikuwa namuweka Bench sema alikuwa mkali nilimzidi uzuri mungu kamjalia yeye ukipa aliona ndio nzuri kwake mie sikuutilia maanani, Namuombea kila zuri aendeleze Fani yake. Jamaa alikuwa anadaka vizuri tu bahati mbaya au nzuri wengine tulikuwa na wazazi wanaona mpira sio elimu wala kitu cha kufanya kizuri sasa hivi wanaanza duh kumbe chech anakula pesa kazaa tulibanwa na masomo. Shaban endelea utafika mbele inshallah.

    ReplyDelete
  4. Huyu Shabani Dihile na makipa wengine wote walioko Taifa Stars, hakuna mwenye kiwango bora anayestahili kuchezea kikosi hicho, ndio maana hata kwenye michuano ya Challenge tuliboronga na kutolewa kutokana na ubovu wa makipa, nashangaa kocha Marcio Maximo hakubaini hilo mapema. Hakika kusema kweli mpaka sasa ni makipa wawili tu wanaostahili kuidakia Taifa Stars na ikafanya vizuri, Juma Kaseja na Ivo Mapunda. Wengine wote wababaishaji!

    ReplyDelete
  5. Asante Balozi Michuzi kwa kuanza kututundikia wasifu wa wachezaji wa Taifa watakao kwenda Ivory Coast.

    Watanzania tuwape sapoti hawa wachezaji watakao tuwakilisha, tutashinda pamoja na tutaanguka pamoja, timu ni wachezaji wa Taifa, kocha na sisi washabiki, hivyo tuwe wamoja ktk hili.

    Kuhusu Kaseja, Kaseja sio professional, 'ataharibu hali ya hewa kambini' si tunakumbuka kuwa yeye hana marafiki au washikaji au mashemeji.

    mchezaji wa taifa inatakiwa awe proffessional ndani ya kambi na nje ya kambi.

    tatu, kaseja aendelee kujifunza toka kwa kocha Yanga na kocha wa sasa wa taifa Maximo, ajirekebishe na aendelee kujifua zaidi, labda ataweza kuitwa Taifa baada ya CHAN Ivory Coast.
    Mdau
    Abidjan
    Cote de Ivore

    ReplyDelete
  6. Makocha wa nje sasa....kibao!

    ReplyDelete
  7. Tusidanganywe na Maximo, hatuna kipa hapa.

    ReplyDelete
  8. TANZANIA ONE NI MWAMEJA TU WALA HATATOKEA MWINGINE ZAIDI YAKE. MAKIPA WALIKUWA AKINA FATHER (IDD PAZI) NA MAHADHI TU HAWATATOKEA WENGINE NG'OOOO

    ReplyDelete
  9. Sio kosa la Dihile kwamba taifa halina makipa wa kututoa mashabiki ugonjwa wa moyo. Dihile, Munishi na Ramadhan wanaenda kutuwakilisha na tunaamini watajituma kwa kadri ya uwezo wao kuliletea taifa sifa.
    Tuwakumbusheni tu lakini kwamba nyote bado mna safari ndefu kufikia viwango walivyofikia watu kama Mohamed Mwameja na Juma Pondamali enzi zao ambao walikuwa wakisimama hatuna wasiwasi golini. Panapo mazoezi, mazoezi binafsi, bidii, nidhamu na mafunzo mna uwezo kabisa wa kuwafikia si hao tu bali hata kina Van de Saar na Iker Casillas.

    ReplyDelete
  10. Huyo Kaseja kama angekuwa kipa mzuri si angekuwa anacheza ulaya. Hata Yanga amefungwa goli mengi kuliko mzungu. Achenu hizo zenu za kuleta. Mdau Abidjani umeongea ukweli.
    Huyo kaseja siyo kwamba hajawahi kuitwa timu ya taifa, amecheza sana lakini hakuna lolote alilokuwa anafanya ni kufungwa tu.
    Kwa taarifa yenu hata Erick Cantona pamoja ya kwamba Man Utd wanamchukulia kama ni mmoja wa wachezaji bora kabisa waliowahi kuichezea hiyo timu lakini hajawahi kuitwa timu yake ya taifa ua ufaransa kwa ajiri ya uchafuzi wa hali ya hela. Mwacheni Maximo afanye kazi yake tukifungwa tumefungwa lakini ameonyesha kuwa ni kocha mzuri asiyojali majina wala umri.

    ReplyDelete
  11. Real Tanzania namba wani:
    Omar Mahadhi Bin Jabir
    Athumani Mambosasa
    Juma Pondamali Mensah
    Madata Lubigisa
    Mohamed Mwameja
    Idi Pazi
    Isega Isindani
    Hassan Mlapakolo
    Elias Michael
    Muhidin Fadhili

    ReplyDelete
  12. Wabongo wana mambo ya ajabu kabisa. Wakiwekwa wazee wanasema tunataka timu ijengwa na vijana na siyo kuchagua majina makubwa. Wakiwekwa vijana wnataka wazee tena. Kwa kweli Africa haiwezi kuendelea ni majungu tu.

    ReplyDelete
  13. Anony wa February 18, 2009 12:09 AM, hayo magoli mengi aliyefungwa Kaseja Yanga ni yapi? Kwa taarifa yako Yanga imefungwa magoli matano (5) tuu msimu mzima! This must be somekind of a record, don't you think?

    Anony wa February 18, 2009 3:09 AM, nadhani unasahau kuwa nikname ya Tanzania One alipewa Sahau Kambi - hao uliowataja hapo ni kwamba walikuwa makipa namba moja Taifa Stars nyakati tofauti.

    Acheni longolongo - Maximo anapenda makipa warefu na Kaseja japo yawezekana ni kipa mzuri lakini mwili unamuangusha na ndio maana Maximo hajamchagua tena tokea mwaka wake wa kwanza wa Ukocha Tanzania. Dihile is a good keeper, he may be raw but he has room for improvement. Ni kipa mzuri kabisa hana matatizo.

    Vijana wa Yanga mkirudi toka huko Al Ahly wanawasubiri!

    ReplyDelete
  14. nimegundua kuwa wachache sana mlio comment hapa ni wapenzi wa mpifa na waenda mpirani.
    kaseja ni kipa mzuri kuliko wote waliopo sasa.huyo maximo wacha abane tu wakija wengine watampanga.lakini katika historia jamani..hakuna kama Mambosasa Athumani kama ambavyo hajatokea fowadi mzuri kama abbas dilunga au kiungo mshambuliaji kama sunday Manara

    ReplyDelete
  15. Haya kama watu wanataka kuleta sera za kuangalia nyuma badala ya future, basi na mimi ntasema real England one ni:

    Peter Shilton
    Gordon Banks
    David Seaman
    Ray Clemence
    Tim Flowers
    ....


    Yaani watu wamengangana na Mahadhi, Pondamali, etc ishapita hio na hairudi tena, tengenza wapya!

    ReplyDelete
  16. the funny part ni pale maximo anaposimama kwenye bench na kuwapa wachezaji wake majukumu wakati game inachezwa halafu maskini wa kina DIHILE hawamuelewi wanaoanza kumuelewa ni wachezaji wa timu pinzani kwahio mi ushauri wangu maximo anyamaze tu akielekeza kiingereza kabla dihile hajaelewa mpinzani atakuwa keshayafanyia kazi maelekezo,kwahio itakuwa kama tunaempa mshahara maximo atuangamize sie bora aelekezane no hivyohivyo kibububu hao kina dihile hukohuko mazoezini kwao sio kwenye game

    ReplyDelete
  17. Kaseja ni "ballcatcher".................tunahitaji "goalkeeper"

    ReplyDelete
  18. Aisee kitambo kweli saivi tuna Akina aishi manula

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...