
Kwa mwaka wa pili mfululizo, Vodacom imetangaza rasmi ushiriki na udhamini wake katika mashindano ya Kilimarathon 2009 ambayo yanatarajiwa kufanyika mkoani Kilimanjaro tarehe 1 March. Thamani ya udhamini ni zaidi Tsh 50 million.
Udhamini huo ni wa mbio fupi za burudani maarufu kama Kilimarathon Vodacom 5Km FUN RUN ambazo ni mbio zenye kuvutia wakimbiaji wengi hususani wale wanaopendelea kushiriki katika mashindano haya ya kimataifa kwa kukimbia mbio fupi.
Ushiriki wa Vodacom katika mbio hizi umeleta misisimuko na hamasa kubwa sana kiasi cha kuvutia idadi ya wakimbiaji kuongezeka mpaka zaidi ya 2000 mwaka jana. Mwaka huu tumejiandaa vizuri sana, na tunaamini wakimbiaji wataongezaka zaidi ya Mwaka jana.
Kama ilivyokuwa ada ya mbio hizi, wakimbiaji wote watakaoshiriki na kumaliza mbio hizi watakuwa ni washindi, na watazawadiwa zawadi kem kem kutoka Vodacom. Mbali na mbio hizi, Vodacom imeongeza vionjo zaidi ili kutoa burudani kwa kuanzisha mbio zingine mpya kwa ajili ya wadau wake wakubwa ambazo zitakuwa ni mbio za kupokezana vijiti na zitajulikana kama “Vodacom Corporate Relay”.
Ili kupata mshindi/washindi wakimbiaji watatakiwa kukimbia pamoja na kumaliza pamoja, ili kudumisha mbiu yetu ya “PAMOJA DAIMA”. Washiriki wa mbio hizi ni makampuni yanayofanya biashara na Vodacom “Vodacom Business partners”.
Vilevile kupitia Vodacom Foundation pamoja na warembo, Vodacom Miss Tanzania na Miss Kilimanjario, zaidi ya vituo 10 vya watoto yatima vitatoa washiriki kwenye mbio za Vodaocom 5Km FUN RUN, lengo ikiwa ni kuwapa changamoto na kuweza kuwajenga kimichezo.
Baada ya mbio watapokea zawadi mbalimbali kutoka Vodacom zikiwemo vyakula na viburudisho. Vodacom Tanzania wanajisikia faraja sana kuhusishwa na mbio hizi, kwa kuwa mbali na kutoa burudani na kujenga vipaji na afya za wanamichezo amabao watalitangaza Taifa letu katika michezo ya kimataifa, vilevile mbio hizi ni za kimataifa na zinavutia washiriki wengi kutoka nje ya nchi pamoja na vyombo vya habari vya kimataifa.
Kwa maana hiyo udhamini huu unaunga mkono juhudi za serikali za kujenga na kukuza utalii hapa nchini ikiwa ni pamoja na mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama na utamaduni wetu. Vodacom itaendelea kudhamini michezo mbalimbali hapa nchini, tukiwa na lengo la kunyanyua na kukuza vipaji na kuongeza ajira na kujenga uchumi wa taifa letu.
Mbali ya mbio Vodacom inadhamini mpira wa miguu, mashindano ya urembo, kuogelea, golf, tennis, mashindano ya baiskeli na mingineyo mingi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...