Makamu wa Rais Dk, Ali Mohamed Shein akiwa na Governor General wa Australia Quentin Bryce katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere leo tayari kuanza ziara rasmi ya siku tatu nchini


PS: wataalamu wadau wa lugha tunaomba tafsiri sahihi ya governor general

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. unajua uko Australia kuna provinces ambazo ni kama states zilivyo US kwa hiyo hizi provinces zina ma-governors ambao wana-run day to day activities za provincials govts sasa huyu mama ni mkuu wa hao ma-governor kwa hiyo tuseme cheo chake ni kama Mizengo hapa TZ yaani top guy in the running govt while Au PM is the state top guy! hivi ndo ninayvoelewa

    ReplyDelete
  2. Gavana Mkuu.

    ReplyDelete
  3. Ahaa! ndiyo maana ile bendera ina nyota tano zile ni alama za majimbo!!!

    Halafu ile ni sehemu ya UK mbona kuna ka-bendera ka uk!!

    ReplyDelete
  4. Governor General ni mwakilishi mkuu wa malikia wa uingereza nchini Australia, ni kama vili Governer General wa Canada.

    Kwa kiswahili utamwita Gavana Mkuu Mwakilishi na anfanya kazi kama malikia kwa hapo mahali.

    ReplyDelete
  5. Wewe mdau hapo juu wacha kupoteza watu
    Governer General ipo kwenye nchi ambazo Malkia ni head of state
    Huyu anakaimu majukumu ya Queen pale Australia
    http://en.wikipedia.org/wiki/Governor-General
    profile yake hii
    http://en.wikipedia.org/wiki/Governor-General_of_Australia

    ReplyDelete
  6. Australia si Jamhuri, kama Tanzania.

    Waziri Mkuu wa Australia anatokana na chama-tawala. Ni Mkuu wa Serikali iliyotokana na chama-tawala.

    Mpaka sasa Mkuu wa Dola (State) ni Malkia wa Uingereza. Australia inatunga miswada na kuwa sheria. Lakini sheria hizo ni lazima ziidhinishwe na Malkia wa Uingereza. Na wakati mwingine mtu wa kufanya hivyo ni Mwakilishi wake, Gavana-Mkuu.

    Nchi nyingi za Madola (zamani makoloni ya Uingereza) ambazo si jamhuri zina utaratibu wa nmana hii.

    Mkitadha wa hoja hii unakuza pia suala la kuita ma-Balozi wa Nchi za Madola kama High Commissioners!

    Tuchukue mfano wa Uingereza na Nchi za madola zisizo Jamhuri: Mwakilishi wa Dola ni Gavana-Mkuu; na Balozi anawakilisha serikali.

    Kusema kweli si sawa kumwita Balozi wa Tanzania nchini Australia au Uingereza kuwa ni High Commissioner! Ni Ambassador!

    Lakini Balozi wa Uingereza nchini Tanzania ni High Commissioner!

    Tulizoea tu kuwaita ma-balozi wetu katika Nchi za Madola, "High Commissioners" kwa sababu tulikuwa bado kuwa Jamhuri!

    BAP

    ReplyDelete
  7. UK,CANADA ,AUSTRALIA NA NEWZELAND ZOTE ZIKO CHINI YA MALIKIA WA UINGEREZA(ENGLAND).
    MBONA CANADA NA UK HAKUNA MAGAVANA?

    ReplyDelete
  8. The Governor-General is The Queen's representative in Australia. As such, he or she performs the same constitutional role in Australia as The Queen does in the United Kingdom.

    The Queen maintains direct contact with the Governor-General, although she delegates executive power to him or her in virtually every respect.

    The present Governor-General of Australia is Her Excellency Ms Quentin Bryce AC.

    Duties which the Governor-General carries out in the name of The Queen include opening and dissolving the Australian Parliament; commissioning the Prime Minister and appointing other Ministers after elections; giving assent to laws when they have been passed by the two Houses of Parliament; and appointing Federal judges and ambassadors and high commissioners to overseas countries.

    The Governor-General is the Commander-in-Chief of the Australian Defence Force, although in practice he or she acts only on the advice of Ministers. As Commander-in-Chief, the Governor-General has an important ceremonial role to play.

    He or she attends military parades and special occasions such as Anzac Day, and presents colours and other insignia to units of the Australian Defence Force.



    As The Queen's representative, the Governor-General also receives and entertains official visitors to Australia; conducts investitures at which people receive awards for notable service to the community; and entertains many Australian citizens active in the life of the community.

    Both the Governor-General and The Queen send congratulatory messages to people celebrating notable birthdays and wedding anniversaries
    Source:
    www.royal.gov.uk/MonarchAndCommonwealth/Australia/AusGovGen.aspx

    Mdau
    Visiwa vya Papua New Guinea.

    ReplyDelete
  9. Michu,

    Huu ni mfumo wa kiutawala wa kigeni..Kwetu (waswahili)sema ma-liwali, ma-diwani, wandewa n.k. Ndo kusema hapa yabidi kutohoa kufuatia mifano sambamba kama vile luteni-jenerali, meja-jenerali, brigedia-jenerali nk..Sababu neno 'gavana' limekubalika kiswahili basi huyu mama kicheo waweza kabisa muita 'Gavana-jenerali'...

    ReplyDelete
  10. Anon wa March 30, 2009 9:49 PM:

    Uingereza haiwezi kuwa na Governor-General wa kutoka Nchi za Madola. Inawakilishwa na ma-balozi. na ma-Balozi kutoka nchi za Dominions huitwa High Commissioners!

    Soma kwa makini maelezo yangu hapo juu.

    Kanada ina Gavana-Mkuu. Ni mama m-Kanada mwenye asili ya Haiti. Yafuatayo ni wasifu wake kwa kifupi:

    Her Excellency the Right Honourable Michaƫlle Jean, C.C., C.M.M., C.O.M., C.D., Governor General and Commander-in-Chief of Canada

    Biography:

    Michaƫlle Jean was born in Port au Prince, Haiti. She immigrated to Canada with her family in 1968, fleeing the dictatorial regime of the time.

    After pursuing Masters studies in comparative literature at the University of Montreal she taught at the Faculty of Italian Studies at the same university. Three scholarships allowed her to pursue her studies at the University of Perugia, the University of Florence...

    BAP

    ReplyDelete
  11. SASA NI NINI KIGUMUHAPO KUFASIRI? governor general

    hebu tuanze kuchambua hayo maneno
    Governor = huyu ni kiongozi wa benki kuu; Benki kuu ni BOT

    Pia governor waweza sema ni mdhibiti


    General = ni cheo jeshini kiswahili chake ni jenerali/jemedari


    Mana ingine ya General ni ujumla

    Kwa ivo Governor General itakuwa ni sawa na kusema jemedari wa Benki kuu. Au mdhibiti wa jumla

    ReplyDelete
  12. Ni kama Sir Richard Turnbull au Edward Twinning hapa kwetu?

    ReplyDelete
  13. Duu! Kumbe kuna wadau wanawakilisha Papua New Guinea! Kuna wazushi wanadai kuna maeneo huko Papua yabidi uwe makini kwa sababu yana cannibalism. Habari ina ukweli hii?

    ReplyDelete
  14. Ni kama Sir Richard Turnbull au hapa kwetu?

    Hapana!

    Edward Twinning alifika na kuondoka akiwa Gavana (mkuu wakoloni)!

    Richard Turnbull: Alikuja Tanganyika akitokea Kenya alipokuwa namba mbili kwa Gavana wa Kenya.

    Aliondoka Tanganyika akiwa ni Gavana-Mkuu wa nchi iliyojitawla lakini bila kuwa Jamhuri.

    BAP


    Yametosha!

    ReplyDelete
  15. Australia is one of the most beautiful places I tell you! Uzuri wake ni kwamba hata wanafunzi wengi wa Tanzania wanaoenda kusoma kule huwa wanaishia kusoma kweli sababu nchi ile ipo very strict. Sio kama US au UK ambako mtu anasoma semester moja then inayofuata anafanya kazi unakuta degree ya miaka mitatu njemba inasoma kwa miaka sita!!!
    Nimebahatika kusoma Australia my undergraduate degree for 4 yrs and spent another year having a good time travelling (backpacking) all over Australia before coming back to Tanzania to work and live for good even though its a lovely place home is always best especially when you actually have a home to come to (hapa najifagilia kidogo) wadau wala msimind ni ukweli, bongo tunaipenda sema wanasiasa wanachafua sana nchi! Tanzania sio masikini ila tunapokwenda tutakuwa masikini wa kweli maana madini tumeyafuja wageni wanayamaliza na kuishia makwao; viwanda tumeua na kubinafsisha ingawa hatuoni faida yake tumesoma weweeee na sasa wanasiasa wanataka kutufanya hatuna akili kwa kutupeleka kiholela holela.
    Dawa yao iko jikoni.
    Hatuwezi kufikia kiwango cha Australia hata siku moja sababu ya Ubinafsi tulionao! We fail to have common goals for the country, everyone wanna drive a BMW or a Prado instead of kujenga nchi tunajenga matumbo yetu binafsi! Bloody hopeless I tell ya'.
    Asante ~ AngeL_Eyez

    ReplyDelete
  16. asante BAP kwa kutufungua macho

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...