
JK katika picha ya pamoja na viongozi wenzie wa SADC kwenye jumba la kifalme la Lozitha huko Swaziland, leo. Wengine toka shoto baada ya JK ni Rais Robert Mugabe of Zimbabwe, Mfalme Mswati III wa Swaziland, Rais Khaglema Montlante wa Afrika ya Kusini, Rais Joseph Kabila wa Kongo DRC), na Rais Armando Guebuza wa Msumbiji. Wengine yuma toka shoto Waziri Mkuu Phakalitha Mosisili wa Lesotho, Rais Bingu wa Mutharikawa Malawi na Rais Rupia Banda wa Zambia. Picha na Mdau Freddy Maro wa Ikulu

JK akiongea na Rais aliyeondolewa madarakani wa Madagascar Marc Ravalomanana mjini Manzini, Swalizand, asubuhi ya leo muda mfupi kabla ya kuanza mkutano wa viongozi wa nchi za maendeleo ya kusini mwa afrika SADC.
Huyo FISADI MKUBWA Marc Ravalomanana anatafuta nini huko wakati wananchi wake wenyewe hawampendi ??? Unajua hii aina ya viongozi kama huyu wa AFRIKA wanapochukua madaraka wanajisahau na kuanza kujilimbikizia MALI mpaka wananchi wanachuki ndio wasiotakiwa. Kwani naye aliingia madarakanai kwa STYLE aliyoingia nayo KIONGOZI wa MAPINDUZI wa sasa. Sasa anaenda huko SWAZILAND anafikiri hao marais watamsaidia ikiwa wananchi wake wenyewe hawamtaki ?????? Huyo ni bora arudi nyumbani kwao au aende uhamishoni kwani alishaharibu na HAWEZI kurudi tena madarakani hata akienda kwa waganga wa kienyeji !!!!!
ReplyDeleteRAI KWA VIONGOZI WENGINE WA AFRIKA
Muingiapo madarakani jaribuni kutekeleza na kukamilisha matakwa ya wananchi kama ambavyo mnakuwa mmewaahidi na sio kwenda IKULU kwa tamaa na ULAFI mpaka uongozi unakuwa umekushinda.
TUPELEKE JESHI NA HUKOLIKAFANYE MAZOEZI KIDOGO KAMA ILIVYOKUWA KOMORO...MUDA SASA HATUJAPIGANA VITA JAMANI
ReplyDeleteNa nyie wa-TZ, mambo yenu wakati mwingine valuvalu! Ki-Anjoun! Halafu, Madag itajiunga na TZ!
ReplyDeleteina maana hiyo mswati hana hata suti siku nyingine awe serious na mambo muhimu kama hayo,sasa hivyo vikanga si anawadisturb wenzie sana kwanza nahisi kikwapa kitakuwa kinatena,afadhali angevaa shati na suruali akafunga lubenga juu.
ReplyDeleteKing amecheza heko kimavazi. Anaonyesha kutokuta mtumwa wa mawazo ya magharibi kwamba kuvaa suti na tai ndio unakuwa mheshimiwa.
ReplyDeleteKing Mswati....Bravo! Ila punguza hiyo ya vidogo dogo! Inadhalilisha utu na heshima ya akina mama!
ReplyDeleteJamani mwenzenu anaomba hifadhi huyo wala si kingine
ReplyDeleteKWANI KUANZIA LNI IMEKUWA KUVAA SUTI NDIO USTAARABU?
ReplyDeleteHUO NI UKOLONI MAMBOLEO TU, KATIKA ULIMWENGU HUU WA LEO WAAFRIKA TUWE NA MAWAZO MAPANA NA FIKRA HURU, TUACHANE NA FIKRA ZA KUTAWALIWA.
VAZI LA SUTI NI MATOKEO TU YA KUTAWALIWA, WALA SI CHENGINE.
MDAU WA 5:48 NAONA MWENZETU UMEJAWA NA KASUMBA ZA WAKOLONI, NA KUONA KUWA SUTI NDO BAB KUBWA.
KWA TAARIFA YAKO ULIMWENGUNI KUNA TAMADUNI KEDE KEDE, NA ISIKUPITIKIE KUWA KUVAA SUTI NDIO USTAARABU WA MWANZO.
IMANCIPATE YOURSELVES FROM MENTAL SLAVERY, NON BT OURSELVES CAN FREE OUR MIND
Mndengereko, Ukerewe
Kingi Mswati wa Tatu pokea zangu tano. Muda wa kuwa na serikali ya muungano wa mataifa ya afrika ukiwadia ninapendekeza APEWE URAIS wa kwanza.
ReplyDeleteUnajua ravo anamwabiaje kikwete
ReplyDeleteRavo: Kuna kaDJ kameleta rabsha sijui itakuwaje ndugu?
Kikwete: Hawa maDJ balaa kabisaa kuna moja anaitwa Mbowe analeta za kuleta bongo...ila uzuri siyo muraa
Ravo: Peleka vijana wako basi bwana
Kikwete: Ahh! ongea na Qadafi ndio mkuu wetu sasa!
Dah nilidhani King ni mwanamke na hiyo nguo aliyovaa!
ReplyDeletekama wewe basha hiyo kanga itakudisturb
ReplyDelete