Mama Salma Kikwete akimjulia hali Bi Jacqueline Mayemba na mtoto wake mchanga Claudia aliyejifungua katika Hospitali ya Tosamaganga inayomilikiwa na kanisa Katoliki Jimbo la Iringa na sasa ni hospitali teule ya wilaya ya Iringa vijijini.Akiwa hospitalini hapo mama Kikwete alitoa msaada wa vitanda sita maalum vya wagonjwa kila kimoja kikiwa na thamani ya jumla ya Shilingi milioni moja na nusu. Mama Kikwete alikuwa mkoani Iringa hivi karibuni kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo pamoja na mambo mengine alifungua kongamano linalohusu ukimwi na jinsia.
Mama Salma Kikwete akigawa vitabu kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Idodi iliyopo jimbo la Isimani Iringa vijijini.Vitabu hivyo vya masomo mbalimbali vimetolewa kwa hisani ya taasisi ya Wanawake na Maendelo(WAMA) chini ya Uenyekiti wa Mama Salma Kikwete. Aliyesimana pemkbeni ya Mama Salma ni Mbunge wa Isimani William Lukuvi ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Dodoma


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Vyema kuhusu misaada lakini mi niungane na wadau waliopita kwenye picha za hivi karibuni kumpongeza kwa 1st lady anavyopiga pamba,lol anapendeza. Niliangalia 1st lady wa Kenya alivyokuwa ana waonya press kuhusu kufatilia ndoa yake, yani gauni la kitenge oversize juu kaweka mkanda mweusi kama wa suruali etc etc angalia mwenyewe youtube (Kibaki: I have only one wife) jamani kwani ma 1stlady si wana watu specialwa kuwa dress na fungu lao? au huyu wa Kenya,hashauriki kwaiyo anatoka kivyakevyake??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...