Naomba ufafanuzi juu ya risiti za LUKU zitolewazo na Tanesco.Nimenunua umeme wa LUKU na kukutana na kitu kinachoitwa VAT 20% AND EWURA 1% hii imeandikwa mara tatu na mara mbili nimekatwa hela sh. 1,251.91 na 483.63 na pia kuna kitu kinaitwa FIXED COSTS COLLECTED ambayo nilikatwa sh. 2,303.00

Wanabidii makato haya yote ni ya nini kama sio wizi nimetoa sh 10,000 matokeo yake nimeishia kupata umeme wa sh 5,961.46
Gharama hizi za mara tatu ni kwa ajili ya nani?

Je huu sio wizi kwa walala hoi?

KUDOJA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Mramba aliposema mtakula nyasi alikuwa hamaanishi majani.. bali alikuwa anamaanisha vitu kama hivi, na naona mnazila tena kwelikweli hizo nyasi,hapo ndigi yangu unalipia CAPACITY CHARGE ya iliyokuwa Richmond,zile takribani bilioni 3 kila mwezi wanazolipwa IPTL na TANESCO bila ya kufanyakazi yeyote, ndio hizi ambazo raia wanachangishwa n.k chaguo ni lako ndugu kuendelea na CCM ama la... kuhusu wizi ama si wizi jibu unalo ndugu, ngoja niendelee kupiga zangu box nikirudi nachimba kisima changu kirefu na kununua powerful solar systems hizi hela za kuwachangia wachache mimi sina jamani.

    ReplyDelete
  2. mtaibiwa na mtanyonywa mpaka mfe hakuna kiongozi yeyote nchi hio anajali maslahi ya jamiii kila mtu kivakevake tu hio ndo nchi ya amani bana wewe utalalama mpaka utapasuka kichwa hakuna hata atakae kusikia watu wanajilia mapesa yao ya epaaa kwa kwenda mbele na familia zao zipo matawi ya kuleee hawana wasiwasi wa maisha goodluck 4zat

    ReplyDelete
  3. kwakweli hata mimi hili suala la FIXED COST HUWA SILIELEWI KABISA.Watanzania tunaibiwa sana jamani..roho inaniuma pale napokwenda na sh 5,000/= kununua Luku naishia kupata unit za usiku mmoja tu.Tanesco management ur not doing fair at all,iondoeni hiyo fixed deposit ni ya nini??? kwani mita si tunazilipia hata kabla hazijafungwa!! it pains a lot,the pinch is very bitter and so hard to carry!! Punguzeni basi angalau iwe sh mia mbili!!! Inatumiaka kufanya nini hii fixed deposit!!!?? Can you account for it!!!

    ReplyDelete
  4. Karibu kwenye "Soko Huria"..

    ReplyDelete
  5. Hicho kitu wadudi wanakiita kupigwa bao

    ReplyDelete
  6. wizi mtupu!Piga viboko hao kama wanafunzi wa Uganda wamemtandika mwalimu wao mkuu na kumtembeza KM12kwa mkaguzi ili amuondoe na ikakubalika.Hebu MICHUZI tuletee hiyo makala kutoka The monitor la Uganda.Hawaoneani aibu huko..!

    ReplyDelete
  7. Na bado, hiyo umeiona, lakini zipo nyingi unakatwa kila siku huzioni.

    ReplyDelete
  8. Huu ni utapeli unaofanywa na Tanesco, tatizo hili limeshawatokea watu wengi sana pasipo kupata majibu yanayoridhisha, Tunaomba tanesco watuambie Fixed cost hiyo ni ya nini, inakatwa kwa wateja wa namna gani, na utaratibu gani (formula gani) unatumika kukata kiwango hicho. Tuoneeni huruma watanzania tulio wengi ambao kipato chetu na maisha yetu ni duni mno.

    Watanzania tutabiwa mpaka lini?????????

    ReplyDelete
  9. Toa e mail yako nitakupatia jibu baadae, nitaulizia kwa uongozi wa TANESCO

    ReplyDelete
  10. Assalam aleykum kaka Michuzi, kuhusu hili naomba kama mwana habari ambao ndio mnatuwakilisha kufika kwa wahusika na kuwahoji na kutuletea majibu kupitia vyombo vya habari kama gazeti tando hili, sasa kaka tunaomba ufanye utafiti, wadau wamelijadili sana sauala hili kwa blog yako hii, tafadhali tunaomba uwahoji watu wa TANESCO wenye majibu ya maswali yetu haya halafu uturushie kama unavyoturushia habari zingine, ni kweli watu wengi tuna maswali lakini nani atatujibu hata mtumishi wa kawaida wa TANESCO hajui hizi gharama tunazokatwa kila tukinunua umeme ni za nini, yaani hana maelezo. kuliko kuendelea kuandika comments kwa hisia kali tutafutie majibu.
    mdau mkereketwa.
    dsm

    ReplyDelete
  11. dawa ya moto ni moto, na dawa ya mwizi ni mwizi, dawa yao ni kubana 2!!!!

    ReplyDelete
  12. Hapo hamna wizi ndugu yangu hiyo umekatwa halali tu kwa mujibu wa serikali ya Tanzania. Ingekua kama unaibiwa ungelalamika na mngeingia barabarani.Tatizo hapa ni kwamba Watanzania tunasema ni wajajna lakini katika watu sio sisi ni namba moja.
    Kwanza mtu kulipia kitu kwa gharama kubwa anaona ufahali. Nauli za daladala hadi sumatra walikua wanawashauri mkomae lakini wapi bado nauli halali zajulikana na watu sehemu nyingine wanalipa zaidi na wala hawalalamiki.
    Mafuta yameshushwa bei na EWURA japo bado ni ghali sana lakini watu bado wanauziwa dizeli 1380 hadi 1400 kwa Dar Es Salaam na watu hawalalamiki wala nini wapo tu tena wanaona fahari
    Soda hazijapandishwa bei lakini Dar es Salaam kwenye watu wengi waliosoma wanaojiita wajanja wanauziwa sh.400 badala ya sh. 350 halali wametulia tuu wanaona fahari
    DSTV bongo wanalipia kwa US $70 kwa mwezi(japo si halali kuuziwa vitu kwa dola kwani ikipanda kama sasa wanaumia) cha ajabu haohao DSTV wanatoza kwao South US$25 tu,hata kama hatujui jamani miaka yote hiyo tangu 1998 bado hawajabreak even tu?
    Ukiingia pale Mlimani City kwenye maduka ya Mr.Price utashangaa, maduka yale South ni ya watu wa chini watu toka maeneo kama Soweto hivi,jamaa wanatarget low income people,huko nguo za rand 45,70 yaani bei mbaya ni rand 150 (1rand ya SA ni Tsh 140 hivi) sasa kinyume na Mr.Price ya bongo bei rahisi nguo kuanzia Tsh.22000(utasema labda kodi wapi Botswana kuna Mr.Price bei ni zilezile pula 20,30 yani be za kawaida tu)waTZ mnaona sawa tu siku zinaenda
    Wapo wabongo wakazi wa Tabata,ubungo,kimara,mbezi,wanalipia bili za maji kila mwezi japo hkuna miezi mingine wanapata maji mara moja tu au wasipate kabisa kwa mwezi lakini nani alishawahi kuandamana na kulalamika?
    Sasa hivi kuna ishu ya kununua mitambo chakavu ya Dowans kisa Idrisa Rashid(aliyekua gavana wa Benk kuu aliyeshindwa kuishauri serikali isiue NBC)kasema December nchi itakua giza! Nifahamuvyo mimi mitambo hiyo ni haramu,kwa mfano jeshi la polisi likikamata silaha kwenye ujambazi hata kama ni silaha halisi na zinazofaa kwa kujilinda au kushambulia, wao huzichoma moto kwa kigezo kwamba ni haramu,sasa iwaje leo scrap Dowans ionekane ni mkombozi,yet wabongo tumeachia magazeti tu yapambane na hii daylight robbery.
    Ndugu yangu hiyo mikodi haina wizi wala nini ni halali.
    Mbona hujahoji the crazy PAYE,hadi sometimes unatamani upate mshahara mdogo vinginevyo ni sawa na unagawana na TRA tu ukipata 1m basi laki3 ni ya TRA!
    MBOGO TAJIRI BWANA!

    ReplyDelete
  13. Anon wa March 07, 2009 12:07 AM...AMEN
    Umeongea point sana. Wabongo tunaenda tu kila siku kama kondoo bwana. Inabidi sasa tuanze kudinda. Mafuta bei juu, umeme bei juu, maji unalipia huku hupati...alafu wakija kuomba kura wanawanunulia bia...hehehe...wacha nifurahi mie hapa bwana. Bongo harudi mtu!

    mtoto

    ReplyDelete
  14. annon #12.07am

    umenifanya nilie machozi,yan km ulikua katika akili yangu aya ndo mambo ya kuandikwa na kutangazwa TV na radio
    yan kuna wezi hii nchi??hakuna kiongozi atayetetea aya mana wanacholipwa na marupurupu basi.

    ASA SUALA LA KODI P.A.Y.E YAN TWALA NA TRA,NA BADO MIKODI YOOTE UTALIPA TU KM RAIA ALIE NA MATUMIZI
    NDO MANA WATU WANAKWEPA KULIPA KODI

    shezi taipu!!

    ReplyDelete
  15. APA NI KUTOLIPA TUU IZO KODI ZINGINE

    VAT 20%hii ktk kila kitu unachotumia km mwanadamu Tz.
    EWURA 1%
    CAPACITY CHARGE%
    PAYE 26%-30% asa wanaolipwa salary kubwa.adi unajuta why umesoma na kupata kazi inayolipa.
    ALLOWANCES % nazo wanataka kukata.

    annon apo juu:bora ununue solar na chimba kisima kirefu basi.me ndo nafanya ivo kwangu

    ReplyDelete
  16. E-MAIL YA TANESCO NIKITAKA KUWASILIANA NAO HASA KUHUSU LUKU, NAITAPATAJE?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...