Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (kulia) akishiriki mbio za Km 5 za Vodacom katika mashindano ya mbio ya Kimataifa ya Kilimajaro Marathon, mjini Moshi jana. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom, Efraem Mafuru, Meneja wa Kampuni ya Bia Tanzania Kanda ya Kaskazini Mashariki, James Bokela, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera na Mwenyekiti wa Chama cha Wachezaji wa Soka wa zamani, (SIPUTANZA), Venance Mwamoto
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe (kushoto), akishikana mkono na Mtoto yatima Omari Khamis alipokuwa akikabidhi msaada wa vyakula kwa vituo vitano vya kulelea watoto yatima vya mkoani Kilimanjaro. Msaada huo uliotolewa na Vodacom Foundation ulikabidhiwa baada ya mbio za Kili Marathon kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu kIshiriki cha Ushirika na Elimu ya Biashara, mjini Moshi jana. Wengine kutoka kulia ni Miss Vodacom Tanzania, Bi. Nasreem Karim, Mkuu wa Vodacom Foundation, Bi. Mwamvita Makamba na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Bw. Joel Bendera.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. hongereni kwa kutoa misaada pia,
    hii marathon niliiona mara ya kwanza kwenye 2002/3 sikujua kama ingeendelea na kuwa maarufu hivi.Nilichopenda zaidi ni point ya kusaidia yatima.

    ReplyDelete
  2. Sasa jamani utakimbiaje Marathon na Mkanda na suruali ya kawaida badala ya Track-suit? mbona makubwa haya..si suruali itakukata nanihii zako wakati unakimbia?

    ReplyDelete
  3. waziri alikosa track suit ya kukimbilia wajemeni?kaulamba na mkanda halafu marathoni wapi na wapi?

    ReplyDelete
  4. Hata mie nimeshangaa yaani Waziri kapiga suruali ya kaki na mkanda juu as if anakwenda pub jioni:-)

    Wangalimpatia track suit kama Mzee mzima Mgosi Bendera...

    ReplyDelete
  5. YANI ANNON WA #1 NA #2
    KAMA MLIKUA AKILINI MWANGU,,YAN KUONA TU IYO PICHA NKACHOKA KABISAAAAAA!!sooo funny hahahahaaa
    "kweli kusoma si kuelimika" yan alikulupushwa au hana track?au ndo uzee?

    hii ni aibu tena pic iko published ktk newz-pepaz zinazosomwa na watu wenye akili zao

    hahahahaaaa,bongo mteremko

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...