
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete ameipongeza timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, kwa mafanikio iliyoyapata katika Mashindano ya Ubingwa wa Afrika (CHAN) pamoja na kwamba Stars ilitolewa kwenye mashindano hayo usiku wa jana, Jumamosi, Februari 28, 2009.
Rais Kikwete amesema kuwa amefurahishwa sana na maendeleo ambayo Tanzania imepata katika soka.
Rais Kikwete pia amewapongeza Watanzania kwa kuiunga mkono timu hiyo, na pia amewapongeza makocha wa timu hiyo kwa kazi nzuri waliyoifanya kuinua kiwango cha timu hiyo.
Aidha Rais ameahidi kuendelea kuiunga mkono “timu yetu mpaka tufike pale tunapopata sote” na pia ameupongeza uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa uongozi wao mzuri katika suala hilo.
Rais amesema kuwa amesikitishwa sana na Taifa Stars kutolewa dakika za mwisho na za majeruhi za mechi ya jana usiku kati yake na timu ya taifa ya Zambia, Chipolopolo katika mechi hiyo iliyochezwa mjini Bouake, nchini Ivory Coast ambako CHAN yanafanyika.
Timu hizo zilitoka sare 1-1 na hivyo kuifanya Taifa Stars kuikosa nafasi ya kucheza nusu fainali kwa unyoya tu.
Stars imemaliza mechi zake ikiwa na pointi nne baada ya kuwashinda wenyeji Ivory Coast 1-0, ikatoka sare na Zambia 1-1 na kufungwa 1-0 na Senegal.
Nchi za Zambia na Senegal zimesonga mbele kutoka kundi hilo kwa kupata pointi tano kila moja.
Hadi dakika ya 90 za mechi ya jana, Taifa Stars ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa kwa penelti katika dakika ya 87 na nahodha wa timu hiyo, Sahdrack Nsajigwa baada ya mlinzi mmoja wa Chipolopolo kuunawa mpira katika eneo la penelti.
Mwamuzi wa mechi hiyo aliongeza dakika tano baada ya kumalizika kwa muda wa kawaida wa mchezo, na Rais Kikwete amesema: “Nimesikitika sana tumetolewa dakika za majeruhi.”
Lakini ameongeza Rais ambaye amekuwa shabiki nambari moja wa Taifa Stars: “ Lakini nimefurahi sana kwa hatua tulifikia katika maendeleo ya soka. Sasa tunatambulika na kuheshimika katika ulimwengu wa soka Barani Afrika.”
Ameongeza Rais: “Tuongeze bidii, tusirudi nyuma, bali twende mbele.
Nawapongeza wachezaji kwa juhudi zao. Nawapongeza walimu kwa kazi waliyoifanya kuinua kiwango cha soka nchini. Nawapongeza viongozi wa TFF kwa uongozi wao mzuri.”
Kuhusu Watanzania, Rais amesisistiza: “Nawapongeza Watanzania kwa kuiunga mkono timu yenu. Mmekuwa chachu ya mafanikio hayo. Watanzania wenzangu tufe moyo, mwanzo mgumu. Tumeanza vizuri na tumefika pazuri. Tuendelee kuiunga mkono timu yetu.”
Kuhusu ahadi yake kwa timu hiyo, Rais amewahakikishia wachezaji wa timu hiyo na Watanzania wote: “ Mimi naahidi kuendelea kuiunga mkono timu yetu mpaka tufike pale tunapopata sote.”
Mashindano ya CHAN yanashirikisha wachezaji wanaocheza katika ligi za soka za nyumbani Barani Afrika, na hii imekuwa mara ya kwanza kwa Tanzania kufanikiwa kuingia katika fainali za Kombe la Afrika katika miaka 28.
Mara ya mwisho, Tanzania ilifikia hatua hiyo ilikuwa mwaka 1980 katika mashindano yaliyochezwa Lagos, Nigeria. Kwa namna pekee ya kihistoria, Tanzania iliingia fainali za 1980 kwa kuitoa Zambia.
Katika hotuba yake ya Desemba 30, mwaka 2005, baada ya kuwa ameapishwa kuwa kuongoza Tanzania, Rais Kikwete aliahidi kuendeleza michezo na katika moja ya hatua zake kufanikisha dhamira hiyo ilikuwa ni kuajiri kocha wa kulipwa wa Taifa Stars, Marcio Maximo kutoka Brazil ambaye ameinua sana kiwango cha Stars.
michuzi naomba ui post hii article peke yake watu waijadili ni uozo wa wizara ya utalii na ubalozi wa TZ london hawa watu wanapitia kenya
ReplyDeletehalafu kila siku wanajitamba tunafanya hivi na vile.....
na wakati matukio kama haya wamelala tu....
A host of showbusiness names including Cheryl Cole, bandmate Kimberley Walsh and Take That's Gary Barlow have set off in a bid to climb Mount Kilimanjaro.
It's all to raise cash for this year's Red Nose Day campaign and more than £460,000 has been donated already.
The stars flew out from Heathrow on a Kenya Airways plane with its nose painted red for the occasion.
Boyzone frontman Ronan Keating nearly missed the outbound flight from Heathrow after his connection from Dublin was delayed by an hour-and-a-half.
The star had to be driven across the Heathrow Tarmac in order to catch the waiting flight.
A Comic Relief spokeswoman explained: "Ronan nearly didn't make it, it was touch and go.
"His flight from Dublin was delayed and once he did arrive at Heathrow he had to be driven over to the plane, luckily he was just in time."
Barlow said: "We've been planning to climb Mount Kilimanjaro for so long, it's only now that we're boarding the plane that it's really dawned on me just how tough this could be!"
Mount Kilimanjaro stands at 19,340ft above sea level, is the tallest mountain in Africa and the highest free-standing mountain in the world.
mdau uk
MIMI KAMA MKEREKETWA NA MSHABIKI WA TIMU YA TAIFA, NAOMBA NITOE MCHANGO WANGU.
ReplyDeleteILI TIMU YETU IFANR ZAIDI, INABIBIDI KOCHA WETU PAMOJA NA WACHEZAJI WAKE WOTE WACHAPWE NA WAZIRI WA MICHEZO
BAADA YA HAPO WAZIRI NAYE APEWE MBOKO NA RAIS. HAPO TUTAONA UZEMBE UNAPUNGUA NA KOMBE LINAKUJA NCHINI KWETU.
SAMAHANI WADAU, NIMEPOTEA KIDOGO, MASWALA YA KIUCHUMI YANAYOTIKISA DUNIA YALINITIKISA HATA SHILLIMI ALFU YA KUJA KWENYE CAFE NILIKOSA.
MH. RAIS, NAOMBA MSSADA WAKO KWA SABABU NCHI ZA WATU MASIKINI WANASAIDIWA, NA MIMI KAMA MKEREKETWA NA SHABIKI WAKO NAMBA RI WANI, NADHANI OMBI LANGU LITAKUWA RAISI SANA KUTEKELEZA.
ZIDUMU FIKRA ZA MZEE WA PAMBA JK
ZIDUMU
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
KIDUMU
MAFISADI YOTE NAYO YACHAPWE MBOKO
YACHAPWE
mkuu wa wilaya mtarajiwa 2015 chini ya mashaka, january na shayo
MKEREKETWA, YOMBO VITUKA !!!!
-----------------------------------
dakika 30 za Internet Café Zimekwisha
WATANZANIA TUNAKUSHUKURU SANA MUHESHIMWA RAIS KWA KUONYESHA MAPENZI KATIKA MICHEZO NA MCHANGO WAKO MKUBWA KULETEA KOCHA MAXIMO,INGAWA KUNA WACHACHE WENYE MAWAZO YA 47 KUTAKA KUMKATISHA TAMAA KOCHA ILI AFUNGE VIRAGO.NAAMINI WATANZANIA WALIO WENGI TUNA MUUNGA MKONO KWA KAZI KUBWA ALIOIFANYA MPAKA SASA NA KUZINGATIA AMELETA MATUMAINI MAPYA NA MAENDELEO KWA MUDA MFUPI.IFANYIKE JITAHADA YA KUMUONGEZEA MKATABA ILI AWEZE KUMALIZIA PROGAM ZAKE,ENDAPO TUTA LETA KOCHA MWINGINE NI LAZIMA ATAKUWA NA PROGRAM ZAKE TOFAUTI NA HALI KAMA HIYO INAWEZA KUCHANGIA KURUDI NYUMA HATUA KUMI NTUTAMJUTIA BAADAE,NAAMINI TFF INAONGOZWA NA WATU MAKINI AWEZI KUFANYA KOSA KATIKA ILO.PONGEZI NYINGI KWA VIJANA WETU WAMEFANYA KAZI NZURI NA WAMEJITENGENEZEA CV NZURI.BILA KUKOSA KUTOA PONGEZI KWA WADAU WOTE WA SOKA BONGO NA WACHAMBUZI FLIP!FLOP! WAMICHEZO,DAIMA MBELE NYUAMA MWIKO,UBAYA UBWEELE!
ReplyDeleteMambo mswano kwa JK Boyz wameonyesha soka nzuri sana.
ReplyDeletePia thanks kwa Bro kwa kutupa news ..as they are happening!
Keep it up!
Kwa JK ....thumb up!
NB:ombi kwako mwenyekiti wa jamvi hili:uwe unaweka Quotation!..source ya habari!hii itasaidia watu wengine wanaotumia habari zako!
Vinginevyo ...utakuwa unafanya kama blogu zingine ambazo kama ni ku-copy na ku-paste news za wengine
Mdau,
wa Kwa Malkia!...aka..ukerewe
Safi sana President JK!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteHiyo ni hope kubwa iliyojaa na imani kwa timu yetu ya strs pamoja na Taifa zima, ni kweli inauma sana ila tumepata changamoto ya uhakika wa kufanya vizuri zaidi na kulishangaza Bara la africa pale tutakapo ibuka na kuwa mabingwa wa soka Barani Africa!!!!!!!!!
Mungu ibariki Africa!!!
Mungu ibariki Tanzania!!!
Mungu mbariki Rais wetu JK!!!
Mdau canada!
Hail to the taifa Stars, but Almost doesn't count , Also how about them Liverpool aka Bwawa la mainzi Ooops Maini ?? I tell you what !!, you just need to get rid of Rafa Benitez for you to be premier champs’ just take a look of his records since he took charge of Kop some years ago, Liverpool have been seriously competing in only one level which is the champion's league and better yet can't compete in the domestic level( inconstant) why kwanini???and lately he kept coming out with whole bunch of excuses and demands like the dismissal of rick parry (chief exc). Benitez can not escape from the truth that he's at the point of diminishing returns and I bet you know what comes next after getting to that point. The time is winding down and I guess now it's time to part company with the manager for the sake of glory.. Well,i got to go but the answer will soon be revealed after the conclusion of this season, Congratulations to MANU, good looking !!
ReplyDeleteDon’t touch the dial and stay tuned .
Mdau Jombi
Bariad
asante Sana T Stars for contributing to those winning moments za wa-Zambia!
ReplyDeleteHakuna mshindi bila mshindwa!
WIZI MTUPU,DC MNALI ANAFAA KUWA MENEJA WA TAIFA STARS KUMBE
ReplyDeleteBAADA YA KUIFUNGA TIMU MBOVU YA IC TULIONA KUWA NDIYO KIPIMO CHETU CHA UBORA NA TUKAYADHARAU MABAO MATATU WALIYOFUNGWA IC NA ZAMBIA SISI TUKAJIONA BORA ZAIDI NA KUSEMA TUTAWAFUNGA ZAMBIA! SASA TUMEYAONA, LAZIMA TUBADILI TABIA YETU YA KUJIPIMA UBORA WETU TUNAPOZISHINDA TIMU MBOVU.
ReplyDeleteMheshimiwa rais wetu JK
ReplyDeleteNdugu watanzania wenzangu,
Ama kwa hakika safari ya kilometa elfu moja ndio kwanza zinaanza na sasa tumemaliza kilometa moja na nusu za lami, huko tuendako barabara ya mafanikio ya kandanda la tanzania itakuwa ni ngumu zaidi kwa maana ya kuwa wapinzani wetu kisoka watataka kutuyumbisha zaidi.
Watu wa mpira nao watakuja na "dream zaidi", wakipendekeza mabadiliko ya "maneno zaidi" huku Presd JK akifanya "vitendo zaidi" kwa support yake hadharani zaidi.
Presd JK hajataka kuweka wazi tu, me naomba nimsemee japo sio rasmi
(Mafanikio ya Taifa Stars yatamfanya Presd JK hata akikutana na Rais wa Egypty ama Nigeria ama Tunisia wakijadili mambo ya kandanda ni wazi atajibodoa kuwa TZ pia kuna timu kali ya Taifa, hawatombishia kihivyo japo mafanikio yetu ndiyo yanachomoza )
Kidiplomasia inaleta heshima kimtindo,
Kwao Stars na benchi zima, nawapa tano, washkaji hawakwenda kuwakilisha wameshindana na wote tumeona ama kusikia matokeo yao
Kimsingi tumefarijika
Kwa TFF sisi watanzania wanazi wa Kandanda tunasema WE WANT MORE THAN THAT, kumbe tunaweza kabisa kupoteza game moja na kushinda game mbili out of three!!!!
Tafadhali, TFF wakati umefika waambieni wachezaji wetu kuwa kushinda na kushindwa tofauti huwa ni kiduchu sana ingawa
"kumbukumbu" hubaki daima na milele.
Nawasilisha,
Mungu Ibariki Tanzania
Mdau
Nelspruit
RSA
Jamani, mpira si umechezwa juzi tu na leo tunapata comments? Vipi issue ya Kiwira?
ReplyDeleteKikwete ame-dye nywele? He looks good.
ReplyDelete