Na Anna Nkinda – Maelezo 

Serikali imesema kuwa ndani ya wiki moja kuanzia leo mtambo wa kuzalisha umeme wa Kampuni ya Songas ulioharibika utakuwa tayari na kuanza kufanya kazi kama kawaida. 
  
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja alipofanya ziara ya kutembelea mitambo hiyo iliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam ili kuona maendeleo ya matengenezo ya mitambo miwili iliyosababisha upungufu wa megawati 50 za umeme katika gridi ya Taifa. 
  
“Kwa taratibu za kawaida matengenezo ya mtambo huu yangechukua miezi mitatu hadi minne ila mafundi wanafanya kazi ya matengenezo  kwa bidii na hatua waliyofikia  watachukua muda mfupi kumaliza kazi hii”, alisema waziri Ngelleja. 
  
Aliendelea kusema kuwa mgao unaoendelea ni kutokana na ajali ya kuharibika kwa mtambo mmoja kwani mtambo mwingine uko katika matengenezo ya kawaida ila baada ya kuharibika kwa mtambo huo ndiyo tatizo limeongezeka zaidi. 
  
Ngelleja alisema kuwa, “Serikali haina mpango wa kuwafanya wananchi waishi gizani zipo hatua nyingi ambazo wanazichukua na watazitolea ufafanuzi kadri siku zinavyokwenda”. 
  
Waziri huyo alimalizia kwa kusema kuwa hivi sasa tatizo wanalolifanyia kazi ni  kuongezeka kwa mahitaji ya umeme  kuliko uwezo wa kuzalisha. 
  
Mtambo wa pili wenye uwezo wa kuzalisha megawati 35 ambao uko katika matengenezo ya kawaida unatarajia kuanza kazi baada ya  wiki mbili tangu kuanza kwa matengenezo hayo. 
  
Hivi sasa mtambo ulioharibika  umefumuliwa na kuanza kutengenezwa upya na una uwezo wa kuzalisha megawati  20 za umeme kama utaanza kazi utakuwa umepunguza makali ya mgao wa umeme kwa kiasi fulani. 
  
Kuanzia Alhamisi wiki hii jijini Dar es Salaam kumeanza mgao wa umeme ambao unaleta usumbufu kwa wananchi  kutokana na kuharibika kwa mitambo hiyo 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. POLITICS WHILE THE POWER RATIONING BITES.....AAaaagh.

    ReplyDelete
  2. Hizo ni story tuuuu. Kila mara mnatisha mtanzania umeme umeme wakati JK akiwa nje ya nchi akirudi tuuu umeme unakuwa upo jamani jamani mnaharibia mzee wa watu next year... acheni ufisadi mmezoea kuonea watz...tulikuwa tumelala sasa basi jamani... tupeane kidogo cha nchi ni mali ya watanzania wote

    Mnyonge.....

    ReplyDelete
  3. Na mnukuu waziri "kwa taratibu za kawaida magengenezo yangechukua miezi 3 - 4 ila mafundi wanafanya kazi kwa bidii na hatua waliofikia watachukua muda mfupi kumaliza kazi hii" hii imekaaje? taratibu za kawaida hawafanyikazi kwa bidii?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...