Huyu ndiye mwenyekiti Mpya wa
Wanafunzi wa Kitanzania mjini Mysore
India, Mh. Mwinga Mungwe

Jumuiya ya Wanafunzi wa Kitanzania wanaoishi Mysore jana jioni walifanya uchaguzi wa kuchagua viongozi wapya watakaoongoza kwa mwaka 2009-2010.

Katika uchaguzi huo ambao watu 155 walipiga kura, ulihusisha nafasi ya Mwenyekiti, Mwinga Mungwena makamu wake walikuwa Aisha Machano, Aliko Mwakasitu na makamu wake alikuwa Hassan Ahmed wakati nafasi ya ukatibu ilikuwa inagombewa na Sonia Mlaki akiwa na msaidizi wake Irene Mwambene, McSweney Lupembe akisaidiwa na Kelvin Mwakalindile wakati nafasi za mweka hazina zilikuwa zili ombewa na Neema Salula na Diana Mzirai.

Hadi mwisho wa Uchaguzi mwanadada Mwinga Mungwe ndio alichaguliwa kuwa mwenyekiti pamoja na makamo wake Bi.Aisha Machano,nafasi ya ukatibu ilichukuliwa na MacSweney Lupembe na msaidizi wake Kelvin Mwakalindile na nafasi ya mweka hazina ilichukuliwa na Diana Mzirai.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Mwenyekiti ana jina zuri sana nimelipenda.

    ReplyDelete
  2. Wadau hii imekaaje?
    Mysore au Mbeya?
    1) Mwinga - Mungena, any relationship with our Mwinga Mwanjala? - Mbeya line
    2) Aliko Mwakasitu _ Mbeya line
    3) Irene Mwambene - Mbeya line
    4) Kelvin Mwakalindile - Mbeya line

    Vipi hawa ndugu zangu wa Mbeya? wapenda uongozi au ndio wapo wengi huko?

    Anyway big-up ndugu zangu.

    ReplyDelete
  3. Wabongo kiboko. Ghafla uchaguzi umeibua masuala ya ukabila!!!

    ReplyDelete
  4. WATZ BWANA YAANI UKABILA KILA KONA WENZAKO WAMEFANYA UCHAGUZI WW UNACHUNGUZA WAMETOKA MKOA GANI MTONI SIE HATUJARI UKABILA TAMBAFU

    ReplyDelete
  5. KWANI KUNA UBAYA GANI WA MTU KUULIZA? LABDA ANAFANYA RESEARCH YA KUJUA SEHEM GANI YA TANZANIA WATU WANAPENDA UONGOZI?

    UHURU WA KUONGEA .......

    ReplyDelete
  6. Big up ma gal u'l mek a perfect leader!

    ReplyDelete
  7. Mwenyekiti mzuri lakini duuh, ingebidi kidogo awe prizentabo kama huyu dada yetu wa UK bi nanihii, Katibu wa nini sijui. Maana angepiga kamsasa kidogo awe na kahadhi ka uenyekiti ili akisimama jukwaani tumkubali. Mengine anajitahidi, Wanawake mpo juu.
    Hongereni

    ReplyDelete
  8. ...Wala hakuwa na haja ya kuchunguza. It was there for anybody with inquistive mind to see...!! Naomba email yake.

    ReplyDelete
  9. Kuna mtu kauliza hapo juu sio Mbeya line Mdau hiyo ni Singida line.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...