
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Meja Jenerali Mstaafu Said Kalembo, ( kulia) akifurahia jambo kati yake na Msimamizi wa kituo cha Soko kuu la Morogoro cha kupigia Kura za maoni ya watu wanaotuhumiwa na mauji ya Albino, vikongwe pamoja na dawa za kulevya na Ujambazi, WP Jamila ( katikati). Shoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Mogorogo, Raphael Ndunguru. Hadi viongozi hao wanafika kituoni hapo milango ya saa nne na nusu hakuna kura iliyokuwa imepigwa.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Meja Jenerali Mstaafu Said Kalembo akimsikiliza Ofisa Mtendaji wa Serikali ya Kijiji cha Gwata, Wilaya ya Morogoro, Salehe Mangala ( kulia) kuhusiana na jinsi ya idadi ya watu 30 hadi kufikia mchana jana walivyoweza kuitikia wito wa kupiga kura za maoni kwa wauaji wa maalbino, vikongwe na wale wanajihusisha na dawa za kulevya na ujambazi. Kijiji hicho kina jumla ya wakazi 2,110.
Picha na habari na John Nditi, Morogoro
WAKAZI wa Mkoa wa Morogoro wameshindwa kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono Serikali katika zoezi la kupiga kura za maoni kwa ajili ya kuwafichua wauaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi ( maalbino) , vikongwe, wazalishaji, wauzaji, wasambazaji na watumiaji wa dawa za kulevya na majambazi wa kutumia silaha.
Haya yamebainika katika ziara ya Mkuu wa Mkoa huo, Meja Jenerali Mstaafu, Said Kalembo jana wakati alipovitembelea baadhi ya vituo vya kupingia kura hizo katika Halmashauri mbili za Wilaya ya Morogoro.
Ziara hiyo iliyofanyika majira ya saa nne asubuhi ya siku ya upigaji wa kura hizo, akiambatana na Mkuu wa Wilaya hiyo, Said Mwambungu, katika kituo cha Soko Kuu la Morogoro lenye mkusanyiko mkubwa wa watu hapakutokea mtu hata mmoja kuweza kupiga kura hizo.
Hata hivyo katika kituo kilichopo shule ya Msingi Msamvu, Manispaa ya Morogoro hadi muda huo ni watu sita tu waliweza kujitokeza kupinga kura hizo , ambapo katika kituo cha Kihonda mtu mmoja alikuwa ameshapiga kura hizo.
Hata hivyo Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, katika vituo vyake viwili watu waliweza kujitokeza hasa katika kituo cha Gwata,ambapo idadi ya watu 30 walipiga kura zao za maoni hadi mchana wa siku hiyo.
Kituo kingine wambacho kilitembelewa na Mkuu hiyo wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ni cha Kitongoji cha Kiroka Soweto ambapo idadi ya watu saba walijitokeza kupiga kura hizo za maoni hadi muda huo.
Ofisa Mtendaji wa Serikali ya Kijiji cha Gwata, Salehe Mangala, alisema mafanikio hayo yalichangiwa na viongozi wa serikali ya kijiji na Diwani wa Kata hiyo kuwahamasisha wananchi uhumimu wa upigaji wa kura hizo za maoni.
Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji huyo, Kijiji hicho kina jumla ya vitongoji vitano na idadi ya wakazi ni 2,110 na kujitokeza kwao kutaisaidia Serikali kuwabaini waharifu hasa wa ujambazi na dawa za kulevya.
Naye Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kihonda, Manispaa ya Morogoro, Winfrida Chausi, alisema kushindwa kujitokeza kwa wingi wa wananchi wa eneo hilo kupiga kura za maoni kumetokana na wengi wao kwenda katika shughuli zao za kibinafsi na hivyo kusubiri nyakati za alasiri.
Mkuu wa Wilaya hiyo, Said Mwambungu, alisema takwimu za idadi ya kura hizo za maoni zitatolewa wakati muafaka mara baada zoezi hilo kamilika katika vituo vyote vya Halmashaui ya Wilaya na Manispaa.
Naye Mkuu wa Mkoa huyo, alisema ingawa idadi ya waliojitokeza kupiga kura hizo za maoni si wengi, lakini kwa uchache wao , kura hizo zitaisaidia Serikali kuweza kufanya uchambuzi na uchunguzi wa kina kuwabaini wahalifu ili wawezekuchukuliwa hatua za kisheria.
Hata hivyo alisikitishwa kwa kuona wakazi wa Manispaa ya Morogoro waameshindwa kujitokeza kutumia nafasi hiyo, licha ya Mkoa kutokuwa na matukio ya mauaji ya maalbino na vikongwe.
Hivyo alisema wananchi hao walikuwa na fursa ya kutumia siku ya zoezi hilo kuweza kuwapingia kura za maoni wa uharifu wengine wanaowafahamu hasa wale wa naojihusisha na dawa za kulevya pamoja na ujambazi wa kutumia silaha.
“ Mkoa hauna historia ya mauaji ya maalbino wala vikongwe …lakini tatizo la ujambazi linaweza kuwepo hasa kwa wale wanaotokea Jijini Dar es Salaam na kujificha Mkoani mwetu hivyo kura zao za maoni zingweza kuisaidia Serikali “ alisema Kalembo
Mkoa wa Morogoro katika zoezi hilo ulijumuishwa katika Kanda ya Mashariki wenye Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam, ambapo vituo 1,959 viliainishwa katika kila Wilaya na kukadiriwa zaidi ya watu 927,593 kushiriki zoezi hilo la upigaji kura za maoni.
hii imekaa vizuri,inamaanisha kama huyu anapiga kura , alikuw anamhisi mharifu mmoja wapo wa makundi hayo matatu,swali la kujiuliz ani kwamba naye alisubiri hadi itokee chance hii ndo aact, au hapo wanatuzuga. bahati mbaya wanasiasa wanakasumba ya kuchangany ishu serious na siasa. kimtazamo zoezi lote ni kama linapoteza mwelekeo.
ReplyDeleteHIVI KARIBUNI RAISI ALISIKIKA AKISEMA ANAYO MAJINA YA WATU WANAOKWEPA KULIPA KODI, SIJUI NA YEYE ANASUBIRI SIKU YA KUPIGA KURA ZA WANAOWAFAHAMU WAKWEPA KODI NDIPO AKAWATAJE?
ReplyDelete