Balozi wa Rwanda Nchini Zeno Mutimura akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya habari maelezo leo juu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini humo mwaka 1994 miaka 15 iliyopita yanayotarajiwa kufanyika kesho kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar.
Katika maadhimisho hayo pia kutakuwa na wimbo maalum uliotungwa na mwanamuziki Nakaaya Sumari unaoitwa 'I am in Africa' unaohamasisha kuachana na mambo ambayo yanaweza kuchochea kwa mauaji kama yaliyotokea Rwanda. Pia wimbo huo unazungumzia kampeni ya kuwasaidia yatima walioko nchini Rwanda waliopoteza wazazi kutokana na mauaji hayo.
Wadau mbalimbali na mashirika wameombwa kuchangia kuazia dola moja na kuendelea.
Balozi Mutimura amezitaja akaunti zitakazotumika kukusanya michango hiyo kuwa ni
National Bank of Commerce
Embassy of Rwanda
Acc No. USD:012105025668
na
Acc no: Tsh: 012103016937
kampeni hii itaendeshwa kwa muda wa siku 100 ili kukusanya michango hii katika picha kushoto ni Usia Nkhoma afisa habari wa umoja wa mataifa.
Nakaaya Sumari akielezea wandishi wa habari juu ya wimbo wake wa 'I am in Africa' alioutunga maalum kwa ajili ya kampeni ya kusaidia yatima waliotokana na mauaji ya kimbari mwaka 1994 nchini Rwanda.
Ubalozi wa Rwanda nchini kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa wataadhimisha kukumbuka mauaji hayo kesho kwenye ukumbi wa Karimjee jijini.
Siwezi kuamini miaka 15 imepita kwa kasi.Nilikuwa ndo naanza Form one wakati mauaji haya yanatokea.Anyway,haya na matunda ya mambo ya ukabila.Hawa watu(Watutsi na Wahutu) sijui ni kwa nini hawapatani? Ni ajabu sana.Unakuta wako nje ya Rwanda na Burundi lakini chuki zao zipo pale pale au hata wale waliozaliwa nje ya mataifa hayo(R&B) wanarithishwa Upumbavu huu. Heri ya Generation yangu haikuzaliwa Burundi maana ingekuwa balaa.
ReplyDeleteJAMAA MAADILI MBONA TENA YANAZIDI TU KUPEPERUKA?
ReplyDeleteKWANI HUWEZI KUWA MWANAMUZIKI WA KIZAZI KIPYA MPAKA SHARTI UIGE MAVAZI YA KUTAMANISHA NA KUWA KIDUCHU UMEMWAGA RAZI?
MAANA KILA UKIONA PICHA MAGAZETINI ZA HAWA WA KIZAZI KIPYA BASI WENGI WAO LAZIMA WAWE WAMEACHA SEHEMU NYETI ZIONEKANE NA HADHIRINA, HII NDIO NINI? MAANA SISI WATU WAZIMA BADO HATUJAPATA UFAHAMU WAKE.
NA KAMA HIYO HAITOSHI, USISHANGAE HATA KIDOGO NYAKATI ZA SASA KUSIKIA MARA WANA KIZAZI KIPYA WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UHALIFU WA KITOTO KABISA..
MARA WAMEBAMBWA NA UNGA...
ALI MRADI NI SHOMBO TUPU WENGI WA HAWA WANAMUZIKI WA BONGO FLAVA.
SAMBAMBA NA KUWA NA MAPROMOTA, WAJITOKEZE WABONGO WASOMEE MASUALA YA USHAURI ILI WAWASAIDIE VIJANA HAWA, WENGI WAO WANAKOSA SENSE, PIA HAWA VIJANA WAWE NA JOPO LA WATENDA KAZI=KAMA WENZAO HUKO AMERIKA-ILI WAWAFUNDISHE NI KIPI KIVALIWE WAPI.
SIYO KUTUKALIA UCHI TU HATA KATIKA MIKUSANYIKO YENYE HESHIMA KAMA HUU WA KUCHANGIA WAHANGA.
ELIMIKENI NYIE VIJANA, ALA!!
mimi ndio nilikua namaliza form six.Time flies
ReplyDeletelakini ndugu yangu mbona hiyo blouse a little bit loose up there? nadhani hakukusudia kufanya hivyo. huyu namfagilia sana sidhani kuwa anaweza kuvaa nguo ya kuonyesha matiti kwenye siku kama hiyo kwa makusudi. labda hakuona masikini hiyo blouse ...hawezi kumruhusu stylist wake amvalishe uchi uchi kwa vile mambo yake yanajipangilia kweli siku hizi....
murakoze!
ReplyDeleteUS-BLOGGER)
ReplyDeleteMTAKATIFU YOHANA MASHAKA, HAPO VIPI INABIDI UJUMUIKE HUKO
US-BLOGGER
Tunapowaunga mkono wenzetu hawa ni vizuri tutumie muda huu kama watanzania kurekebesha mambo kadhaa yanayoanza kututenga kwa misingi ya makabila au dini zetu. Tukumbuke jambo moja ndugu zangu, sisi hatuna asili ya kubaguana, kila harufu ya ubaguzi inayokuja ni msukumo kutoka nje ya jamii yetu. Shime watanzania tukatae kwa nguvu zote kushawishiwa kuvuruga amani tuliyonayo. JK tuongoze baba, Mungu tusaidie.
ReplyDeleteWEWE! NAKAAYA !MAVAZI MENGINE UWE UNAJITAZAMA !MARA MBILI KATIKA KIOO!PIA UWE NA MSHAURI KUHUSU MAVAZI!NA SEHEMU ZA KUJIWAKILISHA NA MAVAZI YAKO! VINGINEVYO UNACHEMSHA,ENTERTAIMENT NI BIASHARA MAKINI NA INAENDANA NA MASWALA YA JAMII!!
ReplyDeleteSASA HIKI KIVAZI CHAKO KAMA KATUNI!FULANI AU KARAGOSI!!!
Kaka , please change jina la afisa habari wa umoja wa mataifa. Anaitwa Usia Nkhoma-Ledama ( Sio Usia Nkhoma any more) - confirm it on her business card.
ReplyDelete