Home
Unlabelled
JK mgeni rasmi hafla ya arobaini ya kiongozi wa CUF leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
İNAPENDA SANAA WAMEKUTANA NA WANAFURAHI.LAKINI ISIWE MWISHO WA KUKOSOANA KAMA İNCHİ İNAKWENDA MRAMA
ReplyDeletedua ni swala la kidini au chamasi kwamab dua ni swala ya kislamu,sasa inaingia vipi katika siasa hadi bendera mbili zinawekwa katika swala hiyo.halafu CUF wakiambiwa ni chama cha kidini watakataa. wanasisa wetu wanatakiwa kuwa makini, kwani shughuli hiyo kwa maoni yangu ni ya kidini zaidi na sio chama,wala haikuwa na haja kuvalia vazi rasmi la kiume la kiislamu, na kuweka bendera ya cuf na taifa. Nachelea kuamini pia kuamini kuwa kikwete kendsa kama raisi au mwislamu safi, kwani naona kama mwaliko wa kidini.
ReplyDeleteVIONGOZI KUWENI MAKINI NA MAMBO HAYA MADOGO ,LAKINI TAFASIRI YAKE YAWEZA KUWA KUBWA NA MBAYA.
Jamani nisaidieni.
ReplyDeleteHii staili ya kuvaa koti la suti na kanzu ilitoka wapi, kwa sababu suti ni vazi la kikristo na kanzu ni vazi la kiislamu.
Sasa inakuwaje hapo?
Kweli wanasiasa wanafki! Hebu ona hilo cheko!! Mhhhhh!!!
ReplyDeleteHuu ndio upinzani tunaoutaka TZ
ReplyDeletewatu washikane makoo kwenye kutafuta maslahi ya w waTZ lakini kwenye mambo ya msiba wawe kitu kimoja.
Sisi wote ni waTZ na ndugu.
Ninampa Rais wetu, heshima zote.
ReplyDeleteinapendeza sana kuona viongozi wetu wanakuwa kitu kimoja
ReplyDeleteHuyu ndyo mwanasiasa.Yaani hamjui tu,lakini picha kama hizi tukiziona tunapata relief kubwa sana ya hayo tunayoafikiria.
ReplyDeletePicha kama hizi zina-easy tension mioyoni mwa sisi wananchi kwa kuona,alllah!kumbe waha wanaweza kukaa na kucheka pamoja,inatia raha sana kwa kweli.
Pia nikiangalia hivyo vicheko,sioni kicheko cha kutengeneza hata kimoja "plastic smiles",bali vyote naona ni vile vinavyotoka mioyoni kabisaaa.Nimejisikia raha sana kwa kweli ingawa na mimi ni mzalendo ninayeishi chini ya dola moja kwa siku.The fact that I have been brought up in lovely,peacefully place Tanzania,it really gives me huge relief to see these kind of pictures.
.....Tanzaniaaa Tanzaaaaaaa....
..Nakupenda kwa moyo woteeeeee....
Mkulima-Kijijini Gezaulole.
HOW ON EARTH A PARTY FLAG BE EQUAL TO THAT OF OUR NATION, I KNOW THEY WOULD ARGUE SIMPLY THAT IS FOR KIKWETE BECAUSE IS A PRESIDENT,BUT MIND YOU THE NATION FLAG IS OT FOR A PRESIDENT IS FOR NATION, PRESIENT HAS HIS OWN FLAG IF THAT WAS LOGIC, I WOULD UNDERSTAND IF CUF PUT THERE A CCM FLAG WHICHIS EQUAL TO CUF FLAG PROTOCALLY, THIS ALL IS HATE ARCHITECTURE OF CUF AND LACK OF PROTOCOL. AFTER ALL THAT IS PRIVATE MATTER THERE IS NO NEED OF NATION FLAG ON TABLE.
ReplyDeleteINAPENDEZA KUONA RAIS NA WAPINZANI WALIWA PAMOJA KWENYE MAMBO YA JAMII HII NI MOJA WAPO YA ISHARA KWAMBA WAMEKOMAA KISIASA
ReplyDeleteHii ni furaha ya amani ambayo inaumiza mioyo ya wasiopenda amani wengi ndani na nje ya Tanzania.
ReplyDeleteNinavyojua mimi arobaini huwa inafanywa na familia naona sasa tunaenda kubaya. Kwa mfano huyo mzee angekuwa anaabudu mashetani, Je viongozi wa CUF wangefanya ibada ya kishetani? Viongozi wa kisiasa hawakatazi kwenda kwenye shughuli kama hizi ila ziandaliwe na familia na viongozi wa kidini. Watu mkipigwa vibao mnaanza kulalamika.
ReplyDeleteTANZANIA HATUNA VONGOZI WATAKAO TUONGOZA TUNAKO TAKA KWENDA.TUMEKOSA MSIMAMO KABISA NA HATUJUI IPI LA KUFANYA. NI WATU TUNAO TAKA KILA KITU NA KILA MAHALI. KANZU NA BENDERA ZA TAIFA NA SIASA WAPI NA WAPI.PENGINE BENDERA ILIMFATA RAISI MAANA BILA HIYO ETI SI RAISI LAKINI YOTE KATKA YOTE HATUNA VIONGOZI .
ReplyDeleteKUMBUKEN YALITOKEA NCHINI ALGERIA ?WATU WAIVIONA VYAMA VYA KIDINI WAKAVIACHA MWISHO WAO UKAWA NDIO HUO HADI LEO NCHI HAIJATENGAMA BAADA YA KUPOTEZA MAMILION YA WATU.
ReplyDeleteANGALIENI.
MBOWE ALIIWAKILISHA CHADEMA HIVI KARIBUNI HAI-MOSHI KWENYE SHUGHULI YA KUMTAWAZA ASKOFU.JEE CHADEMA CHAMA CHA WAKRISTU?
ReplyDeleteAnon wa April 04, 2009 8:57 PM acha hisia za kidini jua uhuru wa kikatiba.
ReplyDeleteAnon wa April 04, 2009 9:09 PM, kuanzia mwanzo mpaka ufunuo hamna mstari wowote unosema koti au suti ni vazi la kikristo bali kanzu ndo vazi la kikristo. We umetoa wapi dhana hiyo?
ReplyDeleteKumenti za mashambulizi ya kidini yatokanayo na watu wenye hisia za kidini na udini zimekuwa nyingi kwenye blog hii, michuzi ongeza makali.
ReplyDeleteTanzania tunajitahidi kwa demokrasia japo bado changa.
ReplyDeleteJAKAYA amesoma na seif sharif Hamadi university of Daresalaam darasa moja na walikuwa ni marafiki wakaribu sana
ReplyDeleteHallo, Poleni na hongereni sana CUF kwa kumpa heshima Kiongozi wenu mstaafu inaonyesha mnafaa kupewa nchi...kikwete umeonyesha Ustaarabu mkubwa sana (Civic) huo ndio utanzania tunaoutaka...CUF na CCM jifunzeni kwa kifo hicho kwamba kila moja atakufa ni vizuri mkakaa na ku-reconcile conflict zenu kabla mauti haijawafikia maana mtaulizwa
ReplyDeleteKumbe Tanzania yenye Muafaka wa Zanzibar inawezekana...
ReplyDeleteHata south africa sera za kibaguzi zisingeisha kirahisi kama De Klerk na Mandela wasingekaa meza moja na kukubaliana kuzikomesha. HONGERENI.
ReplyDeleteSasa limebaki ziara za RAIS na waziri mkuu zisihusishwe na msuala ya kichama
MIMI NAONA HAWAJAVAA KIISLAMU WALA KIKRISTO HILO VAZI NI LA WAHAYA NA BANGADA HUKO UGANDA.
ReplyDeleteSafi sana JK na Lipumba.hawa wenye hisia za udini ni wachovu.
ReplyDeletewiki iliyopita JK kachagua wakuu wa wilaya 15 wapya na waislam ni watatu tu.waliobaki wakristu.
jana kateua katibu mkuu na naibu mwanasheria mkuu wote wakristu.
nyie wakristu mnamsakama na udini mbona JK anawabeba nyinyi?
Akina mama wapo wapi katika uongozi wa vyama na nchi yetu? Wakati umefika tufikirie kwa dhati kabisa kuwa na Rais mwanamama. Kama mwanaume naamini akina mama ni wadau kamili katika uongozi na hatma ya nchi yetu.
ReplyDeleteKatika kanuni za bunge, hili nalo ni vasi rasmi. Yaani ukitaka kuvaa kofia basi lazima iwe na kanzu na koti.
ReplyDeleteUkitaka kuvaa kanzu tu hairuhusiwi. Halikadhalika, koti na shati lazima uweke na ulimi (tai) na kwa kinamama kofia eti lazima uvae na gloves!!!
kwa ufahamisho kivazi hiki pia ndio kivasi rasmi cha kiasili kabila la kihaya na waganda hata kabla ya kuingia uisilamu au kuja kwa warabu ambao walikuja na misuri tu. Kanzu ya darizi pia ilivaliwa na waarabu wa Omani waliokuja Zanzibar miaka mia mbili tu wkat tayari kanzu ilishamiri sana sawa na viwanda vya vya nguo vya Tanganyika kaskazini kabla ya mageuzi ya viwanda ya ulaya. Sijui ilikuwaje hivyo viwanda vya asili vilikuja kufa na hata hiyo kanzu kuwa adimu Tanaganyika.
Vazi la kanzu pia ni vazi la makabila kadhaa ya kibantu ya Afrika magharibi hasa wa hausa hata kabla ya kuja dini za mashariki ya kati. Sishangai kuwa sasa wanaona kanzu ni vazi la kigeni, maana hata kuku wakubwa tunawaita wa kizungu na nyumba nzuri ni nyumba ulaya.
Tunahitaji tusome historia ya nchi yetu ( na sio ile inayosema mtu wa kwanza kuuona Kilimanjaro ni Rebman)
HIVI YANAYO TOKEA ZANZIBAR HAMYAONI? NYIE NAFIKIRI HADI MUONE ALQAIDA YA TANZANIA NDIO MSEME KWELI WALISEMA. DINI NI KITU KIBAYA SANA KWENYE SIASA NA TUSIOMBE WATU WAAMINI CHAMA KWA SABABU YA DINI. TATIZO NI KWAMBA HATUTKI KUKUBALI ?NA HATA KAMA MIMI NI MUISLAM SIKUBALIANI KABISA MTU KUTUMIA MWAVULI WA DINI KUJIKUSANYIA WANACHAMA .
ReplyDelete