mpiganaji athumani hamisi akila tizi kwenye kituo cha Medcare jijini Johannesburg iliyo karibu na makao makuu ya shirika la utangazaji la sauzi SABC
wapiganaji athumani hamisi na paschal mayala wakiwa hospitali ya medcare leo. wote wapo hapo kwa matibabu kufuatia ajali walizopata nyakati tofauti
Mpigapicha wa Magazeti ya Serikali, Daily News na Habari Leo, Athumani Hamisi aliyelazwa Hospitali ya Milpark nchini Afrika Kusini kwa takriban miezi mitatu, ameishatoka katika hospitali hiyo kufuatia afya yake kuendelea vizuri ambapo sasa hapo amehamishiwa hospitali nyingine ya Medcare mahsusi kwa mazoezi ya viungo.
Mwandishi wa PPR aliyemtembelea Athumani Hamisi hospitalini hapo, alimshuhudia akifanya mazoezi ya viungo ikiwa ni pamoja na mazoezi ya kusimama kwa kwa msaada wa mashine maalum.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Athumani Hamisi amesema anaendelea vizuri ila amewaomba Watanzania wazidi kumuombea.
Ametoa shukrani za dhati kwa Rais Kikwete aliyemtembelea mara mbili, pia anaishukuru serikali na mwajiri wake kwa huduma zote anazopata ukiwemo ujumbe mahsusi toka Deily News ambao humtembelea kila mwezi.
Pia anaishukuru sana familia yake akiwemo mchumba wake aliyeko Nchini Marekani kwa jitihada zao kwake katika kipindi chote tangu kuugua kwake.
Mwandishi wa habari hizi pia alimshuhudia Mwandishi mwingine wa Habari na Mtangazaji wa kujitegemea Pascal Mayalla aliyekuwa hospitalini hapo kufanyiwa uchunguzi wa Afya yake kufuatia ajali ya pikipiki mjini Dodoma iliyovunja mkono wake.
Mayala ambaye alishatibiwa nchini India, amesema anaendelea vizuri kwa mkono uliovunjika kupona japo bado umepoteza fahamu.
Wakati huo huo inasemekana kwamba aliyekuwa Katibu Mkuu wa Rais enzi za Mwalimu Nyerere, Mzee Timothy Apiyo, pia amelazwa katika hospitali hiyo ya Milpark nchini Afrika Kusini. Taarifa kuhusu amelazwa tokea lini ama anasumbuliwa na ugonjwa gani hazikuweza kupatikana mara moja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Kwa nini Tanzania hatuwezi kutibu watu wetu?

    ReplyDelete
  2. Have faith brother, Mungu ndie wa kuombwa.

    ReplyDelete
  3. April 04, 2009 9:10 PM

    Ili Tanzania iweze kuwekeza katika modern healthcare sysytem na si katika kufanya mambo yasiyo na tija kama vitambulisho vya kielectronic, basi ipitishwe sheria kuwa Kiongozi yoyote serikali awe mstaafu au aliye madarakani akiumwa ni marufuku kukimbilia nje ya nchi kwa matibabu, abaki Tanzania na kupata huduma zote ndani kama ambavyo watanzania wengi walio masikini wanapata.

    Hii itawafanya kufikiria kuwekeza katika Modern healthcare system ili wasije kufia Tanzania wanapopata magonjwa. Vinginevyo wataendelea kujilimbikizia malia ili wapate pesa za kukimbilia nje wakiugua badala ya kuwekeza kwenye modern hospitals na kulipa vizuri wataalam ili kuwa retain.

    ReplyDelete
  4. Mkono umepoteza fahamu ????? Mbona mpya hiyo......

    ReplyDelete
  5. Mungu awajarie heri wapiganaji hawa ili warejee vitani tena.Kwani tunamis sana Mayalla.

    ReplyDelete
  6. Mtawatibu na madktari wa kudesadesa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...