katika siku za hivi karibuni aghalabu utakuta bendera ya taifa ikipeperushwa na wadau wengi na karibu kila sehemu kwa kile kinachosemekana na uzalendo wa hali ya juu wa kuona fahari kuwa na bendera ya taifa na kuipenda nchi. wadau hili limekaaje maana enzi za mwalimu mambo haya yalikuwa hakuna kabisa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Mambo ya kupeperusha bendera ya taifa kiholela hayo hayakuwepo enzi za Mwalimu na uzalendo ulikuwa ni wa hali ya juu kabisa. Hapa nadhani tunaiga wadhungu tu. Punde utaiona bendera kwenye bikini.

    ReplyDelete
  2. HUYU MTOA MAONI WA 8:29 ALIKUWEPO WAKATI WA MWALIMU AU KASIMULIWA TU?
    MAANA WADAU WENGI KAMA YEYE HUZUNGUMZA MAMBO HUMU KWA KUWA TU WALIMSIKIA FULANI AKIYAZUNGUMZA.
    NANI KASEMA WAKATI ULE WA AWAMU YA KWANZA TULIKUWA NA UZALENDO ZAIDI YA LEO?
    KWA MIFANO GANI?
    MIMI KWA MAONI YANGU TANZANIA ILE ILIJAWA NA WOGA! UZALENDO ULIOONEKANA KUTEKELEZWA KTK AWAMU ILE SANA SANA ULIKUWA NI MATOKEO YA KUOGOPEA CONSEQUENSES ZAKE, NDIO UKAKUTA TUMESHINDISHWA SANA JUANI UWANJA WA TAIFA KUMSIKILIZA MTU MMOJA TU, NA KUMPONGEZA KWA KILA ALICHOSEMA, HATA KAMA KILITUATHIRI KIASI GANI!
    MAGAZETI MAWILI TU, UHURU NA DAILY NEWS, MOJA LA SIRIKALI NA LA PILI LA CHAMA.
    USIKU HAUKUWA WA CHOMBEZA TAIM, BADALA YAKE NI "UJUMBE WA LEO", MAANA KABLA HAMJALALA KWANZA MSIKIE NENO LA MKUU.
    KWA KIFUPI TAIFA LILE LILIKUWA, ASHAKUM SI MATUSI, LA VIPOFU WATUPU, TUKIONGOZWA KWA MJELEDI, MAANA HATA UKIMWONA MGAMBO MBELE YAKO HATA KAMA HUNA KOSA UNATIMKA MBIO.
    WE UNADHANI NANI KTK TANZANIA YA LEO ATAKUBALI KUBURUZWA KAMA TULIVYOBURUZWA KTK AWAMU ILE? SUBUUUUTUUU1!!
    MIMI KWA MAONI YANGU SIKUONA UZALENDO KTK AWAMU ILE BALI VITISHO. VIONGOZI WALIKUWA WATAWALA, KIONGOZI MKUU WA NCHI ALIKUWA UNTOUCHABLE, UNCRITISIZED, IKULU PALIKUWA PAHALA PATAKATIFU, MEDIA ILIKUWA MFUKONI MWA WANASIASA, BUNGE LILIKUWA "HEWALLA MZEE", NA KWA KWELI UZELENDO MWINGI ULIKUWA NI MATOKEO YA WOGA, UMBUMBUMBU, NA UKOSEFU WA MWAMKO.
    TENA WE JAMAA USITUKUMBUSHE KABISA KIAMA KILE, NI EXPERIENCE INAYOTISHA MNO, KWA MFANO, KUONA JAMAA WAKIPACHIKWA SIFA YA "WAZURURAJI" KISHA WAKATUPWA GEZAULOLE NA KIBUGUMO NA HATIMAYE KUVAMIWA NA WANYAMA MWITU BILA YA MSAADA WALA MTU WA KUWATETEA AU KUNYANUA KINYWA KUWALAUMU WATAWALA.
    JAMAA KAMA HAMYAJUI MAMBO WAULIZENI ANAOYAJUA. EBO!
    Mndengereko, Ukerewe

    ReplyDelete
  3. lakini enzi za mwalimu pia ufisadi ulikua hamna.a gap btn masikini na matajiri ilikua sio kubwa kama sasa hivi....ahhh kupenda nchi hivi mbona kutamu

    ReplyDelete
  4. Kimahesabu tungesema kuna uwiano usiowianika wa uzalendo na upeperushaji bendera. Uzalendo ulipokuwa juu, upeperushaji bendera mitaani ulikuwa haupo. Kadri uzalendo unavyozidi kupungua ndivyo upeperushaji bendera unavyozidi kuongezeka.

    ReplyDelete
  5. Hakuna uzuri bila doa. It is true kuwa Enzi za awamu ya Julius kulikuwa na IMLA. Lakini baada ya kutafakari za naona kulikuwa na sababu tosha ya Imla ile. Kwanza tulikuwa ndio kwaza tunatoka katika ukoloni. Mengi tulikuwa hatuyajui. We needed a discipline. Leo Hii discipline hakuna. Ndiyo maana tumepata uhuru wa kusema na kufanya kila tutakalo lakini je matokeo yake si mnayaona? Manyanga'au yanavyotufanza? Ninakubaliana na mzee Karl Max katika dhana yake ya maendeleo ya jamii. Tulitoka katika Ujima na kuchupa katika Ujamaa, ukashindwa na sasa tunajibandika Ubepari ambao nao hatumo. Lakini suala la bendera sioni ubaya wowote kupepea kila kona hata T- shirt, I dont care hata chupi, paint nyumba rangi ya Taifa poa. What is the problem?

    ReplyDelete
  6. Naomba niruhusiwe kuichoma moto mafisadi wanapozidi. Ni aibu kuipepea wakati ufisadi unazidi...au tuanze kupeperusha ya China maana vitu feki vyote mjini vyatoka China. Au ya Marekani maana wanaume wazima na akili zao kila kukicha Obama, Obama..so stupid.

    ReplyDelete
  7. nani kawaambia bendera inapeperushwa kwa ajili ya uzalendo wala wanaopeperusha hawahusiani na siasa watu walianza kupeperush bendera kwa ajili ya timu ya taifa inapocheza na laiti ingekuwa taifa staz wanatumia bendera ya TFF ungeiona hiyo ndiyo inapepea fanya utafiti waulize wenye hizo bendera nini chanzo atakuambia niliweka labda siku staz inacheza na kamerun au ghana au timu ingine yoyote hicho ndio hasa kimefanya watu kupeperusha bendera na si kuwa wanaipenda serikali kihivyo

    ReplyDelete
  8. Hiyo imekaa sawa kabisaaaa!sisi tunaoishi nchi za wenzetu tunaona wanavyo tumia bendera zao..yaani kila kitu na hakuna matatizo yoyote..ni vizuri na kwa namna fulani inaongeza ile hari ya kupenda nchi(patriotism)na wala si kitu kibaya.Hata wageni wakija wanaweza nunua na kuweza kuitangaza nchi.kama tunataka ulimwengu kuijua Tanzania basi hiyo iachwe iendelee kama ilivyo mimi nina jezi yangu hapa ya Taifa stars huwa naiva kila mara hapa US na watu wanauliza hiyo ni timu gani na mimi kwa furaha kabisa nawaambia ni Taifa Stars....bado natafuta hiyo benedra niiweke ndani kwangu

    ReplyDelete
  9. JAMANI ANGALIENI HIYO PICHA VIZURI HIYO FOLENI DEFU NI YA NINI? MANAKE MINSHAKUWA MSHAMBA?

    ReplyDelete
  10. MTABISHANA SANA ILA KWA WENYE AKILI HASA WAHINDI IS JUST ANOTHER BUSINESS OPPORTUNITY.. KWANI KUPEPEA BENDERA WAKATI TAIFA STARS INACHEZA TUU NDIO UZALENDO?? HAIINGII AKILINI. MBONA SIKU YA YANGA NA AL AHLY HATUKUZIONA? NDIO KWANZA WASHABIKI WA SIMBA WAKASHANGILIA AL AHLY

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...