
Balozi wa Ireland nchini, Anne Barrington ( wa pili kutoka kulia) akizungumza kwa niaba ya Mabalozi wenzake na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa yakiwemo ya WB na ADB mbele ya Viongozi wa Serikali , akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika , Mohamed Muya (hayupo pichani) wa kwanza kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha SUA, Profesa Gerald Monela na kushoto kwa Balozi ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro , Said Mwambugu ambaye ni Kaimu Mkuu wa Mkoa huo

Mkuu wa Kitengo cha Sayansi ya Mimea na Kaimu Mkuu wa Idara hiyo wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo ( SUA), Dk Deodous Msogoya ( kushoto) akiwaonyesha baadhi ya Mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa juu ya uoteshaji mimea ya aina mbalimbali ikiwemo migomba na minanasi kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kimaabara SUA , ( wanne kutoka kulia ) ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirikia, Mohamed Muya, wakati wa ziara Ujumbe huo ulipotembelea maeneo ya utafiti wa mazao ya Kilimo ya SUA , Mkoa wa Morogoro.

Baadhi ya Mabalozi wa nchi za Ulaya hapa Tanzania wakaiwemo wawakilishi wa mashirika ya kimataifa juzi wakijadiliana mambo mbalimbali ya msingi ya sekta ya Kilimo mara baada ya kupata taarifa ya Uongozi wa Kiwanda cha kusindika matunda cha UNNAT cha Mjini Morogoro ambacho kinanunua matunda aina ya machungwa na mananasi kutoka kwa wakulima.

Kamishina wa Jumuiya ya nchi za Ulaya hapa nchini ( EU), Timothy Clarke , akiangalia miongioni mwa mbegu chafu kabla ya kufanyiwa usafi cha kitengo cha usafi wa mbegu cha Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) juzi wakati ujumbe wa Mabalozi ulipotembelea Chuo hicho katika moja ya kuangalia kazi mbalimbali za utafiti kuhusiana na sayansi ya mimea ya Kilimo.
Picha na mdau wa mji kasoro bahari John Nditi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...