Ni ukweli usiopingika kuwa angalau watanzania wanapata maoni na ushauri na kusikilizwa matatizo yao(ingawa informal) lakini tunafurahia na kujihisi wewe ni mwenzetu! Angalau unajua kila uchochoro wa jimbo lako na matatizo yake!
Nakukumbuka sana mwaka 2000 ulipoji introduce ukiwa na Waziri wa Mambo ya Nje enzi hizo.enzi hizo nilikuwa kidato cha tano Pugu sec.Kwa kweli ni viongozi wa chache wa mfano wako!
Naamini kwa style hii umejua furaha na machungu ya wananchi wako yakoje!
Labda kwa kifupi nitoe yangu yasiyonipendeza baada ya kutoa niliyofurahia!
Sijafurahia namna Serikali ilivyolishughulikia suala la DECI.
Haiwezekani watu waanzshi kitu haramu kwa miaka mitatu serikali inaangalia tu! Serikali inatakiwa ijiulize maswali
*kwa nini wananchi hawaendi kwenye mabenk?
*kwanini riba za kwenye asasi za fedha ziko juu?
*kwanini hakuna asasi za kifedha zilizo mbadala kuboresha maisha ya mtanzania wa kipato cha chini?
*kwanini huduma bora mfano makazi bora bado imekua kikwazo kwa mtanzania wa chini? ( nimewahi kusoma Thesis yako, housing cooperatives)
*nini kifanyike kurasimisha vilivyo vigumu kurasimisha?
Ni dhahiri wananchi walio maskini wamechoka kusikia ule wimbo wa “NO HURRY IN AFRICA”, hawaoni njia mbadala ya kutatua matatizo ya maisha yao!
Wengi bila kujua kuwa hiyo DECI sio rasmi wamejunga, wengine wakipeleka PENSHENI WALIZOLIPWA HIVI KARIBUNI ILI WAVUNE!
Matokeo yake serikali kupitia BOT imetangaza haijaipa DECI leseni ya kufanya hiyo kazi inayofanya! Zaidi kuwaambia kuwa katika DECI unahatarisha mtaji wako! Sipingi Tangazo hili, ila siungi mkono WAKATI uliotolewa!
NAJIULIZA,
*waliotoa Tangazo la kutoitambua DECI walikuwepo wapi kwa miaka 3 hadi watoe leo?
*kama walikua na shughuli nyingine, je ni ipi ya maana zaidi inayozidi inayogusa “majority”?
*inakuaje Dini na Biashara? Alafu tunaangalia tu?
*inakuaje iwe imetokea nchi jirani, watu wakalizwa kama kawaida alafu serikali isiwe makini kuangalia watu wake wanajiunga vitu gain?
MAONI YANGU
*Sio wakati muafaka kutoa Tangazo kama hilo!
*maelfu ya watu wamejiandikisha na kutoa mabilioni yao, tutumie busara zaidi kutatua mgogoro huu!
*tuangalie side effect baada ya “kuwaliza machozi ya damu” watanzania hawa wasio na hatia kisa tu eti ni “uzembe” kutowajibika kwa wachache kulize wengi!
ni vyema serikali iweke mkono wake, iwajibike kwa hasara yoyote inayoelekea kutokea kwani ni wazi ni uzembe wa serikali!
*kuwajibika kwake ni kurekebisha kasoro ( subsidize any financial loss, kasoro za kitaalamu) za asasi hii na kuirasimisha ili iweze kuendelea na kazi zake kawaida (iwe sustainable).
*tuna wataalamu wa uchumi na fedha, ni kweli hakuna sustainability kwenye ishu kama hii, wa kwanza hucheka hadi machozi na wa mwisho hulia hadi machozi, lakini through this concept we can conceptualize and develop do modeling to develop models in which such kind of revolving fund can be sustainable.
*tutumie mikakati shirikishi, wananchi walio wengi wanapenda kuachwa waamue wao na serikali iwape ushauri wa kitaalamu na kuwaelekeza na sio kupigapiga marufuku tu bila kutoa njia mbadala.
Naipenda nchi yangu,
Siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.
Nitasema kweli daima,
Fitina kwangu ni mwiko.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi
Mdau Mwana Bidii
Ni kweli uliloongea ni la maana. Na hii financial crisis halafu watu uwaache pesa zao zipotee,serikali inabidi ihurumie wananchi wake. maisha bora kwa Mtanzania yataendelea kuwa ndoto.
ReplyDeletemmmh!
ReplyDeletecaveat emptor!
ina maana hamjasikia NICOL wala UTT kwa uchache.. na CRDB inakuja?
Pamoja na maoni yako kuwa mazuri, lakini jambo kubwa ambalo watanzania hatutaki kulisikia ni mtu kuwajibika kutokana na maamuzi na vitendo vyake. Haiwezekani kuwa leo hii mtu anafanya maamuzi yake binafsi mabovu kwa kutegemea serikali itaiingilia kati imwambie kuwa maamuzi yako ni mabovu, hiyo serikali haijaundwa hapa duniani.
ReplyDeleteWale wote ambao wameingia katika DECI walikuwa na akili timamu na waliridhika na kupeleka hela zao. Sasa iweje tunaigeukia serikali kwa kuilaumu, au tunataka kuhalalisha kutowajibika kwetu kwa kuisingizia srikali?
Wananchi inabidi waamke watambue kuwa kila mtu atawajibika kwa vitendo na maamuzi yake atakayoyachukua. Vinginevyo kama wanaona kuwa maamuzi yao yalikuwa sahihi na sasa wamelizwa basi waende katikka vyombo husika vya sheria wapeleke malalamiko yao huko.
Mimi binafsi sina huruma na wazembe ambao wanataka short cut ya kujipatia pesa bila ya kufanya kazi. Endapo watu wa namna hii wanapeleka fedha zao wasipokujua na bila ya kuumiza vichwa basi hakuna benki hata moja itakayoweza kuwakopesha wazembe hawa.
Ninawashauri next time walau wajaribu kuumiza vihwa kwa kufanya utafiti wa kina wa namna gani pesa zao zitaweza kuwa salama.
There's no need to justify uzembe dhidi ya huruma and don't expect the government will do everything for you.
Mtoa mada umechemaka kidogo pale unaposema kuwa serikali inapiga marufuku bila ya kutoa maelezo mbadala. Si kweli kwamba serikali haijafanya kazi yake jkatika hili. Serikali imejitahidi kuweka miundombinu kama vile ya uanzishwaji wa SACCOS, UTT Fund, IPOs nk.
ReplyDeleteSasa unaposema serikali haijaonesha njia mbadala una maana gani?
Kuna soko la hisa, unaweza kununua hisa, unaweza kuweka na kukopa kwenye saccos, unaweza kununua hisa kama zimetegwa kwa ajili ya public (IPO). Maeneo ni mengi fanyeni utafiti kabla hamjavaa mikenge.
Ni kweli kabisa maisha bora kwa kila mtanzania bado ni ndoto hasa pale ule usemi wa "ALIYESHIBA HAMJUI MWENYE NJAA" unapoendelea kuonekana kila siku, sasa hapo wanapotaka kuwagusa watanzania kipindi hiki cha kampeni ya 2010, tunapaswa kuliangalia vema na kwa umakini sana swala hili, wananchi wanatapatapa kutafuta unafuu wa maisha na kujikomboa katika umaskini bado kuna wanaowavuta mashati kuwarejesha nyuma. Yale maneno ya hekima a mwalimu Nyerere alisema AFADHALI TUWE NA CHAKULA KIDOGO TUKAGAWANA KIDOGOKIDOGO KULIKO KUWA NA CHAKULA KINGI TUKAANZA KUGOMBEA. watanzania tuwe na fikira mpya na waweza timiza wajibu wako, mdau sema sema usiogope se.
ReplyDeleteKwakweli inasikitisha! nadhani nilikuwa mtu wa kwanza kugundua hatari zilizomo ndani ya Deci. Nimemaliza chuo kikuu cha Dar es salaam mwaka jana mwezi wa tano, lakini kabla sijamaliza nakumbuka tulipewa assignment na Lecturer wetu mmoja ambaye sipendi kumtaja. Assignment hiyo ilikuwa inatutaka tupite kwenye mojawapo ya hizi financial institutions tufanye research ni jinsi gani wanavyo operate chini ya sheria za BOT. vitu vya kuangalia vilikuwa katika areas za deposit taking, investments, Funds tranfer, Risk management, the way wanavyo weza ku-match liabilities and assets etc.
ReplyDeleteNilikwenda DECI kwa sababu ilikuwa ni jirani na sehemu ninayokaa, nilikwenda na confidence zote huku nimebeba vitambulisho vyangu pamoja na introduction letter niliyopewa chuoni. Nilikutana na jamaa mmoja nikajitambulisha vizuri, nikampatia documents nilizobeba pamoja na kumueleza azma yangu ya kutaka kufanya ka-research kadogo.
Huwezi kuamini jamaa alinitoa mkuku hata sikuamini, tena kwa kashfa akaniambia "hatuhitaji mtu kuja kufanya research si tuna jinsi zetu za kuji-evaluate". Tunamtegemea Mungu zaidi tukipanda mbegu tunamwomba Mungu baadaye anasaidia afu afu tunavuna, kwa hivo tupo kiimani zaidi. Duh! jamaa aliharibu theory zangu zote nilizokuwa nazo kichwani kwani chuo sikufundishwa kwamba ukiwa una-operate hizi Microfinance ukiwa na imani utapata pesa na utaweza kulipa watu riba. Kwenye uchumi pia nilijifunza "no free lunch".
Sasa nilikuwa najiuliza na mpaka sasa najiuliza ni nature gani ya business ambayo inafanyika DECI ambayo inawezesha watu kuvuna kiasi hicho kikubwa cha pesa na huku ikaendelea ku-cover operating expenses? Haiingii akilini hata kama wana-compensate na sadaka!
Kuna wingu zito limetanda DECI na hivo mimi binafsi ninashukuru serikali kutoa tamko hili japo imechelewa kufanya hivo, nasema hivo kwani DECI ilikuwa ni kivutio cha watu wengi na wengi walikuwa na plan za kujiunga.
Dear Michuzi na wanajamii wote!
ReplyDeleteNaomba nimpongeze sana MWANA BIDII kwa (maoni ya kitaaluma)professional advise zake katika swala hili la DECI. Kwa kweli serikali itakuwa ya kwanza kulaumiwa kama haitachukua professional measures ku-make professional decision on this issue.
Mwana Bidii na Michuzi kaka yangu, nina mambo mawili nataka kuelezea, ambayo bado yananichanganya kuhusu DECI.
Kwanza Mimi mwenyewe, mwaka jana 2008 mwezi wa nane, nilitaka kushawishika kuingia DECI lakini nikaona bora nicheki kwanza uhalali wake. Nilipiga simu BOT, na baada ya simu yangu kuwa transfered mara kibao, nikaongea na Mkuu wa kitengo kinachoitwa "Non Banking Institutions" kuulizia uhalali wa DECI. Kweli hakuwa anaifahamu DECI, na wala haikuwa imesajiliwa kwenye kitengo chake. Nilijitahidi sana kujieleza na kumwelezea jinsi inavyofanya kazi kwani nilikuwa nimeshailewa vizuri sana na hasa baada ya kuongea kwa simu na viongozi wakuu wa DECI. Yule bwana alisema kisheria, kukusanya pesa from the public kwa ajili ya collective investment ni makosa kisheria kama hiyo public sio wanachama wa kundi fulani.Pia alijitahidi kunielezea saana madhara yake.
Pili, nili-google kwenye mtandao kuhusu DECI tanzania, nikaona huko mkoani Tanga last year walifungua branch, na mkuu wa wilaya ndiyo alikuwa mgeni rasmi na alitoa speech ya kushawishi watu kujiunga ili wawezeshwe!... jamani!
Jambo jingine linalonitatiza ni kwamba, DECI ina branches 37 country-wide, hizi ni zaidi ya branches za CRDB Bank, na bank nyingine kubwa... Inakuwaje mpaka leo isijulikane inafanya biashara haramu??....Haiingii akilini wadau..
Maoni kwa Serikali, BOT na CMSA.
Kwanza.Wanahabari ni watendaji wazuri ambao taaluma yao hivi karibuni imetumika ipasavyo kuibua issues Tanzania, lakini tusiwaachie watuongozee nchi kwani baadaye madhara yanaweza kujitokeza!,Swala hili limeanzishwa na wana-habari! tujifunze kutokana na makosa kibao tuliyofanya kwa EPA, Richmond, DOWANS na swala zima la UFISADI ambapo pamoja na kuwa na wataalamu waliosomeshwa na pesa kibao,waandishi ndo wanawafanyia kazi zao, nao wanalipwa pesa kibao! Tusiwachoshe!
Pili. Tutafute wataalamu ambao tunao wengi sana, wafanye professional evaluation ya DECI, watoe professional advice ambayo haitamwathiri mwekezaji hata kidogo.
Tatu. Ukiangalia wingi wa wanachama, kweli utajua watanzania wana shida ya pesa/maisha magumu, na wala sio kuwa na tamaa kama inavyoripotiwa, serikali itafute njia mbadala, mabilioni ya kikwete yamefeli!!!!!
BOT na CMSA wawajibike kama wawekezaji watapoteza amana zao, kwani tahadhari wanayotoa sasa ilitakiwa kutolewa toka DECI walivyofanya licence application wakakosa miaka mitatu iliyopita.
Naipenda Nchi Yangu,
Naheshimu Utaalamu na Uongozi.
Wataalamu msaidieni Rais wetu ana NIA NJEMA WAANANCHI.
Ni wakati umefika kwa wataalamu kuacha Ofisi zao na kutoka nje, kuona 'Real Life Out there!
libeneke la DECI: Wajinga ndio waliwao???
ReplyDeleteWarning Guys!
That's known as pyramid scheme. Very few people get rich, the ones who run this idiotic scheme. It has made a lot of people more poor. It operated in South Africa, Zimbabwe, Germany and UK. In actual fact its a criminal offence in UK and if caught you end up in Jail.
Unaweza google au nenda wikipedia na search Pyramid scheme. Mchongo wenyewe wa kuingizana mjini inakuwa kama ilivyoelezwa hapo chini
--------------------------------------------------
1: Kijiji kina watu 10000
2. Watu wa 10 wa kwanza wasio na fedha wanaanzisha mradi wa DECI. Wanasema kujiunga nao ni Shs. 200,000Watu 1000 wanajiunga kwa kutoa Tsh200,000 kila mmoja. (Kijiji kinabakia na watu 8990. Kwa kiyo Mtaji wa kwanza ni: Tsh. 200,000,000 (za wale watu 10)Hawa wanaambiwa wasubiri miezi minne ili “wavune” faida.
3. Wanatangaza na watu wengine 1500 wanajiunga kijiji kinabakiwa na watu 7490Watu wale 1500 wanaleta mtaji mpya wa milioni 300,000,000 Miezi minne inapopita wale 1000 wa kwanza wanalipwa fedha yao milioni 200, na kila mmoja anapata “faida” ya laki moja moja hivyo kila aliyeingia na laki mbili miezi minne anatoka na laki tatu!
4. Wanaingia watu wengi zaidi sasa nao wanafikia 2000 nao wanataka haya mavuno! Kijiji kinabakiwa na watu 5490 ambao sio wanachama.
5. Wale watu 2000 wanaingia na mtaji wa 400,000,000. Sasa hapa ndipo kuna kitu cha kuangalia vizuria. kuna watu 1500 ambao wanatakiwa kulipwa laki mbili zao (kwa jumla ya milioni 300 za mbegu). Lakini pia wanatajia kupata kila mmoja laki moja zaidi kama faida.b. Hivyo pamoja na kiasi hicho unatakiwa mradi wa milioni 150 zaidi kama faida ya kundi lile la pili.c. Kiasi hicho kinatolewa kwa wale waliokuwa na milioni 400 na hivyo kufanya wale wanaoingia na milioni mia nne kimsingi kuwa wamekingia na milioni 250! (hilo si tatizo kwa sasa). d. So wale wa kundi la pili wanaondoka na wao na laki tatu tatu kwa furaha ya “mvunaji”
6. Hivyo kampuni yetu inaanzisha recruitment drive nyingine na watu wengine 3000 wanajiunga na kampuni yetu hii ya mavuno. Kijiji kinabakiwa na 2490 ambao wengi wao wanaonekana kuwa ni wanachama wa JF!! Hao nao wanaingia na mtaji wa 600,000,000!
7. Hivyo muda umefika wa kuwalipa walioingia na milioni 400! So wale milioni mia nne kwanza wanalipwa “seed money yao) ambayo ni kiasi hicho hicho. Lakini wanataka faida yao ya laki moja moja kila mmoja. - Hivyo zinahitajika milioni 200 nyingine na hivyo kuchukua kabisa mtaji wa wale wa milioni 600, kuwalipa wao na hivyo wale wa milioni 600. So wale wa milioni mia nne wanaondoka kwa furaha kwani wamepata fedha yao.
8 Wale wa milioni mia sita (ambao ni wengi zaidi – 3000) na wenyewe wanaambiwa wasubiri fedha zao hadi mwisho wa miezi minna. 9. Sasa recruitment inaenda na kuwashawishi wale 2490 waliosalia kijijini kujiunga ili “wavune. Nao wanaingia na mtaji wa 498000! (mara moja tunaona kuwa wanaingia na kiasi pungufu. Kampuni yetu ifanye nini basi; 10. Kampuni inawashawishi wale waliokwisha pewa mavuno yao kuzizungusha fedha hizo hizo tena kwenye mfumo huo. Kwa hiyo wale wa 1000, na wale 1500 na wanatakiwa kuzungusha fedha zao humo kwa humo.
NOW THIS HOW THE SYSTEM COLLAPSES
SCENARIO ONE:
a. Baada ya wale 2490 kuingia na kulipa milioni 498 wale wa milioni 600 watajikuta wanapungukiwa Sh 102! Bila ya fedha kuzungushwa tena kundi la milioni 600 wataanza kulalamika.
b. Wakati hao wanaanza kulalamika kundi lile la 2490 linasubiri kiasi walichoingia nacho (kwa maana angalau waliokwishalipwa awali idadi kama yao wawe wamzungusha tena fedha). Na pia wanasubiri milioni 249 kama faida! (kwa maana ya kwamba wanahitajika watu wengine kama 50 hivi kujiunga kuweza kuzalisha hiyo faida.
SCENARIO TWO:
a. Hii inategemea idadi ya watu ambao wako tayari kuzungusha fedha zao ndani kwa ndani. Kinachofanyika hapa ni saikolojia ya fedha. Wakikupa laki moja faida na wakakuambia uziingize tena kwenye system itabadi urudishe laki mbili kwao tena, na wewe unabakiwa na laki moja! Katika mfano halisi wa DECI ni kwamba wanakulipa laki tatu, na unaweza kuzirudisha kwa mafungu laki mbili mbili, hivyo utarudisha kwao zile za kwako (laki mbili) za kwao (laki mbili) na wewe unabakia na laki moja! Ulichofurahia kimsingi ni wewe kuwa na “laki tatu” kwa muda fulani, siyo kuzitumia.
b. Hili hata hivyo linatabia ya kuchosha huwezi kuwa na fedha usiyoitumia! Hivyo collapse ya pili itatokea pale watu ambao wamekuwa wakizungusha fedha zao huko kwenye kampuni watakapoamua kuziondoa kwenye mzunguko! Kwa maneno mengine wale 1000, na wale 2000 na wale wa 3000 watakapoamua kuondoka na fedha zao wale wa mwisho 2490 watajikuta wameliwa karibu milioni 500!
Hahahahaaa, Hapo wadau mkilizwa kwa kuingia mkenge huu kicha kichwa msianze oooohh hamkutustua mapema, mara ooooohh JK mbaya kuruhusu haya, mara oooooohhh kwa nini serikali isipige marufuku kama ilivyokuwa Kenya. Eh Kalagheni baho, ila mnaambiwa hii ni kanyaboya mwenye macho asikie na mwenye masikio na aone!
Nimefurahi sana kusoma maoni ya Watanzania wenzangu kuhusu hii issue ya DECI. nimefarajika kwamba watanzania wengi wanaofuatilia suala hili wanatoa maoni mazuri hata kama wanatofautiana.
ReplyDeleteKwa maoni yangu, suala la DECI ni moja ya kielelezo cha matatizo mengi yanayoikumba jamii yetu. kupitia suala hili, unaweza kuona ni kwa namna gani taasisi au asasi za Kifedha zilizopo nchini haziwafikii watu wengi kwa kuwa na masharti magumu ya mikopo. hivyo kwa wale wanaoilaumu serikali kwa hili nakubaliana nao kabisa. hata kuwa na akaunti kwenye mabenki yetu utadaiwa mpaka barua ya balozi na vitu vingi vya kijinga!
mfumo wa mikopo ndio kabisa usiseme. ni watu wangapi wanaweza kukopa katika benki za Tanzania?. watu wamelalamika, na wataendelea kulalamika, nani anasikia?
Pili, Suala la DECI linaweza kuwa pia kielelezo cha ujinga walionao watanzania. kwa jamii iliyoelimika kidogo (hata kama watu hawakwenda kabisa darasani) huwezi kutafuta njia ya mkato ya kupata utajiri. huwezi kujiunga na taasisi inayoahidi kukupatia faida kubwa kwa muda mfupi bila kujua faida hiyo inatoka wapi! dhana hii inakwenda sawa na wale wanaokwenda makanisani kwa sababu ya kuamini miujiza! na kwa sababu DECI imeanzishwa na watu wanaohubiri dha hii, ni rahisi kuuona dhahiri ujinga wa watanzania hawa. tusaidiane kuwaamsha hawa wenzetu waliolala, kwamba ukitaka kufanikiwa hakuna njia ya mkato. ni kufanya kazi tu. kwamba ni kazi tu ndiyo itakayobadilisha maisha yako. unaweza kupiga porojo za kisiasa, unaweza kuingiza imani yako ya kidini kwamba ukimwomba Mungu utapata kila kitu, nk. lakini nakwamba hakika, bila kufanya kazi, umasikini wetu hauwezi kuondoka.
tatu, Suala la DECI ni kielelezo cha uozo wa serikali yetu kushindwa kufuatilia na kuwalinda raia wake kwa kusimamia sheria zilizopo. uzembe huu ndio unaoleta maafa kila siku katika nchi hii. haiwezekani katika nchi ambayo inafuata utawala wa sheria kikundi kikaanza kufanya biashara ya mabilioni (huku kikilipa kodi?) bila kuulizwa kama wana kibali cha kufanya kazi hiyo. nchi hii ina ugonjwa hatari sana, wanasiasa wanajua sana kutunga sheria, lakini hawajui kabisa kusimamia sheria wanazotunga!tukumbuke, ni kwa kufuata sheria na taratibu ndipo sisi binadamu tunaweza kutofautishwa na wanyama. hata kile kinachoitwa 'Ustaarabu" hakina maana nyingine zaidi ya kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizokubalika. tatizo kubwa ambalo litaifanya hii nchi kuwa kama pori la wanyama siku si nyingi, ni watu kuachiwa kufanya kila kitu bila kuulizwa kwa nini wanafanya hivyo. kila mtu anafanya atakavyo kwa sababu anajua hakuna atakayemwuliza. kwa hiyo hata hao viongozi wa dini hawakuwa na kosa kuanzisha biashara hata bila ya kuwa na kibali. wanahitaji kibali cha nini wakati wenzao wa Sabato masalia wamekwenda uwanja wa ndege wakitaka kusafiri kwenda ng'ambo bila kuwa na tiketi au passport, na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa?, kwa nini wahitaji kibali kama wanashuhudia wamachinga wanapanga bidhaa zao katikati ya barabara na hakuna mtu anayewauliza?
Tunaelekea pabaya sana. hakuna majibu rahisi kuhusu hatima yetu kwa sababu mfumo wote umeoza. tunatakiwa kuubomoa na kuanza kujenga upya.
Kweli kaka ulichokisema ni point,hii serikali yetu ni fitina na majungu na ufisadi umewatawala ina maana miaka yote mitatu hakujua kama kuna DECI?Vikongwe vya watu vinaweka ndio vinaishi then mnasema sio halali huyo kikwete anaweza kuwalisha na huku bado anawadanganya eti maisha bora kwa mtanzania kwa lipi?Acha DECI wawape watu maisha ikaifa basi hayo ni matokeo.
ReplyDeletewewe anonymous wa April 09, 2009 10:38 AM, mbona unafuka na kuchemka vibaya????? Hivi serikali unaitaka iwajibike kny DECI tuu?? Vp mambo mengine ya msingi zaidi km kuwajibika kny miundombinu, kuwawajibisha kikamilifu wahujumu uchumi, kuwajibika kny manunuzi ya vitanda mahospitalini etc. Wee umeona iwajibike kny DECI tuu !!
ReplyDeleteAma kweli bongo na watu wake km wewe apo tambarare...
People don't hate don't hate please.
ReplyDeleteLazima mjue kwamba maisha ni piramidi. Ndio maana kuna vigogo wanalamba milioni 10 kwa mwezi wakati wenzangu na mie tunaisotea hiyo milioni 10 kwa mwaka au miaka kadhaa.
It's called FOOD CHAIN. Kwa system za kawaida aliye chini siku zote huwa analiwa.
Ila kwa system ya DECI hata wa chini naye ana nafasi ya kula bingo.
Kuna SACCOS uchwara kibao hapa nchini ambazo zinadai zinawakomboa maskini kwa kuwapa mikopo yenye riba 48% mpaka 60%
Pia SACCOs hizo uchwara wanajifanya hawajui kabisa maana ya TIME VALUE OF MONEY.
Ukikopa ukazungusha pesa na kulipa deni lote ndani ya mwezi mmoja utadaiwa riba kiasi kile kile kama mwingine anayelipa deni baada ya mwaka mmoja.
Huo ni wizi wa mchana kweupeee na BoT na Financial Intelligence Unit wanafumbia macho suala hilo.
Lakini DECI imeshatajirisha watu. Kama kuna watu watapoteza pesa DECI sio ishu ya ajabu maana mfumo mzima wa pesa ndio ulivyo, kwamba hatuwezi wote kuwa na pesa la sivyo hiyo pesa itakuwa haina thamani.
Mwananchi maskini anayenyonywa riba ya 48% mpaka 60% na SACCOS sometime mpaka anashindwa kulipa anakuja kunyang'anywa makochi na vitu vingine vya ndani huyo na yeye anaibiwa.
Amepoteza pesa, na hana tofauti na mtu atakayepoteza pesa kupitia DECI.
Sema zikipita propaganda za "kisomi" na "kitaalamu" somehow watu wanadanganyika na faraja bandia kwamba kuibiwa na SACCOS ni sahihi.
Wake up guys. This is Bongo. Akili kumkichwa.

a.Inasikitisha viongozi wa dini eti wanapaayuka na kutumia jina la mungu kutetea utapeli wa DECI au na wao waishalambishwa?
ReplyDeleteb. Inasikitisha kuona gazeti kama Mtanzania Jumapili 5 inaunga mkono utapeli wa DECI na kuandika makala kwamba eti i mkombozi wa maskini. Huu ni utapeli tu. Lakini gazeti la fisadi likiunga mkono utapeli labda haishangazi sana kama inavyoshangaza viongozi wa dini kuungamkono utapeli wa DECI.
c. Ukimya wa BOT, CMSA na serikali kwa ujumla na kushindwa kwao kuchukua hatua kwa miaka mitatu kunatisha. Maana yake hakuna uwajibikaji. Na hivi sasa muda umekwenda mno kutoa tahadhari maana wengi tayari watalizwa tu na matamshi ya sasa yanashindana na ya wale waliotangulia ambao katika pyramid/ponzi scheme lazima wanufaike kwa gharama ya wanaofuata.Wasichojua wanaofuata ni kwamba watalizwa maan pesa zao zinawalipa waliotangulia.
d. Ni vema tuchunguze vile vile je katika vyombo hivi vya usimamizi na serikali pia kuna watendaji walishiriki na kunufaika katika DECI? Kama ndiyo, inawezekana ndiyo maana hawakuchukua hatua mapema.
e. Kumbukeni ulikuwapo upatu kama huu ulifanyika miaka si mingi sana enzi za rais Mkapa na vigogo (hasa wake zao)walishiriki kama waanzilishi na bila shaka walionufaika vile vile- swala likaisha hivi hivi. Si jabau basi kwamba sasa Ponzi schemes zinazidi kuibuka. Maana zilipoibuka kwanza hakuna hatua zilizochukuliwa sasa ukichukua hatua sasa si watu watauliza na zile Ponzi sceme za awali imekuwaje? Patamu hapo!! Michuzi usiibanie hii tafadhali!!!!!!!!!!!!!
e.Anaesema DECi irasimishwe anaweza kujibiwa kwa namna mbili.Kwanza ita=kuwa ni aibu kurasimisha utapeli. Pili labda utapeli umekwish rasimishwa maana tumeona ya Kagoda, EPA, Green Company na kadhalika na pesa zimechotwa kwa saada wa maafisa wa serikali mna vyombo vyake na hakuna kilichotokea au hatua zinachukuliwa kwa kusuasua na kwa kuchagua sana ni yupi achukuliwe hatua na yuoi asichukuliwe hatua.Ni vigumu kwa serikali hiyo hiyo moja kuichukulia hatua DECI ya litapeli lakini isiichukulie hatua Green Company au Kagoda za kitapeli.
f. Ni muhimu serikali ichukue hatua haraka iwezekanavyo, sasa hivi, japokuwa imechelewa sana, ili watu watakaolizwa asiendelee kuongezeka.
NIMESOMA MAONI YA WOTE WALIOPITA AN MIE NAKUBALIANA NAO ILA NAPENDA KUONGEZA TU MSIMAMO WANGU KUHUSU NAFASI YA SERIKALI KATIKA HILI. SERIKALI KAMA MLEZI WA WANANCHI KUPITIA TAASISI ZAKE INA WAJIBU WA KUJUA KILA KITU KINACHOTOKEA NA PIA KUWAELIMISHA WANANCHI MADHARA YA VITU KAMA DECI NA MENGINEO.
ReplyDeleteILA TATIZO TUNA VIONGOZI AMBAO WANALIPWA MISHAHARA MIKUBWA LAKINI HAWAJUI "JOB DESCRIPTION" ZAO NA WANAFANYA KAZI KWA MAZOEA NA MTINDO WA ZIMAMOTO.
POLENI WOTE MLIOJIUNGA NA TAASISI HII YA DECI.

WATANZANIA TUACHE UJINGA WA KUFANYA UZEMBE ALAFU TUILAUMU SERIKALI. WEWE UNAONA HATARI NA KWAMBA HAKUNA NAMNA UTAPATA FAIDA ASILIMIA MIA KWA KUZUNGUZHA HELA BADALA YA KUZALISHA. WOTE TUANJUA PYRAMID SCHEMES NA JIRANI ZETU KENYA WAMEONJA HASARA. SASA TUNALILIA KUENDELEA NA UJINGA. BENKI KUU INATUONYA, SERIKALI INASEMA NI SCHEME WRONG. HEBU TUWE SERIOUS. TUNAHITAJI KUWA RESPONSBLE KWA MAAMUZI YETU NA TUSIFANYE UJINGA ALAFU TUNATAKA SERIKALI ITUOKOE. WANAOWEKA FEDHA DECI WAACHWE WAENDELEE NA UJINGA WAO NA WAAMBIWE HIVO MTOTO AKILILIA WEMBE MPE TENA IKIWEZEKANA MPE MBILI
ReplyDeletesitaki ata kuamini!!
ReplyDeleteyani miaka yoooote iyo leo ndo BOT mwaibukia wapi?
"'\*$<<;" zenu sana nyie wote.
yan ni mara 100 DECI iendelee tu,kuliko hii mibenki yenye wizi mkubwa ajabu kwa kumkaba mwanainchi duni,
yan me nshafikilia ata kutoa pesa yooote benki,zibakie tu mshahara unapopita,shenzi taipu
ila ktk aya yote na Kristo asimame hakika,if DECI ni wizi basi tujue kuna watu fulani ktk mamlaka ya serikali hii wali-wezika pamoja na DECI,uwezi kaa kimya miaka 3??yan newz ya ajabu sana.
pili,sijaelewa vizuri ina maana imeshapigwa stop na ofisi zake kufungwa na serikali?au ni angalizo tu na watu waendelee cheza?
Ukianzisha pyramid scheme unafungwa marekani. bernad mardof anatarajiwa kufungwa miaka 150 jela. alianzisha pyramid scheme ya dola billion 50. tofauti ya bernad ni kwamba liadanganya watu na ndo maana anafungwa.
ReplyDeletetanzania lazima iwe na sheria za kuwalinda wasio na elimu na ujuzi. walionzisha hii kitu wanajua kabisa wengi wa wanachama hawajanda shule. waanzishi wanatakiwa kwenda jela for misleeding public (force promises).
nilikuwa arusha tech rafiki yangu aliweka hela kwenye uwizi kama huu mwaka 1999 hakuambulia chochote. binamu yangu naye aliweka laki unusu mwaka 1998 hakuambulia kitu. hii siyo mara ya kwanza kwa huu upuuzi kutokea bongo. watu wafungwe miaka ya kutosha wakaolewe jela ndio wajifunze. mnalalmika ufisadi wa wakubwa lakini kuna wajanja wengine majirni zako unataka kuwalinda.
"Haloo we Mtanzania!..Hii ni DECI vs Mamilioni ya Kikwete..Unachagua ipi?"
ReplyDelete1.Naomba tusichanganye mambo.Kwenye UTT na (CRDB Bank hivi karibuni) unapotoa pesa unapata certificate ikionyesha unamiliki hisa katika kampuni fulani. Certificate ya UTT ni kwamba ni cocktail of shares in different companies.You actually own part or parts of a business ambayo wewe ni mdau katika hasara au faida- zipo kampuni ambazo zinafanya biashara zinazoeleweka na wewe ni mwanahisa.Inapopata faida basi management inaweza kuomba ridhaa ya bodi kutoa gawio kutokana na profit na kiasi kingine kiendelee kutumika au kiwekezwe upya tena katika hiyo biashara.Lakini sasa ukweli wa mabo ni bila kauli za wazi na elimu kwa umma kutolewa na BOT na CMSA haraka na kwa wakati basi nji rahisi kwa layman/wananchi mwa kawaida kutoelewa na kwa hiyo hata inapotokea fursa nzuri ya kuwekeza akaogopa- maana alishaumwa na nyoka basi akiona mjusi........ This is proof if ever it were needed kwamaba we n=rushed into capitalism without preparing and educating our people.So in the current rush of confusion we will be taken advantage of by wajanja wa kigeni na wa hapa hapa na saa zingine wajanja hawa watashirikiana (k.m. mikataba ya madini)!
ReplyDelete2.NICOL kwa kweli sijui vizuri. Mimi nadhani ni muhimu ikaanza kununua hisa au kubuni biashara na mihela iliyokusanya.Kasi yake ya investment haifurahishi- huwezi kukusanya mihela alafu ukaweka kwenye fixed deposit tu.Lakini nina hakika siyo pyramid scheme maana si kwamba wanaovuna wanavuna kutokana na pesa walizoweka wengine waliyowafuata.In fact hawajawahi kutoa dividend.
3. Ila kinachotisha zaidi ni kwamba wananchi hawaamini taasisi za umma.Pamoja na kwamba BOT imechelewa kutoa tahadhari BOT is right kutoa tahadhari na kwa kweli ilitakiwa ichukue hatua kali zaidi ya kuzuia kabisa na kuadhibu kisheria ponzi schemes. Lakini hata inapotoa tahadhari ya kweli wananchi ni kama hawaelewi na mbaya zaidi hawaiamini BOT na wanaendelea kupeleka pesa DECI na kuitetea kwa maandamano na jazba kabisa.It is a pity kwa sababu mwananchi wa kawaida ndiye atakae umia mna DECI. This is a major crisis of confidence!!BOT haiaminiwi na wananchi japokuwa inasema ukweli sasa. BOT needs to work very hard about its image na bila shaka kutoaminika kwake kunatokana namdudu kama EPA, OGL, Twin Towers na kashifa zingine za utendaji na watendaji wake.Kwa kweli bila kurekebisha image ake BOT will fail to be effective.
Anon wa April 10, 2009 1:19 AM
ReplyDeleteHili ndio tatizo. Pesa Tanzania haizunguki. Taasisi ambazo zinatambuliwa na BoT kazi yao ni kukalia mabilioni lakini hawasumbuki kutafuta njia za kuwawezesha wananchi.
Zile pesa za EPA awape DECI angalau Bilion 2 JK fanya kweli basi
ReplyDeleteKaka michuzi mi nimewekeza pesa yangu Deci nakula laki tano kwa wiki sawa na mbili kwa mwezi.
ReplyDeletePesa yangu ilisharudi zamani na ninaendelea kula faida. Haiingii akilini na hata sitaelewa mtu yeyote na nadharia yake. Nakaribia kumalizia kigorofa changu, benki nilikosa mkopo eti kiwanja hakijapimwa sijuvi vitu gani kibao!
Kakobe mtumishi wa Mungu ameilaani Deci, sawa sikatai ye si anamapato ya kanisa kubwa kabisa africa mashariki na kati! acha na wengine wale kivingine kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake, si vema kukashifu taasisi nyingine yako inausafi gani watu hawavai pete, hereni, kujifunga vitambaa kichwani n.k! Kila mtu na mipango yake.
Deci Oyeee!