Ndugu Wazalendo,
Kwa Masikitiko makubwa TPN inatangaza kifo cha mwanachama mwenzetu Mz. ERIC MUNISI ambaye amefariki usiku wa Jumatano Kuamkia Alhamisi akiwa usingizini.
Mz. ERIC MUNISI alikuwa ni Mwanachama hai wa TPN; Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TPN; Pia alikuwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Fortune Real Estate moja ya makampuni yaliyoanzishwa chini ya kimvuli TPN. Pia alikuwa moja kati ya Wanahisa wa Kampuni nyingine ya Ukulima na Ufugaji ya FUGALIMA ambayo pia ilianzishwa chini ya kivuli cha TPN. Mbali ya kujishughulisha na TPN pia alikuwa ni mjasiliamali ambaye alikuwa akiendesha kampuni zake.
Kesho saa sita kamili (Saa 6.00 Kamili Mchana) kutakuwa na utaratibu wa kuuaga mwili wa Marehemu mpendwa wetu ERIC MUNISI nyumbani kwa kijana wake maeneo ya Msasani Karibu na kwa Warioba. Kwa mawasiliano ya location tunaweza kuwasiliana na:
Mz. Fadhili No. 0763 820 045
Mz. Ndanshao : 0754 266 054
na
Mz. Consolata Tel. 0713 334 078
Tumepanga kama TPN tufike msibani saa tano asubuhi. TPN itatoa barua ya rambirambi kwa niaba ya wanachama wote na TZS 200,000. Tunawaomba wanachama wote wenye nia ya kutoa rambirambi binafsi wawasiliane na Mhazini Consolata 0713 334 078 ili zikusanywe kwa pamoja na kuikabidhi familia.
Baada ya kuuaga, mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda mkoani Kilimanjaro kwa Mazishi siku ya Jumanne.
Tuungane na familia ya wafiwa kumwomba Mungu awafariji na kuwapa nguvu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Wasalaam
Sanctus Mtsimbe
President TPN
TPN ni Tanganyika Packers?
ReplyDeleteMstimbe TPN ndo nini, Maana ndo mara yangu ya kwanza kusikia TPN.
ReplyDeleteKwa nini usieleze kwa kirefu kwani hayamkini inawezekana kuna watu ambao ni mara yao ya kwanza kusikia hilo kama nilivyo.
kweli anony wa pili, mmojawapo wa hao unaowasema ni mimi. Hii ni sawa na kusema "kitu hicho" wakati hata hujataja kitu chenyewe.
ReplyDeleteNyie TPN,kuna siku mlijitangaza humu,nikaingia kwenye website yenu nikaomba unachama,yapata miezi kama mitatu au minne hivi imepita hakuna jibu.mnanipa wasiwasi.Anayebisha tuwasiliane nimpe maelezo.atyini@yahoo.com
ReplyDelete