Mgeni wa heshima Dk. Switebert Mkama akikabidhi Kombe kwa kepteni wa Simba Vicent Ndusilo
furaha ya ushindi
kushinda kutamu, hasa ikiwa umembenjua mtani wa jadi
watoto wa msimbazi
wana wa jangwani

Simba yairarua Yanga 3-2 Marekani 

Na Ripota wa Globu ya Jamii,Washington DC

TIMU inayoundwa na washabiki wa klabu ya Simba wanaokula maisha Mamtoni hapa Washington DC, jana iliwalaza wenzao wa Yanga kwa mabao 3-2 katika mchezo ambao hautasahauliwa kwa miaka mingi ijayo. 

Simba ilipata mabao yote matatu katika kipindi cha kwanza ambacho mwamuzi wa mchezo huo, Abuu Gadhafi, alilazimika kukikatisha ili kuiokoa Yanga isimalizwe na mnyama mkali. 

Bao la kwanza la Simba lilifungwa na Vincent Ndusilo kwa shuti kali kunako dakika ya 20 baada ya kupokea pasi murwa kutoka kwa kiungo machachari, Liberatus Mwang’omba.  

Haikuchukua muda, kwenye dakika ya 28 Vincent tena alimsalia mlinda mlango wa Yanga, Lucas ‘Kinyang’anyiro’ Mukami, kwa mpira wa kichwa. Lucas pia ni kocha msaidizi wa Yanga. 

Ikicheza kwa kasi na nguvu, Simba ilipata bao la tatu kwenye dakika 33 kupitia kwa mchezaji wake wa kulipwa iliyemsajili kutoka Nigeria, Gilles Che ‘Obina Orji’ baada ya kupokea pasi kutoka kwa Liberatus. 

Wakati wa mapumziko baadhi ya wana Yanga walitoa wazo la kuweka mpira kwapani lakini kocha wao, Yassin Matola ‘Kondic’ alipinga hatua hiyo huku mwenzake wa Simba, Marko Mbullu ‘Phiri’ akishangilia. 

Bahati mbaya vijana wa Simba walilewa moshi wa nyama ya kuchoma ulioshamiri uwanjani hapo, na ndipo wana Yanga walipotumia mwanya huo kusawazisha bao la kwanza kunako dakika ya 55. Alikuwa ni Diddy Rouba aliyewahi kuichezea Miembeni ya Zanzibar, ambaye alibaki na kipa Charles Mbah, mzaliwa wa Nigeria na kupiga shuti wavuni. 

Huku muda ukiyoyoma, Yanga walianza kucheza mchezo wa rafu na ubabe ili kuwakabili Simba waliokuwa wakipepea kama nyuki, lakini mwamuzi Gadhafi ambaye miaka ya nyuma aliwahi kuichezea Yanga, hakuna na kadi nyekundu mfukoni.  

Katika moja ya udhibiti mkali wa mabeki wa Yanga, kunako dakika ya 80 Aristotle Maruma alilazimika kumkaba shingo mshambuliaji hatari wa Simba, Gilles, kwa staili ya Athuman Juma Chama na Mogella enzi za miaka ya 1980. Mwamuzi alitoa adhabu ndogo ambayo haikuzaa matunda. 

Hatimaye Yanga walifanikiwa kupata bao la pili la kusawazisha kwenye dakika ya 91 lililofungwa tena na Diddy kwa shuti kali la mita 40 na juhudi za mwamuzi kuongeza dakika nane zaidi hazikufanikiwa kuikoa Yanga. 

Mgeni wa heshima katika mchezo huo, Ofisa Ubalozi wa Tanzania mjini Washington, Dkt. Switbert Mkama, alikabidhi kombe la ushindi kwa nahodha wa Simba, Vincent Ndusilo na kuhitimisha mchezo huo. Baada ya hapo sherehe kubwa ya kutafuna nyama za kuchoma na vinywaji ilishamiri. 

Ghafla baada ya mchezo, kiongozi wa Simba, Rashid Mkakile ‘Bamchawi’ ambaye anadaiwa alilala uwanjani hapo kugangua, aliibuka na kutamka kuwa Yanga haitashinda kamwe kwenye uwanja huo wa Meadlebrook, uliopo kwenye kitongoji wa Silver Spring, kilomita chache kutoka kwenye maraha ya Washington DC. 

Aidha katika hali ya kufurahisha, timu hizo zilitumia jezi zilizonunuliwa mwei huu Kariakoo jijini Dar es Salaam ili kuonesha uzalendo kwa nchi yao badala ya kununua jezi kwenye nchi ya kigeni. 

Mdhamini wa Yanga, Said ‘Warren Buffett’ Nassoro, ameahidi kusajili wachezaji zaidi kwa ajili ya mchezo ujao ambao haujapangwa utafanyika lini. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Ila wachezaji punguzeni hivyo Vitambi ili muonekane Sports Guyz wa ukweli.

    ReplyDelete
  2. Hi Bro MICHUZI...
    UKIANGALIA MTIRIRIRKO WA HABARI NZIMA IMEJAA UNAZI MTUPU!!!
    ALIYE LETA RIPOTI HII AMEIANDIKA KIUSHABIKI SANA KIASI KWAMBA HAINA MVUTO...
    AKITAKA NA SISI TUANDIKE TUTAANDIKA....
    MICHUZI NISAIDIE KUMWAMBIA AACHE UNAZI WA KIZAMANI...

    ReplyDelete
  3. Libe wapopo hao msiwachanganye week chache zijazo wakati wana waHtown au wanajiji kubwa watakapo wapeleka puta puta

    ReplyDelete
  4. Aah! Angalau ''mnyama'' ajisikie kidogo, kateseka sana mwaka huu!! Kombe la mchangani kama kawa! Na alivyoitafuta hiyo nafasi ya pili, kaa! Utadhani ndo kawa bingwa!

    ReplyDelete
  5. Mdau huyu mwandishi wa huko Marekani hunifurahisha aina yake ya uandishi.

    Nafikiri TASWA (chama cha waandishi wa michezo Tz) wafikirie kumweka ktk kinyanganyiro cha mwandishi bora 2009.

    Mwisho michezo ni dawa ya mujarabu kwa kunyosha viungo vya wabeba boksi na kupunguza msongo wa mawazo ughaibuni, hongereni wadau wa marekani na Nordic countries kubaini hilo.

    ReplyDelete
  6. Mimi napongeza timu zote mbili haswa Diddy(Rouba)aliyewahi pia kuchezea timu ya madison ya kule mji zanzibar.na nawataka pia vijana wetu wa kitanzania mnaoishi canada na vitongoji vyake mfanye vitu kama hivi

    ReplyDelete
  7. Maraha ya DC. Hahahahahahaha hiyo line tamu kweli sema haiendani na DC=Distric of Crack

    ReplyDelete
  8. DAH DUNIA IMEKUA NDOGO. HONGERA SANA ANKO VICENT NDUSILO. TUMEFURAHI KUONA UMZIMA NA BADO UNAENDELEA NA MPIRA. SALAAM NYINGI SANA TOKA KWA MANSUR PAMOJA NA DAD. DENMMARK WISHING YOU LONG LIFE

    ReplyDelete
  9. Sio vitambi hivyo, hapo unaona misuli tupu!

    ReplyDelete
  10. Ndusilo waaaaaaaaaaaaaapi???!!

    ReplyDelete
  11. wajamaa tafuteni viwanja vya maana huo uwanja mbaya sana

    ReplyDelete
  12. Mwandishi wa habari unawaharibia wenzako. Mchezo mzuri, madhumuni madhuri (kununua jersey bongo) . lakini hadithi porojo tupu. Maraha gani unayokula hapa DC. Unawadanganya wadangajika weweeeee. We unaishi wapi hapa DC unakula raha?

    ReplyDelete
  13. Mimi ninachoomba tu, ni kwamba SIMBA acheni uchawi huu, LILE TOGWA MLILO KUWA MNAWAPA WACHEZAJI WENU LILITOKA WAPI?

    Kuna malalamiko KUTOKA KWA Wachezaji wa Yanga kwamba kila walipokuwa wakitaka kuweka mabao walijisikia kama haja kubwa inatoka na ikabidi waache kupiga ndukis, na matokeo yake mabeki wa Simba wanaokoa.

    Huyo Bamchawi Mwambieni angalie kwani mechi ijayo yanga hawatokaa kimya , Watahakikisha huyo Bamchawi anakutwa uwanjani asubuhi anacheza manyago.

    TUTAMWENDEA, KILOSA,SIMBAWANGA NA TANGA.
    MTAJIJU.

    Wenu

    ReplyDelete
  14. SIMBA TUNAGAWA UMASIKINI TU.

    IT IS WHAT IT IS.

    ReplyDelete
  15. Combine Simba na Yanga plus wa-nigeria then njooni Wichita mpigwe bao na vitanbi vyenu.Libe na Ismail wana habari nzuri ya kikosi cha Wichita.Pumbavu!!?!

    ReplyDelete
  16. Mechi ya simba na yanga kurudiwa May 23 katika 3-day wabongo reunion extravaganza in DC metro area. Visit www.wabongoreuniondc.com for more info

    ReplyDelete
  17. Watu Washington wamegawanyika, kuna wanaosota na wanaokula raha. Mwandishi usiwahifadhi watu, wengine hapo hawajui kona yoyote ya maraha zaidi ya vilabu vichafu vya pombe, na wengine wanatamani wangezipata pombe za kienyeji na vikuku vichafu.

    ReplyDelete
  18. wabeba box oyee

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...