Mtoto wa Mama Bishanga  Bwana Kilian Kamota  mgosi wa Tanga alimeremeta pale Walsh University Ohio alipokabidhiwa nondozzz ya MASTERS OF FINANCE AND STRATEGIC MANAGEMENT. Mama Bishanga aliwachanganya wazungu pale alipopiga kile  kigelegele cha kiafrika huku akipepea kitenge chenye bendera ya Tanzania hicho alichoshika hapo kwenye picha.
mdau Kilian Kimota baada ya kula nondozzz zake
 Mama Bishanga  akiwa na Kilian Kamota baada ya kula nondozzz. Wengine kwenye picha ni Papaa Martin Yohana na Mr Joe Ngwilizi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Congratulations Kilian. Job Well Done!

    ReplyDelete
  2. Duuuh Huyu Jamaa alikuwa Mwenyekiti wa serikali ya wanafunzi Minaki enzi zetu. Hongera kaka. Mgeta - UK

    ReplyDelete
  3. Muya naona mambo si mchezo.

    ReplyDelete
  4. Mama Bishanga tabasamu mpaka jino la Christmas limeonekana. Mtakuwa mlizinywa mpaka asubuhi

    ReplyDelete
  5. Hongera Sana Muya...Mungu akujalie maisha marefu na kukuongezea busara mara dufu. Many are called but few are chosen one who is the object of choice or(of divine favor : an elect person.Wakilisha Kaka...Mwezako akinyolewa nyele tia maji... I Salute you Comrade !!! Mama Hongera kwa kutupa Kamanda.Aluta Continuer...! Gluck Muya!!!

    ReplyDelete
  6. A pie/chapati too many?

    ReplyDelete
  7. jamani wadau wa ughaibuni niambieni, maana napenda vigelegele lkn ninavyosikia huko ughaibuni hawapendi makelele sasa kupiga vigelegele sio kelele kwao? maana naskia wenyewe hawapendi makelele, sasa hapo haiwezi kuwa ishu ukafatwa hata na police? nisaidieni wandugu.

    mdau dar

    ReplyDelete
  8. Kumbe mpaka Marekani kuna akina Papaa .......! Mi nilifikiri ni Tanzania na Congo tu!

    ReplyDelete
  9. JAMANI NISAIDIE WADAU HICHO KITENGE NIMEKIPENDA WDAU NIELEKEZENI WAPI NAWEZA PATA KWA HAPA DAR, MAANA KARIAKOO ZIMEJAA WAX ZA NIGERIA NA CONGO

    ReplyDelete
  10. Wasambaa wamezidi!!!!!

    ReplyDelete
  11. Kaka nimekubali kaka.
    Keep it up man!!Naona darasa letu linazidi kutesa tu(form 6-Minaki).

    Hongera sana kaka.

    Nduguyo,
    Hamza.

    ReplyDelete
  12. Kilian,
    Huyo jamaa wa pembeni hapo sio Lushinge huyo?
    Duh,Long time mazee.

    Hamza.

    ReplyDelete
  13. Watoto wa Canton naona mnajitahidi kufuata nyayo za kaka zetu. Good job vijana

    ReplyDelete
  14. Mzee muya naona bado mwendo ni uleule-kasi ya unyoya. Safi sana.

    Musa
    Sweden

    ReplyDelete
  15. Naona timu ya makamanda wote wa Canton mli-gather 2gether. Samahani sikuweza kufika wazee.

    Saleh

    ReplyDelete
  16. Naielewa furaha ya mzazi kwa mwanae kufanikiwa hivyo,natamani mama yangu angekuwa hai anione mwanae nikigraduate soon,umenitoa machozi mama.
    Hongera zenu wote wewe na mwanao kwani si safari rahisi,
    Mungu azidi kuwajalia.

    ReplyDelete
  17. Kilian
    Hongera mwanangu, Watoto wa Mjale naona tuna muhenzi sana Mzee wetu.
    Kazi haiishii hapa Kijana! Lazima gurudumu tulisogeze kuelekea kwenye Mvinyo Town.

    Those year ilikuwa Serikali ya Wanafunzi, 2015/2025 itakuwa ni serikali ya Wananchi.

    Good job

    Mdau AL

    ReplyDelete
  18. Hongera Kilian! Hongera Mama Bishanga! Aisei, hata mimi nikienda kwenye shughuli za wanangu napigaga vigelegele. Watu wengine wanaogopa....mama moja (tena mweusi) kaniambia, "I'm scared of you!".

    Mama Bishanga I know you are proud today! Mungu awabariki.

    ReplyDelete
  19. hongera sana kaka yetu kilian.big up sana and stay blessed......dada yako itika mwakasula..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...