nanihii

MDAU MPENDWA,

REJEA KICHWA CHA HABARI HAPO JUU.
MADHUMUNI YA WARAKA HUU NI KUOMBA KWA UNYENYEKEVU KUBADILI JINA LA LIBENEKE LETU HILI KUTOKA "GLOBU YA JAMII"  NA KUWA MOJA KATIKA MAJINA HAYO MATANO KAMA ILIVYOPENDEKEZWA KUWE NA UCHAGUZI. AIDHA, JINA AMBALO HALIPO HAPO LAWEZA KUPENDEKEZWA NA WADAU WALIJADILI KAMA LITATUFAA: 

1. GLOBU YA UMMA
2. IBAKI KUWA GLOBU YA JAMII
3. GLOBU YA KISWAHILI
4. GLOBU YETU
5. GLOBU YA NANIHII

MIE BINAFSI NINAOMBA IITWE "GLOBU YA UMMA"

SABABU KUU YA KUTOA OMBI HILI KWAKO NI KUTAKA KULETA JINA AMBALO LITATAMBULISHA GLOBU HII KIPEKEE, IKIWA BILA KUHUSISHWA NA AINA YOYOTE INGINE YA LIBENEKE LA JAMII.

VILE VILE GLOBU HII SASA IMEJIKITA MIKONONI MWA WADAU AMBAO NDIO UMMA WENYEWE WA KISWAHILI (KWA MAANA YA WATUMIAJI WA LUGHA YA KISWAHILI NA SI VINGINEVYO) NA AMBAO NDIO WAAJILI WA MWENDESHAJI WAKE.

NATUMAI OMBI LANGU LITAKUBALIWA NA NASUBIRI JIBU LAKO KWA HAMU KABLA YA UTEKELEZAJI AMBAO UTATEGEMEA MAJIBU HAYO. KAMA ILIVYO KAWAIDA, SITHUBUTU KUFANYA JAMBO BILA YA IDHINI YAKO.

WAKATABAHU
WAKO MTUMISHI MTIIFU
-MICHUZI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 49 mpaka sasa

  1. ManU 3 - A'Villa 2. Tumerudi kwenye kiti chetu kabla hamja kizoea.

    Mi nafikiri isiwe Umma, iwe "Globu Ya WOTE"

    ReplyDelete
  2. Ombi lako zuri. na hebu fanya hivyo. Na wale wanaokutumia makala ziwe ni za Kiswahili.

    ReplyDelete
  3. WEKA MAJINA MA 5 Watu wa Chague Alafu ndio Uanike lililopata watu wengi. Itakuwa Vizuri pengine hatutoona kuhusu Bwawa La Maini sana.

    ReplyDelete
  4. Piruu, OmanApril 05, 2009

    Jamii siku hizi kila mtu anaitumia, naona Umma itakuwa pahala pake, ila kama ungetoa majina matatu hivi wadau wakapiga kura ingekuwa mswano zaidi.

    ReplyDelete
  5. Sioni sababu ya msingi ya kubadilisha jina. Haitaongeza kitu!

    ReplyDelete
  6. kama sababu ni kwa ajili ya jamii inao ongea kiswahili nijambo zuri nahao walio ombwa mara chungu mzima waandike kwa kiswahili hawataki wafungulie ya kwao kwani sio lazima uandike kiingereza ndio uonekane msomi

    ReplyDelete
  7. Blogu ya Naninhii.

    ReplyDelete
  8. Let do a short critique of your request.

    1.Seems like you already have a choice in mind and thats why you posted your opinoin,Oops!!Its not even opinion,Its your desire right from the begging.You just want to formalise,right??

    2.Dont you see that you will be intimidating us by posting what you thing right at the beggining.Why didnt you provide a list of "clear" option for the users/subscribers to decide.

    3.The fact that the list of 5 options is ambigous gives your individual desire to be at a better position over the rest.

    4.The reasons for the change are still not convincing,can you try to elaborate it a bit more.

    5.Will it make any difference by changing the name?

    6.Should we expect any consequences as outcomes of the change once we agree?

    Mkulima-Kijijini Gezaulole.

    ReplyDelete
  9. Mazoea mabaya, hiohio ya jamii ibakie

    ReplyDelete
  10. GLOBU YETU ndio mwake

    Mh Balozi,
    Kwanza nafurahi kwa kuleta hoja hii (binafsi) kwa wadauzi hapa.

    Ni vyema kwa kuweka watu wapige kura ni ipi bora zaidi.

    Kwa maoni yangu,maana kutumia jina JAMII linaingiliana na libeneke jipya na Mjengwa la Kwanza Jamii.Vile vile ukija kwenye hii UMMA sasahivi kila kona ni UMMA, kama vile mashirika ya umma, Sauti ya Umma (chama cha siasa), nk. Kwa maoni yangu, GLOBU YETU ni bora zaidi.Kwanza inaonesha umiliki wa globu hii ni YETU wadau wote.

    Naamini wadau wengi watatoa maoni yao hapa ipi iwe bora zaidi.Na pia kama uwekano wa kupiga kura ni vyema kabisa.

    MAKULILO Jr,
    www.makulilo.blogspot.com

    ReplyDelete
  11. Nashauri tuite BLOGU YA MZAWA,
    mdau london.

    ReplyDelete
  12. Kwa Mtumishi wangu mtiifuu,
    Assalam Alaykum.
    Mimi naona katika majina hayo uliyotoa ni bora tuiite "BLOG YA UMMA", (not GLOBU).
    Ingependeza kuwa "BLOG YA UMMA WA KISWAHILI" au "BLOG YA KISWAHILI YA UMMA", Lakini tumeshuhudia wengine humu hutumia lugha mbali mbali mpaka "kwishney" imetumika!

    ReplyDelete
  13. kwa upande wangu napendekeza.Kuwa blog ya jamii. ndio jina halisi linalounganisha jamii nzima ya, Kitanzania,

    ReplyDelete
  14. mie nawaomba mnipe tofauti kubwa ya Umma na Jamii ili niweze kufanikisha kura yangu ipasavyo.
    Pia,kwani kumetokea athari gani zaidi ktk hilo jina la "Blogu ya Jamii?"
    kama sababu ni kutumiwa na wengi,hata hilo neno Umma laweza kutumiwa na wengi kwani huwezi kumzuia mtu kutumia neno ama jina fulani.haswa ikizingatiwa kwamba Watu wanapenda saaaaana kuiga ya wenzao!!!!

    ReplyDelete
  15. We aliyekwambia kuandika au kuongea kiingereza ndio usomi?
    Nyie ndi mnakimbilia kupeleka watoto shule za nchi jirani kisa wakajue kiingereza.
    Mtu mzima hovyo!!

    ReplyDelete
  16. Unaweza kuiita chochote unachotaka sidhani kama inajalisha, la msingi nikupata news that what matter.

    ReplyDelete
  17. nadhani jamii ipo mahala pake husika, maana tukizungumzia kiswahili basi jamii imechukua kila aina ya binaadam nikimaanisha watoto,vijana na hata watu wazima na jamii hiyo hiyo bado inazungumzia rangi za watu na makabila yao.......nahitimisha kwamba jamii ndio yenyewe kaka michuzi! ahsanteni....

    ReplyDelete
  18. Bro Michuzi, yatengenezee majina yatakayopendekezwa 'banner' na watu wayapigie kura live, huku matokeo yakionekana baada ya mtu kuweka kura yake. Michuzi Blog ni jina zuri, asilia na la kipekee, hivyo libaki. Pendekezo la Blog kuwa ni ya kiswahili ni zuri. Ila unaweza kuwafungulia hao limbukeni wa lugha za kigeni ya kwao bro, sio siri wanaboa sana!! Ya kwao Uiite blog ya Wachumi, au wasomi, au maprofessor, au Mjinius, au ma Albert Einstein...waendeleze misifa yao huko!

    ReplyDelete
  19. MwanamapinduziApril 06, 2009

    Mie naona Issa unazeeka vibaya! Hii sio blog ya jamii wala ya umma! Hii ni blog ya CCM-wanamtandao! Na ipo kwa faida yao. "Meseji" yoyote inayowelenga wana mtandao haioni juwa (ikiwemo hii nnayo iandika). Issa umewekwa makusudi na CCM kuwapumbaza watanzania wenye fikra za ukombozi kwa kuwapoteza malengo ya kuwaondoa CCM madarakani. Wewe ni zaidi ya mpiga picha wa daily newz, wewe Issa ni shushushu kwenye kitengo maalum cha mawasiliano, ikiwemo hii ya internet! Ila siku zenu zinahesabika!

    ReplyDelete
  20. UNAVOSEMA MWENYEWE
    "GLOBU" YA JAMII NI POA....UMMA....????? TUTAANZA KUWA CCM HAPA

    AU GLOBU YA LIBENEKE...MANAKE HUMU KAZI YAKO KILA SIKU NI CHAP CHAP INAHITAJI MAKOFI PWA PWA...WEEEEEEWEEEE

    ReplyDelete
  21. Mi ndugu yangu Mkuu wa wilaya ya nanii, napendekeza iitwe BWAWA LA MAINI! Aaah,mbona mnaanza kuchonga ni maoni tu.
    THE KOP
    MSOLWA KISAYANI
    MKURANGA
    PWANI.

    ReplyDelete
  22. Bwana Michuzi injinia ni wewe! Tunakupa ruhusa kufanya mabadiliko yoyote roho yako inavyopenda. Unaweza ukaiita majina tele wala haitabadilisha chochote, sisi tunachotaka ni kuburudika na Information za Issa Michuzi.
    Cha msingi ni usiiondoe hewani, ippmedia wanachemsha babu kubwa, link zao zote ni mbovu wanaishiwa habari wamebaki kuweka headlines lakini hupati habari kamili.
    Lakini kwa Issa Michuzi tunapata habari motomoto pamoja na picha.
    Michuzi Oyeeeeeeeee Michuzi Oyeeeeee! Watu Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee, Tunakuombea uishi miaka mingi.

    ReplyDelete
  23. Michuzi hamna kitu hapo hii ni blogu ya waosha vinywa kama wewe unavyoosha kinywa. Sijapata kuona blog inayoharibu lugha ya kiswahili kama hii; mfano unaposema 'barabara ya nyerere road'au 'breaking nyuuuuuz' na mengine mengi. Mpaka utakapojirekebisha na kuacha kuosha kinywa hutaona watu makini wakichangia mada humu.

    ReplyDelete
  24. It doesn't matter at all, you may call anything you wanna call it.

    ReplyDelete
  25. mimi sijui nimeseme ipi ndiyo iwe bora kuliko nyingine ila cha msingi angalia ipi iliyo pigiwa kura nyingi basi hiyo ndiyo itakuwa imeshachaguliwa jina halafu tunaomba matokeo ya kila jina limepata kura ngapi.ila na mimi kama walivyo wadau wengine jina la globu ya kiswali itakuwa mahala pake kwani mambo mengi sana yanaelezwa kwa kiswahili
    ASANTE

    ReplyDelete
  26. IWE BLOG YETU

    ReplyDelete
  27. Mimi ninapendekeza iitwe
    "WAGAGAGIGIKOKO"

    Neno globu sio lazima litokee katika jina halisi. Hili jina litaibainisha bila kupotosha malengo yake ya kuhudumia jamii au umma.

    ReplyDelete
  28. Naona iwe Globu ya Wazalendo

    ReplyDelete
  29. GLOBU YA JAMII

    ReplyDelete
  30. mimi naoana ibaki kuwa Glob ya jamii,japo kuwa inaitwa glob ya jamii ukituma swala lako linalo husu jamii linakwa kapuni.mii na pendekeza libaki kuwa GLOB ya JAMII kuepusha usumbufu kwa vistor wengine.

    ReplyDelete
  31. Michu,
    Jina la 'Globu ya Jamii' tayari lina goodwill. Never loose it!.
    Pasco

    ReplyDelete
  32. GLOBU NA BLOG VINA MAANA SAWA? MIMI MNANICHANGANYA SASA NASHINDWA HATA KUFANYA UCHAGUZI

    ReplyDelete
  33. IENDELEE KUITWA GLOBU YA JAMII WATU WOTE WAMEZOEA KWA JINA HILO,VILE VILE KUBADILI JINA HAKUONGEZI CHOCHOTE WALA KUBADILI CHOCHOTE,

    ASANTE,MDAU WA KAMPALA,UG

    ReplyDelete
  34. Heri mimi sijasema!!
    AAAH, Hapana ngoja niseme, iitwe `blog yetu' inatosha, iwe jamii au umma. Kwani nahisi ukisema `ya- jamii' inaweza ikawahusu jamii fulani tu,kama vile wana CCM, tu. Na ukisema ya Umma, pia inawezekana ikawa sawa, sio mbaya. Lakini `Blog yetu' haipwekeshi.
    Yote tisa uamuzi mzuri unatoka kwako, kwani kama tutakuwa hatuna shukurani, tutakuwa sio waungwana, umatusaidia sana kuanzisha hiki kitu. Zipo kasoro,lakini niza-kibinaadamu, na uzuri wake kasoro hurekebishwa, na warekebishaji ni sisi sote.
    M3

    ReplyDelete
  35. Kaka Michuzi,

    Una nia ya kubadili jina. Ila kabla ya kufanya hivyo unapaswa kuwa na lengo. Tayari globu hii ina identity. Na ukishatengeneza identity ni muhimu sana kuwa consistent; hiyo ndo namna unaweza kuiwezesha globu isimame kama BRAND. Zaidi unaweza labda kuongeza vionjo ili kuhakikisha kuwa globu inawavuta watu kuitembelea; kwa sababu inakidhi mahitaji yao. Labda suala linabaki namna ya ku-ibrand ili iendelee kuwa chaguo la kwanza kwa kila m-bongo. Usijali wanaoiga; hawawezi kuiga uniqueness yake. Unatakiwa kuangalia namna ya kuongeza vijimambo, sio kubadili jina. Tayari jina inalo. Ushauri wa mwisho: itapendeza kama mtu akifungua akute la globu kwa juu: Globu ya jamii (mbona jina tamu sana?), ndipo tangazo la mdhamini wetu lifuate. Hilo jina linaweza kutengenezwa kwa design maalum, hivyo inakuwa ni logo yake, ambayo ni vizuri ukaisajili (iwe trade mark) Pia unataka kubadili na anuani ya tovuti? Mie m-bishi kweli. Nadhani hatuna issamichuzi mwingine. Endeleza libeneke mwanawane. Imesimama tu. Naitwa Nyanda. Najibobeza katika BRANDING. Pia unaweza kunidondoshea mawili matatu kama kuna haja hiyo kupitia: nyandaj2000@gmail.com

    ReplyDelete
  36. nadhani iitwe blog ya michuzi, kwani wewe ndio ulioianzisha na ni lazima tangazo lipitie kwao na ulikubali la sivyo halitaonekana , hii ni blog yako , blog ya michuzi.

    ReplyDelete
  37. IITWE GLOBU YA MAFISADI

    ReplyDelete
  38. MICHUZI,
    MIMI SIONI HAJA YA KUJADILI MAJINA, WAKATI MAJINA YENYEWE TUNAYAONGEA MDOMONI. SIJAONA SEHEMU YOYOTE JINA LA BLOG LILIPOANDIKWA, ISIPOKUWA HUSIKIA TU WATU WAKIITA KWA MDOMO AU MAANDISHI KWENYE MJADALA. NIJUAVYO HII NI BLOG YA MICHUZI, KIMAANDISHI KWENYE UKURASA WAKO JUU KABISA.


    USHAURI: -
    1)WEKA JINA LITAKALOKUBALIKA JUU KABISA YA UKURASA WA BLOGU YAKO.

    2) KUITA "GLOBU" NI JINA LA KIHUNI AU KIJIWENI. TUITE "BLOGU".

    3) JINA LINALOPENDEZA NI "BLOGU YA UMMA" KAMA ULIVYOPENDEKEZA WEWE NA SABABU ZAKO NAONA NI ZA MSINGI.

    Maana tayari kuna "JAMII FORUM" nk...

    ReplyDelete
  39. IITWE KIJIWENI.

    AU MICHUZI
    KWANZA SIKUJUWA KAMA INAITWA BLOG YA JAMII SIKUZOTE NA SARCH KAMA MICHUZI.

    AU KIJIWENI.

    ReplyDelete
  40. napendekeza iitwe globu ya nanihii!

    ReplyDelete
  41. Ewe mtumishi wangu tafadhari usipotoke baada ya kukupa haya madaraka sasa naona unaanza kuleta mbwembwe. Kwataarifa yako mimi nina kura ya veto hivyo bugolu hii itaendelea kuitwa ya jamii. Umma umejaza mafisadi glopu hii haina mafisadi. Naomba kufunga mada hii. GUBOLU Ya JAMII OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE. DK

    ReplyDelete
  42. NAMPENDEKEZA IENDELEE KUITWA
    "BLOGU YA JAMII" USIBADILI CHOCHOTE
    MCHUMBA WA NANIHII

    ReplyDelete
  43. jina kubwa lenye kujiuza lenyewe MICHUZI

    ReplyDelete
  44. hehehehehe
    michu ukibadili jina la blog ya jamii basi na wewe ubadili fulanazzz yako hiyo.maana hiyo ni fulana ya jamii

    ReplyDelete
  45. Tayari uchanguzi umesha ufanya. Unacho tafuta hapa ni pendekezo. Mimi ningependelea ibaki kama iliyo.

    ReplyDelete
  46. GLOBU YA NANIHII Baaab kubwa.

    ReplyDelete
  47. JINA LIBAKIE BLOG YA JAMII!

    ReplyDelete
  48. Nanihii, hebu tulia. kubadilisha jina haibadilishi kitu hapa, nadhani wadau wengi wamependekeza pamoja na mimi ibaki kuwa "blog ya jamii" na kuna mdau juu kabisa amekuambia jina lililopo lina "goodwill" ukibadilisha jina nitajua/tutajua hautujali wadau wa blog hii ya JAMII.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...