Bosi wa Masoko na Mawasiliano wa NMB Imani Kajula akizungumza wakati akikabithi vifaa kwa Taifa Stars. Kulia ni Katibu Mkuu wa TFF Fredrick Mwakalebela.
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa Marcio Maximo na nahodha wa Taifa Stars Nsajigwa wakiangalia baadhi ya vifaa vilivyokabithiwa na bosi  wa Masoko wa NMB Imani Kajula.

Kocha mkuu wa Timu wa Congo akiongea na wanahabari juu ya mechi kati yao na Taifa Stars. Kocha huyo alimwaga sifa kibao kwa kiwango Taifa Stars ilichoonyesha wakati wa CHAN. Kesho DRC itacheza na Taifa Stars mechi ya kirafiki ya kimataifa uwanja mpya wa neshno

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 08, 2009

    Kocha wa Congo na fulanaz ya Arsenal, makubwa!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 08, 2009

    hivi jamani, mbona kila mtu anakimbilia kwenye mpira tu. Kuna matangazo kwenye TVs na radio ya kuchangia vifaa vya elimu kwa watoto wenye ulemavu, mbona sioni kampuni kubwa kama voda, or even banks like this one wakichangia? Au wanachangia kimya kimya?

    ReplyDelete
  3. david villaMay 08, 2009

    Hivi Jezi za timu yetu ya Taifa mni rangi zipi na zipi?Na rangi nyeupe imo?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 08, 2009

    Wabongo bwana,hizo nyeupe ni casual wear for players. Taifa Stars jerseys ni rangi blue kwa home na away ni nyeupe. NMB imekuwa inathamini football three years now.

    Tenga amesaidia kurudisha imani ya sponsors kuliko watu kama Riadha na ndondi ambako mara mtu kakutwa na unga mara Nyambui kapeleka watu sio wanariadha nani atatia mguu uangushe brand yake?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 08, 2009

    Spidi ya Kajula kuelekea uzeeni mbona ni kali sana? Kajula, unahitaji kufunga gavana

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 08, 2009

    - Mdau May 08, 2009 2:43 PM, Arsenal hawajawahi kuwa na jezi style hiyo..Labda tuseme t-shirt yenye nembo ya Arsenal..
    -inaonekana 'ma-nmb' yao hayapendi soka. Sijuwi wangekuwa mbali kiasi gani..

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 08, 2009

    Misaada ingepelekwa kwa kina mama na watoto wasiojiweza hususani kwenye mahospital. kuna watu hawana hata uwezo wa kununu dawa, wana kufa kwa malaria.
    Michuzi fikisha ujumbe mbona wanakazania mjini tuu, uko mijini na vijijini takribani asilimia 80 ya watanzania hawana msaada wowote . hizo milllions zingesaidia sana sana!
    Huo ni ushamba wa kutaka jina na sifa mjini,its pain kwanini hamtoi misaada hinapo hitajika ? nani hatawasaidia hao wasiojiweza hususani kina mamam na watoto??
    mpaka haje mzungu kusaidia?? . hiyo timu ya taifa stars serekali inabidi hiwazamini..
    wengine wananunua mabasi ya yanga na simba wizi mtupu!!

    ReplyDelete
  8. Baba UbayaMay 08, 2009

    hiyo timu ya taifa ya Congo hawana na jezi ya kocha ama inakuwaje?yani kweli Afrika moto.haha yani ni sawa na Maximo avae jezi la Chelsea wakati yuko na Starz,yani haijakaa sawa.haha

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 08, 2009

    Mie nakereketwa. Kwanini hizi benki zisichangie kwa watoto yatima? Wawasaidie wapate kula, elimu,mavazi na tiba? Watoto ndio taifa la kesho. Huo mpira unasaidiaje nchi????? kwa mfano kila siku unasikia mama kajifungua mtoto amekufa kwanini? Hizo pesa zinazopelekwa kwenye burdani kwanini zisisaidie kupunguza matatizo ya wakina mama na waja wazito wapate huduma nzuri wakati wa clinic na uzazi? Tafadhalini tafadhalini kuna mambo muhimu jamani.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 08, 2009

    Mkuu wa nanihii nashukuru kwa kutupa uwanja wa kuelimika na kuelimishana. Leo ningependa kutoa darasa dogo juu ya tofauti ya Sponsorship na Donation. Sponsorship ni mkakati wenye lengo la kutangaza biashara zaidi, hivyo makampuni yanaangalia zaidi eneo lenye kupendwa zaidi au lenye uelekeo wa kupendwa hivyo kulitumia kujitangaza. Ndiyo maana World Cup ni gharama kubwa kuandaa lakini inamanufaa makubwa kimasoko. South Africa itatumia USD 4 Billion kwa world cup!!!, leo hii utalii unaingiza fedha zaidi South Africa kuliko Gold!!!!.

    Donation au Corporate Social Responsibility; Huu ni mkakati wa kuirudishia jamii sehemu ya faida. lengo kuu ni kujenga ukaribu na jamii inayokuzunguka. NMB Jana tu imetoa 25 millioni kwa waanga wa mabomu mbagala. kulingana na Annual report yao wanatumia Tzs 500 millioni kusaidia Elimu, Afya na ujasiliamali.

    Nathani maelezo haya madogo watawezesha wachangiaji kuelewa tofauti. Mpira wa miguu ni mchezo unaopendwa zaidi duniani hivyo ni eneo ambalo makampuni mengi yanapigana vikumbo kulitumia kujitangaza. Nathani mnajua kuwa wakati wa mechi kubwa wakina baba huwa wanaweka kando hata..... . Kitu ambacho wanawake wa Kenya wametumia kuwashurutisha wanaume kuleta maelewano ya kisiasa kwa kuwanyima!. Wangefanya wakati wa world cup hawampati mtu ngoo.

    Mdau ( Business Lecturer Mzumbe)

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 08, 2009

    Haya makampuni yako kwa ajiri ya biashara, yanachangia sehemu ambayo watapata faida. Badala ya kuchukua hela na kutengeneza matangazo ya TV, ni rahisi mno kwa ujumbe kuwafikia watu kwa njia ya mpira. Kama TV watu wana flip channel wakati wa matangazo sasa sijui ukiwa uwanjani uta flip macho. Kwa nini AIG ifadhiri Man Utd timu tajiri duniani badala ya kufadhiri watoto yatima Afrika au hata ombaomba wa Marekani? Ujamaa umewaharibu.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 09, 2009

    Mdau amefafanua vema. Misaada kwa Taifa Stars ni aina ya matangazo ya biashara. Ndio maana TBL wakazidhamini Simba na Yanga, timu zenye mashabiki wengi kuliko zote Tanzania badala ya kuidhamini Villa Squad ambayo ilikuwa na uhitaji zaidi. Kadhalika ndio sababu Serengeti Bia wameidhamini Toto Afrika badala ya timu ya Dar. Uwepo wa Serengeti Bia huko kanda ya ziwa ni mkubwa, hawataki TBL wawatilie sumu.
    Mwisho nikumbushe tena, kabla ya kulaani kwa nini sehemu moja au nyingine haipati misaada tujiulize kwa nini hatukusanyi kodi ya kutosha kujitegemea?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...