Pichani ni mdau Carlos Muhuga akiwa na mai waifu wake Layla  baada ya kumeremeta katika kanisa la Mtakatifu Joseph na baadaye mnuso wa haja Msasani Beach club, Dar. Wanashukuru Mwenyezi  Mungu  kwa kuwajaalia kufikia tarehe hii wakiwa pamoja na salama na zaidi ya yote kuwajaalia Mtoto mmoja anayeitwa Roberto Carlos Muhuga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 12, 2009

    Mbona mwanaumme emoro!!mfupi sana mwanaumme...

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 12, 2009

    Jamaa kauchuna kinoma atakuwa rud sana kwa mkewe mama pole na pia hongereni!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 12, 2009

    Biutifuli. God bless ur marriage.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 12, 2009

    mke mzuri,ana jina zuri na hata tabia yaonyesha nzuri kwani mtu mkishazaa ni mda wa kutosha kumjuwa tabia yake. HONGERENI SANA MBARIKIWE

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 12, 2009

    hongereni sana. Wadau kidogo nielimisheni Roberto Carlos umaarufu wake nini tena?

    ReplyDelete
  6. Al MusomaMay 13, 2009

    Hongereni, ingawa inanichanganya kidogo kuona kwamba ndo kwanza mnameremeta na hapo hapo mmejaaliwa mtoto anaitwa Roberto Carlos Muhuga. Au mimi tu?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 13, 2009

    Mmependeza sana!

    Kila siku naona watu wanaoa wadada wazuri. Mie niko ughaibuni napenda kuoa lakini sijaona mwanamke wa kitanzania alietulia na mzuri.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 13, 2009

    we uliyedai uko ughaibuni hujaona mwanamke wa kitanzania mzuri na ALIYETULIA unachekesha sana...
    post your full phone with profile/Bio Attached then tutajua kwa nini upati wanawake hahahah

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 13, 2009

    Hongera sana Carlos. Nimefurahishwa na hatua uliyofikia. Mwanafunzi mwenzako wa zamani IFM.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 13, 2009

    CHA AJABU NINI,UNASHANGAA KWAMBA WANA MTOTO TAYARI, WAO SIO WA KWANZA WALA WA MWISHO, SI AFADHALI WAO WAMEFANYA JAMBO LA BUSARA KUHALALISHA KUWA KWAO PAMOJA, WENGINE KAZI KUTOA MIMBA NA KULALA NA KILA ANAEKATIZA KARIBU YAO, MUNGU AMEWASAMEHE NA WAZAZI WAMEWAPA BARAKA WEWE JE???? ACHA PUMBA NA ROHO YA CHUKI WAPE HAKI YAO, WAMEPENDEZA VIJANA WAZURI, MASHALAHAAAAH.MJALIWE WATOTO ZAIDI.AMINA.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 13, 2009

    Mie wanawake wazuri wazuri NAWAOGOPA, sitaki kuibiwa na MIBASHA mijizi, nataka mke wangu SURA BAYUUUU, awe wangu mwenyewe, hasa wale walio kama Vimodel Modo, sitaki kabisa maana hata wazungu wanawataka. HONGERENI LAKINI.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 13, 2009

    Cheers and its so beautiful.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 13, 2009

    Dah! we Carlos yaani tangu uoe sasa ni mwaka na miezi kadhaa, imekuwaje ndo unakuja kutundika picha leo?????????????????????????

    ReplyDelete
  14. Hongera sana Carlos.Mbarikiwe kwa maisha mapya.

    Tutafutane: gaphiz@yahoo.com

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 13, 2009

    Mnaotuma hizi habari muwe makini la sivyo mtamix mambo.watu ndo wanameremeta halafu wanashukuru kupata mtoto,sasa hiyo harusi au kubariki ndoa.pengine mi sijaelewa hapo ila kama ni hivyo.hilo jambo halimpendezi mungu kabisa.Tueleweshe kama unaripoti harusi ya mwaka uliopita au vip?

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 13, 2009

    khaaa
    mbona wee annon cjui uko majuu,eti huoni mwanamke mTz kuoa hawajatulia,wewe UMETULIA????????

    hongeren maharusi sana sana na baby wenu pia

    nyie mnaouliza jina la mtoto wee jina lako umelitoa wapi na lina mana gani!!

    roho za kwanini!!!

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 13, 2009

    Wewe unayeuliza habari za kumeremeta na kuwa na mtoto tayari, huo mbona ndio mtindo wa siku hizi, sio wanawake sio wanaume, hakuna wanapenda kuuziwa mbuzi kwenye gunia. tunashuhudia mabiharusi kibao wanakuwa tayari na vitumbo wakati wa kuoana. na pia kupata ujauzito ni mtindo wa kulazimisha ndoa hasa kama mwanaume mwenyewe haeleweki eleweki hivi. wajanja wa mjini huwa wanaita ndoa kama hizo "kupasha kiporo"

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 13, 2009

    we vipi hakuna anayekubali kuuziwa mbuzi kwenye gunia? Yani na wewe na akili zako zoote unaunga mkono uzinifu....Japo mambo haya yapo katika jamii yetu sasa hivi lakini tujaribu kuwakumbusha watu kuwa Kuna makatazo ya Mungu. Mtoto umleavyo hata siku moja usimwambie ukifanya utumie condom msisitize usifanye Mungu kakataza ni dhambi..ndipo baadae umkumbushe condom.......Kaka Michuzi na wewe lini utabariki ndoa yako???????

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 13, 2009

    Waka siwapi hongera....ni waizi hao..walishaibana kwanza ndipo wanafunga ndoa...Walivunja amri....NO NO NO NO...Washindwe kwa jina la Yesu

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 13, 2009

    Wala siwapi hongera...Yani wameshaibana weeee...sasa ndio wanajua kuwa kuna Mungu wanafunga ndoa!!!! Hata mmea wameshaupanda umeota....HAPANA

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 13, 2009

    Kwa mnaojiuliza maswali mengi hapo juu:
    Wawili hawa walishaoana kitambo, zaidi ya mwaka, sasa wamejaaliwa mtoto ndo wanashukuru kupata mtoto na kuwa salama na pamoja mpaka leo.
    Maybe wangeleta picha ambayo siyo ya harusi, maana hii imechanganya wengi

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 13, 2009

    mwanamke ameshazaa halafu anavaa "shela", hiyo kali.mimi najua binti kuvaa shela ambayo ni nguo nyeupe ya harusi inaashiria binti alikuwa safi yaani hajaguswa.huu mtindo wa kuvaa shela wakati tayari una mtoto au mimba ni kuidhalilisha hiyo nguo pamoja na mvaaji pia na dini yake.yafaa tuache. kama unabariki ndoa vaa mavazi mengine lakini siyo shela.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 13, 2009

    Bibie umependeza. Alafu una uzuri wa asili sio wa mipambo, utafikiri kama wewe sio mbongo, manake wabongo kwa michubuo nao hawajambo, wewe uko asilia, natural beuty,African queen,

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 13, 2009

    Kuna watu mnaandika humu kama vile ndiyo mmeamka kutoka kwenye coma/kupoteza fahamu tangu miaka ya 1953 na ndiyo mnaamka na kushtukia maisha ya leo!! Au kama vile ndiyo mmeshuka toka sayari ya Neptune na kuingia sayari hii earth!
    Na nyie mnaojifanya watu wa dini sana ebu jiangalieni na mji hukumu kwa ukweli wote.....acheni kujifanya kuwa watakatifu; unafiki mtupu. Shela zinavaliwa na yeyote.

    Hongereni waarusi na tunawatakia maisha marefu ya furaha, amani na uaminifu.

    J.
    Toronto Canada.

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 13, 2009

    hongereni kwa kujaliwa mtoto na ndoa bora!..
    samahani layla naomba kuuliza kama ni wewe tuliosoma pamoja shule ya msingi lugalo au nimekufananisha maana hii sura c ngeni kwangu!...
    Hongereni sana

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 13, 2009

    Humu ndani ndio utagundua ni jinsi gani Akili za watu zilizo hazina Akili na comment zao za kipumbavu mara "mbona jamaa kauchuna atakuwa rud"

    Hivi kweli binadamu aliye kamili anaweza kutoa comment ya kipumbavu na kipuuzi kama hiyo hapo kwenye mabano.Amakweli bado kuna wajinga wengi sana kwenye jamii yetu na watu kama hawa wanabidi waelimishwe.

    Kenge

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 13, 2009

    michu umenibania tangu jana, nimeuliza Roberto Carlos original ana shughuli gani au ni nani?

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 13, 2009

    Wazee wa darajani hatukubali, tutaandamana dogo second-born aitwe John Terry Muhuga!! Kazi kwenu na wajaluo wakitaka Barack Obama Muhuga! Hongereni. Ndoa yenu na idumu katika Jina la Yesu Amen!

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 13, 2009

    Hey Carlos, next time uwe careful, picha za bibie poa, utaibiwa. Hongereni, keep her up

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 14, 2009

    HUYO ANAESEMA SHERA LINAASHIRIA BIBI HARUSI HAJAGUSWA MSAFI NADHANI HAJUI ALICHOKIANDIKA NA HAJUI ASILI YA SHERA SIO UTAMADUNI WA MWAFRICA HALIKUANZIA AFRICA!!
    SO HAO WAZUNGU AMBAO NDIO TAMADUNI ZAO HAKUNA AMBAYE ANAOLEWA AKIWA BIKRA!!WANALAMBANA WEE MWISHO WANAISHIA KTK NDOA ZAO ZA MIKATABA SASA UNATAKA KUSEMA HIZO K ZAO ZILIKUA HAZIJAGUSWA?MAANA WENGI WAO WANAKUA TAYARI WAPO KTK FAMILIA

    ACHENI KUBWABWAJA

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 14, 2009

    Nyinyi mnaofagilia kulambana hadi mimba ndo mvae shela hamuelewi maana ya shela.kama huwa mnaenda kuabudu dini yoyote waulizeni walimu wenu wa dini watawaeleza.na msichukue mifano ya wazungu kuvaa shela wakati tayari wana watoto bali mfuate kitu gani kinatakiwa kulingana na mafundisho ya dini yenu.naona ninyi ni wakware kama wanavyosema watoto wa mjini.tena mshindwe kwa jina la Yesu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...