Home
Unlabelled
CCM yakanusha vikali ripoti ya kuzomewa viongozi wake
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
dah!kaka tambwe nakukumbuka sanaa enzi zile za CUF tmk leo umevaa jezi ya njano!dah maisha kwelı kıbao,
ReplyDeleteKwa UFISADI wa sasa mtazomewa sana tuu,Mchuzi katuchukulie video kusiwe na ubishi.
ReplyDeleteanony wa 11:27, nakubaliana nawe kabisa nadhani picha za video sio suala gumu sana siku hizi.
ReplyDeleteKama anabisha (mkuchika) sasa kwanini wameamua kufanya kampeni za ndani kama siyo kuogopa kuzomewa? Na kama hawazomewi walw wamafunzi wa shule ya sekondari Butundwe kwa nini walichapwa viboko?
Tanzania tubadilike kweli Mwanafunzi wa Secondary leo hii wanahadhibiwa kwa bakola?
ReplyDeleteNapenda kutuma salamu kwa ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo.
ReplyDeleteUjumbe nasema: kuzomea na kushangilia yote ni makelele!!!
-Bingwa wa salamu
Hizo kazi waachieni vijana wa ccm nchi za nje maana wao ndio wenye mwamuko wa kulisaidia taifa letu sio nyie kuangalia matumbo yenu tu. Tunafuraishwa sana na wenzenu wanavyojitaidi kulitangaza taifa letu huko ng'ambo,sio tu kuiba mali za babu zetu.
ReplyDeleteChadema nangojea sana mambo yenu, sio hawa chama cha majungu (ccm)
I will say it bluntly, obesity may have adverse affect on one's health and it might instigate fatal chronic diseases. The question to be asked is if a person can not take care of his/her body then why should expect him/her to take care of the country?
ReplyDeleteForget about the election for a minute; these people need to find way that will enable them to shed some pounds
Mi si shabiki wa chama chochote ila inachusha siyo kuchosha yanayotendwa na cCm. Kwanza kwenda kwenye Waathirika wa mabom mmevaa tshirt za ccm mnataka kusema walolipua ni upinzani? Je jeshi lipo kwa chama gani kama si kwa wananchi wote? iweje watoa misaada wanajitambulisha kivyama ili waathirika iwaingie akilini wale walowasaidia kama si rushwa ya mkono mwingine?
ReplyDeleteIweje mpaka mwenyekiti wa mtaa anadiriki kujiudhuru wazifa kunusuru watu wake?
Si siri twajua wote wasomi na mbumbumubu kuwa ili upate hata leseni ya biashara yabidi ujiunge na chama cha mapinduzi.
Time will tell, not all athe time you will cheat and win.
Waangalie hao viongozi walivyofura si kupendeza ila epa inafanya kazi na watakwenda wote. pole pole.
Mbona kuna kero nyingi sana zinazowakabili wananchi kuliko kupoteza muda na kujadili mambo ya kuzomewa? Who cares?
ReplyDeletemdau ughaibuni!
ila kiukweli CCM ulaji upo huyo Tambwe alivyokuwa CUF alikuwa choka mbaya!
ReplyDeleteMbona hata mimi nilizomea sasa mwamdanganya nani kama hamjazomewa?
ReplyDeleteMlipowafikisha wanyonge wa nchi hii...MTAZOMEWA TU....hiyo haitakuwa ajabu.
ReplyDeleteNa inaonekana huu ni mwanzo....kuna siku mizomeo itazidi mpaka mtashangaaa
KISA? Tamaaaaaaa zenu....simple.
Mngetenda kazi kwa ufanisi, yasingewakuta yanayoanza kuwakuta sasa...
WAPINZANI WAKIZOMEWA CCM HUWA MBELE KUSEMA HAWANA SERA, CCM IKIZOMEWA INAANZA PROPAGANDA ZA KISOSHALISTI KUWA WALIKUWA WAKIPONGEZWA ILA MWANDISHI HAKUEELEWA! DUH! CCM KUBALINI TU KWANI KUZOMEWA NI SEHEMU YA MAISHA ILA MBAYA PALE MNAPOAMUA KUWACHAPA VIBOKO WATOTO WANAOWAZOMEA NA MBAYA ZAIDI NI KUWA MNAWAFUNDISHA WAANZE KUWACHUKIA WAKIWA WANGALI WADOGO SIJUI UKUBWANI ITAKUWAJE. UCHENI UFISADI ILI MSIZOMEWE DUNIA INABADILIKA SI YA ENZI ZA PROPAGANDA, NA KAMA ISINGEZOMEWA ISINGEKUWAPO HAJA YA CCM KUJIBU SHUTUMA KWA KUTUMIA VIONGOZI WA PROPAGANDA YAANI VIONGOZI WENYE UJUZI WA KUSHAWISHI UONGO UWE UKWELI NA UKWELI UWE UONGO. CCM IMEWATUMIA TAMBWE NA MKUCHKIKA KWA KUAMINI KUWA WANAWEZA KUSHAWISHI UKWELI UONEKANE NI UONGO.
ReplyDeletedawa yao ni video tu bro michuzi, mana mimi mwenyewe ni mmoja ya waliozomea, iweje wakane, wajue busanda si yao tena (wakubali tu jimbo washaliuza) wamegawa maeneo yetu wanategemea tuwape tena
ReplyDeleteMimi ninawashangaa kwelikweli, simnajiita kuwa mumekomaa kisiasa kidemokrasia, sasa kwanini mkatae `chalenji'
ReplyDeleteKuzomewa nisehemu ya kundi la watu kutoa maoni yao kwa `njia hiyo' na hiyo ni demokrasia . Je mlitaka kila mara muimbiwe nyimbo za kuwatukuza tu, hamuoni mkifanyiwa hivyo mtalemaa,na watakaowafanyia hivyo watakuwa wanawadanganya, sifa sifa sifa..kwani nyie manabii, kwani nyie nana,hapana.lazima mpate msukosuko ili mjue nini kinachowasibu raia.
Kama mtabakia kujibu kuwa ` hapana hatukuzomewa' basi nahisi hamna kazi ya kufanya. Jibuni nini wananchi wanataka, wamekosa nini mpaka wafanye hivyo!
M3
na bado,,,
ReplyDeletena kadri mnavochapa watu ndivo mnavoonyesha madhambi yenu na ndivo mtakavyochukiwa
nchi sio ya kijeshi hii
Loo, madaraka matamu sana! Kuandika wamezomewa imekuwa nongwa, mtakapokosa jimbo mtamtafuta mchawi! Kutawala mnapenda lakini kuwajibika hamtaki. Wenzetu ughaibuni ndege ilipita chinichini isivyo kawaida viongozi wakawajibika, sisi WATU WANAKUFA KWA MABOMU MBAGALA hakuna hata kiongozi mmoja aliyewajibika!!
ReplyDeletehaoooo hayoooo majiziiiii,mafisadiiiii ccm hayooo.haya Tambwe hiza kanusha pia hilo mie nimezomea
ReplyDeletejamani tatizo wengi hawakuwa wanajua kuwa PROPOGANDA maana yake ni kusema UONGO.sasa Mkuu wa kusema uongo ni HUYO si ndo huyo Tambwe? kapelekwa kubadili ukweli kuwa uongo hapo juu kuna wadau wanazomemea ila michuzi anawabania.
ReplyDeleteMNAJIPA MOYO KUSEMA KUWA CCM IMEZOMEWA. BASI IWEJE VYOVYOTE WATU WANA IMANI NA CCM NA USHINDI NI WA CCM. MLIE TU. WATANZANIA SI WAJINGA. WANATAMBUA MAENDELEO YALIYOLETWA NA CCM. KUIMBA WIMBO WA UFISADI BILA KUWAAMBIA WANANCHI MTAWAFANYIA NINI HAKUTAWAPENI USHINDI!!SERA YENU NI UFISADI TU??CCM JUU, JUU ZAIDI!!!
ReplyDeletePOLE sana momba tambwe,ngoja Magesa apate nauli aje mjini.atawazomea yeye kwa kuwawakilisha wana Busanda.aah natania tu mjomba ila tahamaki ushindi huo
ReplyDeleteMICHUZI NINAKUOMBA UWATUMIE ANUANI YA BLOG YAKO AKINA TAMBWE NA MKUCHIKA ILI WAONE KUWA HAO WALIOWAZOMEA NI SEHEMU TU YA WATANZANIA WALIOWACHOKA WANACCM KUTOKANA NA UFISADI ULIOKITHIRI KIASI CHA KUFANYA BAADHI YA WAKAZI WA JIJI LA DAR KUISHI SEHEMU ZILIZOKITHIRI KWA UCHAFU NA TOPE HATA WENGINE WANISHI KAMA SAMAKI NYUMBA ZAO ZIKIWA ZIMEJAA MAJI NDANI. SEHEMU TUNAZOISHI HATA MBWA WAFUGWAO NA HAO WAHESHIWA HAWAWEZI KUKUBALI KUISHI, NGUO ZAO SAFI SANA ZINANG'AA KIJANI LAKINI ROHOZAO ZIMEJAA UFISADI.
ReplyDeletekama hawazomewi kwanini wananua pasi za kupigia kura? wadau angalieni dullonet umati wa watu chadema (bonge la suprise)na wanafunzi butundwe walichapwa kwa nini? tumechokaaaaaaaaaaaaaa.....
ReplyDeleteMWANZA ni moja kati ya ngome kuu za ccm,kama nao wamebadilika basi 2010 ni upunzani ikulu OTHERWISE PLEASE REMEMBER WAT HAPPENED IN KENYA AFTER 2007 GENERAL ELECTION
TZ ONE DAY "YES"
Sipendi kuusifia upande wowote bali wapiga kura wenyewe ndio waamuzi.Lakini ukweli halisi wa matukio katika hizi Kampeni za kisiasa ni lazima usemwe bila kupendelea upande wowote.Mimi binafsi nilikuwepo kijiji cha Nyarugusu siku CCM walipokuja kuhutubia wananchi wa pale katika uzinduzi wao wa Kampeni za Uchaguzi ambazo ziliongozwa na Mh.John Malecela wakiwemo kina Capt.Komba na kundi zima la TOT.Mh. Pius Msekwa hakuwepo Nyarugusu siku hiyo,kwa hiyo sio ujanja kusema kwamba na yeye pia alikuwepo wakati hakuwepo.Baadhi ya Magazeti nchini yaliripoti siku hiyo kwamba Mzee Malecela na Mzee Pius Msekwa walizomewa katika mkutano huo wa hadhara.HILO SILO KWELI,MIMI BINAFSI NILIKUWEPO,NA MIMI SINA CHAMA CHA SIASA!Nina kazi zangu nyingine tu binafsi.Kwa hiyo kwamba Msekwa naye alizomewa sio kweli.Tukija kwa Mzee Malecela naye pia kwa mchambuzi wa siasa huwezi kusema kwamba alizomewa na hadhara iliyokuwepo pale mkutanoni.SIYO SAHIHI.Kwanza lazima upate tathmini ya makundi ya watu waliohudhuria mkutano ule.Idadi kubwa ilikuwa ya kina Mama na Watu Wazima,wote hao karibu Theluthi Mbili ya watu wote waliohudhuria mkutano ule.Theluthi Moja iliyobaki ilikuwa ya VIJANA WACHIMBAJI WADOGO WADOGO WA DHAHABU.Mzee Malecela alichukua muda usiopungua Nusu Saa Nzima kunadi sera za CCM ikiwa ni pamoja ni pamoja na kumnadi Mgombea wa CCM.Kelele za Vijana Wachimbaji wa Dhahabu zilianza kusikika pale Mzee Malecela alipoanza kugusia sekta ya uchimbaji wa dhahabu pamoja matatizo yanayo wakabili wachimbaji hao na jinsi serikali ya CCM ilivyodhamiria kukabiliana nayo.HAPO NDIPO KELELE ZILIPOSIKIKA kwamba wachimbaji wamesahaulika,serikali yao haiwathamini wala kuwajali bali imekumbatia zaidi wawekezaji wa kigeni kuliko wachimbaji wadogo wadogo wazalendo.Kila Mzee Malecela alipojaribu kuwatuliza Vijana wale Wachimbaji japo watulie wasikilize nini CCM imedhamiria kufanya kutanzua baadhi ya matatizo yao,wale Vijana walizidisha kelele juu zaidi na huku wakinyoosha juu Vidole Viwili vya Ushindi wakiashiria kwamba wata ipa support CHADEMA badala yake.Nilipomuuliza kijana mmoja mchimbaji mdogo wa dhahabu kwanini waliamua kufanya vile iwapo wao ni wafuasi wa CHADEMA na mkutano ule haukuwa wa Chadema bali wa CCM,alinijibu kifupi tu kwamba "wamechoka kwa manyanyaso wanayoyapata,ya kufukuzwa fukuzwa katika maeneo yao ya asili ya uchimbaji wa dhahabu na badala yake kuna mchezo mchafu unaofanywa na baadhi ya watendaji wakuu wa Wizara ya Madini kumega eneo kubwa kupita kiasi na kuwagawia Kampuni Moja tu ya I AM GOLD ambayo awali ikijulikana kwa jina la EAST AFRICA MINES,kwa mfano!Na wao kuachwa wakitangatanga kama Wakimbizi katika ardhi yao wenyewe.Na hilo ni mbali na Zana Duni na Ukosefu wa Mitaji na Miundo Mbinu bora kwa Wachimbaji hao wadogo,JAMBO AMBALO MZEE MALECELA ALIKIRI LIPO NA LINAFANYIWA KAZI hususan baada ya Tume ya uchunguzi katika sekta ya madini iliyo ongozwa na Jaji Bomani kuwasilisha ripoti yake serikalini.SASA UKITAKA KUYAITA HAYO MALALAMIKO YA VIJANA KWA MZEE MALECELA kwamba ALIZOMEWA basi huo ni uamuzi wako.Nimelitolea ufafanuzi jambo hilo kwa faida ya Watanzania walioko sehemu zingine mbali kabisa na eneo hili la Kampeni za Busanda.Walioripoti habari hiyo katika magazeti kadhaa likiwemo la Mwananchi mimi naweza kusema kwamba "That was Cheap Reporting!I wouldn't even call it Biased Reporting.Utaandikaje ripoti kwa habari za kudandia tu na wewe mwandishi ukiwa sehemu nyingine kabisa na ukaamini ulicho ambiwa ni sahihi kabla ya kuchukua tahadhari kulinda jina lako na heshima yako katika Fani ya Uandishi wa Habari?Pity on You Cheap Reporters!ANDIKENI UKWELI JAMANI.kama kweli mtu akizomewa basi andikeni lakini sio kuleta Uzushi ili kuuza kwa sana Magazeti yenu au ili uonekane ni Ripota unaye jituma saaaana!
ReplyDeleteMh. Tambwe anafaidi matunda ya ufisadi ndiyo maana kakaa kifisadi. Mcheki hilo tambi!!!!!!!!!!
ReplyDeletewadau unajua hawa jamaa wanadhani wataendelea kila siku kuongopa na kukubaliwa na wananchi? Kiukweli nchi ipo wakati mgumu sana, Kipindi ambacho akina mama wajawazito 24 wanafariki kila siku na huku chama tawala wakifungua matawi mapya ughaibuni, kesi za wala fedha za umma zikitaka kufutwa kwa kukosekana kwa ushahidi, asilimia karibu 30 ya fedha za bajeti zikipotea mikononi, wabunge wakijadili kuongezewa posho na ulaji mwengine, walimu wakisubiri mishahara yao halali kwa miezi mitatu na zaidi, madaktari wakigomea posho ndogo wanazopewa, madawa yakiuzwa madukani, shule bila vitabu, madawati, na walimu,
ReplyDeleteduhh! kila la heri nchi yangu!
CCM JUU, CCM MAREKANI JUU. NILIFURAISHWA SANA NA KITENDO CHA WANA CCM MAREKANI KUONNYESHA SINEMA INAYOHUSU TANZANIA NA KUWAALIKA WATU MUHIMU KUTOKA SERIKALINI KAMA VILE MEYA NA VIONGOZI WA NGAZI ZA JUU KUONA SINEMA ZA NCHI YETU.
ReplyDeleteHAYO NI MABO MUHIMU KWA TAIFA LETU. NAWAPONGEZA SANA VIJANA.
Du??We Mkuchika kuzomewa tu mnataka kusoma Albadili. Hebu jielekezeni kwenye kampeni za maana. Kuzomewa ni jambo la kawaida. Na nyie si muwaambie mashabiki wenu nao wakawazomee CHADFEMA na wengineo. Aah
ReplyDeleteMtoa maoni Tarehe May 12, 2009 3:38 PM, Umesema hivi
ReplyDelete``HAPO NDIPO KELELE ZILIPOSIKIKA kwamba wachimbaji wamesahaulika,serikali yao haiwathamini wala kuwajali bali imekumbatia zaidi wawekezaji wa kigeni kuliko wachimbaji wadogo wadogo wazalendo.Kila Mzee Malecela alipojaribu kuwatuliza Vijana wale Wachimbaji japo watulie wasikilize nini CCM imedhamiria kufanya kutanzua baadhi ya matatizo yao,wale Vijana walizidisha kelele juu zaidi na huku wakinyoosha juu Vidole Viwili vya Ushindi wakiashiria kwamba wata ipa support CHADEMA badala yake.''
Makelele sio kuzomea? Swala la muhimu hapo,sio kupinga kuzomewa , swala la muhimu ni kujibu matatizo yao. Kwanini tunapenda kusifiwa sifiwa tu, nguo nyeupe ina madoa ya uchafu,hamtaki muambiwe huo ni uchafu mnang'ang'ania hayo ni maua. Jamani itafika siku hamtazomewa tu...
TANZANIA DAIMA LINARIPOTI HII
ReplyDeleteDiwani wa CCM Busanda anaswa akinunua shahada
• Adai ameagizwa na viongozi wa juu CCM
na Kulwa Karedia, Busanda
JESHI la Polisi wilayani Geita, mkoani Mwanza, linamshikilia Diwani wa Kata ya Busanda kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa tuhuma za kununua shahada za kupigia kura, kinyume cha sheria.
Diwani huyo, Alfonce Mbogo Matonange, alikamatwa juzi usiku majira ya saa 5 katika Kijiji cha Shilungure, wilayani hapa, akinunua shahada hizo kwa madai kuwa ameagizwa na viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho.
“Hata mkinikamata sawa, lakini mimi natekeleza maagizo ya viongozi wangu wa ngazi za juu, ambao wametaka tufanye zoezi hili kwa ajili ya kujiandaa na uchaguzi huu, sasa naona kama mnanionea tu mimi,” alisema diwani huyo wakati akiingizwa kwenye gari la Polisi aina ya Defender, lenye namba za usajili, PT 0901.
Pamoja na kauli hiyo, diwani hakuwa tayari kuwataja viongozi hao wa ngazi za juu waliomtuma, kwa madai kuwa akifanya hivyo, atakuwa amekiuka utaratibu wa chama.
Shukrani kwa mdau usiye na chama kwa kutufafanulia yaliyojiri. Kimsingi nimeelewa kwamba Malecela hakuzomewa. Kilichotokea ni KELELE ZILISIKIKA. Kwa maneno mengine habari ingekuwa iliripotiwa kwa usahihi zaidi kama ingesema CCM WAPIGIWA KELELE badala ya CCM WAZOMEWA.
ReplyDeleteKwa kuwa huyo Anony hapo juu anayesema si shabiki wa chama chochote, amesema ninayo haki ya kutafsiri ninavyotaka: maneno yake yafuatayo mimi nayaita kuzomea:
ReplyDelete"Kelele za Vijana Wachimbaji wa Dhahabu zilianza kusikika pale Mzee Malecela alipoanza kugusia sekta ya uchimbaji wa dhahabu pamoja matatizo yanayo wakabili wachimbaji hao na jinsi serikali ya CCM ilivyodhamiria kukabiliana nayo.HAPO NDIPO KELELE ZILIPOSIKIKA kwamba wachimbaji wamesahaulika,serikali yao haiwathamini wala kuwajali bali imekumbatia zaidi wawekezaji wa kigeni kuliko wachimbaji wadogo wadogo wazalendo.Kila Mzee Malecela alipojaribu kuwatuliza Vijana wale Wachimbaji japo watulie wasikilize nini CCM imedhamiria kufanya kutanzua baadhi ya matatizo yao,wale Vijana walizidisha kelele juu zaidi na huku wakinyoosha juu Vidole Viwili vya Ushindi wakiashiria kwamba wata ipa support CHADEMA badala yake.Nilipomuuliza kijana mmoja mchimbaji mdogo wa dhahabu kwanini waliamua kufanya vile iwapo wao ni wafuasi wa CHADEMA na mkutano ule haukuwa wa Chadema bali wa CCM,alinijibu kifupi tu kwamba"
Wewe anony wawa saa 4:12, ccm marekani gani unayoongelea? Hayo mambo yako huko ulaya marekani hayapo. kama unadai yapo hebu tatajie ni ccm tawi la wapi? Marekani watu wanatafuta mkwanja siyo mambo yakutegemea kuja kubebwa na chama kilichojifia.
ReplyDeleteHalafu wewe Tambwe Hiza kuja hapa kujifanya kukanusha eti ulikuweko kwenye mkutano haisaidii kwani wenyewe wamekiri kuna watu wameandaliwa sijui kutoka Tarime na tueleze kama hawazomewi iweje waamue kufanya mikutano ya ndani.
KUZOMEA AU KUPIGA MAKOFI KWA FURAHA NI MOJA YA UHURU WA KUJISEMEA
ReplyDelete(FREEDOM OF SPEECH) KWENYE DEMOKRASI - (THAT IS IF WE HAVE DEMOCRACY) TUWEZE KUJIELEZA BILA YA KUOGOPA AU KUADHIBIWA. WANANCHI WANAOFUTA TU KAMA VIPOFU - HAISAIDII KUENDLEZA NCHI, KILA WACHOFANYA VIONGOZI SIO LAZIMA KUWA NI SAWA AU VIZURI.
TULIONA HII HUKO ZIMBAMBWE RAIA WANATESWA AU KUULIWA IWAPO HUKUBALIANI NA CHAMA AU SERIKALI - HIYO NI DICTATORSHIP NA AGAINST HUMAN RIGHTS - TANZANIA LET'S GROW UP POLITICALLY, ECONOMICALLY & SOCIALLY
Wakati huo huo, CCM wilayani Geita kimekiri kwamba viongozi vigogo wa Chama hicho, walizomewa katika mkutano wa hadhara ulioanyika katika mkutano Katoro katika jimbo la Busanda.
ReplyDeleteChama hicho kimekiri suala hilo, siku chache baada ya uongozi wa Makao Makuu ya CCM kikanusha taarifa hizo.
Hivi karibuni baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa Makamu Mwenyekiti Pius Msekwa na Makamu Mstaafu, John Malecela, walizomewa na wananchi katika mkutano wa hadhara.
Akizungumza na waandishi wa habari wilayani Geita Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Busanda Dani Mollel, alisema tayari amepokea barua ya CCM ikilalamikia hatua ya viongozi wake kuzomewa.
Alisema amepata barua hiyo ya CCM iliyoeleza kwamba kuna chama kimekodi vijana kutoka nje ya jimbo la Busanda kwa ajili ya kufanya kazi ya kuzomea viongozi wao.
“Nimepata barua ya malalamiko kwamba kuna chama kimeleta vijana kutoka nje ya jimbo kwa lengo la kuhudhuria mikutano na kujipanga barabarani ili kuwazomea viongozi wakuu,”alisema msimamizi huyo.
Kufuatia malalamiko hayo Mollel alisema amelazimika kuitisha kikao cha dharura kujadili suala hilo.
Alisema ili kukomesha tabia hiyo, ameona ni vema aitishe kikao cha majadiliano baina ya vyama vyote ili kufikia muafaka.
“Nimeamua leo (jana) mchana kuitisha kikao ambacho kitawajumuisha makatibu wa vyama vyote vinne ambavyo vimesimamisha wagombea, ili tujadiliane pamoja kwa upendo ili kufikia muafaka wa jambo hili,” alisema Msimamizi huyo.
Hata hivyo msimamizi huyo alisema hadi sasa hapajatokea tukio kubwa la kuashiria uvunjifu wa amani au lenye lengo la kuvuruga mwenendo wa kampeni za vyama hivyo zinazoendelea.
Mollel alivionya vyama vyote vinavyoshiriki kuhakikisha wagombea wao wanakuwa wavumilivu, watulivu, wenye kueneza sera zao wakati wa kampeni, badala ya kufanya vitendo viovu.
“Najua maneno ya vijembe kwenye kampeni au kwenye siasa kwa ujumla haviepukiki, lakini mambo ya uvunjifu wa sheria hayafai, na ni kinyume cha sheria ya uchaguzi,”alisema Msimamizi huyo.
Alisema kimsingi vyama vyote vimekuwa vikiwasilisha malalamiko kwake, lakini akasema malalamiko mengine ni madogo mno na mengine hayana msingi kabisa.