Ras Makunja

Radio Free Africa Kumrusha Live !kiongozi wa The Ngoma Africa Band!
Bwana Kichwa Ngumu Ras Makunja!!!
 
Siku ya jumamosi ya 09-Mai-2009, wasikilizaji wa Radio Free Africa (RFA) watapata nafasi ya kusikiliza mahojiano Live! kati ya RFA na Kiongozi Kiongozi wa bendi maarufu barani ulaya The Ngoma Africa aka FFU! aka The Golden Voice of East Africa,mwanamziki,Ebrahim Makunja aka Ras makunja alimaarufu Bw.Kichwa Ngumu,mtunzi na mwimbaji mchokozi.

Mwanamziki huyo atapeperushwa hewani kwa maswali na mtangazaji Bw.Baina Kamukulu kutoka Radio Free Africa inayorusha matangazo yake mjini Mwanza.

wasikilizaji watege sikio kusikia maohijiano hayo kati ya mwanamziki huyo mwenye kukomaa kichwa katika majukwaa ya kimataifa na kikosi chake cha The Ngoma Africa Band,bendi ambayo imejizolea umaarufu huko ughaibuni kwa kutumia mziki wa dansi wa bongo.bendi hiyo yenye mtaji wa maelfu ya washabiki barani ulaya na kila kona duniani, ni mashuhuri kwa kuwatia kiwewe washabiki kila wanapotumbuiza.

Nini?kitakachozungumziwa katika mahojiano hayo kati ya Bw.Kichwa Ngumu Ras Makunja
 na RFA ni kitendawili ambacho kitapata jibu siku ya Jumamosi 09-Mai 2009 kuanzia saa 4.00 asubuhi.Tega sikio ! 

Pia unaweza kuwafuata ngoma africa hapa 
www.twitter.com/thengomaafrica 
au sikiliza
www.myspace.com/thengomaafrica

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2009

    kicha wetu,simba usielala usingizi!
    ustaadhi bwana kichwa ngumu wa madongo mazito karibu Mwanza,hapa sangara,sato wa kumwaga tuuu!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 05, 2009

    te!!!te!!!te!!!! ziwa victoria sasa limeingia luba?
    kamanda wa FFU ndani ya nyumba?
    Mwanawane hi!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 05, 2009

    mungu wangu,gwaride ndani rfa?
    kaka mie uniacha hoi unaporusha madongo,nakuwavalia miwani unaowarushia

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 05, 2009

    eh! ras makunja! ulivyotabasamu utafikiri mtu !kumbe simba unapokuwa kazini kwako,heri yako kaka

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 05, 2009

    Kaka braza makunja,vipi?yule nyau? aliyekula kitoweo cha ffu? nasikia mlimaliziana na mmiliki wake au?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 05, 2009

    bro,kaka ras makunja,vipi?madongo yako?tunasikia unarusha mahala popote hata penye nyumba za kuabudia!ukiona kuna linalokukera basi lazima uyarushe,kweli wewe kifaa cha kazi

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 05, 2009

    Kichaa wetu,vipi?hizi habari wanazovumisha wadaku kuwa nasikia
    mama kimwaga wa kitaliano Donatela Versace kakushikisha kitu kidogo!tufafanulie basi hili tugawane

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 05, 2009

    Kamanda ras makunja,nakuamini na ffu wako,vipi sasa huku sweden baridi hakuna msimu wa joto umeshaanza lini ?mtakuja na gwaride?

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 05, 2009

    kaka braza ras makunja bin madongo,mie nasubiri nikusike una wito gani? kwa wanamziki wenzio wanao pigwa na jua hapa bongo.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 06, 2009

    Sasa nimekubali kua Ras Makunja, akijulikana kama kichwa ngumu, mambo yako sio mchezo.nimekukubali kamanda wetu na kundi lako la FFU.
    Itabidi nikusikilize kwa makini sana siku ya maojiano yako.
    Tumekua na kiu cha kukusikia kwa muda mrefu sana, nyimbo zako tunazisikia lakini wewe mwenyewe sijapata bahati ya kukusikia ukitoa husia kwa watu tulio kuapo hapa bongo.
    Nakutakia kila la heri na mungu atakusaidia utafika safari yako ya kimuziki,ukizingatia unanidhamu ya hali ya juu katika fanni yako ya muziki.
    Mdau Iringa

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 06, 2009

    Haya kaka Makunja, tunategeme kua utakuja kuturusha roho na sisi hapa Holland,tumekua tukikusoma kwenye magazeti tu ya hapa, na kukusikia kwenye radio, sasa tunaomba utukumbuke na sisi summer hii,tunakusubiri kwa hamu kubwa.
    Mdau NL

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 07, 2009

    Mkuu Ras Makuja na kikosi chako FFU aka The Ngoma Afr!ca inayochezesha mpaka makasisi wa dini zote,Kamanda ombi langu nakuomba mje huku Iceland,tunahamu ya kucheza mdundo wenu usiokuwa na mpinzani.
    Mdau wa Barafuni aka Iceland

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...