Cover Kiswahili kwa Waswidi
Waandishi wa Kitabu Kiswahili kwa Waswaidi Imma na Karin walipohojiwa na magazeti wiki moja kabla ya uzinduzi.
Waandishi wa kitabu na pulisher wao katikati Lars Hjalmarsson
Wageni wakikaribishwa sambusa na Cider
Wageni  wakiingia katika ukumbi wa sherehe.

Kampuni ya Watatu Textile AB katika harakati zake za kukiendeleza kiswahili ng’ambo kimetoa kitabu ”Swahili för svenskar” (Kiswahili kwa Waswidi).
Waandishi wa kitabu hicho ni Imma Mpili Andersson na Karin Zetterqvist.

Sherehe ya uzinduzi wa kitabu hicho ilifanyika katika Ukumbi wa ABF-huset mjini Stockholm tarehe 28 April 2009. Kati ya waliohudhuria kulikuwa na wawakilishi toka Balozi za Kenya na Tanzania.

Kitabu hicho ni cha aina yake kwa kuwasaidia Waswidi watalii na Waswidi wanaofanyakazi katika miradi mbali, katika nchi za Afrika Mashariki kule Kiswahili kinazungumzwa.

Kamusi ya Kiswahili-Kiswidi, Kiswidi-Kiswahili ipo tangu zaman. Lakini kitabu cha kuwasiaidia wageni kutunga sentensi fupi za kuombea maji au kuuliza njia ya kwenda stesheni hakikuwepo. Kipo kimoja kilichotolewa miaka 40 iliyopita.

Kwanza kwa kuzingatia kuwa Kiswahili kimepiga hatua, na pili mahitaji ya kitabu Kiswahili-Kiswidi tuliona wakati umefika wa kutoa kitabu kipya.

Shukrani nyingi kwa ndugu na marafiki nyumbani Tanzania waliotusaidia kufanikisha kitabu hicho. Bila wao tusingeweza kupata Kiswahili sanifu cha kisasa. 

Asanteni sana.

Waandishi wa Kitabu:
Imma Mpili Andersson na Karin Zetterqvist
Sweden

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hur läget
    jätt bra bra braaaa vi behover den
    swahili för svenskar.SFS

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 08, 2009

    acheni ubaguzi wa sentensi sio kusema kitabu hicho kusudi ni kwa waswedi wanaoenda easte afrika babili pia hata wabongo wanaoenda uswidi

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 08, 2009

    Anony May 08, 2009 2:29PM umea mbiwa kitabu hiki ni mahsusi kwa Waswidi wasiofahamu kiswahili ili wakija ktk nchi zinazoongea kiswahili Afrika angalau waweze kuombea maji au kuuliza kituo cha reli au mabasi n.k sasa hapo kuna ubaguzi gani?

    Labda siku za usoni kutatokea waandishi watakaotunga kitabu kwa waswahili ili nasi tuweze kuombea maji au kuulizia stesheni ya reli tukienda Sweden.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 08, 2009

    SAFI SANA WADAU. TENGENEZENI/FYATUENI NA CD ZAKE MTATENGENEZA HELS ZAIDI.

    MDAU UK

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 08, 2009

    Michuzi, uyo mama wa kizungu picha ya pili bado yuko single? Nimependezeshwa na tabasamu lake. Nitafutie email yake

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 09, 2009

    safi sana tupeni vitabu kwa ajili ya kufundisha wasio jua kiswahili sio wazungu tu hata watanzania wenye fikra za kitumwa tutawafundisha namna ya kujidai na lugha yao ya taifa na kuondokana na dhana za kishamba vichwani mwao

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 10, 2009

    wacheni kuharibu lugha Hicho ni Kiswahili na sio swahili .tupeni nafasi jamani.Mzee Ali Hassan mwnyi na Mzee aboud jumbe mko wapi mnawachia watu wasiokuwa na chimbuko la kiswahili wanacheza la lafdhi ya kiswahili kiasi hichi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...