JK akimfariji mhariri wa gazeti la mwanahalisi, saeed kubenea, baada ya kujeruhiwa kwa kumwagiwa tindi kali mwaka jana

MAHAKAMA Kuu imewaamuru Mhariri, msambazaji, mchapishaji wa gazeti la Mwanahalisi kumlipa Sh Bilioni tatu Mfanyabiashara Rostam Aziz kwa tuhuma za kuchapisha habari ya kumkashfu kwa kumhusisha kushiriki kwenye tuhuma za kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond.
 
Uamuzi huo ulitolewa April 30, Mwaka huu na  Jaji wa mahakama hiyo  Robert Makaramba, baada ya walalamikiwa kushindwa kutoa utetezi dhidi ya kesi iliyofunguliwa na Rostam ambaye pia ni Mbunge wa Igunga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
 
Katika kesi hiyo, Rostam alilifungulia kesi Gazeti hilo la Mwanahalisi baada ya kuchapisha taarifa ya kumkashifu wakili wa Rostam.
 
 
Katika uamuzi wake Jaji Makaramba alisema kuwa baada ya Rostamu kufungua kesi hiyo Aprili 22, Mwaka jana, walalamikiwa walishindwa kuwasilisha utetezi wao ndani ya siku 21 kwa mujibu wa sheria kitendo kilichomfanya wakili Kennedy Fungamtama anayemtetea Rostam kuiomba mahakama hiyo kutumia vifungu vilivyoko chini ya sheria ya mwenendo wa makosa ya madai kutoa hukumu dhidi ya walalamikiwa, ombi ambalo lilikubaliwa na jaji huyo.
 
 Mbali na kulitaka gazeti hilo kulipa fedha hizo, Mahakama hiyo pia imeliamuru gazeti hilo kukanusha tuhuma hizo na kuomba radhi  katika ukurasa wa mbele wa gazeti hilo haraka iwezekanavyo.
 
Pia mahakama imeitaka gazeti hilo pamoja na mawakala wake kutokana na kulipa kiasi hicho cha fedha kwa kumkashifu mlalamikaji, pia linatakiwa lilipe asilimia 12 ya kiasi hicho kama gharama za kesi.
 
Naye wakili Kennedy Fungamtama, ambaye anamtetea Rostam amelipa gazeti hilo siku 14 za kutimiza amri hizo za mahakama la sivyo watachukua hatua kwa lengo la kumlinda mteja wake.
 
 
Hata hivyo Wakili Gabriel Mnyele ambaye analiwakilisha gazeti hilo katika shauri hilo, alisema  hakubaliani na uamuzi huo wa Mahakama Kuu, hivyo upande wa walalamikiwa utakata rufaa.
 
Katika kesi hiyo Rostam alilalamika kuwa habari hiyo ilimhusisha yeye na vitendo vya rushwa, mtu asiye mwaminifu kutokana na kuhusishwa na habari hiyo kuwa alihusika kwenye mpango wa kufanya ushawishi dhidi ya kampuni hiyo.
 
Katika kesi yake alisema pamoja na kutokuwa ushahidi wa yeye kuhusika kwa namna yeyote ile na madai yaliyokuwemo kwenye habari hiyo lakini gazeti hilo liliendelea kuchapisha habari nyingine kwenye toleo namba 085 la Februari 20 hadi 26 mwaka jana likimhusisha mlalamikaji na kampuni hiyo ya Richmond.
 
Katika kesi hiyo Rostam alisema gazeti hilo lilichapisha tena habari yenye kichwa cha habari kuwa ‘Kikwete amtosha Lowassa’ ambako alitajwa mlalamikaji na biashara zake kuwa alihusika alivyoshiriki kwenye suala la Richmond.
 
Alisema kwa habari hiyo yeye kama mbunge na mfanyabiashara aliathirika kwa kiasi  kikubwa kwani utu wake umedharirishwa mbele ya jamii na imesababisha aonekane mtu asiye mwadilifu na anayekabiliwa na kashfa kadhaa.
 
Rostam alidai kuwa, kutokana na tuhuma hizo za uongo zimemdharirisha hasa likizingatiwa kuwa kabla ya tuhuma hizo alikuwa ni mtu aliyeheshimika kama raia mwema, mfanyabiashara na mwanasiasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 39 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 12, 2009

    Hapo ndipo mtajiju... Kashfa zote wanazomtolea Rostam haziwezi kudhibitishwa mahakamani hata hiyo kigoda hata fingure prints kwenye makaratasi hakuna na watu tunapotezeana muda eti Kigoda ya Rostam! Rostam ameshapiga bao hiyo lazima watu wafike mahali wakubali hilo... wengine wanasema eti Mkapa kanunua Kiwira wakati jina lake halimo kwenye watu wanaomiliki Kiwira, na hata kampuni yake ya ANBEN haimo kwenye makampuni yanayomiliki Kiwira hapo vichaa wengine wanatupotezea muda eti wanadai Mkapa arudishe Kiwira. How?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 12, 2009

    "Rostam alidai kuwa, kutokana na tuhuma hizo za uongo zimemdhalilisha hasa likizingatiwa kuwa kabla ya tuhuma hizo alikuwa ni mtu aliyeheshimika kama raia mwema, mfanyabiashara na mwanasiasa"........Jamaa katuzidi akili inabidi ifike sehemu tukubali.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 12, 2009

    Hapo ndio ninapochoka na hawa waandishi wetu wa habari kumbe kazi yao ni kuandika habari ambazo hazina ushahidi. Rostam kajisafisha mwenyewe hajasafishwa na ccm wala serikali kazi kweli kweli

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 12, 2009

    Hiyo ni indicator kwa Mengi sasa.Mwanume wa shoka Rostam, hahahaha kama kamgalagaza Kubenea mahakamani, huo ndio mti mbichi je Mengi ambaye ni mti mkavu??Yeu macho

    Mdauzzzzzzzzzzzz

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 12, 2009

    Tusubiri tuone nani mkweli kati ya Mengi au Rostam Aziz, miye mijicho ttu yangu.
    Huwezi jua bana kwani wahenga walisema, kongolli koko mng'waliko kolikobodiko yaani WOTE WALIOFUNGWA JELA HAIMAANISHI WALITENDA HAYO MAKOSA YALIYOWAWEKA HUMO. Bye

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 12, 2009

    Jamani mi nakereka kweli kusoma Kiswahili kibovu kama "kudharirisha"

    Tena imerudiwa rudiwa.

    Neno sahihi ni "dhalilika" sio "dharirika"

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 12, 2009

    msitubabaishe huyu anatafuta chenji ya kumlipa Mengi fidia

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 13, 2009

    Mnaofurahia uamuzi wa mahakama hapo juu tulieni kwanza. Jua kuwa huu ni uamuzi uliotolewa kwa mbinu za kisheria (labda sio tafsiri sahihi) kwa kiingereza inaitwa technicality, yani mjibu maombi amechelewa kutoa majibu ndani ya muda unaopaswa na hii inahesabiwa kama ameshindwa kujibu, lakini kiukweli hajashindwakujibu, na kuna mazingira ambayo yalitokea mahakama inaweza kumruhusu kjibu maombi kutoa majibu yake. na so far hatujui angesema nini. Pili, Kumbuka kuwa kna nafasi ya kukata rufaa mahakama ya Rufaa na uamnuzi waweza kuwa tofauti na hivi sasa, so save your celebrations for a moment. Mbona mmefurahi sana nyie ndo mlomwagia Kubenea tindikali nini? lol

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 13, 2009

    Kwani hawezi kuwahonga mahakimu? Acheni kua man'gombe nyinyi. Mmeshaambiwa wamekata rufaa sasa mnatoa kelele za nini Watanzania wengine ni takataka kabisa. Kubenea atashinda tu kesi hiyo hata kama Fisadi lihonge vipi haki yake ipo tu. Hata mwana CCM ukibania hii lakini tunajua wazi mahusiano ya huyu jamaa na mheshimiwa ndio maana mheshimiwa ameanza kurudi nyuma kwenye vita na mafisadi. Na hata tupige kelele vipi huyu jamaa ataendelea kutesa tu

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 13, 2009

    Rostam naomba nikutukane kwa furaha, wewe ndio mwanaume!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 13, 2009

    Muda wa taharuma ya uhandishi kupata heshima yake unakaribia, na watu wote wanaojiingiza katika taharma hii kienyeji ni lazima wapate matokeo ya kuandika uongo. Pia naomba/natoa wito kwa viongozi wengine kufuata mfano wa Rostam pindi wanapochafuliwa bila sababu.Hii itasafisha taharuma ya uandishi, jaribuni kufuata "Rostam style"

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 13, 2009

    Ningekuwa mimi kubenea, kwanza ningechukua kadi ya pili ya CCM (renew my membership), pili, ningewataja watu wote waliokuwa wananipa mabomu ya kulipua na kwenye kesi hawakunisaidia kitu, mwisho ningemuomba msamaha Sir. Rostam Aziz, Esq.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 13, 2009

    kubenea ni mwanachama wa CCM sasa mijitu mingine inafikiria eti yeye ni mpinzani. Kwani Mengi naye ni CHADEMA? Naye ni CCM vile vile.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 13, 2009

    Rostam akigombania urais nitampa kwani ameonyesha uwezo wa kufuata utawala wa sheria na katiba.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 13, 2009

    sasa nimeamini kumbe hawa watu waitwao mafisadi wanasingiziwa tuu. Acheni kuwasingizia hawa watu ni wajasiria mali tu.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 13, 2009

    Kwa bahati mbaya sheria na haki/ukweli ni vitu tofauti kabisa, huyu kashinda kwa technicalities za kisheria na haina maana kuwa alikuwa na haki au ni mkweli.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 13, 2009

    Wewe anon. 1-4, inaonekana kama kwamba ni kibaraka wa mafisadi au la ndiye unayenufaika na ufisadi, kwa taarifa huyo ROSTAM hana namna ya kukwepa hiyo dhambi ya UFISADI. eti oooh sisi kwa vile ni WAHINDI hata kama mngekuwa WAINGEREZA madam mmetenda dhambi hiyo ya ufisadi, dhambi hiyo itawatafuna tuu... Maana mlijifanya wajanja kwa kuwanunua Watanzania weusi kwa umaskini wao, ukasahau kuwa hata watu weusi tuna akili pia, tulikuwa tukiwatazama wakati mkifanya huo USHENZI wenu. Kumbukeni Mungu si ROSTAM wala MENGI, na wakati ni ukuta sasa hizi ndizo siku zenu za kiama. Endeleeni kusoma alama za nyakati, endeleeni kukaa kwenye hivyo vikao vya mikakati na kamati zenu za ufundi, maana vijisenti vya kutumia tumia na kuwapa watu wa kujaribu kuwasaidia kwa muda mfupi mnavyo. Vijana kama hao wa Tabora nao wataendelea kula kama tulivyowashuhudia. Haya yote yana mwisho!!!!!

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 13, 2009

    ameshika nchi...tutamshika tu

    sijasoma ila nimeelewa tu first paragraph "|&%#$(**>:""

    siwezi soma nnatetemeka kwa hasira

    tutafika tu siku

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 13, 2009

    Ndugu Kubenea naomba nikutie moyo, mapambano uliyoyaongoza dhidi ya ufisadi kupitia karam yako yatakumbukwa na kutukuka kwa kila mtanzania mwenye mapenzi mema na nchi yake. Kwa mtu muelewa ushindi wa kimahakama haumanishi kuwa ndio ukweli wa jambo. mahakama zinahusika na vielelezo(facts) na sio KWELI(truth). Tunashuhudia kila kukicha kuwaona watu waliofanya uhalifu waziwazi lakini wakiachiwa huru na mahakama aidha kwa kutokamilika kwa ushahidi ama kwa rushwa, au kwa legal technicalities. Pia tunatakiwa tuujue mfumo wetu wa mahakama na jinsi unavyoendeshwa. Nashawishika kusema kuwa ni "kangaroo court" Nenda magerezani akaone waliofungwa ni akina nani?. Mwisho rostam aziz hawezikusafishika eti kwa kushinda kesi yake dhidi ya Mwanahalisi. Nikwamba maadili na masharti ya kazi zetu hazitupi ruksa kutoa facts thidi ya mtu huyu naye anajua hilo kuwa watu wenyeukweli wa mambo yake hawawezi hata siku moja kujitokeza wazi na kutoa ukweli juu yake na kwa mantiki hiyo itaendelea kuwa shujaa. Lakini kwa kifupi RA anatamba kwasababu tunaendeshwa na mfumo haribifu, uliooza na kusheheni mapooza ktk uongozi na ktk jamii. Ktk mfumo makini RA mahali pake ni KEKO

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 13, 2009

    Tanzania umefikia wakati ambapo tunahitaji ukombozi wa mara ya pili. mara ya kwanza ni uko,mozi kutoka katika ukoroni, na hivi tunayo miaka karibu ya arobaini na kitu. lakini ukombozi tunaohitaji sasa ni muhimu kwani utatufanya watanzania wote tunufaike na utanzania wetu na kufaidi rasilmali zetu na kuondokana na hali yoyote inayotufanya kuwa maskini zaidi. Nani atatupatia ukombozi huu wa pili? Hali yetu watanzania inazidi kuwa mbaya kwani kwa sasa tumegawanyika makundi mawili, matajiri na maskini. wale walionavyo na wale wasiokuwa navyo! Haya ndiyo alikuwa akituambia Mwalimu Nyerere kuwa tusipo angalia tutajenga tanzania yenye matabaka mawili, Matajiri na maskini. Sasa, pamoja na ufisadi, matajiri wanazidi kutajirika na maskini wanazidi kuteketea! Hakuna mtu wa kumtetea maskini! wabunge wanatafuta kuongezewa mishahara na posho, na wanasahau Mtanzania anayepokea kima cha chini cha shillingi 60000! Maskini anakumbukwa tu wakati wa uchaguzi, kuombwa kura! na baada ya hapo, basi! Wanao tuibia wanatuibia! wakiandikwa magazetini, hata kama kilichoandikwa ni kweli, kesi watashinda mahakamani na maskini huyu atapigwa faini ya mabilioni, hata kile kidogo alichonacho kichukuliwe! Nani atasimama tena kuandika? Matokeo yake watu watachukua madaraka na kushika mitutu kuvamia mabenki, hata kama ni mchana kweupe! Ukweli maskini wa Tanzania anazidi kukata tamaa na mwisho wake utakuwa mbaya!

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 13, 2009

    Kama hukumu ilitolewa tarehe 30 april iweje leo ndiyo habari ipatikane? Au hukumu iltolewa kwa njia ya barua,hivyo imefika posta juzi? Hakuna hata gazeti la RA au chombo chochote kilichoitoa hii zaidi ya blog na forum

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 13, 2009

    hakika ndugu wa chini hapo mmenena ya kweli watanzania kinachotakiwa kubadilika kwanza mahakama isiwe chini ya serikali kama ilivyo sasa maana mafisadi wengi wanatumia pesa na mahakama ni chombo cha kuwalinda mafisadi kwa sababu system yote imeoza yaani rushwa.

    wengi wa mafisaidi walimkataa salum ahmed salum kwa kujua ni mtu ambae hataki mchezo na ndio maana pesa nyingi ilitumika kupewa wajumbe wa CCM ili wamchague kikwete kwa kujua watamtumia wanavyotaka.
    lakini mafisadi wakumbuke kuna hukumu ya MUNGU haki ya mtu haitapotea na pia kuna siku zao zitafika watajuta majuto ya ajabu.

    wazungu wanasema kila mwenda juu sana akija kuanguka basi ni kifo tu.

    pia waswahili wengi husema ngoma ikivuma sana mwisho hupasuka.

    kikubwa wananchi mpime mahakama ni chombo cha kumpa nguvu mhalifu na hasa ukiangalia raisi wetu mwenyewe anakemea mambo ya rushwa kisiasa nasiyo ndani ya moyo.

    wana ccm patene huruma na kumuogopa MUNGU mumchague kiongozi wa maana kama warioba au salum hapa nchi itapona vinginevyo nchi italiwa na wachache na mahakama ni jina tu haina chochote zaidi ya uongo na kupokea rushwa.

    wana ccm naomba muwe waadilifu tuache tamaa ya kununuliwa na pesa tufikiri kosa hili la kununuliwa na pesa wangapi linawaumiza masikini.

    kesho kwa MUNGU tutajibu kitu gani.

    kuna wengine humu wanatoa haja zao kwa ubishi lakini MUNGU anakuona na kesho utajibu.

    watanzania kingine nachowaomba ni kusoma madua kwenye misikiti na makanisa hii ni fimbo kubwa sana kwa fisadi tunaweza kufanya siku moja tanzania nzima dua ziombwe na hapa ukweli utajulikana maana mahakama ya haki ni ya MUNGU amen

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 13, 2009

    mi nshatabiri machafuko ya hapo tz yatakuja kuwa mabaya zaidi katika historia pale wasiokuwa nacho watakapoamua kupigania haki yao kutoka kwa watu kama hawa kina rostam,huyu jamaa ubabe huu anautoa wapi jamani??mbona watanzania tunatawaliwa kiasi hiki katika nchi yetu?kuibiwa tuibiwe na hata kudai hatuwezi hata tukiongea tunapelekwa mahakamani hii nchi inaelekea wapi hii??iliobaki sasa ni kuplishwa sumu tufe huyu jamaa alete ndugu zake watupokonye nchi yetu,haya mi yangu macho,lakini ipo siku tu

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 13, 2009

    Nimekasirishwa sana na comments za watu wanaoshangilia Rostam kushinda kesi. Hii inaonyesha jinsi gani kazi ya kumkomboa mtanzania kutoka katika wimbi la umaskini lililosababishwa na walafi wachache kama wakina Rostam na wengine ilivyo ngumu. Nasema hivi kwasababu kama mtu aliyejitolea kwa nguvu zote, bila kuhofia uhai wake, kuibua tuhuma za ufisadi wa Richmond, Dowans na nyinginezo na kulinusuru taifa katika hasara ya mabilion iliyokuwa ikipata kupitia mikataba mibovu, leo hii anahukumiwa kulipa fedha zote hizo, halafu watu wanashangalia, Nasema kazi bado ni pevu. Nashawishika kusema kwamba, hawa walioshangilia kwa hakika nao ni mafisadi. Ila haki itajulikana tu, kama wametumia pesa zao kuhonga mahakama, sawa lakini moto ndo umeshawashwa hautazimika, kuna wazalendo wengi km Mengi, Dk Slaa, Zito Kabwe, Anna Kilango, Tindu Lisu, nk wataendelea kupambana, Hakuna kulala mpaka lieleweke.

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 13, 2009

    Hapa ni mambo ya sheria. Na mwenyepesa si mwenzako,. Cha msingi kaka ni kujipanga upya kama unakata Rufaa anza mapema. Ila huyu jamaa kajiandaa kujisafisha kwa hali na mali. Kazi ipo.

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 13, 2009

    Hata mimi nimekasirika sana kusikia watu wanamshangilia R A. Unajua niliwahi kusoma makala ya Jenerali Ulimwengu akisema kuwa suala la RUSHWA/UFISADI kwa nchi yetu sasa ni suala la MAADILI. Watu wamekua na tamaa sana ya pesa. Mtu anayeiba openly anaonekana ni MJANJA. Utasikia, "...umeona hekalu aliloporomosha jamaa!...umechecki mashine ya fulani!..."

    Mimi si mwanachma wa chama chochote lakini wote tunajua kuwa majority ya waty wanaojiunga na chama tawala au kutafuta nafasi za uongozi au kuanzisha matawi ughaibuni ya chama cha mapinduzi NIA yao ni kujitafutia influence ili WATAJIRIKE.

    Katika nchi za wenzetu hali ikifikia hivi na wanaosema ukweli kufilisiwa JESHI huwa linachukua nchi. Kwa nchi yetu, mkuu wa jeshi na maofisa wa juu wote wanawekwa mikononi mwa mkuu wa chi na mafisadi marafiki zake. Chunguzeni mone jinsi miaka ya karibuni wakuu wetu wa jeshi walivyokuwa matajiri. Hii ni kuanzia kipindi cha Mkapa.

    Sasa Watanzania tumebakisha haki ya kupiga KURA. Asilimia 85 wakikataa serikali hii inayolinda "manyang'au na mafisahi" hata akijaribu kuiba kura watashindwa. Tuwaelimishe ndugu zetu vijijini umuhimu wa kura zao!

    Mungu Ibariki Tanzania!

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 13, 2009

    Kuna watu wanachafua mahakama hapa bila sababu. Kama angepeleka ushahidi wake na mahakama ikatupilia mbali angalau tungekuwa tunafikiria hongo ya namna fulani sasa hata ushahidi hakupeleka sasa hiyo hongo inatoka wapi? Acheni pumba jamani!!!!

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 13, 2009

    kuchelewa kujibu maana yake huna jibu otherwise wangejibu kama wangekuwa na hoja tena walipewa na muda wa nyingeza wa siku 21 bado wakashindwa, kwani wakati wanaitwa mahakamani si walitakiwa wajitayarishe na nondo zao kabisa....hao ndio wameshachemsha wasubiri gazeti lifungwe tu.

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 13, 2009

    Mimi nafikiri tukipata majaji 10 kama huyu aliyehukumu kesi kati ya kubenea na Rostam nchi yetu itapata maendeleo haraka. Siyo siri, vyombo vingi vya habari vinatoa habari za uchunguzi ambazo hawana uthibitisho nazo na wanafanya hivyo kwa kuwa wanajua wananchi wengi wataamini. Wezi wa pesa za umma ndiyo wanaofadhili hao waandishi wabovu. Hii ni kesi ya pili, ya kwanza ile ya gazeti lililomkashifu Sumaye ambalo lilitakiwa kumlipa fidia kwa sababu walikosa ushahidi. siyo siri, Waandishi wengi wa habari ndiyo wanategemea rushwa ili kuendesha maisha yao na ndiyo maana wanaandika habari ambazo hawazifahamu vizuri. Nawashauri waandishi acheni kutumiwa kwani siku ya siku ni nyie mtakayehukumiwa na siyo aliyekufadhili ili utoe habari za hovyo. Mkiendekeza pesa na kuacha maadili mtaipeleka nchi kubaya na ndiyo maana nampongeza huyu jaji na naomba tupate majaji wengi wanaofanana na huyu.

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 13, 2009

    nina shawishika hizi comment za kumsifu Rostam,amezipost yeye mweyewe au kwa kutumia mtu.
    It is very obvious kwamba pesa ya rostam hali yeye peke yake,ana wapambe wake...ambao lazima wamfagilie.
    Rostam,wewe ni fisadi na watanzania tumechoshwa na mafisadi wewe pamoja na wenzio.
    Watanzania hawakupendi..Binafsi mimi hata kubenea simjui wala sisomi gazeti lake,lkn kwa kutizama tuu habari zinavyoenda na jinsi Rostam alivyo tayari hata kwa kuua ili ajisafishe..ni dhahiri hata majaji wanaweza wakawa wamepokea rushwa,kwani wao sio watu? Nani asiyejua rushwa mahakamani?

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 13, 2009

    Ati majaji 10? Upuuzi mtupu..nina hakika huyu rostam hataki kukubali ukweli...lisemwalo lipo na hatuwezi kukataa kama huyu ni fisadi...ofcoz hata mengi alivyosemwa anakataa kulipa mishahara wafanyakazi wake kuna ka ukweli ndani yake na ajirekebishe.
    Rostam,wewe swala lako zito kidogo...hauwezi kujirekebisha kirahisi maana ukiiba hausamehewi mpaka umerudisha ulichoiba.na kwa tamaa ya asili kabisa ya binadamu,hautaweza kurudisha.Busara ndogo tuu unayoweza kuifanya ni kukaa kimya na kuacha kutufanya sisi ni wajinga..

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 13, 2009

    eti majaji 10? ili nchi iende wapi? kuzimu? Haki isitendeke ili iweje?

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 13, 2009

    ROSTAM OYEEEE!!!!

    NYIE MNAONA KUWA ROSTAM HAJASHINDA KESI HII NA KUBENEA NENDENI JAMBOFORUMS MKABISHANE NA KUANDIKA MAMBO YA KUTUNGA (FABRICATION).

    BORA HAPA TUNAINGIA KAMA MAANONOMY KULIKO KULE JAMIIFORUMS MTU MMOJA ANA USER ID KIBAO KAMA YULE MWANAKIJIJI ANA USER IDS 10. ANAANDIKA NA KUJISAPOTI MWENYEWE

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 13, 2009

    NASIKITIKA SANA KUONA WATU WASIO NA AKILI WAKISHANGILIA USHINDI WA AWALI WA RA BILA KUULIZIA MWENENDO WA KESI YENYEWE.
    MSIKILIZENI MABERE MARANDO , WAKILI WA KUBENEA NA GAZETI LAKE.SI RAHIS I RA KUSHINDA KATOKA KESI HII.

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 14, 2009

    Rostam 1, mafisadi 0

    Blogger

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 14, 2009

    naimani watanzania wengi hawapendezewi na ufisadi kwanza raha gani wewe kuwa na mali ya ufisadi, familia yako unailisha haramu na wewe unakula haramu hii moto ndani ya tumbo la mfisadi.

    ukweli nawaomba watanzania waislamu ni kusoma ALLALIBADRI kwa siku 40 zinatosha kutoa hukumu ama ndugu wakristo madua siku ya jumapili makanisani.

    wangapi walikuwa maarufu kwa ubaya leo wanatafuta hata sehemu ya kukaa hakuna.

    naimani siku itafika mtu yeyote fisadi atatafuta sehemu ya kujificha hatapata.

    ufisadi ni kuiba pesa za watanzania milion 40 vipi moyo unakupa jamani.

    jamani mafisadi rejeeni kwa MUNGU mtubu kwa kurejesha mali za watu.


    dua ndugu zangu kitu kikubwa na hasa kwa aliyezulimiwa MUNGU huicha mbingu wazi ili mashitaka yafike haraka amen.

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 14, 2009

    Natamani vyama vya upinzani vifutwe.
    KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
    HONGERA ROSTAM KWA KUPAMBANA NA MAFISADI.

    ReplyDelete
  38. AnonymousMay 14, 2009

    ANGALIA WATANZANIA WALIVYO WAJINGA KWANINI SIKU ZOTE WASIPEWE HATA PANAPOKUJA UCHAGUZI PILI PESA IKIWA ZITATOLEWA SIYO ZA CHAMA BALI ZA SERIKALI WATANZANIA MBONA MNAKUWA WAJINGA WAKUPINDUKIA SERIKALI SIYO CHAMA BALI WATANZANIA WOTE NI KODI ZA WANANCHI ANGILIENI KICHEKO HAPA CHINI.

    Katika hatua nyingine, zaidi ya wakazi 300 wanaowawakilisha wachimbaji wadogo wadogo katika kata ya Katoro jimbo la Busanda, wameamua kuacha kushabikia vyama vya upinzani katika kampeni za uchaguzi mdogo unaoendelea baada ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kuwaahidi kwamba wametengewa hekta 750 na Sh. bilioni 1.5 kwa ajili ya mikopo.

    Walisema hayo jana kufuatia mkutano wao na Waziri Ngeleja uliofanyika juzi ambapo walimlalamikia kuhusu hali duni waliyonayo katika shughuli zao za uchimbaji wa madini.

    Walitangaza kuwa wataacha kupigia kampeni vyama vya upinzani na kuelekeza nguvu zao kwa CCM.

    Mwenyekiti wa wawakilishi hao, Obadia Madini, na makamu wake, Silas Kurwa, waliahidi kwamba watampigia kura mgombea ubunge kupitia CCM, Lolesia Bukwimnba Masele.

    Walidai kuwa walikuwa wakishabikia upinzani kwa kile walichodhani kwamba serikali ilikuwa haiwasaidii vya kutosha katika masuala ya maendeleo.

    ReplyDelete
  39. AnonymousMay 14, 2009

    Ngoma bado mbichi kweli. Unless Rostam is ready to eliminate (because they will not be bought, asilani asijidanganye) some of the most brilliant legal minds in this country Rostam hashindi na Mwanahalisi itashinda baada ya rufaa. Hamuoni Mwanahalisi hawakuhudhuria na mahakam imetoa maamuzi kwa kusikiliza upande mmoja tu? Jamaa wanajipanga na wamekata rufaa mara baada ya hukumu kutolewa, yote hii ni sehemu ya mkakati.
    Aidha, Rostam kachemsha kwenye matamshi yake ya press conference dhidi ya Mengi so many of his allegations against Mengi were based on false or outdated records such that they were so easily refuted by Mengi the next day. I seriously doubt Rostam will fair well in the defamation case brought against him by Mengi.Saed Kubenea oyeee!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...