
Kikundi cha kwaya kutoka kanisa la Azania Front la hapo Dar kipo hapa katika jiji letu la Dallas. Kwa kweli kikundi hiki kimetoa burudani ya hali ya juu katika kanisa letu la Umoja pamoja na kanisa la wamerikani ambao walikuwa wanashangilia kama wabongo.
Kikundi hiki kimeweza kutangaza nchi yetu vema katika jiji la Dallas pamoja na jiji la Oklahoma ambako nako wamefanya vitu vya nguvu. Leo jioni kutakuwa na dhifa maalumu ya kuagana nao katika jiji letu tayari kurudi katika jiji la Oklahoma ambako watafanya maonyesho kadhaa kabla ya kuingia ndani ya pipa tarehe 8 na kurejea nyumbani.
Mwisho kanisa la Umoja linapenda kuishukuru jumuia ya watanzania hapa dallas chini ya mwenyekiti wetu Saimon Nkanda kwa msaada wote waliotoa kuhakikisha kila jambo linakwenda vizuri.
Siku zote Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
Pastor Abisalom Nasuwa
Umoja International Outreach Church
12727 Hillcrest Rd,Dallas Texas 75230
Email:umojachurch@yahoo.com
Tell:214 554 7381

Kwaya ya Azania Front ikiwajibika kiutamaduni

Nyuso zinaonesha furaha

wanakwaya wa Azania front wakiimba Dallas

wametia fora kwa unadhifu na uzuri wa nyimbo zao

tamaduni zote za tanzania zilioneshwa

wanakwaya na wenyeji wao

wanakwaya kinadada walipendeza sana

wahudhuriaji wakiburudika

vifijo kwa kila onesho


Wabongo wanafiki sana. wakiwa home wanaona kuvaa kama hivi ni dhambi/ushamba na upuuzi.Mkija majuu mnataka kufagilia mavazi ya watu.
ReplyDeleteMwaka huu wameleta wamama wote hakuna atakaye baki
ReplyDeleteMdau wa Dallas Pastor Abisalom Nasuwa fanya uturushie video clips za hiyo show kwa Youtube.com
ReplyDeleteOmba msaada kwa wanaojua endapo hufahamu Youtube.com ni kitu gani.
kwa nini mnakuwa wanafiki watumishi wa Mungu? mbona huku hamvai hivyo?
ReplyDeletemulienda kutangaza utamaduni wa kitanzania au kumtumikia Mungu? sasa
kwa nini mnafika huko mnavaa vibwaya kama wacheza ngoma wakati huku hamsubutu kufanya hivyo.
unafiki ni mbaya sana mbele za Mungu.
Mbona mahudhurio yenu hafifu?
ReplyDeleteni annon mahudhurio,ila fahamu watu wengi majuu awaindi kusali wala nini!!ndo mana apo wazee watupu,labda ao watoto wa kibongo
ReplyDeletemungu atusaidie!!
Aliyosema Anonymous 5.53 hapo juu ni kweli kabisa, sielewi sijui ni ushamba au kuwavutia wazungu! Je kweli hao walienda kulitangaza neno la Mungu au kuonyesha mavazi na ngoma za kitamaduni? Neno la Mungu ni lile lile Tanzania au Ulaya, Iweje nyie wabongo muwe hivyo? Acheni unafiki jamani!!!
ReplyDeletemmependeza lakini mgependeza zaid kama mgevaa mavazi yenye asili za kwenu tanzania instead hoyo mavazi na mishono yenu yenye asili ya kihindi wenyewe wanaita sari.
ReplyDeleteGood job guys, you all look cute!
ReplyDeleteNdugu zangu Watanzania wenzangu, hawa wenzenu wamefanya kazi nzuri sana na wanastahili kupongezwa, nyimbo zao na utamaduni waliouonyesha siyo unafiki mbele za Mungu, Hakika mpinga Kristo siku zote huponda kazi ya Mungu. Big Up Azania Front Choir
ReplyDeleteHongereni sana Azania Front, nyimbo zenu zimeonya na kuponya, Mungu apewe sifa, Karibuni sana tena sanaaaa Dalas kwa mara nyingine watoto wa Mungu.
ReplyDeletesafi sana mzee rumisha elri masa, masawe
ReplyDeletesafi sana mzee rumisha elri masa, masawe
ReplyDelete