Wakuu wa Wilaya wapya, sita  wanawake kati ya 15 walioteuliwa na Rais hivi karibuni wakiwa kwenye  picha ya pamoja baada ya kumaliza semina elekezi mjini Morogoro, majina na Wilaya zao kwenye mabano , kutoka kulia ni Fatma Mwassa ( Mvomero), Queen Mlozi ( Ukerewe), Fatma Ally ( Nanyumbu), Mery Silla (Arumeru), Dk Rehema Nchimbi ( Newala) na Angelina Mabula ( Mulemba)., mafunzo hayo ya awali yalifanyika  kuanzia Mei 5,hadi 8, mwaka huu. 
Picha na mdau wa mji kasoro bahati  John Nditi.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 08, 2009

    Huyu Dr Nchimbi ana uhusiano na Dr Nchimbi yule mwingine? Wamesoma chuo kikuu kimoja udokta?
    Duu! Fatuma ameenda hewani utafikiri Hasheem Thabeet!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 08, 2009

    kina mama oyee

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 08, 2009

    Haya ndiyo mambo! One day "we can" mwana mama ataongoza hii nchi na mambo yote yatanyooka! Hongereni na wote wanaonekana ni kina mama wa haja! Kikwete tunakupongeza. Tafadhali ongeza kina mama kwenye serikali yako pia.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 09, 2009

    Huyu Dr Nchimbi (Rehema) ana PhD (History) na alisoma chuo kikuu cha Cape Town, Afrika Kusini.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 09, 2009

    We annon wa kwanza kutoka kulia sio kushoto..aliepanda ni Bi-Angelina Mabula kama ni macho yangu na picha inayonieleza!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 09, 2009

    Mdau hao juu Dr Rehema nchimbi hana undugu na Nchimbi waziri. Ni Majina tu ya Ukoo yanafanana na wote ni Wangoni.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 09, 2009

    Kweli kabisa anony wa 6:42. Huyo anony wa kwanza lazima ana makengeza. Aliye kwenda hewani ni angelina mabula (chata ya kisukuma maana ndio wanawake wanao kuwa warefu). Huyo fatima ni yule tunyetunye wa mwanzo kulia. Anony wa kwanza soma kwanza maelezo siyo kukariri kuwa kila picha ikiwekwa lazima itaandikwa kuanzia kushoto kwenda kulia.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 09, 2009

    Hivi zinatumika criteria gani katika kuwachagua wakuu wa wilaya na mikoa? Elimu za wachaguliwa nazo zinazingatiwa? Kama hazizingatiwi, je hatufikiri kua hii inaweza kuwa ni sababu mojawapo why Tanzania mpaka leo miaka 40 na ushee baada ya uhuru hatuna maendeleo ya kujivunia? Kama ni hivyo, je hatufikiri kwamba itakua ni vyema kubadili style ya kuwachagua hawa watu?

    Huwezi mchagua mtangazaji redio ati kwa kua anatangaza vizuri mpira wa simba na yanga na kumweka kuwa mkuu wa Wilaya, then ukategemea kwamba atafanya wonders kama mtendaji-muhusika (CEO) wa wilaya ama mkoa wakati hajui hata kutengeneza strategic plan ya kaidara kadogo katika ofisi isiyofahamika. Hata kama ukimweka morogoro kwa wiki mbili kumfundisha leadership and administrative skills, ingawa mda huu mara nyingi hutumiwa kuponda maraha zaidi ya kujifunza, vilevile huu ni upotevu wa resources za nchi kwani kuna watu wengi tu ambao wako qualified from the beginning na kama wangepewa mikoa ama wilaya wangeweza boresha mambo from day one wanapoingia ofisini.

    Mwangalieni Obama... Kateua vijana wa miaka 20 na 30 katika administration yake sio kwamba kawapendelea, ila kwa kua anauhakika kwamba they can do the quality job to meet the specifications he wants. Not just because hao jamaa ni ndugu wa shemeji, ama shangazi wa jirani , ama ni nyumba ndogo ya zamani, ama ni nyumba ndogo tegemezi (ya future)

    Lets stop huu utani watanzania. Lets get serious. Kama twataka maendeleo inapaswa kuachana na stereotypes zisizo na tija.

    Kikwete, kazi kwako baba...

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 10, 2009

    Wadau naombeni mnisaidie,sijui ni macho yangu au ni kweli, huyu dada Angelina Mabula nimemfananisha na Angelina Lubala!

    ReplyDelete
  10. Hujakosea ndiye Angeline Lubala unaemfahamu, jina la Mabula nila mume kwakuwa wenzetu huwa wanaazima majina wakiisha olewa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...