
Mama Salma Kikwete akimjuliahali mtoto Sarah Bakari mwenye umri wa miaka miwili na nusu aliyelazwa katika wadi ya Sewahaji Muhimbili baada ya kuumia kichwa na kuathirika miguu kutokana na ajali ya Mabomu yaliyolipuka katika kambi ya jeshi Mbagala jijini Dar wiki iliyopita
Mama Kikwete leo aliwatembelea na kuwajulia hali majeruhi hao katika hospitali za Wilaya ya Temeke na Hospitali ya Taifa Muhimbili. Aliembeba ni Mama wa Mtoto huyo Bi.Hawa Bakari mkazi wa Yombo.

Mama Salma kikwete akimtuliza Bi Sarah Sitta mmoja wa waathirika wa ajali ya Mabomu ya Mbagala aliyelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Temeke jijini Dar.
Bi. Sitta alimweleza Mama Kikwete kuwa alikataliwa kupokelewa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kupewa rufaa na waganga wa hospitali ya Temeke kwenda muhimbili kwa huduma Xray na uchunguzi wa kina kutokana na majeraha ya mgongo.
Bi Sitta alidai kuwa alipofika Muhimbili wahumu walikataa kumpokea wakidai wao hupokea dharura tu na kwamba kama anataka huduma ya X-ray arejee hospitalini hapo ijumaa akiwa na Shilingi 2000.
Bi.Sitta aliendelea kusema kuwa pamoja na kwamba alipelekwa Muhimbili kwa gari la Wagonjwa ambulance akiwa na nesi bado hakufanikiwa kupata huduma na kulazimika kurudi Hospitali ya Temeke ambapo amelazwa mpaka sasa. Mama Kikwete alimfariji Bi Sitta na kuahidi kufikisha taarifa hizo kwa wanaohusika.Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.
there she goes again..gorgeous first lady////this woman anatoka nyoko na every outfit...apunguze uzito kidogo tu
ReplyDeleteBongo bwana! sasa huo tuiiteje? urasimu? ubepari? ufisadi? uzembe? ulimbukeni? Sina jibu!
ReplyDeleteHAPA WOTE WALIOHUSIKA NA HUJUMA DHIDI YA BI SITTA WAWAJIBISHWE MAANAKE NI WAUAJI. WATU GANI WASIO NA HAYA MTU HATA PA KULALA HANA LEO ANAAMBIWA ATOE 2,000 APIGWE X RAY. RAIS, WABUNGE MAWAZIRI AIBU NA NDIYO MAANA HAKUNA NIDHMAMU KAZINI.
ReplyDeleteWWATU HAWAMWOGOPI RAIS SEMBUSE MGANGA WA TEMEKE! NCHI IMEOZA INANUKA RUSHWA. KILA MTU SURA YAKE INA CHAPA YA RUSHWA-KITU KIDOGO.
huu ndio ukiritimba ulioko nchini mwetu sijui utaisha lini
ReplyDeletesasa mama salma kapata hii ngoja tuone mwisho wake
Akiwa kama mke wa Rais anatakiwa oionee uchungu nchi yake na raia wake...Hapo hapo anatakiwa achukue hatua stahili za kuwawajibisha sio kungoja tena...Huu ni udhibitisho tosha ameshaupata kuwa hospitali zetu za serikali zinautendaji upi, zinajali vipi.....UPUMBAVU KABISA HUU NA UFISADI PAPA ULIODHAHIRI
ReplyDeleteAnony. May 07, 2009 10.08 AM. Acha pararira unataka aandikwe kwenye BBC kama Lucy Kibaki hapo mtaa wa pili! mwache atafikisha ujumbe kwa the man incharge himself kikatiba! mana hana mamlaka hayo labda kama angejitolea kutoa msaada lakini isingeleta picha nzuri mana ingekuwa kama kashfa kwa serikali ya mumewe! she is intelligent i assure you that she knows all the protocol na ana roho safi na upendo!
ReplyDeletespeech "sasa uyu mama akija hospitali na uo unoko yan kuchonga sana apo,hatumpi huduma ata kidogo kila siku tutakua round,au vifaa vimeharibika,wee si mtoto wa mkubwa?"
ReplyDeletewadau mtaona
afu jamen ao wahanga wa mabomu wanaudumiwa bure kabisaaaa au kuna vipimo wanalipia??kitanda,chakula,nk nk??
nieleweshen
Pole mama sita kwa maumivu unayo yapata, maana mgongo ni kiungo muhimu sana kwa binadamu then hao wajinga wajinga wanazidi kukuongezea matatizo.
ReplyDeleteKuweni na huruma manesi feki nyie, kweli 2000 ndo iwatoe roho? wakati mkijua historia yake kuwa ni muhanga wa mbagala?
Mimi baba yangu alipatwa na ajali ya gari, akachukuliwa na ambulance akiwa na nesi kukiwa na maelezo yakuwa afikishwe ICU, cha ajabu wakambwaga wodini kwa muda mrefu.
Akatokea ndugu yangu mmoja na kwenda kuwafokea kwa nguvu sana ndo wakampeleka ICU baada ya kama dakika 45 akafariki. Siwezi laumu sana ila hali halisi ya hospital zetu za selikari ndo hivo.
Usipokuwa na hela hakuna atakae kunusa.
Nahisi wahusika wengi huwa hawachek glob ya jamii wangeona haya. Wizi mtupu! Subirini ipo siku!
Jamani eee sasa tunatakujua Uyo mke wa raisi amechukuwa atuwa gani kumsaidia huyu mama sita.???Tanzania is corrupted with full of hatred na Roho za kwa nini
ReplyDeleteJamani eeee! Nampa pole huyo Mama Sita.Mimi mwenyewe nafanya kazi Muhimbili.Hao aliokutana nao ni wafanyakazi ambao wapo pale kufuata maelekezo ya wakubwa wao wanavyowaagiza kiutendaji kazi.Hawana mamlaka yoyote kwenda kinyume mpaka wakubwa wao waidhinishe.Ukikutwa umefanya vinginevyo,basi unaonywa na pia maagizo kwa mhasibu wa shirika ni kwamba,gharama za ki/vipimo hivyo unakatwa kwenye mshahara na kumbu kumbu inabaki kwenye jalada lako!Je,nani alaumiwe??
ReplyDelete