Ofisa Uhusiano wa Tigo, Jackson Mmbando (kulia) akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza wa shindano la Mr & Miss SUA Talent 2009 upande wa wanawake, Pendo Wilson katika shindano lililofanyika kwenye Hoteli ya Savoy mjini Morogoro mwishoni mwa wiki. Tigo ilikuwa mdhamini mkuu wa kinyang’anyiro hicho. Katikati ni Miss SUA 2008, Aneth Kayombo.
Meneja Matangazo wa Tigo Redemptius Masanja (kulia) akikabidhizawadi kwa mshindi wa pili wa shindano la Mr & Miss SUA Talent 2009upande wa wanawake, Mwajabu Juma katika shindano lililofanyika kwenyeHoteli ya Savoy mjini Morogoro mwishoni mwa wiki. Shoto ni Miss SUA 2008, Aneth Kayombo.
Ofisa Uhusiano wa Tigo, Jackson Mmbando (kulia) akikabidhi zawadikwa mshindi wa kwanza wa shindano la Mr & Miss SUA Talent 2009upande wanaume, Amidi Ali katika shindano lililofanyika kwenye Hoteliya Savoy mjini Morogoro mwishoni mwa wiki.  Katikati ni Mr SUA 2008, Frank Mlekwa.
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Salim Saraiakionyesha vazi la ubunifu alilolitangeza kwa majani ya miti wakati washindano la Mr & Miss SUA Talent 2009 kwenye Hoteli ya Savoy mjiniMorogoro mwishoni mwa wiki.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 06, 2009

    Nyie wasomi wa SUA hata kulima hamjajua mshaanza kukimbilia urembo.

    Tutafika kweli?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2009

    Tutafika kweli? Mr. University Talent!!, talenting vazi la majani ya miti in 2009?!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 06, 2009

    Hivi nyie wasomi wa SUA, hiyo "talent" ya kuvaa vazi la majani ya miti lina faida gani kama siyo kuturudisha kwenye ujima! Hilo vazi linasaidiaje kwa baadaye kama kweli mko "serious"!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 06, 2009

    Nilifikiri hapo talent mlimaanisha vipaji vya kitaaluma au utafiti ukizangatia kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa, du kumbe uharibifu wa mazingira mmekwanyua miti laivu halafu mnasema vazi. Du hii kali, Mi naomba michuzi wasiliana na hawa wafadhili watafute njia nzuri ya kuinua vipaji maalum hapo chuoni mfano tafiti za madawa ya kilimo, zana, mbegu bora, wanyama/ndege wafugwao, utunzaji wa mazingira, mazao gani yalimwe wapi n.k.

    Mdau
    Rwechung
    Trd-Norway

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 06, 2009

    Nakubaliana sana na mdau wa nne kutokea Trd-Norway. Kwa kweli tuache mammbo ya kuiga kila kitu hata na hasa kwa sisi tunaosema tumefuta ujinga zaidi. Sasa watu wa SUA na mashindano ya urembo wapi na wapi. Kama mdau wa Norway alivyosema kwanini hawa jamaa wasinge shindania ugunduzi wa vitu vya kitaaluma vya SUA kama usindikaji bora wa vyakula, dawa bora za mifugo kwa mazingira ya kitanzania, mnyambulisho bora wa biashara za kilimo na masoko n.k. Kuna mdau amesema hapo kilimo ni uti wa mgongo ni kweli kabisa na kilimo kwa nchi za Africa ndio zitakwamua nchi hizo sio kilimo cha miaka ya 70 bali kilimo kinachikwenda na usindakaji wa hali ya juu, ubora wa biadhaa ndipo tutaweza kuongeza pato la kilimo cha TZ kwa kukidhi masoko ya ndani na nje ya nchi.

    Mdau wa shamba

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 06, 2009

    TIGO mkosa cha ku-Sponsor? huo upuuzi gani hao jamaa wanafanya na nyie mnatumia mifedha yenu kuwa-sponsor, pelekeni hizo hela kwa yatima na wajane. hao jamaa wanatakiwa wakalime ndio fan yao.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 07, 2009

    huu sio utani wala matukano ila ni ukweli, kwamba wanavyuovikuu wa tanzania ukiwalinganisha uwezo wao wa kufikiri,kupangilia,kubuni,kutoa kiaumbele ktk maswala,na kuchanganua mambo mbalimbali kama wasomi na wanavyuovikuu ktk nchi zilizoendelea utagundua kwamba kunatofauti kubwa sana!!
    ukweli wakati mwingine hata unaona aibu,sijui labda ni mazingira yanachangia hali hii au tatizo huwa linakuwa wapi!!
    hatutakaaa tuendelee kwasababu hatuko tayari kwa maendeleo,maana maendeleo huanzia kichwani kisha huwekwa ktk vitendo. UTAZI UMEZIDI SANA KILA SEHEMU miongoni wa watu,and people are not serious at all zaidi ya kufanya fanya vichekesho[japo sio vibaya] na kupoteza muda bila kufanya kitukinachoweza kubadili level ya maisha ya mtu binafsi,na kulalamika ama kwa serikali ama kwa wazungu[wafadhili] kuwa ndio chanzo cha matatizo yetu. ila tunasahau kuwa good life comes after you have played your role!!
    WASOMI BADILIKENI,THINK REASONABLY,TIMELY,RATIONALY AND PERSPECTIVELY to save yourself&your next generation.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 07, 2009

    Vazi la majani Ubunifu Tosha.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 08, 2009

    mh huyo miss talent kama mwanaume, atakuwa amefanana na baba yake

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 09, 2009

    Ukianganlia mambo kama haya, hutawalaumu wanaoamua kwenda nje kusoma. Ni sababu ya kukazania elimu ya makaratasini ndio maana tunaishia hapa. Hebu jaribu kufikiri ni muda kiasi gani uliotumika kuandaa hilo "shindano" (If i can even call it that). Na Tigo, kama mtandao wa mawasiliano nchini, ingekuwa vema zaidi kama ingetoa kipaumbele katika kuboresha uwezo wa kufikiri katika maswala ya kijamii zaidi, kufaidisha walio wengi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...