Kaka Michuzi nashukuru kwa kufanikisha mawasiliano ya watanzania kutokea sehemu mbali mbali duniani.
Kaka naomba kama inawezekana unirushie kwenye blog yako mswada wangu. Nilikuwa napenda kujua gharama za usafirishaji kwasasa kutoka mikoa ifuatayo kwenda DSM: Iringa, Mbeya, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara. Gharama inaweza kuwa kwa kilogram kwa kilometer au tani kwa kilometer. Gharama hizi hasa ziwe za usafirishaji wa mazao kama mahindi na maharagwe.
Natanguliza shukurani zangu kwako na kwa wale wadai watakaokuwa na muda wa kunisaidia.
--
Mdau FJM


Aisee yaani we unashangaza sana kwani huku bongo huna jamaa wa karibu ambaye ataweza kukufanyia hiyo kazi yako kwa ukaribu Au una cha kuuliza? acha kujitenga na ndugu zako
ReplyDeleteAma kweli hii ni blog ya jamii, kila mwenye goma lake hulicheza!
ReplyDeleteMdau FJM,
ReplyDeleteFanya hivi:
1. Fungua tovuti ya Google.co.tz2. Search "Tanzania Freight Forwarders" (with or without the quotes)
3. Utaona tovuti za makampuni ya usafirishaji wa mizigo (freight forwarders)
4. Wasiliana nao watakupa bei zao.
NENDA KAULIZE STENDI YA FUSO JANGWANI
ReplyDelete