WAPENDWA WADAU,
KATIKA KULIENDELEZA LIBENEKE, LEO NINA FURAHA KUBWA MNO KUWATAMBULISHA KWENU MVUNJA MBAVU MPYA AMBAYE KAJIUNGA KWENYE GLOBU YA JAMII  TAYARI KWA KUTUCHANA MBAVU KWA KATUNI ZAKE MBALIMBALI. 

JINA LAKE SI LINGINE ILA FADHILI MOHAMED A.K.A MTOTO WA USWAZI. NI KIJANA MDOGO BADO NA NI KWELI ANATOKEA USWAZI. HIVYO HABAHATISHI. KILA KITU CHAKE NI ORIJINO TOKA JIKONI....

KATUNI ZA FADHILI MOHAMED, AMBAZO ZIMETAWALA MAGAZETI MBALIMBALI YA KISWAHILI KWA MUDA MREFU, HUWAKILISHA MUONO WA MAISHA KWA JICHO LA MDAU WA USWAZI AMA USWAHILINI AMA WANAKOISHI WALALAHOI. STELINGI  WAKE MKUU ANAITWA KABWELA (TUTAMUONA SIKU ZIJAZO), WAKATI KATUNI ZAKE ZINGINE NI ZA AINA TOFAUTI TOFAUTI. NA LUGHA ANAYOTUMIA NI YA USWAZI PYUA....

 PICHANI JUU NI MTOTO WA USWAZI  FADHILI MOHAMED AKIKABIDHI VITUZZZ AMBAVYO KANIOMBA NIFUNGUE DIMBA NA HIVYO HAPO CHINI VITATU VYA CHAP CHAP. KAZI KWENU WADAU. MAONI YANAKARIBISHWA.

-MICHUZI


-------------------------------------------------------------------------------------------------
-------------------------------------------------------------------------------------------------
-------------------------------------------------------------------------------------------------

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 07, 2009

    Big up dogo! kaza buti!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 07, 2009

    Kazi nzuri kijana ila sura ya cartoon mwanzo nilijuwa ni kabwela. ila jitahidi ni nzuri cartoon ya mwisho ungeweka mateja wawili wamekaa wanaulizana.

    HIVYO RAisi wa Libya na Raisi wa Tanzania ni Ndugu? Teja mwengine anauliza kwanini? alafu anasema Sababu nimeona jana kwenye Luninga wakisema Gadafi Raisi wa LIbya na Kikwete Raisi wa Tanzania inaonesha Baba zao mmoja wote watoto wa Raisi.

    Ila niliona Cartoon moja nilicheka walisema Mpingo alilogwa zamani alikuwa zeruzeru yule. Pazi.

    ReplyDelete
  3. Al MusomaMay 07, 2009

    Ya nwisho inanikumbusha Mchaga aliyeuliza: Hivi rais wa Kenya anaitwa nani? Akaambiwa anaitwa Kenyatta (enzi hizo, hujazaliwa) na ndipo alipo-konkludi: Kumbe yule wa Zambia ni Zambiatta, eh? Recalled from one of the soul-consoling night jokes after the day's hard work at Mafinga JKT (1984) - where you there?

    ReplyDelete
  4. MASHAURIMay 07, 2009

    USHAURI WA BURE:
    Ili sanaa yako ya mkono ikamilike vizuri, ni vema utafute "writting mark" yako, then uachane na ku-type hayo maandishi.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 07, 2009

    Huyu dogo yuko makini tangu 1990s

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 07, 2009

    Ndugu Michuzi asante kwa kutuongezea viburudisho vya akili. mimi ni mpenzi sana wa katuni.
    Ile ya nyumba ndogo imenitoa jasho kidogo!!

    Nitumie nafasi hii kukupongeza kwa kuchukua uamuzi mzuri wa kubadili kuvuli chako cah utambulisho wa blogu ya jamii kutoka kile ulichokuwa na kamba shingoni (mimi huwa ninawaonea huruma wanaoshinda wamejikaba na kamba hizo) na kuingiza hiki ambacho ume-relax (chambilecho waswangreza) katika fulanazzzzzzzzzzzzz.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 07, 2009

    Kazi nzuri kijana, chi hii inahitaji entrepreneurs (nafikiri ni wajasiriamali) kama ninyi. Big up!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 07, 2009

    LMAO!!
    Dude, you are funny! nimecheka kweli...keep it up, talent unayo...

    Lakini wabongo bwana s'times shida tupu!Mfano mzuri huyo anon. wa May 07, 2009 12:42 AM; Badala ya kutoa constructive criticism anaona kapata nafasi ya kutoa joke yake, (which wasn't funny at all to me)anajidai anajua sana cartoon jokes,zako ziko wapi?kazi kudandia tu za watu... anzisha yako tuone...

    ReplyDelete
  9. Safi sana kaka michu. huo ni msaada tosha kwa dogo wa uswazi. dogo kaza buti sasa hii ni nafasi muhimu sana kwako kujiimalisha. kwani kupitia hii blog ya jamii utakuwa na jina kubwa.

    heko michu kwa kumbeba dogo.



    mdau wa k/koo shimoni

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 07, 2009

    Aminia MISUPU, Mlete dogo huyo atupunguzie STRESS mana kila kukicha habari mbaya hazishi.

    AMINIA BABAKE!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 07, 2009

    aaaaaaaaaah huyu jamaa katuni zake huwa nazipenda sana yaaani hapo michuzi umecheza weka nyingi tu kama hiyo katuni nyumba ndogo imeniacha hoi sana kumuuliza buzz lake kama leo katoka fresh au kapalaganya......big up staili ya katuni zako poa sana

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 07, 2009

    SONGA MBELE, USIRUDI NYUMA

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 07, 2009

    kijana una bahati sana wewe, leo comments karibu zote wapo na wewe! sijawahi ona maana kuna waosha vinywa humu, kukosoa hawajambo. Hongera sana

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 07, 2009

    Michu, sisi nyumbani kwetu tuna mtoto wetu mwenye jina la Kabwela sababu ya "hand writting" yake na unene fulani hivi kama wa Kabwela, kwa hiyo naungana na Mashauri aliyetoa ushauri wa bure wa Kwa Fadhil kuachana na ku-type maandishi. Vinginevyo namkubali sana.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 07, 2009

    Katuni nzuri hasa hio ya madam na buzi lake, lakini naona usi type maandishi, kama alivosema mdau hapo juu. tafuta mwandiko wako au hata kama ni wa kompyuta usitumie huu ambao ni coomon sana. Swali hivi katunist wa Tz wanauzaga katun zao kwa watu binafsi? mmoja mmoja kama mimi? nikitaka katuni ya kutoa ujumbe maalum? naweza oda?

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 07, 2009

    Wadau wengine bwana lazima waharibu sijaona kama Anon alikosoa yeye kampa mifano aweke kwenye cartoon jamaa sizani kama nikosa Jamaa dogo katuni zake ni nzuri sana. unaweza usiweze kuchora ila ukawa na ushauri kwa jamaa akazifanyia kazi sizani kama ni kosa eti Wadau? hata maraisi wanawashauri.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 07, 2009

    Mshikaji wewe ndio huchekeshi tizama wenzako wote ni wametaka kuzidi kumsaidia kwam ifano sababu ni kijana mwenye juhudi, wewe unaleta kidogo na maandishi ya kiengereza umepotea kaka tizama wenzako. ongea watu wote wakuelewa kwani si katuni ya kiengereza hiyo ya uswazi. Ongea kiswahili.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 07, 2009

    Habari zenu wadau mtanisamehe kama nimemuuzi mtu yoyote sababu nimeona mdau mmoja kasema kwamba nimemkosoa Kijana, kama anaona hivyo nitaomba msamaha kwa wadau wote mie najaribu tu kumpa changamoto zengine kama wadau wengine tu Ahsanteni. Mdau mwenzenu. Pazi.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 07, 2009

    safi sana utafika tu dogo kazi njema sana

    dah leo michu UMEVAA NINI???

    hahahahahaaaaaaa

    msalimu mai waifu wako!!

    ReplyDelete
  20. Nakumbuka kazi zake, kwenye gazeti la Reta Raha kila Jumapili aposema Cheka kispoti

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 08, 2009

    lol!, funny!

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 08, 2009

    mwana mwaga tuuu katuni zako ni bomba sana achana na huyo mpasua mbao mwenye kutoa ushauri kwani maandishi yanakupunguzia nini au yanaongeza nini kwenye katuni lala mbele ukoo ...mwana we chora katuni andika mwandiko wowote tu sisi tunachota sisis tucheke tuu kafie mbele wewe mwenye ushauri wenye matege......

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 08, 2009

    Namfagilia sana kijana.He got talent.Eti sio wewe ulikuwa unachora katuni anaitwa Matongo?.Kama ni huyu Michu,naomba jibu tafdali!Kama ni wewe uwe unamweka Matongo jamani,tht was the funniest cartoon character (to me).Ahahaha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...