Mwandishi maalum, Songea

WAANDISHI wa habari mkoani Ruvuma wanajutia kibao alichopigwa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, kuwa kimeanza kuwasababishia kazi ngumu kwa kutakiwa kuwa mbali na viongozi wa kitaifa wafanyapo kazi yao.

Hali hiyo imejitiokeza mkoani hapa wakati wa ziara ya siku tatu ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambapo kumekuwa na ulinzi mkali na kuwafanya wapiga picha za mgando na luninga kukosa ubora waliouzoea kutokana na kusisitizwa wawe mbali. 

Sio hao, pia waandishi wa redio walipata wakati mgumu wa kunasa sauti ya Waziri Mkuu kwa kuomba mwandishi wa waziri mkuu Irene Bwire, awachukulie vinasa sauti vyao akavitege jirani na kiongozi huyo.

Baadhi ya waandishi mkoani hapa wameelezea adha hiyo imetokana na kibao alichopigwa Rais Mstaafu Mwinyi (mzee Ruksa) katika Baraza la Maulidi jijini Dar es Salaam mapema mwaka huu. Mwandishi wa Radio Free Africa na Star TV, Adam Nindi, alisema imemuwia vigumu kupata picha na sauti nzuri kwa umbali waliopangiwa.

“kibao cha mzee Mwinyi kitatutesa wote,” alisema Nindi na kufafanua kuwa walinzi wa viongozi na waandishi wa habari ndio watakao onja joto ya jiwe zaidi.

Naye mwandishi wa TBC1 mkoani hapa, Gerson Msigwa, alifananisha kibano hiki pia kimechangiwa na mwandishi wa habari aliyemtupia kiatu Rais wa Marekani kutoka chama cha Republican, Geoge Walker Bush aliyemkabidhi ofisi Rais wa kwanza mweusi Barak Obama.

“Hii ni changamoto kubwa kwa waandishi wa Tanzania kufanya kazi zetu vyema kwa umakini na ubora unaohitajika, “ alisema Msigwa ambaye pia alikwenda nchini Marekani kuripoti kampeni na Uchaguzi za urais wa nchi hiyo yenye nguvu duniani.

Naye mwandishi wa gazeti la Majira mkoani hapa, Joseph Mwambije alisema kibao alichopigwa Mwinyi, wasibebeshwe msalaba waandishi ambao sio wa kwao, kwani aliyefanya hivya hakuwa mwandishiwa habari. “wasitubebeshe msalaba ambao si wa kwetu,’ alisema Mwambije.

 Changamoto ya kibao alichopigwa Mzee Ruksa pia ilijadiliwa mjini Dodoma Aprili 28 mwaka huu, wakati wa Mkutano Mkuu wa Vyama Vya waandishi mikoani, (Press Clubs) ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Muungano wa Klabu za waandishi mikoani (UTPC) Abubakar Karsan, aliwataka viongozi wote wa waandishi kuwa makini kusimamia nidhamu za waandishi wao. 

Alisema ni wajibu waandishi na wadau wa habari kutafuta njia ya kupata vifaa bora na kujifunza jinsi ya kuvitumia kupata ubora wa habari wanazozihitaji kwa matumizi ya umma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 06, 2009

    Waandishi wa habari nawashauri mwasusieni viongozi wanaowapa mikwara na msiwatangazie ziara au shughuli zao. Weeenyewe watawatafuta!
    KILI
    BG

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2009

    Ngugu Waandishi, umefika wakati kwenu wa kwenda na wakati. Suala la ulinzi wa "VIONGOZI" KWA SASA NI SUALA MTAMBUKA. Hakuna na haitotokea kikosi cha ulinzi wa viongozi kubahatisha tena ama kufanya kazi kwa mazowea. Dunia imebadilika. Haitotokea tena kwa namna yoyote muweze kuwasogelea viongozi hao kwa karibu. Cha muhimu ni kuzingatia na kujipanga upya kwa kuwa na mbinu za kufanya kazi kwa ufanisi na haraka na salama. Ni wakati wa kuwa na vyombo vya kisasa kama "kamera" zenye uwezo mkubwa wa kupata matukio toka umbali muafaka kwa wakati muafaka. Niwakati wa kutumia pesa ili mupate pesa. Vinginevyo mtaishia kulalamika na kutukosesha haki ya kupata habari wakati mna akili nyingi na ubunifu wa hali ya juu."WACHENI HIZOOO NA AMKENI SASA"

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 06, 2009

    poleni inabidi mbadilike hapo mjue sayansi na teknolojianikitu gani ama laa sivyo mtaishia kulalamika kumbe tatizo ni nyie

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 07, 2009

    Shehe Yahaya ametabiri viongozi wengi zaidi kuzabwa vibao. Wameanza kuchukua tahadhari.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...