Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akikagua shamba la mahindi la gereza la Mollo wilayani Sumbawanga akiwa katika ziara ya kukagua  maendeleo  ya  kilimo mkoani  Rukwa
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda na Mkuu wa mkoa wa Rukwa,  Mh. Daniel Ole Njoolay  wakitazama mahindi  wakati  walipotembelea   shamba la gereza la Mollo wilayani Sumbawanga 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 11, 2009

    Du kweli mahindi yamekubali ingekuwa mjini hayo yote yangeishia kuibwa na kukutwa yanachomwa mitaani mmoja sijui bado shs 100 au imepanda sasa.

    Ila kinachonishangaza hapo mbona muheshimiwa amejengewa jukwaa karibu na shamba?, ina maana anahutubia mahindi? au. Hii picha haijatulia kabisa. Kampeni za ubunge 2010 zimeanza sasa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 11, 2009

    MOLLO KWA MAHINDI HAWAJASHUKA. TULIPITA KARIBU NA HAPA KWENDA SHULE KANTALAMBA MIAKA YA 1990s. MFANO MZURI WA KUKOMESHA NJAA NCHINI.

    Nilisoma na hawa jamaa. Popote walipo naomba tuwasiliane:-

    Marko Mazombwe, Steven D. Kaggi, Hussein Kitta, Alfred Kituli, Sinkala Kumbakumba, Mathew Mahimbi, Evaristo Haule, Alex Nkondola, Lucas Lukanazya (Dodoma Boy), Daud Lumelezi, Moses (Bishop), Jerome Mwkabaga, Lee Joseph, Mwamafupa, Heri Kayinga, Vituka boy, Songea Boy, Andrew Legembo (Jombi), Marko Mwipopo, Said Hamis, Luca Mpwepwa, Kwame Daniel, Jeremiah Ponera, Mother tongue, Ramadhan Juma Mzarau, na wengine kibao.

    ....... yeyote anayemjua mmojawapo anipe contacts zao/simu au email.

    ReplyDelete
    Replies
    1. alfred kituli yupo uk....mtafute kwenye yahoo messenger utampata

      Delete
  3. AnonymousMay 11, 2009

    Pongezi WM Pinda kwa kuwakalisha kitimoto na kuwafunda wakuu wa mikoa. Kimsingi wengi wa viongozi wetu wanaiona wao ni WATAWALA NA SI VIONGOZI kwa hakika wamepinda. Wanyooshe. Ukweli ni kwamba falsafa ya Maendeleo ya WASU - Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora bado ni endelevu kama alivyobainisha Mwalimu Nyerere. Tatizo ni kwamba falsafa za Julius zimepigwa kisogo. Kila kiongozi anakuja na zake na nyingi kati ya hizo mpya hazina kichwa wala miguu. Hazieleweki. Hazimgusi mtanzania. Hazitoi mwongozo wa ni vipi apambane na ujinga, umaskini na maradhi. Azimio la Arusha ambalo linabezwa na wengi lilikuwa miongozo imara kabisa ya ni namna gani tuweza kujiendeleza kwa kufanya kazi kwa BIDII tena kwa JUHUDI NA MAARIFA.
    WM Pinda kwa kuifuata mafunzo ya Mwalimu ambayo yalilenga kumfikia kila mtanzania mijini na vijijini bila shaka Tanzania itafanikiwa kuyafikia malengo ya milenia. Hongera Mizengo.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 11, 2009

    jamani mnanitamanisha sana ,hayo mahindi nina miaka takribani 10 sijawahi si kuyatia kinywani tu bali hata kuyatia machoni live achilia hii ambayo ni recorded ktk picha.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 11, 2009

    mmhh! Wafungwa wanalima halafu nasikia BBC eti wanapewa msoso ovyo. Zile samaki za Magufuli si wangepelekewa??

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 11, 2009

    MDAU HAPO JUU KUHUSU JUKWAA:WALIONA NI VIZURI MHESHIMIWA AWEKEWE JUKWAA KWAAJILI YA KUMPUNGUZIA MISAFARA YA KUTEMELEA SHAMBA ZIMA. KWANI HAPO ALIPO JUU YA HILO JUKWAA ANALIONA SHAMBA LOTE MPAKA MBALI.
    ILA SASA JAMBO AMBALO HUNISHANGAZA NI PALE AMBAPO TANZANIA KUNA KUWA NA NJAA ZAMBIA KUNA KUWA HAKUNA NJAA. WAKATI WAZAMBIA WANANUNUA CHAKULA TANZANIA.
    USHAURI WA BURE, IFIKIE WAKATI WANANCHI WAFUNDISHWE MBINU NAFUU ZAKUTUNZA MAZAO.MDAU

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 11, 2009

    Kiongozi wa nchi anatakiwa awashinde wote kwa mambo mengi, hata kwa kuwa na kipawa cha kuongea na mimea

    ReplyDelete
  8. DAH-KANTALAMBA!!??(Kantalamba x2 my beloved school,our moto is to aim high and high.....)
    EEH BWANA'MIE NILIKUWA HAPO FORM 1-4(1990-1993) DAH YAANI UME NIFIKISHA MBALI,UNA MKUMBUKA MWALIMU DULE, NA MZEE HUSSEN?INA WEZEKANA WEWE ULIKUJA PALE FOR HIGH SCHOOL NDIYO MLIKUWA MNATOKA NJE,SIE TULIKUWA WA HAPO HAPO-SHULE YA MZINGI NILISOMEA MAZWI NA MWENGE.HANHA S/WANGA OYEEH.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 12, 2009

    SERIKALI INABIDI TUENDELEZE KILIMO,KULIKO KUINVST KWENYE VITU AMBAVYO HAVITUINGIZII KIPATO KWA SANA,KILIMO NI MUHIMU NA SERIKALI IKITILIA MKAZO HUKO NA IKISAIDIA KUTAFUTIA WAKULIMA MASOKO YAMAZAO YAO WAMACHINGA WATAONDOKA MJINI NA WATU WENGI WATARUDI VIJIJINI,HAKUNA MTU ANAEPENDA KUKIMBIZWA NA MGAMBO,HAKUNA MTU ANAEPENDA KUONDOKA KWAKE NA KWENDA MJINI KUPANGA WATU 10 CHUMBA KIMOJA NI SABABU WAMECHOKA KUKAA VIJIJINI KULIMA NA MAZAO KUOZA HAKUNA WAKUYANUNUA,NA MENGINE KUNUNULIWA KWA BEI ZAKIJINGA,HAIWEZEKANI MI NILIME ,THEN NIUZE DEBE LA MAHINDO SHILINGI 100,HUO SI UONEVU HUO.SERIKALI INABIDI KUWATAFUTIA MASOKO WAKULIMA NA KUHAKIKISHA MAZAO YAO YANAKIWANGO SAHIHI.HATAKAMA TUKIWA NA MAZAO MENGI SIO MBAYA KUYAHIFADHI NA MENGINE KUYAUZA KWA NCHI ZINGINE NA SIO KUOZEA MASHAMBANI.TANGA MATUNDA YANAANGUKA NA KUOZA YOTE HIYO CZ HAKUNA WAKUJALI,TUNASHINDWA KUVUNDIKA MATUNDA,KUEXPORT MATUNDA??

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 12, 2009

    Kweli washikaji!! hata mimi nimekumbuka miraba ya Kantalamba....na huo wimbo wa "Kantalamba x2 ma' be loved school...our motto is to aim high...intelligence and discipline.....mwingine amalizie sasa...
    Naomba washikaji wa form four 1992 watie timu humu e-mail na simu, washikaji tukumbukane....tulishasambaa dunia nzima sasa hivi!!
    Nijuzi tu nilisikia kuwa mwl. Simkanga na Mkulikwa eti walishafariki...nilisikitika sana walimu hao walikuwa wataalam wa Kilimo na hesabu...Mungu aziweke roho zao mahari pema peponi.

    Big up Kantalamba 1992, the best class in making but destroyed by Bokera mwalimu alokuwa Konda wa Upangwa investment halafu anafundisha kiingereza...wapi na wapi!!! Nani anasema makonda hawakusoma?...aende Kantalamba.

    Millinga alituuza kwa kuwalegezea walimu ambao mwishowe waliharibu talent zetu...
    Mara mwalimu ni Konda...mara mwalimu ni referee...it was really dreadful.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 12, 2009

    Natamani nzige waje...

    ReplyDelete
  12. KANTALAMBA!!!!
    DAH MDAU HAPO JUU,KWELI MKULIKWA KAFARIKI? ALIKUWA MWALIMU SAFI SANA KWA HESABU(alikuwa anaishi nyumba za nyuma karibu na chuo cha uwalimu na kanisani kama una kwenda mashambani?) BOKERA HAHAH ENZI HIZO NDO MABASI YAMEANZA KUINGIA S/WANGA HATA KAMA ALIKUWA AKIFUNDISHA ANGE AJIA KIPINDI NA KUFUATA BASI AKISIKIA TU MLIOWAKE DAH!!YES H/MASTER MILLINGA ALIKUWA MPOLE SANA.SAMAHANI SIKUMBUKI MANENO MENGINE YA WIMBO HUO LAKINI NINA KUMBUKA SIKU YA MKATE NUSU SIKU BAADA YA KUPANDISHA FLAG HHAHA (JUMA MOSI)WEWE UMEMALIZA 1992 OOHH NA AKINA J. NTULO SIJUI.MIE NI BAADA YAKO SIKUMBUKI NANI ALIKUWA FAMAOUS KTK MWAKA WETU.KANTALAMBA OYEEH

    ReplyDelete
  13. KWENU WADAU WACHANGAIAJI, NASHUKURU SANA KWA MAONI YENU JAPO SIJARIDHIKA KABISA NA MNAYO YAONGEA BAADHI YENU HAPO JUU. iNAOONYESHA NI JINSI GANI WATABNZANIA TUSIVYO FIKIRIA MAMBO YA MSINGI. BAADA YA KUONA HII PICHA NILIFIKIRI NITAKUTA MAONI YENYE MAANA NA YENYE MWELEKEO SAHHIHI. WALAU KUMPONGEZA TUU MR PINDA KWA UAMUZI ALIO FANYA KUFUATILIA SECTA YA KILIMO NCHINI. LAKINI CHA AJABU ETI MLISOMA KANTALAMBA SIJUI NINI NA WAPI , WABONGO YATUPASA TUAMKE NA TUWAZE MBALI. HAYA TUNBAYO YAANDIKA NDIYO TUNAYO YAWAZA KILA SIKU. WATANZANIA TUNAHITAJI VIONGOZI KAMA PINDA ANAYE JUA NINI MWANANCHI WAKAWAIDA ANAFANYA. TUNAHITAJI MOTIVATION NA SI MANENO YA WAKAA UKULU, TUNAHIJATI KUJUA VIONGOZI WANAFIKIRI NINI JUU YA KILA TUNACHO JIBIDISHA KUKIFANYA. PINDA NAMPENDA NA NITAENDELEA KUMPENDA KWANI NIMEIPENDA KAZI YAKE. TUNGEKUWA NA VIONGOZI KAMA PINDA WALAU 20 TANZANIA TUNGEKUWA NCHI INAYO TISHA AFRICA ,UMASKINI TUNGEUSOMA INTENET.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 13, 2009

    WEWE UNAYESEMA SIJUI WATU WASISEME KANTALAMBA BALI WAONGELEE ZIARA YA WAZIRI MKUU, JIKATE HUKO. NANI ALIYEKWAMBIA BLOG HII NI DARASA. DARASA AMBALO UKIKAA DARASANI NI KUFANYA ANAVYOTAKA MWALIMU. UKITAKA BLOG YA STYLE YAKO, ANAZISHA YAKO. NDIYO MAANA IKAITWA BLOG. NI YA WATU MBALIMBALI, WENY FIKRA NA VIONJO MBALIMBALI. VIONJO VYAKO KWA ZIARA YA WAZIRI MKUU NI ISHARA YA UONGOZI BORA. MIMI ISHARA YANGU NI ZIARA YA MAANDALIZI YA KAMPENI ZA JUMLA KWA CHAMA TAWALA KAMA WAZIRI MKUU. JIULIZE NI LINI ALIINGIA MADARAKANI, NA MIKOA MINGAPI AMEFANYA ZIARA KAMA HIYO. JIKATE HUKO!

    Ngoja sie tuimbe:-

    Kantalamba, Kantalamba, my beloved school x2
    Our motto is to aim high, aim high.
    Intelligence and discipline struggle;
    It is a secret of all success,
    It is our tool x2.

    Millinga alikuwa akisema:-

    Ulishaona eeee, yaani Mungu wangu! Mwanfunzi hufanyi mazoezi! Ndiyo maana unakuta wengine vidole vya mikononi vingine vinene mwishoni karibu na kucha, kwasababu "blood circulation" is not even!/............ HE JOKED IKE THAT...

    ANOTHER ONE:

    Eee Mungu wangu, ulishaona eeee?
    Mtu anakulia kijijini, Sumbawanga ndio anafika kwa mara ya kwanza, anapokuja kusoma Kantalamba. Halafu anapata "A" ya Kiingereza. Hajawahi kumwona hata mzungumzaji wa Kiingereza, ila mwalimu wake tu!

    ANOTHER ONE: - Unapoishi familia maskini unafanya kazi ngumu, kama kubeba mizigo mizito kichwani, na yale maumivu ya kazi nzito yanakuharibu sura, maana muda wote unakuwa mwenye huzuni..... Angalia watoto wanaotoka familia nafuu, ni tofauti!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...