TAIFA STARS
DRC
mshambuliaji hatari wa kongo alain kaluyituka dioko
ambaye kaiua taifa stars leo kwa kufunga mabao yote mawili. kijana huyu mwenye umri wa miaka 25 anaichezea T.P Mazembe ya Kinshasa

MABINGWA WA KOMBE LA CHAN TIMU YA TAIFA YA KONGO IMEITUNGUA TAIFA STARS 2-0 KATIKA MCHEZO WA KIMATAIFA WA KIRAFIKI KWENYE WANJA JIPYA LA NESHNO HAPA DAR.

MFUNGAJI WA MABAO YOTE NI HUYO KALUYITUKA DIOKO AMBAYE ALIFUNGUA UKURASA KWA BAO SAFI DAKIKA YA DATO YA MCHEZO NA LA PILI ALILIFUNGA KWA KUMTUNGUA KIPA WA STARS JUMA DIHILE KWA KIKI KALI. NA MPIRA UMESHAMALIZIKA.

UMATI ULIOJITOKEZA KUANGALIA MCHEZO HUU UZALENDO ULIWASHINDA MARA BAADA YA STARS KUPIGA BAO LA PILI MAANA SIO TU WANAWASHANGILIA CHUI WA KABILA KWA NGUVU ZOTE BALI PIA WANAMZOMEA KOCHA WA STARS MARCIO MAXIMO.

LAKINI WANAMUONEA TU MAXIMO, JAMAA MPIRA WANAUJUA NA KOCHA WAO AMEKIRI KWAMBA HII INATOKANA NA MAADALIZI TOKA TIMU ZA VIJANA NA MASHULENI.

KOCHA MAXIMO AMESHUKURU MUNGU KWA KUZOMEWA NA AMESEMA WALIOMZOMEA LEO MWAKA UJAO WATAMPIGIA MAKOFI, NA KWAMBA KONGO SI TIMU NDOGO, NI BINGWA WA CHAN HIVYO9 MECHI ILIKUWA NGUMU SANA. AMEFURAHI KWAMBA WACHEZAJI WAKE WAMEPATA UZOEFU NA PAMOJA NA KUFUNGWA AMEWAPONGEZA WACHEZAJI WA STARS NA KUSEMA TIMU YAKE NI NZURI NA BAADA YA MUDA MATUNDA YATAONEKANA.
KOCHA WA KONGO SANTOS MUNTUBILE AMESWEMA WAO WANA UZOEFU WA WACHEZAJI KUWA PAMOJA KWA MUDA MREFU, NA AMESEME MECHI ILIKUWA NZURI KWA UPANDE WAO KWANI IMEDHIHILISHA WAO NI MABI NGWA WA CHAN. AMEWATAKA MASHABIKI WASIMKATISHE TAMAA MAXIMO ILA WAFANYE SUBIRA WAMUACHE AFANYE KAZI YAKE, KWANI MPIRA SI LELEMAMA - UNATAKA MAANDALIZI YA MUDA MREFU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 09, 2009

    Kila siku wachezaji wapya tunajenga mara tunabomoa hatuna jipya na tutaendelea kuchapwa tukiwa chini ya huyu mnafiki maximo

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 09, 2009

    Michuzi ebutuelezee mpira ulivyokuwa katika timu zote mbili na hasa kwa strs yetu, na inakuwaje washabiki wamzomee kocha wa wa stars because we bilive that soccer is game tell peple the
    truth!!!!

    Mdau canada.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 09, 2009

    Hapa Maximo amekalia kaa la moto.
    Wadau mlioshuhudia vipi, Wabongo tulianza kuhesabu pasi za Wakongo?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 09, 2009

    look at this guy, he is mascular and well trained. our players are weak , we need to build our team from vidudu starting today.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 09, 2009

    MPIRA SIKU ZOTE NI VITENDO NA SIO MANENO. WACHEZAJI WETU WANADHANI KUANGALIA EUROPA SOCCER NDIO SOLUTION. SAHAUNI KABISA, MPIRA UNAHITAJI MAZOEZI, BIDII, NA KUBWA ZAIDI NI DISCIPLINE: HAKUNA MAAJABU KATIKA MPIRA.

    SERIKALI NA WANANCHI WANAJITAHIDI KUWAUNGA MKONO WACHEZAJI WETU, ILIYOBAKI NI KAZI YAO. KWA HALI HII HATA SOMALIA BATATUFUNGA VENYE BANAPENDA.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 09, 2009

    Matatizo yote ya Tanzania hata, kabla Tanzania haijawa huru au nchi,yanatokan an kutoweza kutumia vizuri rasilimali watu; kwa mfano viongozi kujidai wajanja kuwazunguka wanachi na mikataba ya ajabu na wageni ni kutoka enzi za utumwa- maana tulikamatana sisi wenyewe na kuuzana lwa waarabu na wazungu; mikataba ya madini ni habari za vingozi kula na wageni wakijali matumbo yao tu; kushindwa kutrain au kuandaa wananchi katika kila hali kam ni michezo au masomo huku wakubwa wakisomesha watoto nje badal ya kujenga taasisi hizo hapa; wakubwa kutibiwa nje huku wananchi wakisota na huduma ya afya mbovu badala ya kujenga hospitali bora na kuwapa madaktari wa kitanzania mazingira bora ya kufanya kazi wabaki hapa hapa na mifano mingi mingine. Maximo kaja kula nchi, hawezi kuleta miujiza na wachezaji walokomaa wakati viwanja vya michezo vya shule mnawauzia mafisadi na hata shule zingine ni majengo tu hakuna nafasi ya michezo au waalimu wa kutosha ya kuwaanda vijana wakiwa wangali wadogo. Samaki mkunje angali mbichi tunasema sisis wenyewe waswahili lkaini matendo yetu inakuwa kama hatuelewi.
    Alafu mimi niliwahi kusema katika mazungumzo na ndugu zangu fulani kabla ya National na Uhuru Stadia mpya hazijaanza kutumika kwamab hivi viwanja ni maandalizi mazuri ya maeneo ya wageni kuja kutufungia, na kweli sasa tunayaona. Maana yake tunawekeza katika hatua ya mwisho tu kwa watu ambao katika hatua za awali wachezaji wetu hawajawahi kuona viwanja hata vinavyokaribiana na hivyo wakiwa katika ujana wao, no investment at all in sports facilities in schools or at lower levels alafu mnawekeza mabilioni kwenye national stadium. We have no plan no startegy at all- 'Mpira wa Tanzania ni sawa na kichwa cha mwenda wazimu' kingozi moja inasemekana aliwahi kusema, lakini uendawazimu huo si katika mpira tu wala hauanzii hapo tu!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 09, 2009

    Huyohuyo ni kocha huyohuyo ni wakala!, sijui ana leseni ya FIFA? Hatuongei sana maana isije tukaitwa mapapa wa kelele!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 09, 2009

    Watanzania tusitegemee miujiza, hata kocha wa DRC amelisema hilo.

    Juzijuzi mchezaji wetu wa kutegemewa Mrisho Ngassa alipewa nasaha na jopo la West Ham United ya Uingereza kuzingatia lishe, mazoezi,kujenga mwili na nidhamu(ndani na nje ya uwanja).

    Vitu hivyo si kwa Mrisho Ngassa bali kwa wachezaji mpira wote Tanzania kwa kusaidiwa na makocha kama Maximo ,Bushiri, Minziro, Phiri.

    Lakini vipaji vinatakiwa kupatikana ktk ngazi za chini kama shule za msingi na sekondari, hivyo wadau wa mpira na serikali kuu, pamoja na serikali za mitaa zinabidi kuwa na mikakati ya muda mrefu kuwekeza na kuendeleza michezo toka ngazi za chini.

    Mechi hii ya Taifa Stars na DRC imeonyesha changamoto inayotukabili na mikakati itakayo boresha michezo, na sio Maximo au Kaseja wanaoweza kuikweza Tanzania.

    Pamoja tutafanikiwa.
    Mdau
    Rocky.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 09, 2009

    Jamani Watanzania kila kitu ina kuwa mizengwe kwetu kwa sababu ya mdomo. Maneno mingi sana lakini tukija kwenye vitendo tuna babaisha babaisha. Hii itaisha lini? Na ni kasumba kutoka wapi.

    I can't imagine kufungwa na Congo ambao muda wote wapo kwenye matatizo ya vita na wanaweza kuji-organize na kuunda timu nzuri kama hiyo na mengineyo mengi.


    Sasa nauliza Wanzania wenzangu; hii raslimali ya amani ambayo viongozi wetu wamekuwa wakiipigia tarumbeta kila kukicha inatusaidia nini? Enough is Enough Watanzania. Tujengeni mikakati ya kujinasua kwa kulengo la kujenga.

    Asanteni sana;

    Mdau Mzalendo.
    (Idumu Tanzania)

    ReplyDelete
  10. Baba UbayaMay 09, 2009

    huyo mcongo aliepiga bao 2 muda si mrefu utasikia Simba au Yanga wanaanza kumfuatilia,kisa kaipiga bao mbili Staz.hivi hizi Simba na Yanga huwa wanafanya uchunguzi wa kina kabla hawajasajili wachezaji wa kigeni?au ndo mradi wakisikia na kuona idadi ya magoli aliyofunga basi ni repoti tosha kumsajili?

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 09, 2009

    hiviii inakuwaje jamani hapo michuzi ebu niambie hivi bado juma kaseja ana nafasi kweli.. mi kwakweli huyo kocha wa viungo yaaani maximo ajamuona tu uwezo wake jamani hilo li kocha lionoke linapata mshahara wa bure jamani fukuzeni hilo.. aaah mi nimechoka sasa kusikia tunafungwa ......
    mdau uk

    ReplyDelete
  12. Pamoja na mazoezi pia ni lazima wachezaji wa maumbo na mwili ambao utapokea mazoezi, ebu angalia jamaa aliyetufunga alivyojengeka kimwili. Wachezaji wetu wote hawajengeka kimwili na hivyo itakuwa vigumu sana kuweza kushinda mechi za kimataifa.

    Nilazima tupate wachezaji waliojengeka miili kule Mbeya, Mwanza na tuwapatia mafunzo ya kutosha, timu iliyokamilika inatakiwa iwe wachezaji wenye miili midogo wasizidi wawili au watatu wakati mmoja.

    Tatizo jingine la wachezaji wetu ni ulevi na wanapopata pesa wanakunywa sana na kula kidogo, ambapo mpira wa siku hizi huwezi kifanikiwa hata kidogo.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 09, 2009

    Huenda kesho tukasikia Maximo kawatema wachezaji wengine aliowatain kwa mda mreeeeeeeeefu na kutuletea wengine wasio na uzoefu kabisa wa mapambano ya kimataifa! Tusubiri, tutaona!

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 09, 2009

    Michuzi weka rekodi sawa, tafadhali. Kaluyituka Dioko kweli huchezea TP Mazembe ya LUBUMBASHI si Kinshasa..

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 10, 2009

    MDAU KISIJU NAWAKILISHA!.

    TATIZO HATUNA KOCHA ANA MIAKA MITATU ANADAIA ANAJENGA TIMU KILA SIKU.AMUONE KOCHA WA CHELSEA HANA VISINGIZIO.

    OOH WENZETU WAMEANZA NA MPIRA TOKA SEKONDARI NA SISI TUNAO KINA HENRY JOSEPH TOKA MAKONGO, BOBAN NA KASEJA HAWATAKI MAXIMO. HUKO CONGO KUNA SHULE GANI YA MPIRA WAKATI JAMAA WAKO KWENYE VITA?

    NIDHAMU YA NJE NA NDANI SIO KWELI STEVEN GERRARD ALIKUWA NA KESI NA AMELALA POLISI KWA KULEWA BAR,

    CHELSEA JUZI WAMEMALIZA MECHI KILA LAMPARD WAMEENDA CLUB HADI ALFAJIRI BAADA TU YA MECHI,

    MARADONA ALIKUWA ANAKULA MADAWA YA KULEVYA NA BADO KACHEZEA TIMU YA TAIFA, GAZZA NA GEORGE BEST WALIKUWA WALEVI WAKUBWA LAKINI MAKOCHA WAZURI HUCHUKUA KIZURI CHAO NA KIBAYA KUKIREBISHA.

    RIO FERDINAND NI MVUTA BANGI LAKINI FERGUSSON ANA SAIKOLOJIA YA UKOCHA AMEMREKEBISHA NA SASA NI KAPTEN WA TIMU YA MANCHESTER UNITED.

    MAXIMO SIO KOCHA HAKOSI SABABU,ANADANGANYA KUWA ALIPATA TIMU SOUTH AFRICA HAKUENDA KWA VILE ANAIPENDA TANZANIA, SIO KWELI ANAIPENDA WALLET-POCHI YETU TU.

    PIA NANI SOUTH AFRICA ATAKUBALI KUONA NCHI YAO ITASHINDWA KUCHUKUA KIKOMBE CHOCHOTE NA KUMUACHA KOCHA AKIENDELEA TU?

    MAKOCHA ALIOWALETA MAXIMO JUZI WAMESEMA KUWA WAMEKUJA TZ KWA VILE MISHAHARA NI MIKUBWA SANA.

    NANI TFF ALIFUATILIA VYETI VYAO KUJUA KUWA KWELI HAWA JAMAA WANA SIFA HIZO?

    MAXIMO ANA NAFASI KUBWA KWENYE NCHI YETU KULIKO KWAO.

    NIONAVYO MIMI MAXIMO HAONDOKI LEO WALA KESHO HATA TUKIMPIGA NA MAWE.

    KOCHA WA SIMBA AMEKUJA MUDA MFUPI NA AMEBADILISHA MFUMO WA UCHEZAJI WA TIMU. HUYO NI BORA YA MAXIMO.

    MARA ANATAKA WACHEZAJI WATOTO BASI ACHUKUWE TIMU YA VIJANA NA HII SENIOR AWAACHIE WENGINE.

    MARA BOBAN,KASEJA NA CHUJI HAWANA NIDHAMU MBONA KOCHA WA YANGA,SIMBA HAWANALALAMIKI KUWA WACHEZAJI HAWA HAWANA NIDHAMU?

    NI WAKATI WA SERIKALI NA TFF KUMBANA MAXIMO KUONA PESA ZETU HAZIPOTEI BURE.

    KILA MARA ANAONGEZEWA MUDA AU TFF KUNA TEN PERCENT YENU?

    KOMBE LA CHAN HALINA MAFANIKIO YEYOTE KWA MAXIMO KWANI FIFA HAWALITAMBUI PIA TIMU KAMA NIGERIA,MISRI HAZIOKUONA UMUHIMU WA KOMBE HILO KWANI HALINA HADHI KWA KIFUPI UNAWEZA KULIITA KOMBE LA MAXIMO.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 10, 2009

    Kila siku nasema sisi ni nchi ya wajinga. Hata ukisoma blogu tu utaona, acha hao wachezaji.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 10, 2009

    Annon wa 4:16,umeandika PUMBA,huwezi linganisha Chelsea na timu ya taifa ya bongo.Ni sawa na kulinganisha mbingu na nchi.Chelsea wachezaji wote wako fiti toka vidudu na bongo je???Chelsea wameizidi bongo kila idara kuanzia pesa,wachezaji,makocha,viwanja n.k.Think b4 kuandika hizi pumba hapa.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 10, 2009

    leo staz ya maximo

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 10, 2009

    Hii ingia toka ya Maximo inaonehsa wazi kuwa sio kocha anaetufaa. Sasa ni miaka 3 na zaidi bado anadai anatafuta timu, bado hajapata first eleven. Wakati tunaendeleea kufungwa, sisi wadau wazalendo wapenda mpira kwa kweli tunaumia sasa kwa Maximo kutuharibia wachezaji wtu. Wachezaji walio na vipaji anawakataa anachukua wachezaji wa mchangani, lazima wafungwe tu. congo wana mpira gani kutuzidi sisi? Ngasa hawezi kuwika kama hakuna combination ya wachezaji wazoefu akina Moshi na Chuji. tatizo la watu wanaomtete mnaximo haajui mpira. Kwa kiwango chetu cha mchezo miaka ya nyuma sisi tulitakiwa kuwa sawa na Zambia, Kenya, Uganda na DR Congo. Maximo toka aje ametuharibia tu, leo hii timu yetu inazidi kuporomoka katika viwango vya FIFA, majirani zetu wanazidi kupanda. Kwenda CHAN sio tija kikombe hiki hakina umuhimu wowote kwa FIFA. Maximo anawaacha wachezaji wazoefu anadai anaandaa vijana, sasa huku si ndio kuwaharibia hawa wazoefu?.

    ReplyDelete
  20. Baba UbayaMay 10, 2009

    mdau gpublicstrategies,maumbo sio kifezo kivile.swali ni kwamba,je hawa wachezaji wanafuata kweli wanachofundishwa?unajua hata hao wachezaji wa kulipwa kuna baadhi hata makocha wao huwaweka benchi sababu wanapokuwa uwanjani hawafanyi vile kocha alivyomweleza.kila idara ina majukumu yake sasa kama mchezaji anashindwa kujua jukumu lake hapo ushindi ni kitu cha kukiota tu kila leo.
    kuhusu maumbile,Yossi Beneyoun,Wright-Phillips na nwengine wengi wana maumbo madogo lkn wanafuata maelekezo ya mwalimu.
    alafu pia,hii kitu ya kumjenga mchezaji inatakiwa iwe ktk vilabu vyao.wachezaji wanakuwa ktk timu ya taifa kwa muda mfupi kwa maandalizi ya kiufundi juu ya mechi na sio mambo mengine.

    huenda wachezaji wetu wakiingia uwanjani wanasahau kabisa majukumu yao.na hilo ni kosa kubwa ktk soka ya sasa.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 10, 2009

    Chui wa Zabanga wanatisha.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 10, 2009

    oya hao jamaa baada ya game mmewapeleka ngwasuma? na leo waende akudo!

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 10, 2009

    samahani huyu mdau kisiju ni mke/mme?!inavyoonekana huyu ana walakini tu sio bure.eti kisa maradona alivuta unga na sie tukachukue wachezaji wavuta unga what a loose idea?imagine those kind of loosers like him trying to open their stinking mouth to tell us wot to do in football,dam they should go hell i don care.I think if u don have nothin to say u better shut ur zz off.

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 10, 2009

    ukiachilia mbali stamina,kasi ya mbio,ball control na pumzi, mchezaji bora sikuzote lazima awe na akili inayofanya kazi kwa haraka sana,hi sio ktk football tu bali hata ktk michezo mingine pia ikiwemo chess,draft n.k ili kumwezesha kufanya maamuzi ya haraka na kubadili technics,sio tu kama amefundishwa hivi inakuwa ni dogma hawezi kutumia akili yake pia kufanya maamuzi haraka haraka. pia lazima asiwe mchoyo na mtaka sifa binafsi,lazima ajuwe kuwa ushindi huwa ni wa timu nzima,japo kiwango chake binafsi kinamtafutia soko ktk mpira.
    wachezaji wetu wengi bongo lala na niwachoyo[wabinafsi]sana, tena waendekeza mademu na vipombe kutaka sifa mitaani ndiyo maana hawafiki kokote zaidi ya msimbazi.
    mtu asikudanganyeni anaye weza kujituma kwa bidii milango ya mafanikio iko wazi ilimradi tu amenuia,na kama ana kipaji[stamina+speed+pumzi+ubongo mwepesi] mafanikio ni lazima,atapata wa kumpromote tu auzike hata nje.
    lakini kwa style hii ya kucheza uwanjani huku sauti nyororo za kina dada zikisema "USINIUMIZIE" zina walewesha sifa hamfiki kokote!!!
    xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 10, 2009

    WEWE PIMBI WA 9.24 AM KWELI HUNA KITU KAMA MAXIMO TUSIJEFANANISHE NA CHELSEA?TIJUFANANISHE NA TIMU GANI? MSUMBIJI,UGANDA AU SOMALIA?

    KAMA CHELSEA WANA TIMU YA WATOTO KWANINI WALIMNUNUA DROGBA,KALOU ESSIEN?LIVERPOOOL WANA GERRARD NA GARRAGHER TU WENGINE WOTE WANANUNUA KWANINI WASITEGEMEE ACADEMY KISINGIZO CHA MAXIMO.

    TIMU YENYE ACADEMY NZURI NI WEST HAM JEE KWANINI WASIWE MABINGWA?KAMA ISSUE NI CHINI NA MAXIMO ANATAKA KUJENGA MSINGI BASI ACHUKUE TIMU YA ACADEMY AU YA VIJANA NA HII AWACHIE WENZIE.

    KOCHA NI WANGEMUACHA SCHOLARI KWA VILE WANA TIMU YA WATOTO NA PESA.
    TBC INA AIM KUWA KAMA BBC AU CNN HAJILINGANISHI NA ITV YA MENGI AU KBC.

    UNATAKIWA UJIFANANISHE NA ALIYEJUU ZAIDI NA KIGEZO CHA FIFA NI KIMOJA, KWA HIYO UNATAKA STARS INAJIFANISHE NA TIMU YA CONGO AU ANGOLA?

    MAXIMO SIO KOCHA HAKUNA KOCHA DUNIANI ASIYEJUA MIPAKA YA UHURU WAKE,HAKUNA CHOMBO CHA KUMTHIBITI MAXIMO,

    WAMEFUKUZWA
    MAFTAH,BOBAN,KASEJA,CHUJI HAKUNA MTU AU WATANZANIA WANAOJUA NINI KIMETOKEA,NA HAWA WACHEZAJI HAWAJAPEWA NAFASI YA KUSIKILIZWA AU KUWAPA FURSA YA KUSEMA KILICHO MOYONI MWAO.

    WEWE PIMBI UNASEMA KUWA NI THINK BIG KABLA YA KUANDIKA, WEWE MBONA UNA THINK KINYUME CHAKE KWA KUOGOPA KUJIFANANISHA NA CHELSEA?
    MAKOCHA NI KUCHUKUA MAKOMBE, BLACKBURN WALIPOONA HAWAFANYI VYEMA WAKAMCHUKUA BIG SAM NA SASA TIMU IMEBAKI KWENYE BARCLAYS.

    KOCHA PHIRI WA SIMBA AU HATA MINZIRO WAKIPEWA ZANA NA MSAADA WA PESA KAMA ANAUPATA MAXIMO BASI TIMU YETU ITAFIKA MBALI.

    MAXIMO HIVI SASA HANA PRESSURE YEYOTE ANAJUA HATA ASIPOFANYA KAZI YAKE WAKO KINA PIMBI KAMA HUYU WANAMKINGIA KIFUA.

    MARA ASEME HATAKI WACHEZAJI WENYE MIAKA 28 KAMA BONNY JEE LAMPARD ANA MIAKA MINGAPI 30,GIGGS ANA 36 LAKINI FERGUSSON HAWEZI KUMUWEKA NJE KISA CHA UMRI.

    LAZIMA TIMU IWE NA WENYE UZOEFU NA VIJANA.HAMUONI WENGER ANAVYOHANGAIKA KWA KUWA NA SERA YA MAXIMO KUWA ANATAKA VIJANA TU.

    CAF WA BRAZIL AMECHEZEA TIMU YA TAIFA YA BRAZIL HADI AKIWA NA MIAKA 36,YUKO ROBERTS CAROS, KUNA ROGER MILLER N.K

    MAXIMO HATUFAI LAKINI KWA VILE SISI NI WATU WA KUBABAIKIA WEUPE HATA KAMA HAWANA KITU TUMUACHE AENDELEE,LEO IKIPIGWA KURA KUWA YANGA APEWE KONDIC AU PHIRI INGAWA PHIRI AMEMZIDI MBALI KONDIC WATU WENGI WATASEMA APEWE KONDIC KWA VILE NI MZUNGU.

    TIMU YETU TUMEIBINAFSISHA KWA WABRAZIL KAMA TULIVYOUZA VIWANDA VYETU KWA MAKABURU.

    NAULIZA MARADORA NDIO ALIIPATA UBINGWA NAPOLI ITALY JEE PAMOJA NA KUKUTWA ANAKULA MADAWA YA KULEVYA TIMU YAKE YA ARGENTINA HAKUMUACHA KWANI ANA VITU BABKUBWA.

    BOBAN SIO MVUTA BANGI KIASI HICHO MAXIMO ANAKUZA HABARI HII,MBONA MAKOCHA WA VILABU HAWALALAMIKI?

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 11, 2009

    Wadau hebu niulize kwanza hizi stori za chipukizi zinatoka wapi? Listi ilikuwa hivi:
    Shabani Dihile, Shadrack Nsajigwa, Juma Jabu, Salum Sued, Nadir Haroub ‘Canavaro’, Henry Joseph, Mrisho Ngasa, Nurdin Bakari/Jabir Aziz, Jeryson Tegete, Nizar Khalfan/Mussa Hassan ‘Mgosi’ na Mwinyi Kazimoto/Kigi Makasi

    Kwenye hiyo listi ni Mwinyi Kazimoto na Jabir Aziz peke yao ndio unaweza kusema ni wageni kwenye hiyo timu. Wengine wote walicheza dakika nyingi tu CHAN. Huo uchipukizi wa kikosi kilichocheza jana umetokea wapi?
    Tukubali tu kwamba tumezidiwa. Tusiwasingizie wakongwe utoto.

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 11, 2009

    Watanzania tujue kua mpira si kupiga danadana tu. Kuna mambo mengi ambayo mchezaji anahitaji ili aitwe mchezaji.

    Kocha pia sikua mhamasishaji ila unhitaji vitu kadhaa ambavyo nakiri kua MAXIMO hana.!!

    Kiongozi si kuitwa raisi wa .... pia unahitaji uwe na vitu ambavyo kwenye TFF hamna hata mmoja mwanye kuelewa anachofanya.

    Nawashukuru wadau kwa kutoa nasaha na uchungu ambao viongozi wetu wa kiswahili ni kama unampigia mbuzi gitaa. Swali la kujiuliza je kwanye ofisi za TFF INternet ipo?? nA KAMA IPO JE WANAO UBUNIFU WA KUIFAHAMU GLOBU HII?? nA KAMA WANAIJUA MDA WA KUSOMA wanao??

    Nawasihi wadau wenzangu soka tuwaachie wanojua sisi tuangalie fani nyingine. Je hatujasoma kwa ndugu zetu wakenya?? Walipoona soka hawaliwezi wakatoa mijitu inkwenda nduki kama haina akili na ndio wanaotangaza nchi yao??

    Kwa ufupi wadau, mfumo mzima wa soka nchini haufai. Ushauri wangu Maximo apewe timu ya vijana na timu ya Taifa atafutwe kocha mwenye kujali matokeo na uwezo wakumudu wazoefu na wachezaji wenye majina kama Kasejea, Boban, Chuji na Nyoni.

    Mwiso na kuunga mkono mdau KISIJu japo huko nyuma nilikuona kama mchafuaji na papa la kubwata.

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 11, 2009

    heeeeeeeeeeeeeeeee

    jamaa wamekomaa ivo??kama sokwez?apo ajakusogelea na akipumua tu ivi si wazimia?wapi wachezaji wetu wangeweza kupigana buti nao km si kuvunjwa!!

    sawa tu tulivofungwa

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 11, 2009

    Kuna huyo mdau anaitwa kisiju..yeye siku zote anaona mabaya tu..anafananisha chelsea na bongo, anazungumzia habari za akina cafu..anatetea wachezaji wenye upeo mdogo sana kama vile boban na chuji..huyu kisiju ni aina ya wadau waliojaa kwenye vilabu vyetu..ukiwa na akina kisiju mia basi matokeo yake ndio hizi simba na yanga tulizonazo sasa.

    mashindano ya kagame,tusker yanafanyika hapa hapa bongo mara nyingi tu na timu zetu zinashindwa hata kufika fainali..ina maana timu hizo na zenyewe zinafundishwa na maximo?

    wachezaji wetu hawana nguvu kabisaa..ina maana maximo anatakiwa awe anawaamsha kila siku asubuhi na kuwafanyisha mazoezi magumu?..wachezaji wetu wanashindwa kabisa kujitunza..kisiju unataka maximo awe ndio baba na mama yao?

    ngasa kashindwa kucheza west ham kwa sababu uzito wake ni mdogo..kisiju unataka maximo awe ndio mshauri wa karibu wa ngasa kuhusiana na kuitunza afya yake?

    vilabu vyetu ni vibovu lakini kwa sababu ni vilabu vilivyojaa wapuuzi wa kila aina..watu hawaoni kama ni vilabu vibovu na lawama zoote anapelekewa maximo

    wachezaji wetu wanakosa nguvu za kukabiliana na wachezaji wa kigeni, katika mechi ya juzi ni henry joseph na salum sued ndio walioonekana kuweza kupambana na wacongo, wengine woote wliobakia walikuwa wepesi sana..unataka maximo aende kwenye vilabu vyetu aanze kuwasimamia mazoezi binafsi wachezaji wetu?...kisiju leta kocha kutoka hata mwezini lakini kama upumbavu huu ulioko simba na yanga ukiachwa uendelee basi usitegemee maendeleo yoyote yale..kisiju na watu wa aina yako wanawaona boban na chuji kama ni wachezaji wa maana sana...wale wacongo kila mchezaji ana uwezo kama wa boban kuanzia kipa mpaka wachezaji wa akiba...kama ligi yetu ni mbovu na inazalisha wachezaji wavivu na wasiokuwa na upeo..unategemea wachezaji wetu waweze kucheza CAN?..unategema hawa hawa wakina chuji na boban waweze kupambana na akina essien na drogba..kama wanashindwa kucheza na hawa majirani zetu wa kenya uganda na congo, wataweza kupambana na wachezaji wa kulipwa?...kisiju tumia akili kabla hujayatoa maoni yako kwenye mtandao

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 11, 2009

    uwanja naskia haukuwa na watu kabisaaa,cheki apo nyuma na si ilikua bure au kiingilio kilikua sths ngapi??

    waTz wamechoka kwishnei kabisaaa
    aisee burudani tu

    hahahahahaaaaa

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 11, 2009

    KUTOKWENDA UWANJANI NDIKO KULIKOSABABISHA STAZI KUFUNGWA KWANI NGUVU ZOTE MLIMUACHIA MUNGU PEKEYAKE. STAZI ILIKOSA WATU WA KUISHANGILIA, SASA MNALALAMIKA NINI?

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 12, 2009

    NGASSA HAKUACHWA KWA KUKOSA NGUVU.
    KAMA UMETIZAMA MECHI YA MAN U NA MAN CITY.RONALDO KAKISIRIKA KUTOLEWA NA AKAWA ANALIA KWA KOCHA KAMA ANGEKUWA MAXIMO ANGEMFUKUZA TIMU KABISA.UNAWEZA KU GOOGLE-RONALDO IS TOP OF THE STROPS.

    LEDLEY KING WA TOTTENHAM BAADA YA MECHI NA EVERTON JANA JUZI KAENDA BAR NA AKAPIGANA NA ALIWEKWA POLISI KATOKA KWA DHAMANA, INGEKUWA NI CHUJI BASI UNGESIKIA MAXIMO KUWA TAYARI KAWAFUKUZA WA NIDHAMU MBAYA NJE YA UWANJA.MAXIMO AMEKUWA KAMA MWANAMKE MMBEYA HATA KITU KISICHOMUUSU ATAINGILIA.AKIHISI UNAMTETA ANAKUFUKUZA TIMU. MIE NAONA KUWA MWALIMU MAKINI LAZIMA AWE NA ELIMU YA SAIKOLOJIA.

    OKAY KINA BOBAN NI WAVUTA BANGI MAXIMO KASHINDWA KUFANYA KAZI NA WABRAZIL WENZAKE KINA TINOCCO JEE NAO WAVUTA BANGI? KAMA NDUGU ZAKE WAMEMSHINDWA NDIO KINA KASEJA?

    KUNA KIMA HAPO JUU ANASEMA KUWA WACHEZAJI WETU WANAPONZWA NA WASICHANA JEE KINA DROGBA HAWANA WASICHANA? MARA WANAKUNYWA POMBE WACHEZAJI WOTE WA ULAYA POMBE NI KAMA CHAI UKIMUONDOA MICHAEL OWEN PEKE YAKE, KIASI CHA WAKICHUKUA KOMBE LAZIMA WAMWAGE SHAMPEN AU POMBE YEYOTE.

    KUNA KIMA MWINGINE HAPO JUU KAJA NA KINGEREZA ILI AONEKANE ANA HOJA SIJUI NDUGU YETU NI MHAYA,SAMAHANI SINA MUDA NAWE.

    MWISHO MAXIMO NI TEKNISHENI SIO KOCHA MTANIKUMBUKA SANA MIE
    MDAU KISIJU.

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 12, 2009

    Kisiju unafananisha habari za kina cristiano na taifa stars!!..kilichomfanya tinoco aondoke ni uswahili uliopo kwenye soka letu aliwafundisha wachezaji wetu pale karume kwa zaidi ya miezi miwili halafu mwishoni anasikia eti CECAFA haina heal ya kuandaa mashindano ya vijana!!, akaona ni ujinga kuendelea kufanya kazi hapa bongo, ukumbuke kuwa tinoco alikuwa anatoa programu zake kwa TFF halafu TFF wakawa wanashindwa kuzifanyia kazi..akaona ni ujinga kuendelea kufanya kazi katika mazingira ya namna hiyo, hata Itamar alikwera na mambo yetu ya kiswahili pale TFF ndio maana aliporudi Tanzania akawa tayari kufanya kazi Azam...kisiju inabadi uelewe kuwa timu zetu zinaendeshwa kienyeji sana..yanga wakati wanajiandaa kucheza na al ahly hawakuichukulia mechi ile kwa uzito kule walipojiandaa kucheza na simba!!, uone jinsi gani soka letu lilivyojaa wapuuzi.

    hao kina kaseja, chuji , boban kama wangekuwa bora si wangekuwa wanacheza hata hapo afrika kusini?..mbona wanaendelea kuozea hapa hapa bongo?..huo ubora wao wameutoa wapi?..selemani matola aliwahi kucheza afrika ya kusini na tulikuwa tunamwona kwenye super sport

    kisiju unaendekeza sana hadithi za kwenye kahawa, kila siku unaishia kusema maximo ni teknisheni, sidhani kama unaelewa maana ya teknisheni!!

    leta kocha wako kutoka unakokujua wewe mwisho wa siku kocha huyo atawachukuwa wachezaji hawa hawa wa kibongo..wachezaji wanaowaendekeza mashabiki kama wewe..timu zetu zinacheza mechi ngumu za kimataifa mara chache sana..matokeo yake wachezaji wetu wanapokwenda taifa stars wanaishia kuchemsha kwa sababu kule kwenye vilabu kumejaa wapuuzi wenye uwezo mdogo wa kuelewa mahitaji ya soka la kisasa..wapuuzi hawa ndio wanaokuja kuwa viongozi wa timu zetu.

    safari ni ndefu sana na hata akija ferguson au mourinho atakutana na wachezaji hawahawa, wadau kama kisiju pia atakutana viongozi hawahwa wenye mawazo ya kwenye kahawa.

    usimfananishe kabisa cristiano na boban au chuji..yule anafanya mazoezi magumu na anajiheshimu kule hawa wapuuzi wanaobebwa na magazeti ya michezo ya kibongo.

    kisiju nitakuona wa maana kama utaanza kuwashauri wachezaji wetu waanze kujitesa kwa kufanya mazoezi magumu kila siku ili waweze kupata timu huko nje..kuendekeza siasa za akina mziray na wengineo hakukusaidii hata kidogo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...