Mimi ni mtanzania niishiye London - Uingereza na katika muda wangu wa ziada huwa nchukua mafunzo ya kupiga Piano. Sasa katika kupitia pitia nyimbo mbali mbali ambazo huwa nazifanyia mazoezi nikaona bora nijaribu kupiga wimbo wetu wa taifa (Yaani Our National Anthem).
Nikaenda google kutafuta lugha yake ya kimuziki na nikaipata. cha kushangaza ni kwamba yapo maneno paleyameandikwa kuwa wimbo wetu wa taifa unafanana na nyimbo za taifa za Zambia na Afrika ya kusini.
Swali langu ni kuwa je nani alimuiga mwenzie?
je ni sisi au wao?
Na kwakuwa kuna ili suala la haki miliki je kwa kipindi hicho walipoigana nani alimlipa mwenziye?
Aise nitashukuru sana kupata majibu haya kwani hata mwalimu wangu wa piano ameniuliza KULIKONI.
Mdau wa Piano

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 09, 2009

    Mbona swali lako halina uhusiano na kuishi London Uingereza ? Au ndio unataka kutujulisha kuwa uko majuu ?
    Haya tumekupata bwana hongera ila jibu la hilo swali mimi sina.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 09, 2009

    Sasa mpaka tujue kama unaishi London.. Mpaka tujue kama unajifunza kupiga piano?


    Si ungeuliza tu swali lako moja kwa moja? Yaani Kuna watanzania wengine wapuuzi kweli haki ya nani..

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 09, 2009

    South Africa ndiyo wa kwanza mwimbo wao wa taifa una sehemu mbili ya kikaburu(Die Stem) na wapigania uhuru enzi hizo(Nkosi Sikelel' iAfrika).Nkosi Sikelel' iAfrika una melody kama ya mwimbo wa Tanzania wa taifa.Nkosi Sikelel' iAfrika ulikuwa composed mwaka 1867 na Bwana Enoch Sontonga ambaye alikuwa mwalimu wa shule ya misheni ya kimethodisti.Ukatumika kama mwimbo wa kuhamasisha wakati wa freedom rallies huko nyuma.Ila sasa wamezimerge ya kikaburu na huu into one song.
    Kwa hiyo it is very evident tume copy kutoka South Africa.
    Mdau mbalizi

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 09, 2009

    Muulizaji swali lazima atakuwa ni Mhaya aka Mugambire aka Infwakti.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 09, 2009

    Wimbo huu ulikuwa wa kanisani ukijulikana kama "Nkosi Sikeleli Iafrika", na ulitungwa na mwalimu mmoja ajulikanaye kama Enock Sontoga wa huko South Africa karibu miaka 200 iliyopita.

    Ulianza kutumika kama Wimbo wa ANC mwaka 1927 kabla Nyerere hajaupokea kama wimbo wetu wa Taifa mwaka 1961. Baadaye Zambia ilipota Uhuru wake nao wakaupokea kama wimbo wao wa taifa, wakifuatiwa na Zimbabwe na Namibia. Nadhani baadaye Zimbabwe na Namibia waliubadilisha. Baada ya ANC kutawala South Africa, waliupandisha kutoka kuwa wimbo wa ANC na kuwa wimbo wa Taifa wa South Afrika pia.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 09, 2009

    habari zenu jamii wote muliko mbali mbali kaka uliye uliza swahili lako la wimbo wa taifa wala usife moyo kwa waliyo na wivu na chuki yaani naona yote waliyo kusuta roho miyoyo yao wana choyo cha nafsi kina wauma hasa ngunguru akosapo mtoto wa kuku hulalamika ndiyo hao choyo cha nafsi wanakuonea gera upo majuu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 09, 2009

    Isikupe taabu!

    Ulitungwa na mwalimu wa shule ya Methodist, Enoch Mankayi Sontonga 1897 wa Afrika Kusini! Sisi tuliiga tu.

    Maneno hayo yaliigwa wakati wa kukaribia kupata uhuru na kuwa wimbo wa taifa baada ya kikundi cha wana-kanisa huko sehemu za Kusini ya Tanganyika (nadhani Tunduru au Songea) kushinda katika mashindano ya kuandika Wimbo wa Taifa.

    Maneno (lyrics) ni ya kikundi hicho.

    Music ni ule ule wa Enock Sentonga.

    Kwa kifupi, huko Afrika Kusini, ndugu zetu waliteswa na walibaguliwa kwa muda mrefu, mithili ya watumwa wa Amerika.

    Iliwabidi wajenge makanisa yao ili wajione wako nyumbani nao karibu na Mungu.

    Enoch Mankayi Sontonga (natumani na Pasta mwingine m-Ulaya) ndio walitayarisha wimbo huo.

    Hebu fungua:

    http://www.anc.org.za/misc/nkosi.html#hist

    Kuhusu Enoch Mankayi Sontonga, fungua:

    http://www.anc.org.za/people/sontonga.html

    http://www.southafrica.info/about/history/sontonga100.htm

    Born Again Pagan

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 09, 2009

    wewe anoy 7:08 uwakome shemeji zangu, infwakti ningekuwa karibu ningebit, you are mad na kichaa

    ReplyDelete
  9. Baba UbayaMay 09, 2009

    huyu mdau naye m2 wa kujinadai tu hapa hana lolote.kama kweli aliweza kwenda google na kujua nchi zipi zinatumia melody hiyo basi pia aliweza kujua nani alianza ku2mia hiyo melody.google huwa haibahatishi ktk infos hivyo ulipoweza kuupata huo wimbo na info zingine utakuwa ulizipata pia.
    huyu mdau kataka tu ku2julisha kwamba yuko London na pia anajifunza piano ktk muda wake wa ziada.
    mizee mingine hovyooooooooooooooo!!!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 09, 2009

    Mkubwa mimi nafikiri ungejiuliza nani alianza kupata uhuru kwa nchi hizi zote 3 nafikiri ndipo utajua nani kamuiga mwenzie. Changamsha ubongo usipende nyororo

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 09, 2009

    Nimesoma swali lake nafungua comments ili nione jibu lake niaje mara naona hao watu hapo juu majibu yao baaabu kubwa.MHHHHHH

    Communication btn home boys and others is way too difficult. Nimesoma swali lakini hamna mawazo yaliyonijia kichwani kuwa mwandishi huyu anajitangazia kuwa anaishi Uingereza au kuwa anajifunza piano wala nini. Ninachoshangaa hao watu wanaofikiri hivyo sijui ni kwanini?

    Kila siku huku mtu akisema sehemu anayoishi basi watu wanaona kuwa anataka watu wajue yuko majuu. Nyie watu wenye mawazo hayo, I wish ningekua na hela niwalete wooooote tu huku siku moja muone mnachomiss. There is nothing to miss huku jamani. Mtu akisema niko mahali fulani sio kuwa anajionyesha au kujishaua. No big kabisa kuishi huku. Labda kwa vile naishi huku so I am able to think this way. Mtu akiishi huku ni kama vile mtu anyeishi bongo tu na anatafuta maisha kama mbongo vile. I am sure mtu akisema yupo Mwananyamala anajifunza piano msingewaza kuwa anatangazia watu sehemu anayoishi . Sasa kwanini iwe tu kwa wanaotafuta maisha nje ya nch? Kwani hao wanaoishi Dar walizaliwa hapo? Si wana makwao mbona hamsemi that is show off kuishi Dar au kwenye big cities nyingine bongo.

    We all love our country and we all wish could live there basi tu tunaona wote tukiishi hapo patabanana.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 09, 2009

    Basi,msimponde sana,kwani kuna tatizo gani akisema yupo london? Sema nawewe ulipo ili uridhike...is that what u want!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 09, 2009

    Africa ilikuwa na ndoto ya kuwa taifa moja kubwa. Hivyo baadhi ya viongozi waasisi walionelea ni bora kuwa na wimbo mmoja wa taifa utakazoziunganisha nchi zote, ila kila nchi kwa lugha yake. Ndiyo ukachukuliwa huu wimbo na baadhi ya mataifa yaliyokuwa na matumaini katika ndoto hii ambao una mwelekeo wa umoja. Hakuna suala la ku'copy' bali ni mtazamo wa mshikamano

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 09, 2009

    I have often noticed that some people never miss a chance to critisize, misinterpret or wrongly extrapolate intentions from mere statements, as if they can read the hidden intentions of others--this is usually symptomatic of social scarring or some latent simmering bitterness of self insufficiency-carrying a permanent chip on ones shoulder
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 09, 2009

    Kwa kweli hakukuwa na ubaya wowote wa muuliza swali kujitambulisha anakoishi na kuwa anajifunza kupiga piano. Maana huko kujifunza piano na kuwa huwa anafanyia mazoezi nyimbo mbalimbali ndio umekuwa msingi wa swali lake.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 10, 2009

    Mtunga wimbo ni Enock Sontoga wa miaka hiyoooo........Copyright ni ya mtunga wimbo Sontoga (na warithi wake). Lakini mwenye copyright vile vile yuko huru kuitoa au kuigawa kama anavyoweza kugawa shati au peremende kwa kupenda tu, si lazima yawepo malipo. Aidha, haki miliki (copyright) ina kipindi haidumu milele.Huenda imesha-expire.Ukizingatia kwamaba aliutunga kwa nia ya kutumika kuhamasisha malengo au mabo ya kisiasa sidhani kama kuna swala la malipo hapa.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 10, 2009

    Comment zinavyotiririka hua zinafurahisha sana. Criticisms halafu majibu halafu wanakuja wanaowaponda wale wanaocritisize. ;)

    ReplyDelete
  18. afande midakoMay 10, 2009

    huo wimbo una utata, naona wadau wote wamebase google na sirikali yetu haipo google. nijuavyo mimi kutoka vyanzo vya sirikali wimbo huo ulitungwa na mtz mjeshi alikuwa ni captain/luteni miaka ile na south waliupenda na wakaomba nao wautumie kama national anthem. vilevile kuna mtu west/north africa anadai huo wimbo ni wake na mwanzilishi i think ni cape verde. sirikali ijuavyo asili ya wimbo ni tanzania

    ReplyDelete
  19. Anonymous wa 10.26 pm ni sahihi. Kilichotokea ni kuwa kabla ya mwaka 1961 vyama vya wagombea uhuru wa Afrika ambazo zilikuwa wanachama wa PAFMECSA (Pan African Movement for East, Central and Southern Africa) yaani TANU ya Tanganyika, KANU ya Kenya, UNIP ya Zambia, ANC ya South Africa n.k walikubaliana kuwa Afrika itakuwa na Serikali moja kama vile United States of America na wao watakuwa na the United States of Africa na watakuwa na waimbo moja wa taifa. Wimbo waliouchagua ni huo Nkosi Sikeleli Afrika wa ANC. Kwa hiyo Tanganyika ilipopata uhuru 1961 ikautumia, vile vile Zambia, Malawi, Zimbabwe. Wengine kama kawaida wakabadili mawazo (Kenya, Uganda nk). Ninavyofahamu Tanganyika maneno ambayo mpaka leo yanatumika kwenye wimbo huo aliyatunga Padri Muso aliyekuwa Mtaliani akifundisha Tosamaganga Secondary School. Waliosoma enzi hizo kama akina Mheshimiwa BAlozi Dr Mahiga atakumbuka. Hiyo ndiyo historia yenyewe. Sasa suala la haki miliki kama lipo basi anayestahili ni huyo Sopntonga wa AK.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 10, 2009

    Kistaarabu ni vyema mtu akijielezea jina na anuani yake kabla ya maelezo mengine, hii ni kukusaidia msikilizaji umuelewe vema bila kuwa na maswali juu yake. Alichofanya jamaa ni ustaarabu mtupu.

    Nawashauri watu wa nyumbani kuwa na mtazamo chanya (positive) katika issues ili tuwe watu wa maendeleo.

    GJK

    ReplyDelete
  21. Baba UbayaMay 10, 2009

    next time kwa ustaarabu zaidi mtupatie hadi majina ya wajumbe wenu wa nyumba kumi kumi ili tupate uhakika kama kweli mnaishi sehemu hizo.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 10, 2009

    dah !!!sitashangaa siku ndugu zetu walioko bongo wakianzisha kampeni ya kutuangamiza sisi tulioko majuu tukiwa tunakatiza mitaa ya kipawa pale tukitoka zetu majuu na tudolali twetu tulitotubebea boski manaake naona haters kibao...LOOOOL...inasikitisha na kufurahisha pia.wabongo bwana wee waache tu kwi kwi kwi kwi.
    mdau mamtoni....haya nirogeni sasa na mimi manaake niko ulaya mtake msitake

    ReplyDelete
  23. Mdau, pandipiyeriMay 10, 2009

    Bongo raha jamani, yaani raha tu, au niseme laha?? mkabla ya jibu kwanza unapewa za uso, shwari vibaya!!

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 10, 2009

    Mtu kama huwezi kutoa msaada wa kitu ulichoulizwa, usijibu kingine kama hauna jibu. Kama mtu anajibu swali tofauti na kitu kilichoulizwa. Si lazima tusome maoni yako. Kujitambulisha ni kitu cha kawaida kwa binadamu yeyote. Mara mhaya, kwani mhaya aliwafanyia nini? Ni lazima tuwe tunajibu kutokana na swali lililoulizwa sio kujibu tofauti. Kama hauna maoni, usiandike pumba zako hapa. MWEEEE!!!!!!!!

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 10, 2009

    Kweli jamaa yawezekana ni Mhaya kabisa majidai yamezidi au Mkinga mi naona. Kama upo UK hujui kutumia Google ikupeleke kwenye wikipedia hapo utapata majibu ya maswali yako yasio na kichwa wala miguu ukishindwa ndio uulize. WATANZANIA TUNASIFA YA UVIVU WA KUSOMA ILI KUPATA UFUMBUZI WA VITU WEWE NI MMOJA WAPO. HAYA UMEPATA MAJIBU YAONGEZE KWENYE UJUZI WA PIANO YAKO

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 10, 2009

    Piano unapiga, nyimbo zinapigika sasa hilo suali linahusiano gani. Nenda ubalozi wa TANZANIA,ZAMBIA NA SOUTH AFRICA ukaulize

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 11, 2009

    Mimi ni mtanzania niishie Tanzania.. WEWE ANANONIMOUS WA "Tarehe May 09, 2009 6:58 PM", kimekuuma nini huyo mhusika kuanza kwa kueleza story yake kidogo na hasa pale aliposema anaishi London!!??!! Hapo alikuwa anajaribu tu kuelezea mazingira aliyoko kwamba huwa kuna desturi ya kujielimisha kwa kitu kingine.. Mimi na marafiki zangu kwa huku Tanzania (Dar es Salaam), ningeweza kueleza kuwa "..kwa muda wa ziada baada ya kazi, ili kuepukana na adha ya traffic-jam huwa tunakaa sehemu na kuvuta muda kwa kupata chupa moja mbili au kukutana na marafikiri sehemu kama RoseGarden na kubadilishana mawazo ya jamii, kisiasa na kiuchumi). Then baadae ndio ningeweza kuongelea mada yangu ikiwa na uhusiano na mazingira niliyoyatolea maelezo....

    Huyu bwana kaongelea na kuulizia mada yake ya mazoezi ya kupiga piano na kuuliza swali juu ya wimbo wa taifa.. Mbona sisi tumeona kuwa "swali lake kuhusu nyimbo za taifa za nchi 3" ina uhusiano na "maelezo yake kuhusu kupiga piano?"... Hapa inaonyesha kuwa wewe ndio ukuelewa baada ya kutaka kuhusunisha swali na neno London. Na hata sishangai baadae uliposema huna jibu la swali hilo, maana ninatumai hata swali hukulielewa..

    Well, mimi nafikiri nchi ambayo ilipata uhuru mwanzo kabla kati ya nchi hizo 3, ndio nafikiri itakuwa ni ya kwanza kuwa ilianza kuwa na wimbo wa taifa.. Labda tu, kama inatokea nchi ikawa na wimbo wa taifa hata kama ikiwa bado iko chini ya utawala wa kikoloni. Na ukiangalia kwa makini zaidi.. bendera ya taifa ya nchi ya Afrika-Kusini ina shabihiana kwa karibu sana na bendera ya taifa ya Tanzania. Pia tukumbuke kuwa Tanzania ni nchi ambayo imechangai kwa kiasi kikubwa ktk kuchochea upatikanaji wa uhuru wa Afrika-Kusini kwa kuwa na kambi ya mambo ya kisiasa ya Afrika-Kusini (mpaka sasa kule Morogoro kuna makazi maalum ya wananchi wa Afrika-Kusini waliokuja Tz kwa hifadhi). Uhuru wa nchi nyingi za Kusini mwa Afrika ulitiwa motisha na serikali ya Tanzania chini ya Baba wa Taifa Nyerere. Hiyo ni picha nzima kwa ufupi kuhusu Tanzania na Uhuru wa Nchi za Kusini mwa Afrika.

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 11, 2009

    YAMEKUWA HAYOOO!!! NAJUTA KUWAFAHAMU WABONGO, POLE MDAU WA PIANO.

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 11, 2009

    Wadau mliojibu wote nawashukuru japokuwa siye niliyeuliza swali hilo.Unajua katika blog hii kuna watu wengi tu na kila mmoja ana akili yake na kama wahenga walivyosema akili ni nywele lila mtu anazake...!!!!.hivyo tusishangae kuona majibu ya kila aina maana yanatoka kwa watu wenye akili tofauti.
    Hata hivyo na mimi nina swali napenda kuuliza mtunzi wa wimbo
    TANZANIA TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WOTE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...