KAMPUNI YA DMK GLOBAL PROMOTIONS
ONCE AGAIN
INA WAKARIBISHA KWENYE DC CARNIVAL WEEK END.
***FRIDAY JUN 26 - A PRE- CARNIVAL PARTY- AT LUX LOUNGE DC ***INVITEE- ALL AFRICANS & CARIBEANS
***SATURDAY JUNE 27- HII NDIO SIKU YA CARNIVAL YENYEWE **PARADE ITAANZA SAA 5 ASUBUHI@
MISSOURY & GEORGIA AVENUE TO HOWARD UNIV.

** LOOK FOR A BIG TRACK SAYS AFRICARNIVAL WITH BIG MUSIC & AFRICANS MODELS.
***ALAFU USIKU WENYEWE SASA WA AFRICARNIVAL AFTER PARTY ITAKUWA
** **** GALLERY LOUNGE
1115 EAST WEST HIGH WAY
SILVER SPRING,MD,20910
***MUZIK BY CAT DADDY -DJ JOE 93.9WKYS FM & DJ CHICK FROM LUX ***AFRICANS & CARIBEANS-
***PLEASE DRESS FASHIONABLY
***PLEASE COME FASHIONABLY EARLY
- DOORS OPEN AT 9PM
RSVP PLEASE GO TO
ALSO MAELEZO ZAIDI -
CALL DICKSON # 301-661-6207
AU VISIT-
WWW.DMKPRODUCTION.COM ,

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 25, 2009

    Ndugu zangu watanzania.
    Sidhani kama ni busara kuhudhuria paredi la africanival.Sina tatizo kabisa na after paredi party/Disco.Tatizo langu ni kuwa paredi hilo linalojumuisha wakaribian(watoka visiwani) karibu wote waoishi hapa US ni aibu tupu.Akina dada wana vaa chupi mostly thongs na sidiria ndogo zonazofunika chuchu,wanajipaka majivu usoni na manyoya kichwani na kudai kuwa huo ni utamaduni wa kiafrika ingawa bado sijajua ni Afrika ipi wanayoizungumzia.Nashukuru kuwa watanzania hapa DC tupo wengi sana,mimi nimeishi hapa karibu miaka ishirini sijaona wala kusikia baadhi yetu tumeshiriki paredi hili.Naomba tuendelee na moyo huo.Ningependa sana kupata picha ili niwawekee mjionee wenyewe lakini inabidi niwapeleke watoto wangu Ocean city hadi hilo wingu la paredi lipite.Kwa rafiki zangu mnaoishi DC ambo mnastaajabu ya Musa mkitaka kuyaona ya Firahuni nendeni mkachungulie.Msisahau kamera.Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 26, 2009

    Kaka MIchuzi naomba usiibanie hii msg yangu ili nimjibu huyo mtu hapo juu.wewe dada hapo juu ingawa umeficha jina lako lakini sisi tumeisha kujua,Kwanza- event inasema AFRICARNIVAL hata kuspell kwenyewe umespell wrong,wewe unaongelea Caribbeans,Pia maelezo hayo kwenye event yanasema look for big track says Africarnival na sio carnival-this is pure african track likiwa ma model wa kiafrica na costume za kiafrica sio za Caribbean.Sasa wewe kama hujui unacho kiongea usiwakatishe tamaa wenzio,kama tatizo lako kubwa ni chupi mostly thongs sasa kwanini unasema unawapeleka watoto wako ocean city? Do you know kwamba ocean city is a beach area mahari ambapo CHUPI na THONGS ndio mahari pake?Dada inaonekana umetaka tu kuwaambia watu kuwa unaenda ocean city maana sidhani kama wewe unaishi Georgia avenue maana parade wanasema inaanzia Missouri to howard university,tumekuwa tuna udhuria every year yaani sasa hivi kwasabau tu one of the Tanzanian ana host ndio maana tunakatishana tamaa watanzania jamani tupendane,sisi tuko mbali huku!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 26, 2009

    Asanteni sana kwa kutukaribisha kwenye paredi ili tukapate laana.Namuunga mkono huyo dada anayewapeleka watoto wake Ocean city kuogelea.Mimi nimeoa mjamaika na ameniambia kuvuta bangi wakati wa paredi ruksa kulingana na utamaduni wao.Kwenye disco lako mkurugenzi wetu wa DC tutakuja kukuunga mkono maana daima tunakutakia mema na mafanikio lakini kwenye paredi tunaomba utusamehe.Hayo mambo ni kinyume na utamaduni wetu kaka.peace.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 26, 2009

    Sisi ni watanzania. Upendo na amani ndio nguzo zetu za kujivunia. Watu inabidi tuwe waangalifu na maoni yetu tuyatoayo ili yasilenge kwenye chuki na aibu.Watu wengine wasiokuwa na busara tena wana familia zao walishakuwa addicted na mtandao uliofungwa wa ze utamu hivyo wanajisikia kutoa maoni tu ya kipumbavu hata kama hayana malengo. Wameishabobea kwenye kashfa, chuki na matusi. Ndugu yetu michuzi waangalie hao watu wasije kuharibu website yako yenye heshima.Kwa hapa Washington DC na Maryland watu hao wanajulikana na ni hao hao wanakuwa kwenye circle ya kutukanana na chuki.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 28, 2009

    PEACE AND LOVE IN WASHINGTON DC.MJADALA UMEFUNGWA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...