vipaji bwelele bongo siku hizi. leo globu ya jamii inawaletea barnaba na pipi. haya ndiyo baadhi ya matunda ya Tanzania House of Talent (THT)
Home
Unlabelled
barnaba na pipi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
vipaji bwelele bongo siku hizi. leo globu ya jamii inawaletea barnaba na pipi. haya ndiyo baadhi ya matunda ya Tanzania House of Talent (THT)
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Honestly,nimeangalia video hii huku mwili unasisimuka.
ReplyDeleteSABABU:
1.Kuna kitu ndani yake ambacho siwezi kueleza ni nini,lakini kinamahusiano ya moja kwa moja na hisia zangu.
2.Video inaonyesha hali halisi ya maisha ya kawaida ya walio wengi,Nina maana si ya chini sana na wala si ya juu.Hata usafiri uliotumika ni "CHENGE TRANS"
3.Sauti zimepangiliwa vilivyo,na vitendo vinaendana sawia na maneno yanayoimbwa.
4.Nina hakika hawa vijana ni "threat" kwa wasanii fulani wa Bongo ambao wana majina makubwa,kwa sababu wanaweza wakawapoteza muda si mrefu,yaani hawa ni "funiko bovu".
5.Mwisho nitakua mchoyo wa shukrani na fadhila endapo sitokili kwamba kuna ukweli na mahusiano dhahiri na kazi ilofanyika hapa,yaani Tanzania House of Talents.
Ndimi,
Mkulima-Kijijini Gezaulole.
wimbo upo bomba kinoma, sauti zimepangiliwa na zikapangika haswa. kazi nzuri sana. kaka Michuzi asante kwa kutuwekea video za muziki wa bongo blogini angalau na sie tulio mbali na nyumbani tunaenjoy. Keep it up!
ReplyDeleteThis song is 100 percent tight...wat a song???
ReplyDeleteHands up Tanzanians....
Nyimbo nzuri na Lyrics nzuri...
Kitu kimoja tu...We need improvements ktk video, ni hicho tu.
Wadau nisaidie nifanyeje ili nione video hii?
ReplyDelete1.We anony ambaye huwezi kuona hii video, usisubiri ianze yenyewe. ukiona haianzi ku-play baada ya ku-press play,isukume kidogo (drag it forward). Pia mimi nilipata tatizo hilo.
ReplyDelete2.Kwa hawa vijana (Barnaba & Pipi) kwakweli wamefunika. Nilikuwa nasubiri kwa hamu kuona huu wimbo video yake itakuaje maana nimekuwa nikiusikia tu kule JamiiForum. Kwa kweli wamejitahidi sana. Ila wangepunguza kutuonesha vitanda ingekua poa sana. Big up vijana, I hope huko THT mmejifunza pia kupiga instruments, otherwise mtaishia kuimba na CD tu wakati wenzenu wanahamia kwenye live band
Mdau
Cardiff
Wote hii nyimbo kali ila video haina deal sababu kwani walivyoenda kukutana siwangepigiana simu wasubiriane? wakalale mbele.
ReplyDeleteoya michuzi nigee namba ya huyu pipi,mzee mwenzangu!tuheshimiane bwana!ala!
ReplyDeleteyap hapa nimekubali,nilitoa comment moja ya kusisitiza improvement kwa wanamuziki na maproducer wa kibongo, lakini hapa nimekubali bila kinyongo.hawa vijana niwazima.someone can make business with em.
ReplyDeletebravo!
Wimbo ni mzuri sana vijana.Sauti zimepangiliwa vizuri sana.Hakika kila mtu mwenye akili timamu atakayesikiliza atapenda.Hongera sana vijana.Tunajua kua mwanzo ni mgumu,lakini kama huu ndiyo mwanzo basi huko mbele mtakuwa moto wa kuotea mbali.Lakini mtakaporekodi video hapo mbeleni basi matendo yenu yawiane na hisia za wimbo.Mfano binti katangulia kufika,wakati anasubiri anonekana anaongea na simu.Kwanini asimpigie simu kujana kujua kama yupo njiani kabla hajaamua kuondoka.Ama kwanini kijana asimpigie simu binti kujua kama ameshafika nk.Kwanini hamkupigiana simu siku nzima baada ya kukosana maana huo wimbo umeimbwa siku zilizofuatia.Ama basi msingeonyesha kama mnatumia simu kwenye video nzima.Naamini kuwa mlikotoka ni mbali na mnakokwenda ni karibu,kazi nzuri endeleeni na juhudi na nyota yenu itang'ara zaidi na zaidi.
ReplyDeleteHiki kisichana kina macho mazuli!! ah,,,,,hongera mademu wa kibongo
ReplyDeleteHey kuna mchangiaji mmoja alikuwa anajaribu kumponda MARLAW hapo kwenye ule wimbo wa pi-pi eti anatumia lugha gani-akimaanisha kwanini anatumia 'kiswanlish'.Nampenda kumtoa hofu kwamba hicho ni kitu cha kawaida kwenye muziki.
ReplyDeleteMfano:
1:Barnaba ametumia neno la kihispania SENORITA(msichana mzuri?)
2:Michael Jackson(RIP),wimbo wa Liberian girl alitumia kiingereza na kiswahili.
3:Sipho Mabuso(SA) wimbo 'Zanzibar'ametumia kiswahili,kizulu na kiingereza
4:Brenda Fassie wimbo 'Nakupenda'kausikilize
5:Shakira-My Hips don't lie.English+Spanish.
6:Wanamuziki wa Congo ndiyo usiseme.Kiswahili,Kifaransa,Kilingala.Mfamo wimbo wa Yondo.'Nakuwazawaza we binadamu'!!